Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Kwenye CCM nampigania EL kwa nguvu zangu zote kwa sababu naamini ni kwa kupitia yeye, Tanzania itapata ule ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania na pia ili litimie lile neno kuwa "rais wa 2015" lazima atatoke Kaskazini.

Pasco.

Pasco tujipe muda wa kufikiri kidogo, hivi katika miaka yote ambayo Lowassa amekuwepo alisuburi nini kuleta huo ukombozi wa pili? sangarara kauliza kama akifa je, nadhani wale wote waliokwisha kujaribu na kushindwa hawapaswi kupewa nafasi tena, Tanzania ina watu wengi tu wenye uwezo nina amini, kwa hiyo tupumzisheni na huyo Lowassa jamani, kwanza nasikia alitakiwa na ccm aondoke kwa maana kwamba yeye ndo anachafua chama chao na bado hajafanya hivyo, na ccm imeshindwa kumfanya lolote hatutaki kuongozwa na watu wanaolindana, unataka El awe rais ili aje amlinde jk kwa kumlipa fadhila za yeye kutokufikishwa mbele ya sheria kwa ufisadi, Tanzania haitaendelea kwa mtindo huu. na pili nadhani ccm wakubali tu kupumzika wajipange upya badala ya ku force kung'ang'ania madaraka mpaka kufikia kuiweka nchi yetu hapa ilipo sasa including hali ya amani.
 
Mkuu Pasco nakuunga mkono.Ni lazima wabadilike M4C pekee haitoshi.Kuna mikoa mingine hata ofisi hamna unategemea nn.Watu wa makao makuu hawafanyi kaz yao vizur hamna mawasiliano na viongoz wa mikoani.SHITAMBALA wakati anajiunga CCM alitamka kuhusiana na makao makuu kutofanya kaz na viongoz.
Mkuu Magesi, mimi nimeshatimiza wajibu wangu, nimepaza sauti yangu wasikie, baada ya hapo hayo mengine ni mambo ya ndani zaidi.
 
Ombi: Natoa ANGALIZO KWA KIKOSI KINACHOONGOZWA NA NICHOLAS....musijaribu wala kuthubutu ku-quote coment za watu kama Zomba,Ritz,Rejeo na company yao yote. Nakuhakikishieni hao watu ni hatari sana watawatoeni kwenye hoja
zenu mzuri na watawapelekeni kwenye viroja mfu na mkija kushituka mtakuwa off point...unless waje na hoja mzuri ndipo
muwajibu. Ni ushauri tu
 
Pasco tujipe muda wa kufikiri kidogo, hivi katika miaka yote ambayo Lowassa amekuwepo alisuburi nini kuleta huo ukombozi wa pili? sangarara kauliza kama akifa je, nadhani wale wote waliokwisha kujaribu na kushindwa hawapaswi kupewa nafasi tena, Tanzania ina watu wengi tu wenye uwezo nina amini, kwa hiyo tupumzisheni na huyo Lowassa jamani, kwanza nasikia alitakiwa na ccm aondoke kwa maana kwamba yeye ndo anachafua chama chao na bado hajafanya hivyo, na ccm imeshindwa kumfanya lolote hatutaki kuongozwa na watu wanaolindana, unataka El awe rais ili aje amlinde jk kwa kumlipa fadhila za yeye kutokufikishwa mbele ya sheria kwa ufisadi, Tanzania haitaendelea kwa mtindo huu. na pili nadhani ccm wakubali tu kupumzika wajipange upya badala ya ku force kung'ang'ania madaraka mpaka kufikia kuiweka nchi yetu hapa ilipo sasa including hali ya amani.
Mkuu Lukansola, kwanza nimeipenda objectivity yako kumhusu EL!. Kiukweli kabisa, wapenda mabadiliko wote wa dhati, at heart, ambao wameweka mbele maslahi ya taifa, wakiwemo walioko CCM kwenyewe, wanakubali kuwa CCM imechoka na inahitaji kupumzishwa, ila kiukweli, Chadema ilivyo as it is, bado haijaonyesha utayari wa kupewa dhamana ya ikulu yetu!. M4C is doing a good job so far, lakini Chadema kama chama, kuna yale "mambo yake yale" itake isitake lazima iyabadilishe!.

Sasa kwa vile CCM imechokwa, imeoza na inanuka rushwa kila mahali, ndani ya CCM hiyo hiyo, kuna watu wenye uwezo kuliko watu wowote Chadema ilio nao, na Chadema ndio hivi ilivyo na "yale mambo yake", mimi nimejipambanua wazi kuwa kama CCM itamsimamisha EL, then 2015 ni CCM tena!. Dhambi pekee ya EL ni utajiri wa kutisha na lile zigo la Richmond, lakini uwezo anao!. JK hana kashfa yoyote ya ufisadi, lakini uwezo wake ndio huu uliotufikisha hapa, EL ni fisadi na mlarushwa mkubwa ila ndie pekee mwenye uwezo wa kutuletea ule ukombozi wa pili wa Mtanzania!. Heri fisadi mlarushwa mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko, kuliko mtu safi dhaifu na asiye na uwezo!.

Uzi huu ni kuwaambia Chadema watueleze watatufanyia nini sio tuu kutueleza kile CCM ilichoshindwa kufanya!. Hii inamaanisha, Chadema wakifanya wanachotakiwa kufanya ipasavyo, then hata huyu mgombea wangu ambaye ndio top of the top wa CCM, akisimamishwa, wanaweza angalau kumtikisa!. Watanzania needs assurance ya maisha bora more tha enything else, they are fed up with promises, now they need someone else they can trust, so far EL is the one and only who can be trusted sasa ni kazi kwa Chadema to bring up hopes ili trust ihamishiwe kwao, 2015 wakabidhiwe nchi!.

Pasco.
 
Ombi: Natoa ANGALIZO KWA KIKOSI KINACHOONGOZWA NA NICHOLAS....musijaribu wala kuthubutu ku-quote coment za watu kama Zomba,Ritz,Rejeo na company yao yote. Nakuhakikishieni hao watu ni hatari sana watawatoeni kwenye hoja
zenu mzuri na watawapelekeni kwenye viroja mfu na mkija kushituka mtakuwa off point...unless waje na hoja mzuri ndipo
muwajibu. Ni ushauri tu
Mkuu Mshikachuma, huu sasa unataka kutuletea ubaguzi!. Hoja ya msingi kususia baadhi ya post ni ile ya Mkuu J. Mushi kuwa kuna members humu wanaleta religious provocation ili kuwa provoke watu wa dini fulani. Huu utaratibu wa kunyoosheana vidole fulani na fulani wasijibiwe sasa ni ubaguzi, unless mnataka kujiaminisha hili jukwaa ni la watu wa chama fulani, ili sisi tusio na vyama tujifungashie virago vyetu na kuwaachia jukwaa lenu muendelee kuimbiana nyimbo za sifa na mapambio?!.
 
Hii Thread ni ya muhimu sana kwa mustakabari wa nchi yetu.

Ninauhakika kuna baadhi ya viongozi wa chama tawala na vyama vya upinzani wanaperuzi thread hii.

Wale wanaopenda propaganda am sure wamekasirika - Na wale wanaopenda mabadiliko ya haki basi wamefurahi.
 
Better not leave any stone unturned!

Ujumbe wangu kwa wapenda mabadiliko,nitaanzisha thread ikihitajika!Lakini musimjibu ndugu zomba kwa namna ambayo itaonekana kana kwamba mnadharau imani za wengine!nakuombeni sana,kuliko kuijibu posti yake,basi muignore!lengo lao yeye na mafisadi wenzake, ni kuhakikisha mnatoa majibu ambayo wataya attribute kuwa ndo maoni ama mwelekeo wa chadema.Tafadhalini sana,igonre zomba whenever you can!Ni ombi!wana wafuasi wengine pia,tafadhali soma btn the lines,na kamwe msitukane ama kudhalilisha imani ya wengine no matter how the provocation is!chadema ni ya watanzania wote!Kama unakubaliana na ujumbe huu,waeleze na wapenda mabadiliko wote!God willing!Inshalah!WE WILL BE VICTORIOUS!

Hayo yanasemwa na Mushi, kuna cha kushangaa hapo?
 
Mkuu Mshikachuma, huu sasa unataka kutuletea ubaguzi!. Hoja ya msingi kususia baadhi ya post ni ile ya Mkuu J. Mushi kuwa kuna members humu wanaleta religious provocation ili kuwa provoke watu wa dini fulani. Huu utaratibu wa kunyoosheana vidole fulani na fulani wasijibiwe sasa ni ubaguzi, unless mnataka kujiaminisha hili jukwaa ni la watu wa chama fulani, ili sisi tusio na vyama tujifungashie virago vyetu na kuwaachia jukwaa lenu muendelee kuimbiana nyimbo za sifa na mapambio?!.
Hapana kaka! nakuhakikishia sina ubaguzi wowote...ila kubali kataa hao watu kazi yao ni kuharibu tu! nyeupe wataita nyekundu na nyekundu wataiita nyeupe. wakiona wamebanwa sana kwa hoja utawasikia Padree Slaa,katoliki,kaskazini mara ooh waislaam....yaani ni full propaganda! ndiyo maana nikatoa ANGALIZO hilo
 
Mkuu Lukansola, kwanza nimeipenda objectivity yako kumhusu EL!. Kiukweli kabisa, wapenda mabadiliko wote wa dhati, at heart, ambao wameweka mbele maslahi ya taifa, wakiwemo walioko CCM kwenyewe, wanakubali kuwa CCM imechoka na inahitaji kupumzishwa, ila kiukweli, Chadema ilivyo as it is, bado haijaonyesha utayari wa kupewa dhamana ya ikulu yetu!. M4C is doing a good job so far, lakini Chadema kama chama, kuna yale "mambo yake yale" itake isitake lazima iyabadilishe!.

Sasa kwa vile CCM imechokwa, imeoza na inanuka rushwa kila mahali, ndani ya CCM hiyo hiyo, kuna watu wenye uwezo kuliko watu wowote Chadema ilio nao, na Chadema ndio hivi ilivyo na "yale mambo yake", mimi nimejipambanua wazi kuwa kama CCM itamsimamisha EL, then 2015 ni CCM tena!. Dhambi pekee ya EL ni utajiri wa kutisha na lile zigo la Richmond, lakini uwezo anao!. JK hana kashfa yoyote ya ufisadi, lakini uwezo wake ndio huu uliotufikisha hapa, EL ni fisadi na mlarushwa mkubwa ila ndie pekee mwenye uwezo wa kutuletea ule ukombozi wa pili wa Mtanzania!. Heri fisadi mlarushwa mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko, kuliko mtu safi dhaifu na asiye na uwezo!.

Uzi huu ni kuwaambia Chadema watueleze watatufanyia nini sio tuu kutueleza kile CCM ilichoshindwa kufanya!. Hii inamaanisha, Chadema wakifanya wanachotakiwa kufanya ipasavyo, then hata huyu mgombea wangu ambaye ndio top of the top wa CCM, akisimamishwa, wanaweza angalau kumtikisa!. Watanzania needs assurance ya maisha bora more tha enything else, they are fed up with promises, now they need someone else they can trust, so far EL is the one and only who can be trusted sasa ni kazi kwa Chadema to bring up hopes ili trust ihamishiwe kwao, 2015 wakabidhiwe nchi!.

Pasco.

Nisaidie Pasco, unaweza kunielezea japo kwa ufupi huo uwezo wa EL ni upi? na kwa nini unasema CDM chadema haijawa tayari kuongoza nchi? just briefly...
 
pasco watu wamechoka na ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM na kuwasababishia umaskini mkubwa na hivyo chama mbadala kinachoibua ufisadi huo na kuukemea kwa nguvu zote ni CDM, sio kweli kwamba watu wamechoka tu CCM bila sababu za msingi, kwanini wasishabikie vyama vingine km CUF. TLP. NCCR na vinginevyo? usipotoshe umma,
Mkuu Zumbe Mkuu, yote usemayo ni kweli, watu wamechoshwa na CCM, miaka 50 ya uhuru, taifa letu limekuwa likikabiliwa na hawa maadui wakuu watatu, Umasikini, Ujinga na Maradhi, na sasa wameongezeka wengine wawili, Rushwa na Ufisadi!. Chadema did the right thing, kuuibua, na kuukemea. Kuibua na kukemea, is not reasons enough ya kuipeleka Chadema ikulu hiyo 2015, Chadema inapaswa itupe sababu, reasons za kui vote in, kama CCM imeshindwa kwnya hayo maeneo matano, tunataka blue print ya Chadema itafanya nini kwenye hayo kinyume na ilichofanya CCM?!.

Hizi "hit singles" za listi ya mafisadi, Epa, Richmond, Rada, Gulf Stream, Rushwa etc, by 2015 zitakuwa zimeshashuka chart, Chadema waje na solid plans kwenye Umasikini, Ujinga na Maradhi, Rushwa na Ufisadi! watafanya nini?!. Nyimbo tumeshazikia sana, sasa tunataka mipango mkakati!.

Pasco.
 
Nisaidie Pasco, unaweza kunielezea japo kwa ufupi huo uwezo wa EL ni upi? na kwa nini unasema CDM chadema haijawa tayari kuongoza nchi? just briefly...
Mkuu Luka, kuhusu uwezo wa EL, ujajulikana wazi, na huma ndani, nimeshapandisha threads zaidi ya kumi kumuelezea EL, hii sio thread ya uwezo wa EL, hii ni thread ya Chadema to do things right, waingie Ikulu 2015!. Kama bado una nia ya kuujua uwezo wa EL na nguvu aliyonayo ndani ya CCM na nje ya CCM, tembelea Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa, Then
Hii pia sio thread ya utayari wa Chedema kuongoza nchi, hii ni thread ya uongozi wa Chadema, "kusikiliza, kutenda na kubadilika" kuhusu "mambo flan" ya ndani, ndipo tuwakabidhi Ikulu, ila pia kama una interest ya kuujua utayari wa Chadema kuongoza nchi, tembelea hapa CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015
Ukitembelea huko, ujibu huko huko, ili ya hapa ndio tuyajibu hapa!.

Pasco.
 
Then, Chadema watakuwa wamekabidhiwa nchi kama Mana!.

You got me wrong, namaanisha kwamba Lowasa akifa nini kitakuwa Tarajio la Faraja yako?? Pasco unajua unachokifanya ni sawa sawa kabisa na kusema

"Lowasa wewe ndio mkombozi wangu, wewe ndio Kimbilio langu wakati wa shida na Tabu, Naomba uniangalie kwa macho yako ya huruma na kuniokoa kutoka kwa watesi wangu, kwa Mkono wako wenye Nguvu unishindie vita yangu, wewe ndio mungu wangu".

Unajua?
 
Mkuu Zumbe Mkuu, yote usemayo ni kweli, watu wamechoshwa na CCM, miaka 50 ya uhuru, taifa letu limekuwa likikabiliwa na hawa maadui wakuu watatu, Umasikini, Ujinga na Maradhi, na sasa wameongezeka wengine wawili, Rushwa na Ufisadi!. Chadema did the right thing, kuuibua, na kuukemea. Kuibua na kukemea, is not reasons enough ya kuipeleka Chadema ikulu hiyo 2015, Chadema inapaswa itupe sababu, reasons za kui vote in, kama CCM imeshindwa kwnya hayo maeneo matano, tunataka blue print ya Chadema itafanya nini kwenye hayo kinyume na ilichofanya CCM?!.

Hizi "hit singles" za listi ya mafisadi, Epa, Richmond, Rada, Gulf Stream, Rushwa etc, by 2015 zitakuwa zimeshashuka chart, Chadema waje na solid plans kwenye Umasikini, Ujinga na Maradhi, Rushwa na Ufisadi! watafanya nini?!. Nyimbo tumeshazikia sana, sasa tunataka mipango mkakati!.

Pasco.

Unatuchanga sasa, unataka sera za CHADEMA au unataka ibadirike?
 
Ofcourse CHADEMA inabadilika,na kubadilika ni gradually.....

Pasco,Well done!
Mkuu Ben Saanane, amini nakuambia, Chadema itanusuriwa na watu kama nyinyi ambao mko tayari kusikiliza, kupima mantiki ya unachoambiwa na kisha kuchukua hatua!, hawa washabiki wenu na wapambe ambao kazi yao ni ku "denial every allegations leveled against Chadema, won't help you"!

Kiukweli, Ben, nimeipenda sana approach yako unavyokata issues humu jukwaani, very ipressive na vijana wa sample yako, mna very bright future kwenye politics is you maitain being "who you are" and and thats really "you"!. Approach ya wengi wa members wenu au washabiki wenu is not "who they are", but "what they are!".

Thanks Ben!.

Pasco.
 
Pasco,
Maoni yako ni yapi kwa mgombea binafsi ktk nafasi za ubunge, udiwani pamoja na urais, kuelekea 2015.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Lukansola, kwanza nimeipenda objectivity yako kumhusu EL!. Kiukweli kabisa, wapenda mabadiliko wote wa dhati, at heart, ambao wameweka mbele maslahi ya taifa, wakiwemo walioko CCM kwenyewe, wanakubali kuwa CCM imechoka na inahitaji kupumzishwa, ila kiukweli, Chadema ilivyo as it is, bado haijaonyesha utayari wa kupewa dhamana ya ikulu yetu!. M4C is doing a good job so far, lakini Chadema kama chama, kuna yale "mambo yake yale" itake isitake lazima iyabadilishe!.

Sasa kwa vile CCM imechokwa, imeoza na inanuka rushwa kila mahali, ndani ya CCM hiyo hiyo, kuna watu wenye uwezo kuliko watu wowote Chadema ilio nao, na Chadema ndio hivi ilivyo na "yale mambo yake", mimi nimejipambanua wazi kuwa kama CCM itamsimamisha EL, then 2015 ni CCM tena!. Dhambi pekee ya EL ni utajiri wa kutisha na lile zigo la Richmond, lakini uwezo anao!. JK hana kashfa yoyote ya ufisadi, lakini uwezo wake ndio huu uliotufikisha hapa, EL ni fisadi na mlarushwa mkubwa ila ndie pekee mwenye uwezo wa kutuletea ule ukombozi wa pili wa Mtanzania!. Heri fisadi mlarushwa mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko, kuliko mtu safi dhaifu na asiye na uwezo!.

Uzi huu ni kuwaambia Chadema watueleze watatufanyia nini sio tuu kutueleza kile CCM ilichoshindwa kufanya!. Hii inamaanisha, Chadema wakifanya wanachotakiwa kufanya ipasavyo, then hata huyu mgombea wangu ambaye ndio top of the top wa CCM, akisimamishwa, wanaweza angalau kumtikisa!. Watanzania needs assurance ya maisha bora more tha enything else, they are fed up with promises, now they need someone else they can trust, so far EL is the one and only who can be trusted sasa ni kazi kwa Chadema to bring up hopes ili trust ihamishiwe kwao, 2015 wakabidhiwe nchi!.

Pasco.

Yaani wewe Pasco unaota, nani wa kumwamini Lowasa? kashapewa wizara kibao kuziongoza kazifikisha wapi? kapewa uwaziri mkuu kalifikisha wapi Taifa leo? Pasco narudia tena hacha kuota ndoto za alinacha, watanzania wa leo sio wa 1995, watanzania wa leo wanaitaji mabadiliko kuliko kipindi chochote kingine ktk nchi hii. Alafu unavyoiongelea chadema utafikiri ishawai kutawala hii nchi ikashindwa ndio wakapewa dhamana ccm? what a shame
Mtazamo wangu juu ya Pasco; Mzee Lowasa na Fred Lowasa washakununua au unajipendekeza ktk familia ya Lowasa kwa njaa zako, kwasababu mtu mwenye fikra huru hawezi thubutu kutamka hayo maneno ktk red hapo juu

Hapo ktk red
Unakiri watanzania wanaitaji maisha bora, sasa nani aliyeshai kuwaidi kuwaletea watanzania maisha bora? ni ccm au chadema?
Jawabu kama ni ccm na wameshindwa kutimiza ahadi ya kuwaletea watanzania maisha bora, unavyoona watanzania wataendelea kuamini ahadi za wagombea wa ccm?
 
Last edited by a moderator:
Unatuchanga sasa, unataka sera za CHADEMA au unataka ibadirike?
Mkuu Sangarara, vitu vinavyotakiwa kubadilika ni "mambo flan" ya ndani, viongozi wenu wamekwisha elezwa, hii ni thread ya msisitizo tuu ili wenye macho waone, na wenye masikio, wasikie.

Ila uki insist kujua ni nini haswa Chadema yapaswa kufanya, tembelea hapa CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015 na ukitembelea huko, ujibu huko huko, ili ya hapa ndio tuyajibu hapa!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom