Kubandua Makaratasi ya chupa ya bia.

..akisha maliza kubandua karatasi, atamimina kinywaji chake kwenye glasi-hapo atajaza mpaka imwagike ndo atashtuka kuwa imejaa!

Akiibeba glasi inamwagikia kwenye nguo halafu anainywa kama chai(phooow). domo limelegea macho yamelegea viungo ovyo na kiingereza kinaanza kuchanganya.
 
Yaani hii mada imenikumbusha mbali sana,kuna siku moja nilikua na Makregan wa Origino Komedi ndo nikawa namshangaa anabandua hayo makaratasi nikamuulizo kwa nini unabandua hayo makaratasi akaniambia ni mazoea tu...yaani ndo kashazoea kubandua,ila chakushangaza zaidi nilikuja nikajikuta hata mimi nabandua bila ya kukusudia.
 
Jamani katika maisha ukiwa unafuatilia vitu vidogo vidogo...unaweza cheka cheka mwenyewe kama chizi.Achiliambali kubandua makaratasi ...kuna mijitu mingine ikiwa ina kojoa ina jamba jamba bila kujali kama chooni kuna watu wengine....taabu kweli kweli.
dah!! Hii kali zaidi..
 
Mi bia ya kwanza uwa sibandui ganda,kwa kuwa nkishafika mango garden,cha kwanza mhudumu anajua kuwa uwa naletewa bia mbili za kwanza nakata kiu kwanza. Alaf inakuja na ile glasi ya bia moja na nusu kwa glas moja,kwa iyo wakati muhudumu anarudisha chupa inabidi aje na nyingne. Ivo ivo nachangia pato la taifa! Dah maji ya ilala!goldem water is nice. Kunywa kiasi usilewe. Kuna watu wanakunywa nusu bia wanalewa,wangne bia5,ila wengne bila bia7 usingizi hauji. Bora kula maji ayo kuliko kuonga!
 
Jamani katika maisha ukiwa unafuatilia vitu vidogo vidogo...unaweza cheka cheka mwenyewe kama chizi.
Achiliambali kubandua makaratasi ...kuna mijitu mingine ikiwa ina kojoa ina jamba jamba bila kujali kama chooni kuna watu wengine....taabu kweli kweli.

Kujamba ni part ya kutoa gesi kwa tumbo..mean ile ni ngano bana haiwezi isha kwa kutoka mkojo tu....lazima na gesi itoke...na ndio raha ya beer..ila sasa inatokana na kunywa beer za uvugu uvugu...na nyama choma kujamba lazima kufatane na wewe.
 
Ukiagiza safari au balimi kubandua ni muhimu. sijaona mula henken akibandua
 
Kuna siku nilimuuliza chali mmoja logic ya kubandua label akanijuza kuwa inamprotect mtu kumpa ofa pasipo kupenda maana baa kuna mchezo mtu anakuona unakunywa bia fulani anamwambia mhudumu peleka pale tusker mbili kisa ameona label. Sasa ukibandua hajui ni kinywaji gani unatumia, sasa sijui kama inaukweli?
Huo ni uongo chupa ukiingalia kama ni mnywaji unaijua tu aina ya bia
 
Mimi nabanduaga tu na nikimaliza kubabandua nachezea kisoda imeshakuwa tabia sababu natumia bia baridi baada ya muda Ile karatasi inakuwa laini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom