Kuanguka kwa CCM ni unabii unaotimia. Unabii wa MM Mwanakijiji

Mbassa

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
278
163
Unabii huu ulitabiriwa Na Mzee mwanakijiji, na sasa ni wazi kabisa unatimia. . Kinachonishangaza Ni kwa nini sasa nabii huyu anaukana Unabii wake mwenyewe? Tena katika wakati ambao Unabii huo unatimia? Ni nini hasa kimempata Nabii huyu? Hebu tujikumbushe jinsi Nabii huyu alivyoona Unabii ukitimia.. hii ilikuwa mwaka 2012

Mzee Mwanakijiji 21:43 9th May 2012
NA sasa imekuwa, kama ilivyopaswa kuwa; ndivyo ilivyotakiwa kuwa na naam, imekuwa kama ilivyotabiriwa. Na sasa itakuwa kwa kadiri ya unabii. Ndugu zangu, tunashuhudia kutimilika kwa taratibu kwa unabii ambao habari zake niliziandika tarehe 20 Januari, 2007 na kama nilivyoonesha wakati ule unabii hauepukiki kutimilika. Tunaposhuhudia mamia ya wanachama wa CCM wanapoanza kukikimbia chama hicho kimsingi tunashuhudia kuharakishwa kwa kutimilika kwa unabii huo. Wanachama hawa wanakubali alichosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa “CCM si mama yangu”.

Kwa muda mrefu wamekuwepo Watanzania wengi ambao wanaamini kabisa CCM kwao ni zaidi ya chama tu cha siasa; kwa hawa CCM ni maisha yao, ni uhai wao, ni hatima yao na kwa wengine mapenzi waliyonayo kwa CCM ni kama ya mtoto kwa mzazi wake. Kweli kabisa wapo wengine ambao hata wakizungumza wanazungumza lugha ya mahusiano ya mzazi na mtoto wanaposema: “CCM ni baba ya upinzani” nchini. Wenye mapenzi ya namna hii kwa kweli hawana lolote baya wanaloweza kuliona chini ya CCM na zuri lolote linaloweza kufanywa na CCM litapigiwa mbiu na kufanyiwa sherehe katika hali ya kukitukuza chama.

Mamia haya ya Watanzania hawa waliopofushwa na mapenzi kwa CCM wanajikuta mara zote wakijjisikia kusisimka hadi akili wanapofikiria CCM. Wengine wakiona rangi ya kijani na njano tu fikra zao zote zinapigwa ganzi na lolote litakalosemwa linasuuza mioyo yao. Nimeshuhudia mara kadhaa wakati viongozi wa CCM wanapozungumza na Wana CCM kunakuwa na hali fulani hivi ya kupigwa bumbuwazi la aina fulani kwa wasikilizaji; utaona wengine wanapiga makofi bila sababu, wengine hucheka cheka kwa furaha na wengine hushangilia hata kama kinachosemwa ni kile kile kilichosemwa miaka ishirini iliyopita!

Fikiria kiongozi wa CCM anasimama: “Kuanzia sasa tunataka uwajibikaji” na watu wanashangilia! Ni kana kwamba wamesahau miaka 30 iliyopita walisema hivyo hivyo, miaka ishirini iliyopita walisema hivyo hivyo na miaka mitano iliyopita walisema hivyo hivyo. Leo hii kiongozi wa CCM anasimama na kusema: “Hatutavumilia tena ufujaji wa mali ya umma” na watu wanapiga makofi na kugongesheana; ni kana kwamba wamesahau miaka mitano iliopita viongozi wale wale walisema haya haya na kushangiliwa vile vile!

Sasa, wananchi hawa wengine wameanza kutambua kuwa huwezi kushangilia picha! Wametambua kuwa maji hayafungwi kombe na ya kuwa debe la mende halitwangwi! Wananchi hawa wengi hasa wa vijijini wamefunguliwa; wametambua matumaini waliyokuwa nayo walipoiona “CCM nambari wani” na kuwa “Nyerere yupo Nyerere yupo” yametoweka na kupotelea mbali kama kinda la tetere aliyepotea kiota.

Wamefunguliwa. Kufunguliwa huku kwa kweli ni mafanikio makubwa zaidi ya harakati za mapambano ya kifikra. Nilipoanza kuandika kwa kina zaidi na kusomwa na maelfu ya watu kila Jumatano nilielezea kuwa mabadiliko ya kifikra ndio msingi wa mabadiliko mengine yoyote yale. Huwezi kuwa na mabadiliko ya kiuchumi, kiuongozi au hata kimfumo kama watu bado wanafikra zile zile. Mtumwa mwenye mawazo ya kitumwa huwezi kumpa shamba alime ukamwambie ni lake.

Mara nyingi mtumwa ambaye bado amefungwa kifikra akipewa shamba lake alime atakesha akimuuliza bosi wake nini cha kufanya. Hatojiamini kuwa ni lake na mara zote atakuwa ana wasiwasi kuwa anaweza kunyang’anywa au ataona kama ni mtego fulani hivi. Ndio maana kufunguliwa kwa wafungwa haikuwa tu sala la kuwafungua minyororo yao; kwani mfungwa si lazima awe na minyororo ili atawalike; anahitaji kutawaliwa kifikra tu. Mtu ambaye amezaliwa mtumwa, na kutumikishwa kama mtumwa hata bila minyororo wala mijeledi atajitambua kuwa yeye ni mtumwa. Huyu hahitaji kuvunjiwa makomeo ya malango yake ili awe huru, anahitaji tu kufunguliwa kifikra kujijua yeye ni nani.

Kwa miaka yote iliyopita tangu nitangaze “Kuanguka kwa CCM unabii utatimia” – miaka mitano iliyopita - tumeshuhudia mamia ya kina dada na kaka zetu wakiwekwa huru kifikra. Wakikombolewa na kukumbushwa kuwa wao ndio wenye nguvu kuliko risasi, ndio wenye nguvu kuliko vimulimuli, ndio wenye nguvu kuliko suti na magari yenye bendera. Ndugu zetu ambao walikuwa na mapenzi ya ajabu kwa chama tawala walianza taratibu kukataa CCM kwenye sanduku la kura baada ya kufanikiwa kuikataa kwanza kifikra! Tunakoenda sasa ni kufunguliwa zaidi kwa mamilioni ya wananchi wetu.

Mojawapo ya athari kubwa za ukoloni (colonial legacy) ni kutawaliwa kifikra. Hili ni kweli pia kwenye mfumo wa ubaguzi wa rangi (apartheid) na vile vile ni kweli kwenye mfumo wa ufisadi (corrupt system). Mifumo yote hii ambayo ni kandamizi (oppressive systems) ina madhara ya kwanza kabisa kwenye akili za wanaokandamizwa. Mifumo hii yote athari yake kubwa ni kuwafanya watu wajione duni mbele ya watawala.

Wapo watu ambao hadi leo wanaamini kabisa kuwa wakoloni walikuwa ni watu wema sana na kwa kweli wenye kutupenda kweli kweli; hawa wakimuona Mzungu leo hii wanajisikia kutekenyeka hadi kwenye chembe za mwisho za ubongo wao. Wenye fikra hizi watakataa kwa hasira pendekezo lile lile likitolewa na Mmatumbi mwenzao lakini likitolewa na John Smith watakuwa wa kwanza kulikumbatia tena huku wakitetemeka sauti zao wanaposema “Thank you sir!”

Kwenye ufisadi ni hivyo hivyo, watu wanafika mahali hawaamini kabisa kuwa kuna jambo lolote linaloweza kufanyika likafanikiwa bila vitendo vya rushwa. Nimewahi kusikia simulizi la mwanaharakati mmoja anayepiga vita rushwa ambaye pamoja na kuwa anapiga vita rushwa ilimbidi atoe rushwa aliposimamishwa na polisi ili kuwahi kikao ambacho alikuwa anaenda kuhutubia ubaya wa rushwa katika taasisi za serikali!

Yeye mwenyewe hakuona tatizo hapo kwani kile alichokitoa aliamini ni ‘rushwa ya usumbufu’ kwamba angeweza kuwakatalia polisi na kwenda hadi kituoni na kuandikisha maelezo na hilo lingemletea usumbufu mkubwa! Ni kutawaliwa kiakili! Leo hii, ufisadi umekuwa ni mfumo wa kiuchumi ambapo hata watu ambao wanasema wanapiga vita ufisadi wao wenyewe wanajikuta kwa namna moja au nyingine wananufaika na ufisadi huo huo! Watu wanapiga vita vitendo vya ufisadi lakini makampuni yao yanapoomba tenda serikalini ndio hao hao wanajaribu kuandikiana mikataba mibovu na risiti za uongo ili waweze kugawanya ‘kidogo’!

Sasa, haya yote yanaleta mzigo wa kiakili kwa wananchi. Uzuri wa watu wa kijijini kinyume na mjini hawategemei sana serikali kwenye mambo yao. Mtu atalima na kuvuna mazao yake, atayaanika na hatimaye kuyaweka kwenye gunia. Ataenda kuuza kwa bei ambayo ataikuta huko na akirudi zake nyumbani hiyo ni hela yake. Lakini inapotokea anadhulumiwa bei au fedha za malipo mtu huyo anakuwa na uchungu zaidi kuliko mtu wa mjini ambaye amezoea kuishi kwa mitkasi. Ndio tuliyoyaona Tandahima hivi karibuni na tutaendelea kuyaona kwenye vijiji vingi ambavyo wananchi wake wamefunguliwa!

Kufunguliwa huku kwa kiakili kunaiweka CCM kwenye nafasi mbaya zaidi kuliko wakati mwingine wowote wa historia yake. Ikumbukwe kuwa kwa miaka karibu thelathini CCM ndicho chama pekee kilichokuwa mawazoni mwa Watanzania. Hukuweza kuzungumzia Tanzania bila kuzungumzia CCM na hukuweza kuzungumzia CCM bila kuzungumzia Tanzania. CCM ilitawala kila nyanja za maisha lakini utawala wake mkubwa zaidi haukuwa kwenye taasisi mbalimbali bali ulikuwa kwenye akili za watu. Ilifika mahali watu waliogopa CCM kama walivyoogopa Usalama wa Taifa kwani vyote viwili vilifanya kazi vile vile. Ukiitibua CCM, CCM ilikuwa haina simile. Hivyo, utawala wa CCM pia ulijaa hofu dhidi yake.

Masalio ya hofu hii yapo hadi leo lakini pia hofu hii imekaa kinamna nyingine tena. Kuna hofu ya kujulikana kuwa mtu haipendi CCM. Hofu hii huambatana na hisia ya hatia (guilty feeling). Nimewahi kusikia mara hii pale mtu anaposema “wewe utaikataa vipi CCM wakati ndio imekusomesha bure?” Wakati mwingine inaulizwa “CCM ni kama mama yako huwezi kumkataa mama yako pamoja na mabaya yake yote”. Na ni kweli kabisa wapo watu ambao wanajisikia vibaya na uchungu wakiona CCM inaasemwa vibaya na wengine wanaweza hata kufanya vitu vibaya kwa wale wanaoisema vibaya CCM! Watu hawa wametawaliwa kifikra per excellence.

Hawa hawawezi kufunguliwa; hawafunguki hata kwa kuombewa au kufukiziwa ubani! Wamekuwa watumwa wa kifikra na minyororo iliyofungwa kwenye fikra zao imejichimba kwenye ngozi za mikono na shingo zao na kuwa sehemu yao. Huwezi kukata minyororo hiyo bila kusababisha kuangamia kwao! Hawa hatuwezi kuwasaidia wafunguke!

Ndiyo maana binafsi siamini kabisa kuwa mabadiliko nchini yataletwa na wasomi hasa wale wenye kufurahia utawala wa CCM! Ni sawasawa na hapa Marekani ambapo historia inatuonesha tofauti ya “watumwa wa nyumbani” na “watumwa wa kondeni”.

Watumwa wa nyumbani walikuwa karibu sana na bosi na walipewa mahali pa kula na kulala na walitendewa vizuri zaidi kuliko watumwa wa kondeni. Matokeo yake ni wale watumwa wa kondeni ndio hatimaye waliweza kuwa chachu ya mabadiliko kuliko watumwa wa nyumbani. Maana hawa wanyumbani kuambiwa kuwa kuna uhuru wanajikuta hawaamini; kwamba watoke katika ‘maisha mazuri’ na kwenda kwenye ‘uhuru’ haiingii akilini. Lakini wengine walipoweza kufunguliwa kiakili waligeuka wapelelezi wazuri sana; lakini wengine walikufa wakiwa wanafurahia kuitwa “mtumwa mzuri kwa bwana wake!”

Ndugu zangu, imekuwa na sasa inatimia; waliokuwa wamefungwa wamevunjwa minyororo yao, na waliokuwa wametawaliwa kiakili wamefunguliwa. Na kama ilivyotarajiwa ni wanakijiji ndio wanaongoza wimbi la mabadiliko. Kuanzia Mbozi hadi Meatu, kuanzia Njombe hadi Geita, kutoka kona za Kigoma hadi kwenye vijiji vya Manyara, maelfu ya wananchi wetu wanazidi kufunguliwa wakitupilia mbali kongwa la utumwa wa kifikra; wamekataa wao na uzao wao kuabudu kwenye altare ya CCM. Wamekataa kuitwa ‘watumwa wa nyumbani’!

Mojawapo ya vitu ambavyo CCM imevifanya na haikujua kuwa imepanda maangamizi yake ni kuanzishwa kwa ‘shule za kata’. Shule hizi zimekuwa ni sehemu ya kupandikiza mbegu ya fikra. Watu ambao hawakupata nafasi ya kusoma sasa wamesoma lakini baada ya kushindwa kuendelea namasomo ya juu vijana wengi waliosoma sekondari wamerundikana vijijini wakiwa na fikra zinazowaka bila kukoma kama taa ya chemli; wanachochewa zaidi na zaidi kwa kusikiliza na kufuatilia mambo kupitia njia mbalimbali.

Ndiyo maana naamini kabisa vita kubwa ambayo inakuja kati yetu na watawala itahusiana na uhuru wa vyombo vya habari na mitandao ya intaneti. Naweza kuona kutoka mbali CCM ikijipanga kuleta sheria au sera ambazo zitajaribu kuzuia vyombo vya habari na hasa mitandao ya kijamii. Siyo mitandao tu bali hata watumiaji wake; sote ambao tumekuwa tunaandika kwa uhuru na kuchochea mabadiliko ya kifikra tutajikuta tunaanza kubanwa kwa ama madai ya ‘usalama wa taifa’ au ‘sheria ya vyombo vya habari’. Naweza kuwahakikishia tu kuwa mapambano sasa yanaenda kwenye ngazi tofauti kabisa sasa kwani CCM haiwezi kamwe kuacha twende kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 katika mazingira yale yale ya 2010; hawawezi na kwa hakika watalazimisha watu kubadilika!
Naomba kutangaza mapema, mara moja na daima; nilishavunja kongwa la utumwa wa fikra za CCM, sitompigia mwanadamu yoyote magoti na sitoi sadaka ya sifa za uongo kwa mtu yeyote.

Kwa vile unabii utatimia ulivyo, nawasihi wale wote waliofunguliwa kuwa tayari kwa lolote kwani vichaa wamepewa sime sokoni! Tutakiona cha moto! Kama walivyowahi kusema wengine – ni bora kufa kwa heshima kuliko kuishi kwa aibu! Tuendelee kuwaamsha watu wengi zaidi ili kuhakikisha kuwa pigo la kwanza takatifu, pigo lisilo na huruma, pigo lisilo na onyo liangukie CCM kwenye chaguzi zote zinazokuja kuanzia sasa.

Si kwa sababu tunawachukia wana CCM; la hasha! Hawa ni ndugu zetu, ni rafiki zetu, na wengine ni jamaa zetu wa karibu. Bali kwa sababu wengine tumetambua na kuthibitisha kuwa CCM na sera zake imeshindwa, hatima yake ni kukataliwa, na adhabu ya wanaojaribu kuijenga upya ni kutiwa pingu. Ni matumaini yangu uongozi ujao hautawapepesea macho watawala hawa walioshindwa bali wakae wakijua uongozi mpya utakapochukua nchi utafumua kila kitu chao na kuhakikisha wale wote waliofilisi taifa letu na kugongelea misumari ya kongwa kwenye shingo za watu wetu wanasimamishwa kizimbani! Kuanzia aliye mkuu wao hadi aliye mdogo wao.

Kwani unabii utatimia; ndivyo ilivyopaswa kuwa, nayo itakuwa kwani hivyo ndivyo ilitakiwa iwe. NA ITAKUWA.


Nitafute Facebook: “Mimi Mwanakijiji
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Kinachonishangaza Ni kwa nini sasa Mzee Mwanakijiji amegeuka na kuukana unabii huu unaotimia waziwazi? Naamini yuko humu hebu atueleze nini kimemsibu Nabii huyu?
Waulize akina Mbowe na Tundu Lisu wametoa wapi madodoki ya kumsafisha fisadi papa namba 11? hapo utakuwa umetenda haki za kiuanaharakati na ukombozi. toa boriti iliyoko jichoni mwako ndipo utoe kibanzi kwenye jicho la jirani yako.
 
Kinachonishangaza Ni kwa nini sasa Mzee Mwanakijiji amegeuka na kuukana unabii huu unaotimia waziwazi? Naamini yuko humu hebu atueleze nini kimemsibu Nabii huyu?

Kwakweli mimi ningemuelewa kama angeshambulia wote wenye tuhuma..I mean Lowasa na Magufuli. Lakini huu mchezo wake ni wa kitoto sana. Anadhoofisha upande mwingine means ana-strengthen upande wa pili. Ni vema a-declare interest kwamba yeye ni pro CCM na Pro Magufuli.
 
Leo Mzee Mwanakijiji anataka CCM iendelee kubaki madarakani hadi Dr.W.Slaa atapogombea tena uraisi,kama yule mnafiki Zitto anayetaka yeye awe Mwenyekiti wa chama na agombee uraisi yeye tu ndio CCM itoke madarakani!!

Kweli waafrika akili zetu hata kwa wasomi na wajuzi ni za hovyo,zimejaa unafiki-wengi wao!!

Miafrika ndivyo tulivyo-@Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Waulize akina Mbowe na Tundu Lisu wametoa wapi madodoki ya kumsafisha fisadi papa namba 11? hapo utakuwa umetenda haki za kiuanaharakati na ukombozi. toa boriti iliyoko jichoni mwako ndipo utoe kibanzi kwenye jicho la jirani yako.

Kama wewe ni mfuatiliaji utagundua kuwa katika ile list of shame haikuwa na Lowasa peke yake.. pamoja na wengine Mkapa alikuwemo, Kikwete pia alikuwemo, licha ya Lowasa mwenyewe kukiri kuwa ile dili ilikuwa na ya Mamlaka ya juu, na juzi Lisu kuthibitisha hadharani kuwa Richmond ni ya Kikwete kwa nini sasa anaandamwa Lowasa peke yake?
Tatizo lilikuwa uwaziri mkuu au Richmond? Kama tatizo lilikuwa Richmond kwa nini kamati ya Mwakyembe haikumhoji? TAFAKARI
 
Leo Mzee Mwanakijiji anataka CCM iendelee kubaki madarakani hadi Dr.W.Slaa atapogombea tena uraisi,kama yule mnafiki Zitto anayetaka yeye awe Mwenyekiti wa chama na agombee uraisi yeye tu ndio CCM itoke madarakani!!

Kweli waafrika akili zetu hata kwa wasomi na wajuzi ni za hovyo,zimejaa unafiki-wengi wao!!

Miafrika ndivyo tulivyo-@Nyani Ngabu

Nadhani MM hapendi wale watakaochukua madaraka na mfumo watakaotumia baada ya kuitoa CCM.
Kama nimemwelewa vizuri anahofu kuwa wanaweza kuwa na madhara kuliko hata CCM na kuharibu dhana nzima ya mabadiliko yaliyokuwa yakitafutwa.
Na madhara yake kisiasa na kidemokrasia yatakuwa makubwa pia.
MM nisahihishe kama nimekuelewa vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani MM hapendi wale watakaochukua madaraka na mfumo watakaotumia baada ya kuitoa CCM.
Kama nimemwelewa vizuri anahofu kuwa wanaweza kuwa na madhara kuliko hata CCM na kuharibu dhana nzima ya mabadiliko yaliyokuwa yakitafutwa.
Na madhara yake kisiasa na kidemokrasia yatakuwa makubwa pia.
MM nisahihishe kama nimekuelewa vibaya.

"Tunaposhuhudia mamia ya wanachama wa CCM wanapoanza kukikimbia chama hicho kimsingi tunashuhudia kuharakishwa kwa kutimilika kwa unabii huo. Wanachama hawa wanakubali alichosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa “CCM si mama yangu”.
By Mzee Mwanakijiji
 
Nadhani MM hapendi wale watakaochukua madaraka na mfumo watakaotumia baada ya kuitoa CCM.
Kama nimemwelewa vizuri anahofu kuwa wanaweza kuwa na madhara kuliko hata CCM na kuharibu dhana nzima ya mabadiliko yaliyokuwa yakitafutwa.
Na madhara yake kisiasa na kidemokrasia yatakuwa makubwa pia.
MM nisahihishe kama nimekuelewa vibaya.
Hana lolote ana hofu kuliko mamilioni ya watanzania walioamua kuchagua mabadiliko? Kama ndivyo basi demokrasia imempitia kando atulie
 
Tuache siasa hebu tuelezeni dodoki la kumsafishia hyu mamvi ni la chuma au zege,hatuwaaamini hata kidogo coz mnaonekana mnataka kutupeleka kusiko,tunajitambua anayetufaaa kwa sasa ni magufuli
 
CCM (idea, deeper kuliko chama) ni lazima ishinde mwaka huu.

Ama kwa mgombea wake Magufuli, ama kwa mgombea wake Lowassa.

Upinzani hauna mgombea.

Kwa hivyo, CCM haiwezi kuanguka mwaka huu.

Huwezi kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia makapi ya CCM ambayo hata hayajapata muda wa kuangaliwa ndani ya upunzani.

CHADEMA hamjajifunza kwa Shibuda tu?

Mimi namuelewa Mwanakijiji.
 
Wote mlimtaja kama fisadi papa leo amekuwa lulu mnaonyesha wazi mmefilisika,hakuna haja ya kupoteza muda kiongozi tunaye ni magufuli tu,hapa kazi tu
 
Waulize akina Mbowe na Tundu Lisu wametoa wapi madodoki ya kumsafisha fisadi papa namba 11? hapo utakuwa umetenda haki za kiuanaharakati na ukombozi. toa boriti iliyoko jichoni mwako ndipo utoe kibanzi kwenye jicho la jirani yako.

Hadi ulipofika nambari 11, je hao wengineo kutokea nambari 1 - 10 mbona unawaficha?

Je wao hao 1 ~ 10 wangali wapo wapi?
 
Kinachonishangaza Ni kwa nini sasa Mzee Mwanakijiji amegeuka na kuukana unabii huu unaotimia waziwazi? Naamini yuko humu hebu atueleze nini kimemsibu Nabii huyu?
Tatizo la huyu Nabii alitegemea mabadiliko yaanzie kwake kinyume chake amepishana nayo.
 
Nadhani MM hapendi wale watakaochukua madaraka na mfumo watakaotumia baada ya kuitoa CCM.
Kama nimemwelewa vizuri anahofu kuwa wanaweza kuwa na madhara kuliko hata CCM na kuharibu dhana nzima ya mabadiliko yaliyokuwa yakitafutwa.
Na madhara yake kisiasa na kidemokrasia yatakuwa makubwa pia.
MM nisahihishe kama nimekuelewa vibaya.

Lowassa akishinda hawi Mwenyekiti wa chama,chama na dola haitokuwa kama CCM,Chama kitaisimamia serikali na kuiwajibisha wakati maCCM serikali inakitia chama mfukoni na hakina sauti wala mlio wa huzuni!!!

Lowassa akishinda,Mawaziri baathi yao ni Mbowe,Mbatia,Tundu Lissu,Mnyika,Halima Mdee,Kafulila,Silinde,Habib Mnyaa,Mbarouk etc

Kwenye orodha tajwa hapo,wabunge gani wa maCCM wanawazidi hao tajwa hapo kwa uchapa kazi na uadilifu??!! Utasema January Makamba,Ridhiwani,Ummy Mwalimu,Angela KairukinChenge na kina Mama Sita?!!

Lowassa atarudisha katiba ya Warioba,Magufuli ataweza?! Lowassa atavunja mkataba wa bandari ya Msoga/Bagamoyo na kupeleka mradi Tanga au Mtwara,Magufuli atathubutu?!

Serikali ya UKAWA itatunga upya sheria ya mafuta na gesi na kufuta ile ya CCM ambayo imepitishwa na wabunge 80 tu wa maCCM kati wabunge 400,Magufuli atathubutu au ataishia kuleta ukasuku tu?!!
 
Tatizo la huyu Nabii alitegemea mabadiliko yaanzie kwake kinyume chake amepishana nayo.

Hamumtendei haki mkisema hivyo.

Ukweli ni kwamba CHADEMA wamemsema sana Lowassa, vibaya. Halafu leo wanataka kumnadi kama mtu anayefaa kuwa rais bila kutupa maelezo ya kueleweka.

Kwa mtu anayejali logical consistency, Mwanakijiji yuko consistent. CHADEMA haiko consistent.
 
Back
Top Bottom