Duuh! Hii ya Mil 1.5 imenishtua mkuuKwa lile tamko la ndulu la kufilisi bank tano na wenye hela zao kulipwa mil 1.5 hata kama mtu ana mil 10 inamaanisha watu wengi zaidi wanaenda kukosa imani na bank zetu. Na tutarajie wengi kuficha hela majumbani na kwa wale wahindi wajanja ndiyo wataweka hela zao nje ya nchi au kuzihifadhi katika USD majunbani mwao
Benki gani leo hii itakuwa na uhakika kuwa mikopo ya malori na hata mabasi itaweza kulipika vizuri wakati treni ya kisasa itayofika mpaka bandarini na mikoani inabisha hodi?
Nini kinafanyika kuhakikisha sekta ya usafirishaji kwa maana ya mabasi na malori haitathiriwa na ujio wa treni za kisasa na kutishia utoaji wa mikopo kwa sekta hii ya usafirishaji?
Tatizo ni kuingilia fani za watu wakati huzijui matokeo yake ni kuvurga uchumi na kuharibu maisha ya watu.Wa kulaumiwa ni mkurupukaji na sera zake za kukurupuka. Alikurupuka na kuondoa 1trillion shillings kwenye mzunguko wa pesa nchini mwanzoni mwa 2016 na matokeo yake ndiyo haya. Biashara nyingi nchini zimekufa na juhudi za Serikali kutaka wafanyabiashara wakope kwenye mabenki hivyo kupunguza riba mara mbili toka 16% to 12% kisha to 9% juhudi hizo zimegonga ukuta kutokana na Wafanyabiashara wengi kutokuwa na imani na Serikali. Matokeo yake na mabenki yanaanguka sasa. Tulisema humu jamaa ni janga kubwa la Taifa sasa ushahidi unazidi kuongezeka. Niacheni niinyooshe nchi!!! Kweli nchi INANYOOKA.
Wewe unaongea kama mtoto kuna benki ya wakulima kagera, mtu ana lazimishwa kuweka humo harafu inafiriskaNi ujuha kuweka pesa zako au kuweka amana yako kwenye vibenki vya uchochoroni,binafsi sioni kama ni kuteteleka kwa uchumi labda hizo benki walishindwa kwenye soko na sababu za kufilisika zipo nyingi
Ila yote kwa yote kweli uache NBC ,NMB japo siwakubali ,crdb na diamond ,kcb nk uende vibenki vya uchochoroni,?
Haki yao
kwani ni yericko aliepanga hyo rate ya malipo au BOT yenu!!Yericko mpotoshaji mkuu, sio kweli kwamba wenye peza zaidi ya 1.5M hawatalipwa bali utaratibu wao wa malipo ni tofauti na wale wenye akiba 1.5M au chininya hapo.
ilikuwa je sasa mkasajili benki za uchochoroni nyie maccm?Ni ujuha kuweka pesa zako au kuweka amana yako kwenye vibenki vya uchochoroni,binafsi sioni kama ni kuteteleka kwa uchumi labda hizo benki walishindwa kwenye soko na sababu za kufilisika zipo nyingi
Ila yote kwa yote kweli uache NBC ,NMB japo siwakubali ,crdb na diamond ,kcb nk uende vibenki vya uchochoroni,?
Haki yao
Mkuu kimtazamo km tumefanana, binafsi nafikiria ivyo ivyo kipindi cha utoaji wa leseni vigezo uavikuzingatiwa hasa mitaji na market coverage...ni bora labda vingeanza km saccos wajiimarishe kimtaji nakufikia watu wengi then baadaye wajibadilishe kwenda BankMimi siamini kuwa benki hizi zimekufa kwa sababu ya mdororo wa uchumi; nachoamini huenda Benki kuu walitoa leseni bila ya hizo benki kufikia vigezo vya kimtaji