Kufukuzwa kwa Rais wa Vijana wa ANC Julius Malema na hulka za Viongozi wa Afrika kukimbia Changamoto

Hivi mnamjua vizuri Malema? Huyu jamaa ni political striker isipokuwa ni mla rushwa mkubwa pia. Alipokosea ni pale alipoanzisha move ya kumng'oa Zuma ili makamu wa rais apewe madaraka.
Siamini kabisa katika uongozi wa watu wa aina ya Malema kwenye karne yetu hii. Na jinsi anavyopendwa ANC wana kazi kubwa kukilinda chama chao
 
Ben.....nadhani unaelewa vyema kuwa tunapohitaji viongozi huwa hatutafuti toka kundi la malaika bali miongoni mwetu wanaadam ambao hatuyakosi mapungufu but how we deal with them.
Kama tuna mapungufu sawa lakini si kuyaendekeza.
Katika mtazamo wangu mimi, kwangu Malema alikuwa ni Daytime friend but a night time.............
Tabia ambayo ni moja kwa moja inam disqualify a hero/heroin from the upper position to the root level.

Sir,

Sana sana watu wanahusisha mali alizo nazo.JuJu is rich and he doesn't hide the fact that he is rich. The thing that makes Julius Malema popular with the youth is that he wants other young black South Africans to be rich. They see a young rich man who publicly fights with government, corporate/industry heavyweights and others all in the interest of the youth, they don't care whether he's rich or poor - all they care about is the message that he delivers on their behalf.
 
Malema ndio chanzo cha Mbeki kufukuzwa kabla ya muda na aliwahi kusema yuko tayari kuua kwa ajiri ya Zuma. Ila hana displine kabisa
 
Wakati anaimba hizo nyimbo za kuuwa Boers ambazo hata Mandela aliimba na yeye ndiyo anazitetea, Mandela mwenyewe ameshauzika MKUKI WA TAIFA (Umkontho we sizwe.)

Sasa kama Mandela mwenyewe ameshauzika, wewe kwa nini kijana mdogo ambaye siku hizo ulikuwa unatembea uchi, umepata wapi ujasiri wa kwenda kuufufua huo Mkuki na kuuleta tena kwa watu?

Yaani kakosa nyimbo za kujenga UTAIFA? Nyimbo za URAIA ambazo wote wataimba? Wazungu nao wakianza kuimba nyimbo zao za kibaguzi na kusema "ni sehemu ya historia" je huyu mtu atafurahi?

Mandela akizika Mkuki na kuimba pamoja na Wazungu.

 
Last edited by a moderator:
Suspended ANC Youth League president Julius Malema says: "What I like about these people who have suspended us is that they are brave, they are not scared." Lakini katika siasa za Tanzania, kwa nini wanaofanya maamuzi ndani ya vyama vya siasa wanashindwa kuwa "brave" kufanya maamuzi, badala yake wanakuwa too "scared" hata kufikiria kufanya maamuzi?
 
Sir,

Sana sana watu wanahusisha mali alizo nazo.JuJu is rich and he doesn't hide the fact that he is rich. The thing that makes Julius Malema popular with the youth is that he wants other young black South Africans to be rich. They see a young rich man who publicly fights with government, corporate/industry heavyweights and others all in the interest of the youth, they don't care whether he's rich or poor - all they care about is the message that he delivers on their behalf.

I have a tendency Mr. BIg Man...a tendency of reasoning with people to find where their logic lies, though that wont change mine.
I will try to stand at you angle to see what you see, until then I remain puzzled with you vision on the whole thing
 
I have a tendency Mr. BIg Man...a tendency of reasoning with people to find where their logic lies, though that wont change mine.
I will try to stand at you angle to see what you see, until then I remain puzzled with you vision on the whole thing

Issue hapa ni yale ambayo JUJU amekuwa akiyapigania,social justice,economic prosperity.Inahitajika Radical Reform na South Africa sasa needs to play her role at global stage! ANC hawajatoa solution ya matatizo mazito yaliyoibuliwa yaliyo na backup kutoka vyama vya wafanyakazi na makundi mengine,madai ambayo kimsingi yalifunika kwa kiasi fulani madhambi ya JUJU na mapungufu yake ya kibinadamu

I am kinda predicting a gradual shift from the ANC to the DA party for some of these "black up and coming middle class" elite being created when the poor start attacking the very elite that is being created witin the ranks of the ANC and banging on the doors of the party these guys will have no choice than to shift to a party that might more protect their interests. In case mwanamama Lindiwe Mazibuko atachukua control ya DA kuna uwezekano wa division ndani ya ANC but inahitajika carefully scrutiny ya wale watakaojiunga huko as i dont support such kind of crosscarpeting unless DA change and comromise some values from it s policies modification of it s ideology to contain youths ambitions.
 
Hili jambo linafundisha jambo moja tu hasa kwako wewe ben na ndugu yako Zitto! Ikifika muda na mnayoyafanya tutawaondoa kwenye chama na zingatieni hilo!! Kujua kwenu kusikojua mnaharibu chama chetu!

Ben Saanane huwa hakubali kushindwa. Huyu ni rebellious mara zote hata chaguzi za huku vyuoni yeye akigombea pamoja na kujua kujenga hoja lakini ni mtu mbinu chafu za siasa na mlipaji mzuri wa visasi...... Alichowafanyia akina Lewis Onyoni wa Kenya hadi leo baada ya kumaliza vyuo wanatoleana vitisho mmoja akiwa Kenya na yeye akiwa Tanzania. Wote wanafikiria siku wakitwaa nchi zao wataimaliza nchi nyingine. Ni jambo la hatari mbegu hizi zikiachwa zichipuke.

Hapa tumeona anamtetea Julius Malema kwa kuwa ni Rafiki yake. Nilishawahi kuandika juu ya kuchocheana wanakofanya, nitapata data nitawaeleza ukweli wenyewe na jinsi ambavyo alivyowafundisha akina ole millya kutumia mbinu hiyo ndani ya UVCCM.Ni aibu sana mtu ukiwa chama kingine unaingilia na kuvuruga vyama vingine, je tukuulize ndani ya CCM kuna wasafi? Chama chako kila siku kinawashutumu CCM tangu lini wewe ukaona wasafi hadi uingilie? Tunajua watu ambao unawatumia inachanganya ajenda yako na wenzio ni ipi hasa
 
Malema ndio chanzo cha Mbeki kufukuzwa kabla ya muda na aliwahi kusema yuko tayari kuua kwa ajiri ya Zuma. Ila hana displine kabisa

Ni kweli mkuu huyu jamaa ni mropokaji mno aliwahi kusema mwanamke aliobakwa na Zuma had "a nice time". Hajui kuchagua maneno ya kuongea na alilewa mno kuungwa mkono na wana ANC kiasi cha kuhisi yeye ndiye mwenye mamlaka ya kumweka madarakani rais atakaye.
 


Naongelea vyama vyote.Hakuna chama hata kimoja kimekuwa perfect katika kuhakikisha vijana wanakuwa independent na wana-spear head ajenda zao.Vijana wanatishwa na kamati kuu za vyama vya siasa huku tukijibaraguza wakati wa kura kuhitaji kura zao.Nina uhakika huu ni muendelezo wa madhaifu ndani ya vyama vya siasa na serikali kwa ujumla ndiyo maana hatuna baraza huru la vijana.

Suala la Chadema ni suala lililo ndani ya uwezo wetu tutajadili,tutashinikiza ndani ya chama hiki itakaposhindikana kama ilivyoshindikana ndani ya ANC ndipo tutakapofanya movement za wazi kama alizofanya Julius Malema na ANCYL.Nisome between the line...........!




Hakuna cha ushabiki hapa.Hili ni suala linalohusu vyama vyote ikiwemo CCM.Ni jana tu kuna mijadala iliyokuwa inamuongelea Mwenyekiti wa NCCR na Kafulila,Huko CCM Nape alipokuwa anagombea uenyekiti wa vijana nae alfanyiwa ghiliba,Chadema tuna yetu tunayapigania sitayajadili kwa sasa hadi solution ishindikane, CUF wana yao kwenye nafasi ya ukatibu mkuu,TLP kwa sababu hakuna jumuiya ya vijana wameelekeza nguvu kusikostahili kwa Hamad Tao.Ni yapi yasiyojulikuana saa hizi?

Sijui Nyerere alipokuwa anaongea ukweli kuhusu mapungufu ya chama chake na serikali kwa nini hakufukuzwa.Tuige basi angalao aina ya siasa wanayofanya Raila Odinga na chama cha ODM na Akina Ruto,Kosgey na wenzake.Naona political immaturity na maslahi binafsi vinatuwekea ukungu katikati ya daraja la Demokrasia,daraja lililotoboka! Afrika,eish!
Ben kama usalama wa taifa wameshaku recruit your among the best intelligence personnel we got! Kama bado wanangoja nini? All the best bro! Tutahojiana hapa hapa siku moja when the truth reveled!
 
Ben Saanane tumesoma nae,huwa hakubali kushindwa.Huyu ni rebellious mara zote hata chaguzi za huku vyuoni yeye akigombea pamoja na kujua kujenga hoja lakini ni mtu mbinu chafu za siasa na mlipaji mzuri wa visasi......Alichowafanyia akina Lewis Onyoni wa Kenya hadi leo baada ya kumaliza vyuo wanatoleana vitisho mmoja akiwa Kenya na yeye akiwa Tanzania.Wote wanafikiria siku wakitwaa nchi zao wataimaliza nchi nyingine.Ni jambo la hatari mbegu hizi zikiachwa zichipuke

Hapa tumeona anamtetea Julius Malema kwa kuwa ni Rafiki yake.Nilishawahi kuandika juu ya kuchocheana wanakofanya,nitapata data nitawaeleza ukweli wenyewe na jinsi ambavyo alivyowafundisha akina ole millya kutumia mbinu hiyo ndani ya UVCCM.Ni aibu sana mtu ukiwa chama kingine unaingilia na kuvuruga vyama vingine,je tukuulize ndani ya CCM kuna wasafi?chama chako kila siku kinawashutumu CCM tangu lini wewe ukaona wasafi hadi uingilie?Tunajua watu ambao unawatumia inachanganya ajenda yako na wenzio ni ipi hasa

Duh,umerudi kupotosha watu tena....hizo kambi zenu sijui Nape vs Ole Millya,sijui Ridhiwani vs Benno Malisa ndani ya UVCCM yenu hazinihusu,kwa nini nishughulike na chama ambacho kinakaribia kufa?

Pia,uache kupotosha watu kwani ningekuwa mtu wa visasi kama unavyodai hapa nisingekuwa close na Mwenyekiti wa vijana wa mkoa wa Mbeya kamanda Comrade Emmanuel Mwakajila ambaye nilijua wazi hataniunga mkono kwenye uchaguzi wa vijana wa BAVICHA,na bado tulikaa pamoja hadi leo tuko pamoja katika mambo mbalimbali.Ingekuwa ni huko ndani ya chama chenu tayari mngeshawekeana sumu.Naomba ulete ushahidi wa haya unayoandika.Otherwise you are worth to be ignored!

Ben kama usalama wa taifa wameshaku recruit your among the best intelligence personnel we got! Kama bado wanangoja nini? All the best bro! Tutahojiana hapa hapa siku moja when the truth reveled!

Mtazamo,

Duh......! Tumefika huku tayari.

Nilishasema hili la kusema fulani ni usalama,au katumwa n.k ni njia ya kujihami kwa baadhi ya wanasiasa ambao kila siku wanakula na usalama wa taifa na vyama hasimu bila wanachama wao kujua lakini wakija in public wanavaa usamaria wa kisiasa.

Otherwise thanks,
 
Malema amekuwa mkorofi mno, na amekuwa akitumia vijana for pushing his own agenda, hata baada ya kupewa 'suspended sentence' wengi tulifikiri angejirekebisha lakini alizidisha ukorofi pamoja na back up ya winnie mandela, Tokyo Sexwale, Fikile Mbalula na
wengine ilikuwa ni dhahiri this time asingepona, sidhani kama alikuwa ni mfano mzuri wa kuiga,alijisahau sana na alifikiri he is untouchable

I luv Julius Malema; he is a true son of africa!

 
Last edited by a moderator:
I am kinda predicting a gradual shift from the ANC to the DA party for some of these "black up and coming middle class" elite being created when the poor start attacking the very elite that is being created witin the ranks of the ANC and banging on the doors of the party these guys will have no choice than to shift to a party that might more protect their interests. In case mwanamama Lindiwe Mazibuko atachukua control ya DA kuna uwezekano wa division ndani ya ANC but inahitajika carefully scrutiny ya wale watakaojiunga huko as i dont support such kind of crosscarpeting unless DA change and comromise some values from it s policies modification of it s ideology to contain youths ambitions.

Lindiwe huyu tea girl au mwingine??????????????

 
Last edited by a moderator:
Ben,

Niliifurahia hii thread maana hata mm nilitaka kupost the same jana. Lakini michango ya watu naona ime divert maana nzima. Watu wamebaki kumshambulia na kumjadili Julias na wewe wakaacha jambo la msingi.

Nadhani tulitakiwa kutazama alichokuwa anakifanya, anachosimamia, nafasi yake na yaliyomkuta Julias kama kijana kisha tuone tunajifunza nn ss vjana wa Tz. Hapo tutakuwa tunaitendea haki hii post na itakuwa na maana.

Binafsi naona sisi vijana wa kitz ni waoga, tusiokuwa na msimamo, tunaodanganywa kwa rushwa za kipuuzi na hatuna msimamo hata kwenye mambo yanayotugusa. Na kama tungekuwa tunatakiwa kuwaondoa wakoloni, basi tusinge upata uhuru kabisa! We're very stupd kiasi cha kutumiwa kumnufaisha mtu kisiasa huku tukifahamu kabisa atatutupa akishafikia malengo. Tuna mifano lakini haitujifunzi. Tunaishi kwa kutegemea hisani. Shule tumesoma lakini ni waoga hata kufanya kazi. Kwa kifupi, hiki ni kizazi kinachotegemea ukombozi kutoka kwa watoto wa mtaani, chokoraa, mateja, machalii maana ndio angalau wanaujasiri kidogo!
 
Aina ya wanasiasa kama akuna BEN you will never find them getting chance to lead!

hawa ndio wa caliber ya akina Zito na Omary Lyas wale ambao wako tayari kuandamana wakiwa wawili au mmoja tu!

hawa ni wale tunaowaita radicals kwa sababu ya maslahi yetu na caliber yetu ya ku-compromise na situation!

They are smart, nationalists and ready to do anything to defend rights!

Tatizo wasiojua issues za siasa nchi hii wako tayari kusema lolote lile because of their ignorant

sorry pengine siyo jukwaa lake hili, I have never trusted Mbowe....never

siyo kwa sababu ni mfanyabiashara
siyo kwa sababu ana urafiki na Kikwete na Lowasa
not because he is son of Late Nyerere

ila kwa sababu anawahadaa watanzania na kuwapeleka kusiko! hayuko tatayri kuchukua nchi kutoka CCM hata kwa fimbo!

these people are yudas appear in white garment as angels.....they are there for their matumbo...

If you dont believe my words..wait we have 50 yrs to remove CCM from power.

I will trust akina Ben na timu yake..
 
Ukweli ni kwamba kuna ombwe la uongozi nchini!Si kwamba tunazungumza kwa wivu ila ukweli wewe SI KIONGOZI INGAWA UNAJIBARAGUA KAMA KIONGOZI!Na kwa mantiki hiyo imefikia sehemu hata vijana waliokuwa na mapenzi na nchi yao lakini hawajishughulishi na siasa directly wamefikia hatua ya kuichukia nchi yao!mimi ni mmojawapo!Aina ya vijana nyinyi wakina Ben,malisa,ridhiwani,nape na hata kwa upande mwingine Zitto mmetuharibia sana vision yetu katika politics!!Uwezo hamna wengi mmefika hapo kwa kubebwa au bahati za mtende kama wakina Zitto ingawa leo anajifaragua sana na kwa mtindo wa siasa zake za kuuza sura katika jamii yetu iliyoelemewa na matatizo lukuki kuna kipindi anafanikiwa,kuna kipindi anakoswa taswira kama sasa!!!Kifupi siasa mnazoziendesha hazina tija wala mashiko!!Ni siasa tofauti zilizoendeshwa na vijana wa Afrika kama wakina Sankara,Nyerere,Mugabe na wengineo!!!!na watu wa aina hii ndio muwazibia na wakijitokeza mnafanya hila na pengine nao pasipo kujua hujikuta wameangukia katika style ya siasa zenu!Tunahitaj watu wenye mawazo kweli ya kianamapinduzi!!Hata vijana kama wakina Silinde mmeanza kuwaingiza kwenye siasa zenu chafu na alifika hapo alipo kwa uana mapinduzi wake na sio siasa zenu chafu!Nayasema haya mimi si mwanasiasa!ni mwanataaluma mwingine kabisa and i was there during ZITTO TIMES AT UDSM!!NA SIHITAJ UNIJIBU JUA TU SIASA ZENU HAZINA MASHIKO HATAS KAMA MTAFANIKIWA SIASA ZENU HAZINA MASHIKO NA IPO SIKU MTAANGUKA TU!!
Duh,umerudi kupotosha watu tena....hizo kambi zenu sijui Nape vs Ole Millya,sijui Ridhiwani vs Benno Malisa ndani ya UVCCM yenu hazinihusu,kwa nini nishughulike na chama ambacho kinakaribia kufa?

Pia,uache kupotosha watu kwani ningekuwa mtu wa visasi kama unavyodai hapa nisingekuwa close na Mwenyekiti wa vijana wa mkoa wa Mbeya kamanda Comrade Emmanuel Mwakajila ambaye nilijua wazi hataniunga mkono kwenye uchaguzi wa vijana wa BAVICHA,na bado tulikaa pamoja hadi leo tuko pamoja katika mambo mbalimbali.Ingekuwa ni huko ndani ya chama chenu tayari mngeshawekeana sumu.Naomba ulete ushahidi wa haya unayoandika.Otherwise you are worth to be ignored!



Mtazamo,

Duh......! Tumefika huku tayari.

Nilishasema hili la kusema fulani ni usalama,au katumwa n.k ni njia ya kujihami kwa baadhi ya wanasiasa ambao kila siku wanakula na usalama wa taifa na vyama hasimu bila wanachama wao kujua lakini wakija in public wanavaa usamaria wa kisiasa.

Otherwise thanks,
 
Muda mfupi uliopita kamati ya Nidhamu ya chama cha ANC imemfungia Julius Malema kwa mika mitano na kumvua madaraka ya Urais wa Vijana pamoja na Msemaji wa ANCYL Floyd Shivambu. Malema ameonekana kwamba amechochea mgawanyiko ndani ya chama na serikali

Kilichomponza Julius Malema ni msimamo wake wa kupigania maslahi ya vijana na class ya chini ambayo haioni fursa ya kusonga mbele kwa matumaini huku uchumi wa nchi ukiendelea kuwa mikononi mwa Makaburu. Bado vijana wa Afrika kusini kama walivyo vijana wa Tanzania wanaishi kwa matumaini na hofu juu ya kesho yao. Hoja alizokuwa akipigania Malema za kufanya reforms katika sekta ya madini na Ardhi kwa maslahi ya maskini walio wengi iliungwa mkono kwa nguvu

Hoja nyingine ya kuangusha serikali vibaraka kama Botswana na kumuunga mkono Robert Mugabe imetumika kama chambo tu ili kughilibu matakwa na maslahi ya vijana na maskini wa Afrika kusini ili kukwepa kuwajibika kufanya reforms.Madai ya Julius Malema ni ya Msingi sana kama kweli Afrika kusini inataka Taifa lisonge mbele na kuepuka mapambano ya kitabaka yaani class struggle ambazo zitachochea ubaguzi zaidi.

Kitendo cha kumfukuza Julius Malema ni mwendelezo wa viongozi dhaifu na usaliti kwa umma huku wakijitahidi kukimbia matatizo yanayohitaji suluhisho. Mwenyekiti wa chama Jacob Zuma atawaambia nini au atawapa majibu gani vijana wa Afrika Kusini walioandamana juzi tu tarehe 28-29 mwezi uliopita wakiongozwa na Julius malema katika ku-address matatizo yao? Je kumfukuza Malema na viongozi waandamizi wa ANCYL ni suluhisho au jibu la msingi kwa yale waliyokuwa wanayasimamia?

Inaeleweka wazi sasa viongozi wa Afrika wanapokuwa madarakani hugeuka kuwa masultani na miungu mtu huku wakijitungia kanuni zilizoandikwa au ambazo hazijaandikwa kunyamazisha,kutisha na kuminya demokrasia pale maslahi yao ya kisiasa na kijamii yanapoguswa. Jacob Zuma na viongozi wenzake wanadhihirisha kwamba kuna mstari mwembamba kati ya hulka zao na zile za makaburu na pia mtazamo wao juu ya wananchi wa Afrika kusini na Hatima yao. Jacob Zuma anaonekana kuweka mkakati wa wazi wazi kwa kuhofia uwepo wa Malema ndani ya chama hicho ungemfanya awe one term president kwa sababu Malema alishatangaza kutomuunga mkono Mwenyekiti wake Uchaguzi ujao ndani ya Chama. Zuma anahofia kilichomkuta Thabo mbeki yeye akiwa Kapteni iliyomghilibu Mbeki pamoja na Malema aliyefanya kazi kubwa kwa imani kwamba Zuma angesimamia maslahi ya vijana na wananchi maskini.

Vijana wa Tanzania hatuna tofauti na vijana maskini wa Afrika kusini na pia viongozi wetu ingea si wote katika vyama vyetu vya siasa hawana tofauti na Jacob zuma wa Afrika Kusini. Wote wanataka kuwatumia vijana kwa ajili ya maslahi yao au kama Daraja. Tusikubaliane na hilo ni lazima tuingie mezani tuangalie ni kitu gani ambacho kila mmoja analeta. Najua kwa tabia za kuiga hata mambo yasiyo na faida hata viongozi wetu kwenye vyama vya siasa watakurupuka kuiga na kuifanya ANC kuwa Role model wao katika kunyamzisha sauti zinazohoji au zisizotaka kuburuzwa bila kujua ANC ya sasa ni ya makaburu weusi si ile ya akina Mandela tena.Sasa succeccion battle imekuwa too bitter, ANC itakuwa even more divided. Ni jukumu la Julius Malema na vijana kusimama kidete sasa hadi msaliti wa vijana na maskini wa Afrika Kusini Jacob Zuma aondoke!

Vyama vya siasa vishughulikie matatizo ya msingi na visikilize sauti za vijana. Makosa yarekebishwe, vijana wanastahili kusikilizwa na kusaidiwa na sio kutishwa. ANC itachochea mgawanyiko zaidi na kama vyama vya siasa Tanzania tunataka kutatua migogoro kwa njia hii basi igeni muone


ANC=CCM..ufisadi uliokithiri/utendaji mbovu wa serikali, serikali ya marafiki na washikaji, zuma hana support ya chama chote kama JK, Zuma ni dhaifu kwenye maamuzi kama JK, mgawanyiko wa wazi wazi kwa wale wanaotaka reforms na wale wanaotaka satatus quo iendelee, Duduzane Zuma na kujitajirisha haraka haraka akitumia migongo ya wawekezaji kama Riz1 hapa Tz kinachowasitiri ni kutokua na upinzani wenye umoja na uliokomaa, support ya rural masses ambao bado wana fikra za ANC na CCM kuwa vyama vya vikongwe vyenye uwezo wa kutuliza amani, na mvuto mdogo wa makomredi Mandela na Nyerere katika vyama hivi kwa wapiga kura
 
Back
Top Bottom