Kova apata kigugumizi msimamo wa Gwajima

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
kova.jpg

Kamanda wa Polisi wa kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kwamba haliwezi kuendelea kuongelea suala la mtuhumiwa Joshua Mhindi (31) anayetuhumiwa kumteka na kisha kumdhuru kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, kwa kuwa tayari limeshafikishwa mahakamani.

Msimamo huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uhalifu jijini kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi sasa.

Kamanda Kova alisema katiba ya nchi inamzuia mtu yeyote kuongelea suala lililofikishwa mahakamani kwa kuwa kitendo cha aina hiyo kinatafasiriwa kama kuingilia uhuru wa mahakama, hali inayoweza kusababisha maamuzi ya haki yasifikiwe.

“Najua mnaningoja kwa hamu niizungumzie taarifa iliyotolewa na Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, kuhusiana na mtuhumiwa Mhindi, nasema siwezi kuliongelea suala hilo kwa kuwa liko mahakamani…labda niseme kwamba ile taarifa ya awali niliyowapatia Julai 13 inabaki kama ilivyo, kwa kuwa ina maelezo na ushahidi wote juu ya suala hili,” alisema.

Hata hivyo, Kova alizungumzia baadhi ya hoja zilizotolewa na mchungaji Gwajima likiwemo suala la mtuhumiwa kuwa na matatizo ya akili ambapo alisema sheria za nchi zinawabana wahalifu wote wa makosa ya jinai wakiwemo wenye matatizo ya akili na kwamba ukichaa wa mtu si tiketi ya kutenda jinai bila kuadhibiwa.

Alisema jeshi la polisi haliko kwa ajili ya kulumbana na viongozi wa dini kwa kuwa linawaheshimu na ni wadau wakubwa katika harakati za kudumisha amani nchini na katika dhana nzima ya utii wa sheria bila shuruti.

Kova alisema kwamba kazi ya jeshi la polisi ni kuhakikisha amani inadumu nchini ili viongozi wa dini na waumini wao waweze kufanya ibada zao usiku na mchana kwa amani.

Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko Kawe jijini Dar es Salaam kupitia kwa mchungaji Gwajima juzi kwenye ibada ya Jumapili, lilikana taarifa zilizotolewa na Kamanda Kova kuwa mtuhumiwa Mhindi ambaye ni raia wa Kenya alienda kuungama mbele ya mchungaji huyo kuwa ndiye aliyemteka na kisha kumdhuru Dk. Ulimboka akishirikiana na wenzake wa kikundi cha Gun Star cha nchini Kenya.





CHANZO: NIPASHE

 
Kova this time imekula kwako,na tunahitaji more information na hatuna maelezo yako ya mwanzo so tunaomba utupe more info plz

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom