bachelor sugu
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 2,689
- 3,643
Kiukweli inasikitisha unapoandika li thread lirefuuuuu kumbe umejaza utaahira wako,ukiuizwa sasa hapo kipi bora km mtanzania nchi kuwa salama au kutokuwa salama?nyuma kulikuwa na matatizo kibao NCHI ILIKUWA SALAMA ila sasa hv Matatizo yanatatuliwa NCHI SIO SALAMA.Watanzania ni watu wa ajabu Sana, wakati nyara za taifa zinaporwa nchi ilikua salama, wakati, kodi za wananchi zikilipwa mishahara hewa nchi ilikua salama, wakati watoto wa maskini wengi walishindwa kupata elimu Kwa kua walishindwa kumudu Karo na michango, nchi ilikua salama, wakati serikali ilpolaumiwa Kwa kua na shirika la ndege lisilo na ndege nchi ilikua salama, wakati wakulima wakikomolewa na kodi nyingi katika mazao yao nchi ilikua salama ,wakati ujambazi nchini na biashara ya madawa ya kulevya ilishamiri nchi ilikua salama, wakati nidhamu ya watumishi wa sekta ya umma ilikua poor, nchi ilikua salama, wakati misamaha ya kodi ilikithiri nchi ilikua salama, wakati madini yalipokua yanatoroshwa Nje ya nchi, nchi ilikua salama ,ccm ilipopuuza madai ya wapinzani nchi ilikua salama, wakati bajeti ya huduma za afya ilikua chini, Nchi ilikua salama, wakati uvuvi haramu ulishamiri nchi ilikua salama, wakati migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji ilishamiri nchi ilikua salama,
Rais Magufuli umefanyia kazi changamoto hizi Kwa muda mfupi, kwa weledi wa hali ya juu, ukishirikiana na wasaidizi wako makini, , nchi si salama ,miradi mikubwa ya miundo mbinu imeanzishwa na inatekelezwa nchi sio salama. Lipi jema Kwa wanadamu?, usinge fanya kazi wangesema unaona ccm ni walewale
Ama kweli, duniani tenda wema wende zako , usingoje shukrani .
Mkuu rais, kuna kundi la watu wachache, wana nafasi nzuri kiuchumi ,tena baadhi si fedha halali walilipora taifa , waliamini nchi ni mali yao binafsi, walifanya watakavyo kulihujumu taifa, umegusa maslahi yao, wanatumia kila njia kuhakikisha unakwama, wananunua watu,na magazetini ya ndani na nje kuhakikisha nchi haisongi mbele, ili wapigiwe magoti.
Mkuu rais, songa mbele, ukisita tu,mahasimu watachukua point, usisite wananchi wengi wamekuelewa, wanaimani kubwa kwako, usituangushe,
Hizi kelele nyingi ni za wafa maji, waliozoea kitonga, ninyooshee mkuu!
KWETU WATANZANIA USALAMA WA NCHI YETU NDICHO KIPAUMBELE so km nchi yetu sio salama elewa tu hayo yote hayana maana kwetu.Afterall elewa kuwa kuna watu wamesababishiwa maumivu yasiyofutika kamwe mioyoni mwao.Walobomolewa Nyumba zao ubungo kimara, wakati mwanza wanaambiwa wasibomolewe kwa kuwa hawakumchagua ili awaumize na mengine lundo ya moyoni,kamwe usalama utakuwa ndoto.
Ila mkumbuke tu nyie wana Lumumba kuwa Nguruwe aliyezaa usipomlisha vizuri basi hula alivyovizaa kimoja baada ya kingine so ukimaliza wapinzani subirieni na nyie atawageukia tu.Laana zote mbaya ziwe juu yenu na mlipwe hapahapa duniani.