Kongamano la Wanawake Chuo cha Utumishi wa Umma, Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MHE. MARTHA GWAU MGENI RASMI KWENYE KONGAMANO LA WANAWAKE CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA CAMPUS YA SINGIDA.

Mhe. Martha Nehemia Gwau Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Singida amekuwa mgeni Rasmi kwenye kongamano la wanawake pamoja na kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiongoza Serikali ya Awamu ya Sita kwa mafanikio makubwa ndani ya miaka miwili ya uongozi wake.

Mheshimiwa Mbunge, Martha Nehemia Gwau amewataka mabinti kujiandaa na maisha baada ya Chuo kwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazoletwa na serikali ya awamu ya sita kwaajili yao.

Vilevile, Mhe. Martha Nehemia Gwau amewaasa wanawake na mabinti wote kuthamini na kupambania ndoto zao kwa nguvu zote ili waweze kuwa wakombozi kweli wa familia na jamii zetu.

Mwisho, Mhe. Martha Nehemia Gwau aliwapongeza waandaaji wa kongamano hilo na kuahidi kuwa ataandaa kungamano lingine kubwa lenye muda wa kutosha ili watoa mada wawe wengi na mada ipate muda wa kutosha ili malengo ya kuikomboa jamii ifanikiwe.

Kongamano hilo limeratibiwa na Makamu wa Rais Chuo cha Utumishi wa Umma Campus ya Singida Bi. Farida Omary Mohamed kwa kushirikiana na Serikali ya wanafunzi ya chuo hicho pamoja na uongozi wa chuo na wadau wengine.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Singida.

#MarthaGwauKazini
#KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.10.11(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.10.11(1).jpeg
    108.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.11.21(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.11.21(2).jpeg
    117.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.11.23(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.11.23(1).jpeg
    132.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.11.22(4).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.11.22(4).jpeg
    116.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.11.22(5).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-10 at 22.11.22(5).jpeg
    112.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom