Kufilisika kwa mabenki Tanzania: Ni kukua au kuanguka kwa uchumi?

Kwa lile tamko la ndulu la kufilisi bank tano na wenye hela zao kulipwa mil 1.5 hata kama mtu ana mil 10 inamaanisha watu wengi zaidi wanaenda kukosa imani na bank zetu. Na tutarajie wengi kuficha hela majumbani na kwa wale wahindi wajanja ndiyo wataweka hela zao nje ya nchi au kuzihifadhi katika USD majunbani mwao
 
Kwa lile tamko la ndulu la kufilisi bank tano na wenye hela zao kulipwa mil 1.5 hata kama mtu ana mil 10 inamaanisha watu wengi zaidi wanaenda kukosa imani na bank zetu. Na tutarajie wengi kuficha hela majumbani na kwa wale wahindi wajanja ndiyo wataweka hela zao nje ya nchi au kuzihifadhi katika USD majunbani mwao
Duuh! Hii ya Mil 1.5 imenishtua mkuu
 
Ni wazi kua maamuzi ya kuzifutia leseni benki hizo hayakua kwa utashi wa BOT bali walifanya kwa influence ya magufuri. Alikomalia sana kua mabenki hayo yafutiwe leseni, BOT inapaswa kusaidia ukuaji wa mabenki na sio kuyaua kwa amri za wanasiasa
 
hili la bank kufilisika sio jambo dogo ni kubwa sana. serikali imetangaza tangazo baya sana kwa mabank mengine!! tusitegemee wananchi kuweka pesa zao kwenye mabank yasio na majina na wengine hawataweka kabisa. yaan niweke 100 million nije kulipwa 2.5 million si kuuana huku?? asant JPM tunyooshe baba. baadaye tutaelewana kwamba uchumi umekua ikulu ila huku uraian ni 0
 
Yericko mpotoshaji mkuu, sio kweli kwamba wenye peza zaidi ya 1.5M hawatalipwa bali utaratibu wao wa malipo ni tofauti na wale wenye akiba 1.5M au chininya hapo.
 
Benki gani leo hii itakuwa na uhakika kuwa mikopo ya malori na hata mabasi itaweza kulipika vizuri wakati treni ya kisasa itayofika mpaka bandarini na mikoani inabisha hodi?

Nini kinafanyika kuhakikisha sekta ya usafirishaji kwa maana ya mabasi na malori haitathiriwa na ujio wa treni za kisasa na kutishia utoaji wa mikopo kwa sekta hii ya usafirishaji?

Mkuu haya maswali yako si sawa , Ulaya usafiri wa Reli ni wa uhakika lakini kuna malori na mabasi nayo yafanya biashara.
Na wamiliki hukopa mitaji na fedha za uendeshaji toka Bank.
Mtwara, Lindi,Masasi , Liwale, Turiani, Mpanda, Malinyi ,Kyela kuna Reli?
 
Wa kulaumiwa ni mkurupukaji na sera zake za kukurupuka. Alikurupuka na kuondoa 1trillion shillings kwenye mzunguko wa pesa nchini mwanzoni mwa 2016 na matokeo yake ndiyo haya. Biashara nyingi nchini zimekufa na juhudi za Serikali kutaka wafanyabiashara wakope kwenye mabenki hivyo kupunguza riba mara mbili toka 16% to 12% kisha to 9% juhudi hizo zimegonga ukuta kutokana na Wafanyabiashara wengi kutokuwa na imani na Serikali. Matokeo yake na mabenki yanaanguka sasa. Tulisema humu jamaa ni janga kubwa la Taifa sasa ushahidi unazidi kuongezeka. Niacheni niinyooshe nchi!!! Kweli nchi INANYOOKA.
Tatizo ni kuingilia fani za watu wakati huzijui matokeo yake ni kuvurga uchumi na kuharibu maisha ya watu.

Tuna hasara kubwa sana safari hii.
 
Ni ujuha kuweka pesa zako au kuweka amana yako kwenye vibenki vya uchochoroni,binafsi sioni kama ni kuteteleka kwa uchumi labda hizo benki walishindwa kwenye soko na sababu za kufilisika zipo nyingi

Ila yote kwa yote kweli uache NBC ,NMB japo siwakubali ,crdb na diamond ,kcb nk uende vibenki vya uchochoroni,?

Haki yao
Wewe unaongea kama mtoto kuna benki ya wakulima kagera, mtu ana lazimishwa kuweka humo harafu inafiriska
 
Yericko mpotoshaji mkuu, sio kweli kwamba wenye peza zaidi ya 1.5M hawatalipwa bali utaratibu wao wa malipo ni tofauti na wale wenye akiba 1.5M au chininya hapo.
kwani ni yericko aliepanga hyo rate ya malipo au BOT yenu!!
vyombo vyote vya habari vimemnukuu jamaa yenu kwamba hawatalipa more than 1.5M kwa kiwango chochote unachodai. stupid.
 
Uchumi utadumaa zaidi mimi ninavyoona, hii miundo mbinu iliyokuwa imefanyika ktk awamu ya nne ilikuwa inatosha kuweza kusukuma uchumi wa mkulima kwanza.
Serikali inatakiwa ijikite kumsaidia mkulima kufikia maendeleo ya kuweza kuzalisha kwa mashine na kuacha kutegemea mvua angalau kwa asilimia 20.
Ijikite kukuza soko la mazao kwa kujenga viwanda vya kuongezea mazao thamani ili kumsaidia mkulima na kukuza pato la taifa.
Kuongezea mtaji mabenki madogo yaweze kukopesha wakulima, kwa liba ndogo. Siku serikali ya namna hii itakapotokea TZ ndiyo uchumi wa kati tutakapoanza kuuongelea lkn kwa sasa wizi mtupu unaendelea.

Bunge liwe la watu wanaojitambua, kujaza wasichana wanaoingia humo kwa njia za ajabu ajabu, ni hasara kubwa. Serikali iwasikilize wachumi wa ukweli na siyo waalimu wa mashuleni. Wapo wenye mafanikio ktk shughuli zao na wafanya biashara wakubwa. Na mwisho Ujenzi wa vitu vya gharama kubwa kwa mikopo ni mfrisi wa jamii yetu ya kesho na ufukara mkubwa ujao kwa jamii yetu.
 
Tanzania imegundua mbinu mpya za kukuza uchumi ambazo haziwahi kutokea dunia kote pale, kwa sasa uchumi unakua kwa kasi kubwa na reserve ya fedha za kigeni pale BOT ipo ya kutosha na pia serikali ina hela nyingi tu... HEKO WASOMI WETU KWA KUWA NA AKILI NYINGI KULIKO WASOMI WOOTE DUNIANI..

TANZANIA CHINI YA CCM NDIO NCHI PEKEE DUNIANI YENYE UCHUMI MKUBWA NA KUWA NA WASOMI WALIOBOBEA KIASI CHA MATAIFA MENGINE KUJA KUOMBA MSAADA HAPA, HEKO VIONGOZI WETU NA CHAMA CHETU CCM.. HEKO VIONGOZI WETU KWANI TANZANIA NDIO NCHI YA KWANZA KUMILIKIKI BARABARA ZA JUU NA TRAIN IENDAYO KASI DUNIANI,,, HEKO CCM NA AWAMU YA TANO...
 
Ni ujuha kuweka pesa zako au kuweka amana yako kwenye vibenki vya uchochoroni,binafsi sioni kama ni kuteteleka kwa uchumi labda hizo benki walishindwa kwenye soko na sababu za kufilisika zipo nyingi

Ila yote kwa yote kweli uache NBC ,NMB japo siwakubali ,crdb na diamond ,kcb nk uende vibenki vya uchochoroni,?

Haki yao
ilikuwa je sasa mkasajili benki za uchochoroni nyie maccm?
 
Mimi siamini kuwa benki hizi zimekufa kwa sababu ya mdororo wa uchumi; nachoamini huenda Benki kuu walitoa leseni bila ya hizo benki kufikia vigezo vya kimtaji
Mkuu kimtazamo km tumefanana, binafsi nafikiria ivyo ivyo kipindi cha utoaji wa leseni vigezo uavikuzingatiwa hasa mitaji na market coverage...ni bora labda vingeanza km saccos wajiimarishe kimtaji nakufikia watu wengi then baadaye wajibadilishe kwenda Bank
 
Back
Top Bottom