Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Suala la NIDA. inawezekanaje mtu analala akiwa hajui hatma ya mawasiliano yake? Yaani watu wanakesha kama wanasubiri mwaka mpya. Hawajui kama watafungiwa au la!!

Hii inatisha sana kwa mustakabali wa taifa. Wakati wa kuandikisha wapiga kura na kutoa vitambulisho vya kupigia kura mnafika hadi kwenye kata. iweje hivi vya NIDA serikali ishindwe?

Kuna ulazima gani wa kufanya sasa kwamba lazima kila mtu ajisajili kwa kitambulisho cha NIDA ili hali mkijua hali halisi ilivyo!! Na sheria kandamizi eti ukimsajilia mtu naenda jela?

Ndugu zetu, wazazi wetu huko vijijini tutawasiliana nao vipi na tukiwasajilia huku mnatufunga?

IFIKIE HATUA WATANZANIA TUWE NA HATMA YA MAISHA YETU MIKONONI MWETU. HIKI KIKUNDI CHA WALIOSHIBA MADARAKA KITALIANGAMIZA TAIFA

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
.
tapatalk_1579554207357.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom