Kova chonde chonde

Mkuu rombo

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
1,556
422
wakuu nimefatilia tarifa za habari za stesheni mbalimbali kuna habari moja imeonesha jinsi kamanda kova na jeshi la polisi lilivyo2mia akili za kiitelejensia na kufanikiwa kuwakamata wakenya 3 wakisafirisha pembe za tembo kwenye jeneza lililofunikwa kwa bendera ya taifa kuelekea tarekea,

swali langu lilikuwa ni hivi

kwakuwa dar hakuna tembo izo pembe zimefikaje dar??
Anazungumziaje makontena 2 yalio kamatwa huko india
kama anajukumu la kulinda rahia na mali zake anazungumziaje usafirishaji wa mali ya watanzania wakiwemo twiga?
My fact apigane na walifu papa muda wate kuliko kupoteza muda na visangara wezi wa simu
 
Sijakuelewa? unalalamika au unasifia? jamaa wamekamata jeneza la pembe za tembo halafu bado unawaona wazembe kwa kuwa hawakukamata contena la pembe za tembo? so ulitakaje? au kuna sentensi imefuta kwa ujumbe wako? Mi ningedhani tumpe hongera na tumuumbe kwa wakuu wamungezee nguvu za kukamata makontena so vijeneza peke yake.
 
Kova Handsome Boy wa JESHI LA POLISI naona wkt mwingine anatudanganya,yukowapi MKENYA wa ULIMBOKA. Ni kama ARV FEKI yaani ni UPEPO TU UNAPITA.
 
Wakiishiwa hufanya mambo ya ajabu. Huyo Kova alikuwa wapi wanyama hai waliposafirishwa kwenda Uarabuni? Unafiki mwingine bwana!
 
Majambazi wanaua RPC Mwanza, wanakimbia kuiba Dar !!!! Wanajua kuhoji!
 
MKUU MBONA SIKUELEWI? hiyo dili ilikuwa yako au ya jamaa yako nini, maake ishu sio kumaliza uhalifu, kwa ujumla hakuna nchi iliyofanikiwa kumaliza uhalifu naona umempiga madongo sana jamaa kova. si kaonyesha hata hiko kidogo alichokamata mpe sifa ili akamate nyingine. inabidi nyakati nyingine tutoe sifa ili kuwamotivate jamaa japokuwa kweli mshkaji ni mr misifa!!!! bana mi sidhani kama yupo kiongozi duniani aliyefanya yote sahihi, angalia America, vipi Obama umeona madongo anayopigwa?
 
mkuuu amtafute ulimboka na said kubenea hao ndio watakuwa washaidi namba moja kwenye swala zima la utekaji nyara
 
Sijakuelewa? unalalamika au unasifia? jamaa wamekamata jeneza la pembe za tembo halafu bado unawaona wazembe kwa kuwa hawakukamata contena la pembe za tembo? so ulitakaje? au kuna sentensi imefuta kwa ujumbe wako? Mi ningedhani tumpe hongera na tumuumbe kwa wakuu wamungezee nguvu za kukamata makontena so vijeneza peke yake.

mkuu kova anajukumu la kulinda rahia na mali za zao twiga na pembe za tembo ni mali za watanzania kwa ujumla aingii akilini pembe za tembo na twiga kusafirishwa bila yeye kujua
shwali nii hili mbona madawa ya kulevya huwa yanakamatwa???
 
zinapita nyingi sana pembe kwenda nje ya nchi,hapo ujue walizulumiana tuu wanamtandao ndipo wakachomeana na kukamatwa!zingekamatwa china wangesema zimetoka kenya
 
mkuu bongolala,,,, naunga hoja mkono moja kwa moja hao jamaa kuna fungu hawajampa kamanda ndio maana yamewakuta yalio wakuta...wakati mwingine huwa nafikiria walio muuwa kamanda barow aingii akilini kwa kamanda kova kututangazia wauwaji bila kutuonesha 2wafahamu..anachokifanya ana2onesha bastola short gan na ak 47 2lichokisikia leo ndio kimehishia hapo hapo ha2tasikia wamepandishwa kizimbani
 
Kova Handsome Boy wa JESHI LA POLISI naona wkt mwingine anatudanganya,yukowapi MKENYA wa ULIMBOKA. Ni kama ARV FEKI yaani ni UPEPO TU UNAPITA.
imagejpeg

Du!
Handsome boy wa Polisi!
 
hivi kova anajua kusoma na kuandika? leo amekuja na comedy ingine huyu mshikaji ni zaidi ya mr bean, atuletee video tuone jinsi walivyofanya hiyo mission ya kukamata hao wauaji wa kufikirika, mchizi anachukua bunduki stoo anawaita waandishi wa habari nao wanamsikiliza bila kumhoji sijui walikuwa wa redio uhuru na magazeti ya uhuru na mzalendo.
 
Huyu Kova asiudanganye umma wa watanzania sisi wakazi wa kimara tunajua kila kitu kuhusu hizo pembe za ndovu polisi wake wamevujisha kila kitu toka jana,chanzo za kukamatwa zile pembe ni ile nyumba waliuziwa mali za wizi polisi walivyoenda kutafuta ndo wakakuta hizo pembe na mtuhumiwa alietaja hiyo nyumba anaitwa Sijali anashikiliwa kituo cha polisi mbezi lous
 
Sijakuelewa? unalalamika au unasifia? jamaa wamekamata jeneza la pembe za tembo halafu bado unawaona wazembe kwa kuwa hawakukamata contena la pembe za tembo? so ulitakaje? au kuna sentensi imefuta kwa ujumbe wako? Mi ningedhani tumpe hongera na tumuumbe kwa wakuu wamungezee nguvu za kukamata makontena so vijeneza peke yake.

Kukubali kila kitu eti kwasababu umeelezwa na ZPC nidalili ya kuwa na Mtindio wa Ubongo! Ndani ya jengo hilo tumewahi kuelezwa kuwa vijana wa madini toka Morogoro ni majambazi ikajadhihirika kuwa si kweli,akakamatwa mkenya aliyemteka Dr Ulimboka kesi yake haijulikani mwendelezo wake maana Ulimboka yupo kwanini hatuambiwi akafanye gwaride la utambulisho? Ndani ya jengo hilohilo kuna tuhuma za mke wa bosi wake kutapeli vijana juu ya ajira za USALAMA WA TAIFA mpaka sasa kimya!Kwa hayo machache niliyoyataja angekuwa na nguvu kubwa sana,kama watu wasingekuwa wadadisi.
 
Huyu Kova asiudanganye umma wa watanzania sisi wakazi wa kimara tunajua kila kitu kuhusu hizo pembe za ndovu polisi wake wamevujisha kila kitu toka jana,chanzo za kukamatwa zile pembe ni ile nyumba waliuziwa mali za wizi polisi walivyoenda kutafuta ndo wakakuta hizo pembe na mtuhumiwa alietaja hiyo nyumba anaitwa Sijali anashikiliwa kituo cha polisi mbezi lous

aiseeee unasema kweli mkuu?? Hata mimi nikitaka kwenda kuiba benk kirais lazima nimtarifu kova kuhusu uhalifu huo,,ukiona nimekamatwa ujue nilitaka kumtapeli kovo so analipa kisasi
 
mkuu kova anajukumu la kulinda rahia na mali za zao twiga na pembe za tembo ni mali za watanzania kwa ujumla aingii akilini pembe za tembo na twiga kusafirishwa bila yeye kujua
shwali nii hili mbona madawa ya kulevya huwa yanakamatwa???
Mkuu Rombo nenda kajipange upya. HONGERA Kamanda Kova!
 
Ndugu zangu wana JF kwa nini hatuamwamini m2 hata kama amefanya jambo la kustahili kusifiwa? kwa nini tunaunganisha na mambo ya kifisadi kama wamedhulumiana, hawakumtaarifu n.k; Naungana kabisa na wote waliompongeza kamanda Kova kwa kufanikisha ukamataji huu wa mali ya umma na waliohusika na ujangili huu. Kwamba Dar haina mapori na kwa nini ukamataji ufanyikie Dar hiyo ni siri ya upelelezi. NAKUOMBEA KWA MOLA AKULINDE NA AKUWEZESHE UENDELEE NA MOYO HUU WA KAZI AMINA
 
mkuu usipende kuamini kila kitu unachoambiwa unapaswa kujua,hawa polisi hizi pembe wamezikamata kibahati tu kama si huyu mama kununua vitu vya wizi polisi wasingepata hizo pembe na chanzo cha yote ni godoro,mbona gari la wizi lililokutwa ndani ya hiyo nyumba huyo kova hajalizungumzia?wasitake kutufanya tuamini kila kitwasemacho vingine raia tunajua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom