Korean Air Lines Flight 007: Ndege ya abiria iliyoruka juu ya anga la chuo cha siri cha usalama ikiwa na kamera za upelelezi (Surveillance Cameras)

Mkuu fanya masahihisho kidogo sana kwenye hii story yako. Ina mapungufu madogo. Kwanza route siyo hiyo uliyoisema. Pili hiyo sehemu hakuna chuo cha usalama wa Urusi. Hapo ni Sakhalin ambapo kuna Naval Base ( Nuclear submarines) inayojumlisha pia Military Districts za Far Eastern Front ya Russia. Tatu sequence ya events ni hivi. Kwanza crew wa KAL 007 walikuwa the most exeperienced na Kapteni wa hiyo ndege alikuwa amependekezwa kuwa Pilot wa ndege ya Rais wa Korea Kusini. Kama ujuavyo route ya ndege haswa 747 inakuwa programmed before take off na ndege kama hiyo inakuwa monitored hata kutoka Boeing Hq kwenyewe. Baada ya takeoff kilichowashtua warusi ni ile "pattern" ya flight. Ukiangalia jiografia ya Sakhalin ni kuwa ndege ilikuwa "inadeviate" na kuingia kwenye anga la Sakhalinski halafu inakaa kwa muda halafu inarudi kwenye route yake ya kwaida. Wakati huo huo kulikuwa na "geostationary satellite: kwenye orbit hiyo hiyo kiasi cha kwamba kuna wakati ndege hiyo na satellite hiyo vilikuwa kwenye mstari mmoja. Kamanda wa Eastern front alituma ndege Mig-25 ili aiteremshe kwenye uwanja wo wote wa kiraia kwa ajili ya uchunguzi. Pilot wa Mig-25 aliswitch on international frequency na kuiita lakini pilot wa KAL hakujibu. Akatangulia mbele yake na kumwashia taa kama "follow me" lakini KAL 007 hawakutii. Pilot akaarifu Moscow kwamba ndege hiyo ilikuwa imekaidi jitihada zote na ilikuwa ni ya abiria. Wakati huo KAL 007 walikuwa wamemaliza "pass ya tatu" juu ya Sakhalin na muda si mrefu wangekuwa kwenye "international airspace", hapo ndipo General aliyekuwa zamu Moscow akatoa amri "Take out the target". Ilitunguliwa na makombora mawili.
Mkuu si umalizie mambo ya viporo ayapendezi
 
Hii story ingependeza ingeletwa na the bold, huyu alieileta si msimuliaji mzuri.
Hate speech. Kama unampenda the bold nenda ukasome jabari zake na sio kumkatisha tamaa mwenzio. Kumbuka hatuwezi kuwa sawa. Kila mtu ana namna yake ya kuwasilisha kitu. Usimlazimishe aige kazi ya mtu. Kumbuka halipwi ila kaona sio vibaya kutupa habari hii. Sina chuki ni ushauriu tu
 
Hate speech. Kama unampenda the bold nenda ukasome jabari zake na sio kumkatisha tamaa mwenzio. Kumbuka hatuwezi kuwa sawa. Kila mtu ana namna yake ya kuwasilisha kitu. Usimlazimishe aige kazi ya mtu. Kumbuka halipwi ila kaona sio vibaya kutupa habari hii. Sina chuki ni ushauriu tu
Nilikuwa nawaza tu kwa sauti, nisamehe kama nimekukwaza.
 
Back
Top Bottom