Kuelekea maadhimisho ya wiki ya Elimu ya Sheria nchini 2022, bado kuna kigugumizi kwenye matumizi ya lugha ya Kiswahili

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,177
7,749
Wakati Mahakama Nchini ikielekea katika uzinduzi wa Waki ya elimu ya sheria Nchini kwa mwaka huu 2022.

Wananchi wengi wanashngazwa kwa nini Mahakama zetu bado zina kigugumizi/uzito wa matumizi ya Lugha yetu ya Kiswahili katika kutoa Haki za Wananchi?

Pamoja na Bunge kufanya marekebisho ya Sheria ambayo kimsingi ndiyo ilikuwa kizuizi cha matumizi ya Kiswahili ktk kuandika hukumu na mwenendo wa ushahidi lkn hadi leo hii mwenendo wa kesi pamoja na Hukumu zinaandikwa kwa lugha ya Kiingeraza!

Kinacho fanyika kwa sasa ni kutafasiri kwa kifupi sana Hukumu iliyo andikwa kwa lugha ya kizungu. Jambo hili linafanya wanachi waione Mahakama kama vile haziko tayarai kutumia lugha ya Kiswahili.

Hadi leo bado Mahakimu na Majaji wamekumbatia matumizi ya Lugha ya kizungu katika kutoa Haki za watanzania ambao kila kukicha wapo mahakamani kutafuta haki zao.

Tunaziomba Mahakama zetu zote kuanzia mahakama ya Wilaya hadi Rufaa zitumie Lugha ya Kiswahili kama wanavyo tumia mahakama za Mwanzo.

Mahakama za Mwanzo zote zinatumia kiswahili, ukikata rufaa wilayani unaandikiwa kizungu halafu unatafasiriwa kwa kifupi vivyo hivyo mahakama kuu....n.k, jambo hili sisi wananchi linatuchanganya na kutushangaza sana!!

iweje matumizi ya kiswahili yawe nusunusu wakati sheria imepitishwa na Bunge?!

Kwani Lugha ya kiswahili ni tunu ya Taifa au sio tunu ya Taifa?
kama ni tunu ya Taifa letu kwa nini isitumike kwa ukamilifu wake ktk kutoa Haki kwa wananchi wake?!

Kitu gani haswa kinawapa uzito Mahakimu wetu na Majaji wetu kutumia Lugha yetu ya Kiswahili mwanzo mwisho?!

Kwa nini wanatafasiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili?!
Je? hawaoni huo ni upotezaji wa muda na pia ni usumbufu usio na sababu? si bora waandike tu kwa kiswahili kuliko kufanya kazi mara mbili ya kuandika kizungu kisha badae kutafasiri kwa kiswahili!!! Shida yote ya nini hiyo?!!

Tunamuomba Mhe. Jaji Mkuu pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria na wadau wote wa Haki wahakikishe Jambo hili la matumizi ya lugha ya kiswahili kikamilifu kwa masilahi ya wananchi.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Mahakama.
 
Lengo la kubadili sheria ila kuruhusu matumizi ya Lugha ya Kiswahili ktk mahakama zote lilikuwa ni;

1. Kurahisisha upatikanaji wa Haki za wananchi, kwa matumizi ya lugha mama ni rahi ktk matumizi na hata kueleweka.

Kama tatizo ni misamiati ya kizungu kutafasiri kwenda kwenye kiswahili hilo sio tatizo kwani tunao wataalamu wa kiswahili kama BAKITA, TUKI n.k, lkn pia tunazo kamusi za kisheria ambazo zina weza kutumika.

Tuwe na utashi ktk kutumia lugha yetu ya kiswahili

Tuwahudumia watanzania wenzetu kwa lugha ambayo sisi sote tunaizunhumza na kuielewa kiurahisi.

Matumizi ya Lugha ya Kiswahili yakienda sambamba na matumizi ya teknolojia wananchi watafurahia huduma bora zaidi.
 
Tuliambiwa kwenye historia kuwa kizungu kilikuwa kinatumika ktk kutoa haki za wananchi kuanzia kipindi cha Ukoloni kwa sababu kulikuwa hakuna Majaji wala Mahakimu wa Kitanzania, lakini leo hii Majaji na Mahakimu wote ni watanzania tena wazawa lkn bado kizungu kimewakolea!!
Hapana nadhani sasa ni muda muafaka tubadilike maana wanao tafuta haki mahakamani ni Wananchi wa kitanzania.
 
Elimu ya Sheria inahitajika zaidi vijijini ambapo wananchi wengi wanapoteza Haki zao kwa kutofahamu taratibu za kisheria.
 
Ahsante Mhe. WAZIRI Mkuu Kwa kuhimiza matumizi ya Lugha yetu ya Kiswahili kwenye HUDUMA ZA kijamii haswa ZA utoaji Haki kama vile mahakamani Polisi n.k, hayo ni maeneo muhimu sana.
Watanzania wanatafuta haki zao kila kukicha wapo mahakamani hivyo ni Muhimu sana Mahakama zetu kuanzia wilayani hadi mahakama kuu ziandike hukumu zao pamoja Na mwenendo wa kesi Kwa lugha ya kiswahili.
Kwa kufanya hivyo itakuwa imepunguza ucheleweshwaji wa haki lkn pia uelewa Kwa wananchi utaongezeka.
 
Back
Top Bottom