Kufungiwa umeme kwa mkopo....

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Shirika la umeme Tanzania kwa kushirikiana na bank ya Benki ya biashara ya AKIBA ,wamezindua mradi wa mikopo ya huduma kwa watu binafsi utakaojulikana kwa jina la ACB UMEME LOAN.
1. Nawauliza ninyi TANESCO mita mnazo..........?
2. maombi yaliyowasilishwa kabla na watu wameishalipia mtayamaliza lini kuwafungia umeme kabla ya kuanza utapeli huu.
3. tsh laki tano za sasa wananchi zinatushinda, huko ACB riba yake mmehakikisha tutaimudu...?
 
Duh, kama ndivyo basi tutashukuru sana maana wengine tgueambiwa inahitajika kama nguzo nane ndo umeme ufike kwetu
 
mie ninajamaa zangu toka january wamelipia mpaka dakika hii umeme hawajapa eti kisa mita hakuna. Habari za ndani inasemekana kuna boss aliyesimamishwa kazi hali yakuwa yeye ndiye mtu pekee signature yake inatambulika huko kwenye kampuni iyopewa tenda huko nje. Cha ajabu tulisikia kuwa kuna duka moja lipo mikocheni la kampuni moja inayokuwa inafanya kazi za tanesco kuwa wao mita wanazo ila ukiihitaji eti unapeleka barua ya mahitaji ya dharula kisha wanakuruhusu kwenda kununua kisha unawapelekea mita namba wanaingiza kwenye cctm yao na ina cost eti 260000 sasa nikajiuliza inakuwaje mtu binafsi alete mita eti serikali ishindwe!!! Sasa hili nalo naliona kama maajabu kwani tanesco kama tayari inazo hizo mita basi ilikuwa hakuna sababu yoyote ya wao kufanya wateja wao eti wapitie bank,kwani wao wenyewe wanauwezo wa kuwakopesha hizo mita wateja kwa kuziwekea loan kwe mita namba hizo ili muhusika awe na kiasi maalum atakachotakiwa kulipia kwanza ili aweze kununua luku,yaani kama zile nyumba ambazo hazikuwa na luku na wakawa wanawadai walivyowabafirishia waliingiza deni kwenye mita namba. Watu wa tanesco leteni mchanganuo
 
Back
Top Bottom