Kongamano la Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati Mkoa wa Dar es Salaam

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
MHE. JANEJELLY NTATE AFANYA KONGAMANO LA WALIMU WA SANYANSI NA HISABATI MKOA WA DAR KUTAFUTA CHANZO CHA WANAFUNZI KUTOKUWA NA UFAULU MZURI KATIKA MASOMO HUSIKA HASA WANAFUNZI WA KIKE

Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum Muwakilishi wa Wafanyakazi Tanzania 🇹🇿 amehutubia kongamano lililohusisha Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga

Mhe. Ntate amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi alivyojipambanua na kuwaweka moyoni mwake watumishi wa Tanzania huku akiwaomba watumishi kumuweka Rais Samia mioyoni mwao.

Mhe. Janejelly Ntate amesema lengo la Kongamano ni ili kuongea na Walimu Kupanua mawazo ya kurejesha na kulinda Maadili wa Watoto huku tukiamini Mwalimu ndiye Msingi Mkuu na anakaa na mtoto ambaye ni Mwanafunzi kwa muda mrefu.

Aidha, Mhe. Ntate amesema pia kuona namna ya kurejesha Imani ya Wanafunzi hasa Watoto wa kike kupenda masomo ya Sayansi na Hisabati ili tupate Wanasayansi, Madaktari na Wahandisi wa kutosha nchini

"Tumekuwa tunaongelea kushuka kwa ushindi wa Masomo ya Sayansi na Hisabati. Nimeona turejee kwa Walimu tuongee nao, hawa wakiamua kwa dhati kabisa ndiyo wanaweza wakamaliza tatizo" - Mhe. Janejelly James Ntate

Mhe. Janejelly James Ntate pia amepongezwa na kupewa tuzo kama kumtia moyo kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwawakilisha wafanyakazi wote nchini pindi anapokuwa Bungeni na hata katika ziara za nje ya Bunge

Mhe. Janejelly Ntate amewashukuru wadhamini wa kongamano hilo; Tume ya Sayansi (COSTECH), Mamlaka ya Bandari Tanzania, TTCL, Shirika la Posta, CRDB Benki, NMB Benki, Bodi ya Korosho, Bodi ya Sukari, DAWASA, Bodi ya Kahawa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB)

Mhe. Janejelly Ntate amesema kuwa Makongamano kama haya yatakuwa endelevu jinsi wadhamini watakavyojitokeza kuwashika mkono.

Mwisho, Mhe. Janejelly Ntate amewashukuru sana wadhamini wote wa makampuni waliowashika mkono na kufanikisha kongamano hilo kufanyika.

WhatsApp Image 2023-05-27 at 18.17.45(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-05-27 at 18.23.17.jpeg
WhatsApp Image 2023-05-27 at 16.14.51.jpeg
 
Back
Top Bottom