Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

.
tapatalk_1579554207357.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imebakia robo saa kutimia saa sita kamili ya tarehe 20. January. 2020.. Muda ambao ni kikomo cha mwisho kwa wasiosajiliwa kwa alama za vidole wafanye hivyo la sivyo kuanzia saa sita na dakika moja laini zote ambazo hazijafanya USAJILI WA vidole zitazimwa... Ina maana baada ya hapo laini kwenye simu husika haitafanya kazi tena...

Huu ni mtego wa hatari mno kwa serikali kama haijajipanga vema na tayari kuna baadhi ya wananchi wameshaanza kubeza hiyo hatua kama hili zoezi la kuzima lisipofanyika ama lisipofanikiwa

Kuna machache kwenye mengi ya kujadili hapa...
1. Je serikali imeshafanya upembuzi yakinifu kwenye hili, hasara na faida zake? Je hasara ni zipi na faida ni zipi?

2. Je muda huu mamlaka ya mawasiliano wako kazini wakisubiri dakika zilizobakia waminye kitufe cha kuzima laini? Je mamlaka ina uwezo na zana zenye nguvu za kuweza kuzima laini zaidi ya milioni 20 ambazo bado hazijapata usajili?

3. Je hili haliwezi kuchukuliwa kama uhujumu uchumi kutokana na serikali kukosa mapato makubwa ndani ya saa 24 zijazo? Kuanzia miamala ya pesa, manunuzi ya muda wa maongezi, vifurushi vya data nknk?

4. Je serikali haiwezi kushitakiwa kwa uzembe na usumbufu? kwakuwa kama wangetuma watu wao kwenye vituo vya usajili wangeona wananchi wanavyopatishwa tabu kwenye kupata vitambulisho vya taifa kwa ajili ya kupata usajili wa simcard?

5. Dhihaka ni jambo baya sana kwenye mambo muhimu ya KITAIFA.. Lakini mkuu wa mkoa wa DSM katoa dhihaka kwa wale watakaozimiwa simu zao usiku huu kama ni watu waliokuwa na michepuko... Je ana ushahidi na ithibati kwenye hili? Nini maana ya kuwa kiongozi?

Tayari ni saa sita na dakika tatu siku ya tar 21 January 2020... Nadhani muda huu tayari zoezi la kuzima limeshaanza... Likifanikiwa hili kuna madhara mengi yatatokea usiku huu.. Kuna dharura hazitafanyiwa kazi.. Kuna vifo vitatokea kwa kukosa mawasiliano... Kuna watu watakwama kusafiri, kutuma pesa ya dawa, chakula nk kwa kukosa kufanya miamala nknk...

Kuna nafasi bado ya kutafakari kwenye hili... Lakini je serikali iko tayari kujishusha na kukiri wazi kuwa haikutafari vema kwenye hili? Muda utasema kukipambazuka.. Lakini tayari kejeli zimeshaanza
View attachment 1329002

Jr
Ni saa sita ya tar 21 mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom