Kozi Chuo cha Mipango na Maendeleo Dodoma zinatambulika kwenye mfumo wa kuomba ajira?

frankaisimbo

Member
Sep 3, 2015
10
1
CHANGAMOTO KWA WAHITIMU

Jina La Chuo:
CHUO CHA MIPANGO DODOMA.
Jina La Kozi:
DEVELOPMENT FINANCE & INVESTMENT PLANNING.

Changamoto

---Chuo hiki ni Chuo Kikongwe sana Tanzania. Lakini Chuo Hiki kina changamoto kubwa sana wa kozi zake katika Mfumo wa uombaji kazi za utumishi wa Umma.

---- Mfano: Kozi iliyohainishwa hapo juu, Asilimia kubwa za modules zilizofundishwa katika kozi hii ni modules za kozi za biashara kama tu kozi nyingine za biashara kutoka katika Vyuo vingine lakini linapokuja swala la uombaji kazi katika mfumo wa sekretariet ya Ajira mfumo huu unakuwa hauitambui kozi hii na kushindwa kufanya maombi na kusema kwamba hauna vigezo vya kuomba kazi hiyo Huku wenzetu wa masomo ya biashara kutoka vyuo vingine mfumo unawatambua na kuwakubalia kufanya maombi ya ajira.
Rejea:-
Mwaka 2020
- Mfumo ulishindwa kututambua kufanya maombi ya ajira za TRA.
Mwaka 2021 - Mfumo ulishindwa kututambua kufanya maombi lakini baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wahitimu wa chuo hiko mfumo ulitukubalia kufanya maombi ila changamoto ilikuja kutokea upande wa utumishi
hawakutoa matokeo ya usaili huo.
Mwaka 2022 - Mfumo ulitukubalia kufanya maombi katika kada ya Tax Management na kutukataa kwenye kada ya Customs Management lakini pia baada ya kufanya maombi majina yaliotoka kwaajiri ya usaili wa kuandika hakuna muhitimu hata mmoja aliyechaguliwa kutoka katika chuo cha Mipango.

Ushauri unaohitaji utekelezwaji.
1. KWA VIJANA

- Kuweni Makini sana muda wa uchaguaji wa vyuo kwani itakufanya utumie rasilimali nyingi ambazo baada ya kuhitimu haina impact yoyote katika maisha yako na kubaki na cheti ndani kama mapambo ya ukutani.
2. UONGOZI WA CHUO CHA MIPANGO
- Uongozi wa chuo cha Mipango je changamoto hii ni ngeni kwenu? Je mnashindwa kuitatua maana asilimia 90 ya wahitimu wa chuo cha mipango wana changamoto kubwa sana katika upande wa ajira ukilinganisha na vyuo vingine.

Hakuna Muhitimu kutoka chuo cha Mipango anaekiongelea Vizuri chuo hiko huko uraiani kwa maana wamejitwika mzigo ambao hawakuutegemea.

CHUKUENI HATUA KAMA UONGOZI WA CHUO KITENDO HIKI KITAPUNGUZA IDADI YA WANAFUNZI WAPYA KILA MWAKA CHUONI KWENU
 
๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„ bora we unakashombo ka fainens


hii kozi ya

rijino planing ushawahi ona mhitimu kapata ajira yake km ilivo? hata kujiajiri hajui ajiajirije ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜ช๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„
 
๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜ Kumbe nilishika nikakimbia lkn nina diploma yao but bachelor niko chuo kingine
 
Back
Top Bottom