Komba hoi

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
MBUNGE wa Mbinga Magharibi Kepteni mstaafu, John Damian Komba anadaiwa kuwa yuko hoi nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu, Risasi Mchanganyiko lina mkoba uliojaa habari hii.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa Mhe. Komba aliondoka nchini wiki iliyopita.
Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa za Maonesho la Tanzania One Theatre (TOT) alikwenda nchini humo kwa ajili ya kucheki afya yake lakini amelazimika kufanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kushauriwa na madaktari.

"Awali alikuwa amekwenda kwa lengo la kuangalia afya yake lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi akagundulika kuwa ana matatizo ya nyonga, hivyo akatakiwa kufanyiwa upasuaji haraka sana," kilisema chanzo chetu kimojawapo.

Mmoja wa ndugu wa karibu na Komba, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kwa vile yeye siyo msemaji wa familia, alithibitisha hilo.

Huyu hapa anazungumza: "Ni kweli mzee amekwenda India. Tunashukuru Mungu ameshafanyiwa upasuaji na anaendelea vizuri. Muhimu kwa Watanzania ni kumuombea dua apone haraka."
 
Hapo washachakaua ma Bilioni.. Huduma ziwe DHAIFU Muhimbili,na kwa UDHAIFU wao wakatibiwe India..
Dhaifu ni Dhaifu tu....
 
Mi nilijua kaenda kufanyiwa upasuaji ili asilale tena bungeni... anyway Get well soon sir ili uje ushuhudie chama chako kinavyokufa " mgeni amelala mgeni, mgeni.... mgeni huyu mgeni..."
 
MBUNGE wa Mbinga Magharibi Kepteni mstaafu, John Damian Komba anadaiwa kuwa yuko hoi nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu, Risasi Mchanganyiko lina mkoba uliojaa habari hii.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa Mhe. Komba aliondoka nchini wiki iliyopita.
Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa za Maonesho la Tanzania One Theatre (TOT) alikwenda nchini humo kwa ajili ya kucheki afya yake lakini amelazimika kufanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kushauriwa na madaktari.
"Awali alikuwa amekwenda kwa lengo la kuangalia afya yake lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi akagundulika kuwa ana matatizo ya nyonga, hivyo akatakiwa kufanyiwa upasuaji haraka sana," kilisema chanzo chetu kimojawapo.
Mmoja wa ndugu wa karibu na Komba, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kwa vile yeye siyo msemaji wa familia, alithibitisha hilo.
Huyu hapa anazungumza: "Ni kweli mzee amekwenda India. Tunashukuru Mungu ameshafanyiwa upasuaji na anaendelea vizuri. Muhimu kwa Watanzania ni kumuombea dua apone haraka."

aaaaaa,jamani mbona mnene sana?anaonekana afya yake n nzuri sana tu
 
Tafadhali wabunge wa upinzani waulize hapo bungeni ili tujue BUDGET ya wabunge inayotengwa kwa matibabu yao nchi za nje? Inaelekea hiyo ni siri kubwa sana ya wabunge; tafadhalini wekeni mambo wazi ili tujue kama kweli serikali yetu haina uwezo wa kukidhi mahitaji ya madaktari wetu!!
 
aaaaaa,jamani mbona mnene sana?anaonekana afya yake n nzuri sana tu

Unene sio afya ndugu, ni matatizo tu.
Uwiano sahihi wa uzito na urefu, ni moja kati ya vizingiti muhimu kutambua afya bora ya mtu.
 
Pona haraka uje kutuimbia wimbo wa kusifia chama chetu tawala...hatujakusikia mda mrefu sana
 
yule haponi safari hii,ni mmojawapo wa wapuuzi wanaimiza mizaa kwenye bunge letu

:eek2: Daah ni nini jamani? Pressure, Kisukari? Aisee hiyo lazima ni UMEME baaaaaaaalaa ndio maaana wanawa weka Bungeni watafune pesa bure kabla hawajaenda AHERA. Moto inawasubiri huko kwa ALLAH
 
Risasi ndio source ya hii habari?Honestly huwa siamini kabisa magazeti ya aina hiyo.
 
huyu si ndie alie taka zipigwe bungeni! anataka awape watu mada case bure mtu mwenyewe kajifia mapema!
 
Back
Top Bottom