Kkkt usharika wa sinza kuna nini katika ujenzi

jongoo

Member
Feb 10, 2010
17
3
Kuna ujenzi unaendelea katika kanisa hili ila tatizo kubwa limekuwa ujenzi umekuwa hauendi katika speed inayotakiwa japokuwa hela ya kutosha ipo ya kazi kuendelea

Ujenzi umesimama kwa muda sasa na hatua hata ya kuweka madirisha haiendelei tena na uongozi wa kanisa hausemi lolote.

HELA ZIPO, UJENZI HAUENDELEI, UONGOZI WA KANISA HAUSEMI LOLOTE, KULIKONI?
 
Ahahahahaa...unauhakika pesa zipo?..zipo kiasi gani?,....contractor anakudaini kiasi gani ?...mkataba wa ujenzi ulikuwa wa muda gani?...remedies ambazo contractorn anatakiwa kulipwa kwa kucheleweshewa malipo yake ni kiasi gani say %wise?

kijana suala la mikataba hasa ya majengo ya makanisa huwa kunamatatizo ya malipo kuwa makubwa kutokana na ucheleweshwachi wa pesa za contractor...unakuta contractor ameingia mkataba wa say 1b kujenga kanisa kwa miezi sita...ujenzi unaenda na kuwa miaka mitatu..contrctor anadai malipo (xpenses and loss) pia kuna gharama nyinginezo zinazojitokeza kwa ucheleweshaji wa umalizaji mradi kwa muda muafakaa....soo tafakari nini kimetokea na sio kulalamika tuu mzee
 
Nenda kwanza kaongee na wazee wa usharika halafu ndio uje hapa na majibu sahihi
 
Ahahahahaa...unauhakika pesa zipo?..zipo kiasi gani?,....contractor anakudaini kiasi gani ?.......soo tafakari nini kimetokea na sio kulalamika tuu mzee

Maswali yako yooote ya mwanzo yalikuwa ya msingi ila inaelekea mada hujaielewa ukaharibu na swali lako la mwisho.

Nimepata pia kuwa msharika wa kanisa hili pale sinza kabla ya kuhamwa mwezi uliopita.

- Kwamba kuna uhakika pesa ipo na kiasi gani?
Jibu: kama msharika hatajua ni mpaka aelezwe na wazee wa usharika.

- Mkandarasi anadai kiasi gani?
Jibu: Kwa phase hiyo ya madirisha hapaswi kudai manake harambee ilifanyika na hela kupatikana na usharika ulielezwa kwa taarifa rasmi.

- Mkandarasi anadai remedies kwa kuchelewa mkataba?
Jibu: Chanzo kikuu na pekee cha fedha za ujenzi wa kanisa hili ni washarika hawajaelezwa hilo ili wachange.

maoni: Suala alilioeleze mtoa mada na nalijua kabla sijaondoka ni kwamba kuna fedha ilishachangwa kama sikosei mwezi wa kumi kwa ajili ya phase inayofuata ya tiles na rangi tangu kipindi hicho ipo na hakuna hata dalili kwa sasa ya kuwepo mkandarasi site.

Ni vizuri wanaosimamia ujenzi watoe maelezo kwa washarika ili kufuta sintofahamu. Ni kiu yake kama msharika kuona nyumba ya bwana inakamilika kwa wakati ili apewe sifa na utukufu zaidi. Kuwapa imani washarika si vibaya wakawa na bank statements na msharia atakayependa kuzipitia awe huru
 
Nenda kwanza kaongee na wazee wa usharika halafu ndio uje hapa na majibu sahihi

Tatizo mara nyingi ni mfumo uliopo ambapo washarika wengi wanakuwa waoga kuulizwa kuhofia kutengwa au pia inawezekana kauliza majibu hakuna
 
Buguruni heshima kwako kwa ufafanuzi mzuri na nashauri mtu kabla ya kusiriki mada asome aelewe na si ajibu tu bora kuongeza posts
 
Kuna ujenzi unaendelea katika kanisa hili ila tatizo kubwa limekuwa ujenzi umekuwa hauendi katika speed inayotakiwa japokuwa hela ya kutosha ipo ya kazi kuendelea

Ujenzi umesimama kwa muda sasa na hatua hata ya kuweka madirisha haiendelei tena na uongozi wa kanisa hausemi lolote.

HELA ZIPO, UJENZI HAUENDELEI, UONGOZI WA KANISA HAUSEMI LOLOTE, KULIKONI?

Jongoo,
Swali lako liko very specific, na sidhani kama hapa utaweza kupata jibu. Kama ulivyoshauriwa huko nyuma, njia rahisi kama ukiwa msharika ni kuuliza uongozi wa usharika nini kimekwamisha ujenzi. Mimi nilikuwa msharika sehemu ambayo kulikuwa na shughuli ya ujenzi wa kanisa, nakumbuka ilikuwa hata kabla ya kuleta maombi ya kuwa na harambee ya hatua inayofuata ya ujenzi, kamati ya ujenzi ilikuwa inaanda ripoti na kuiwasilisha kwa washirika. Kuna wakati ripoti yao ilipitishwa kwa shida kwani kuna washirika wali raise issue ya gharama kuwa juu kupita kiasi, lakini angalau kulikuwa na transparency.

Sasa kama hakuna uwazi kwenye ujenzi wa hilo kanisa, ni haki yako kama muumini kujua nini kinaendelea, sometimes kwenye haya makanisa asipotokea mtu wa kuamsha mabadiliko basi waumini wote wataburuzwa. Be part of change, kama kweli hakuna uwazi.
 
Huwa napata shida sana na dini zetu hizi, kama mtu huwezi ukauliza haya maswali kanisani kwa mchungaji wako ambaye ana sura na mfano wa Yesu, kwa nini unauliza humu JF, KKT imekuwa sawa na CCM,KKT ina dola nayo?

kama KKT mTu anakuwa weak kama hivi, je mbele ya CCM?
 
Tatizo mara nyingi ni mfumo uliopo ambapo washarika wengi wanakuwa waoga kuulizwa kuhofia kutengwa au pia inawezekana kauliza majibu hakuna

Hili ndio tatizo! na je wakristo wanafanya nini? naona kabisa kanisa limechangia sana kudumaza maubongo yetu, let be honesty, Mbona Yesu aliku so free, approachable, open, hakuwa mnafiki, na alikuwa na demokrasia hata kwa wale waliotenda dhambi?

what christians do in a matter like this? I find is the problem in almost all churches in our country,
 
.

Ni vizuri wanaosimamia ujenzi watoe maelezo kwa washarika ili kufuta sintofahamu. Ni kiu yake kama msharika kuona nyumba ya bwana inakamilika kwa wakati ili apewe sifa na utukufu zaidi. Kuwapa imani washarika si vibaya wakawa na bank statements na msharia atakayependa kuzipitia awe huru
sasa , haya kama si majungu ninini ?
kwahiyo baraza la wazee ama mchungaji wa ushariki aje atoe majibu humu jamiiforums ? this is too low.
 
Kwangu mimi ujmbe utakuwa umefika na naamini something will be done. For you it is very low that is why your brain is at ICU but to others it is making some sense. God bless you
 
sasa , haya kama si majungu ninini ?
kwahiyo baraza la wazee ama mchungaji wa ushariki aje atoe majibu humu jamiiforums ? this is too low.
Thanks Nguvumali, kwa kuongezea tu mimi ni muumini wa pale, kweli huwa tunatangaziwa update ya ujenzi mara kwa mara lakini mtu yeyote akitaka kujua tumefikia wapi anakaribishwa kufika ofisini kwa mchungaji kupewa updates zote.

Mtoa mada ni mvivu - Cha kufanya kabla ya kuileta jamvini hii thread angefika pale KKKT - usharikani akutane na mchungaji wetu - ana ufahamu mzuri sana - angepewa information zote za ujenzi - then alete hapa jamvini tuzichambue.

kwa sasa hatuwezi kujadili hili jambo sababu hatuna upande wa pili - yaani information from KKKT - Usharikani juu ya ujenzi huu.
 
Na watu kama mtoa mada ndio wanaoharibu sharika za KKKT kwani wana nafasi pana tu ya kuuliza tena kwa uwazi lakini wao wanataka kuonyesha kuwa kuna mambo ambayo siyo yanayoendelea pasipo uthibitisho sahihi
 
Jamani washarika wa Sinza,
hivi unajua huyu Mchungaji wetu amekaa pale kwa miaka 6 sasa? Yaani kashajenga mazoea.

halafu yule mwenyekiti wa kamati ya ujenzi amekuwa na same position kwa zaidi ya miaka 8.

hawa waili wakiondolewa kazi itaenda.

Mimi nimeshaacha kuchangia jengo. Nakumbuka wakati tunaanzisha kanisa 14 years ago tulinunua jengo na plot kwa mkopo wa 50 milion na tukalipa within two years.

Mi nafikiri lazima mwaka huu tuanzishe kasheshe pale wakati wa hesabu za mwaka.

Maswali yako yooote ya mwanzo yalikuwa ya msingi ila inaelekea mada hujaielewa ukaharibu na swali lako la mwisho.

Nimepata pia kuwa msharika wa kanisa hili pale sinza kabla ya kuhamwa mwezi uliopita.

- Kwamba kuna uhakika pesa ipo na kiasi gani?
Jibu: kama msharika hatajua ni mpaka aelezwe na wazee wa usharika.

- Mkandarasi anadai kiasi gani?
Jibu: Kwa phase hiyo ya madirisha hapaswi kudai manake harambee ilifanyika na hela kupatikana na usharika ulielezwa kwa taarifa rasmi.

- Mkandarasi anadai remedies kwa kuchelewa mkataba?
Jibu: Chanzo kikuu na pekee cha fedha za ujenzi wa kanisa hili ni washarika hawajaelezwa hilo ili wachange.

maoni: Suala alilioeleze mtoa mada na nalijua kabla sijaondoka ni kwamba kuna fedha ilishachangwa kama sikosei mwezi wa kumi kwa ajili ya phase inayofuata ya tiles na rangi tangu kipindi hicho ipo na hakuna hata dalili kwa sasa ya kuwepo mkandarasi site.

Ni vizuri wanaosimamia ujenzi watoe maelezo kwa washarika ili kufuta sintofahamu. Ni kiu yake kama msharika kuona nyumba ya bwana inakamilika kwa wakati ili apewe sifa na utukufu zaidi. Kuwapa imani washarika si vibaya wakawa na bank statements na msharia atakayependa kuzipitia awe huru
 
Kusubiri majibu ya kutoka kwa mchungaji tutakuwa tunapoteza muda. Wewe kama ni msharika wa Sinza unajua kuwa update huwa zinasomwa wakati wa misa.Unaweza kuhoji pale? Si utaonekana unavuruga misa? Hasa ukitilia maanani misa ya yule mchungaji inavyoboaga.

Thanks Nguvumali, kwa kuongezea tu mimi ni muumini wa pale, kweli huwa tunatangaziwa update ya ujenzi mara kwa mara lakini mtu yeyote akitaka kujua tumefikia wapi anakaribishwa kufika ofisini kwa mchungaji kupewa updates zote.

Mtoa mada ni mvivu - Cha kufanya kabla ya kuileta jamvini hii thread angefika pale KKKT - usharikani akutane na mchungaji wetu - ana ufahamu mzuri sana - angepewa information zote za ujenzi - then alete hapa jamvini tuzichambue.

kwa sasa hatuwezi kujadili hili jambo sababu hatuna upande wa pili - yaani information from KKKT - Usharikani juu ya ujenzi huu.
 
Jamani washarika wa Sinza,
hivi unajua huyu Mchungaji wetu amekaa pale kwa miaka 6 sasa? Yaani kashajenga mazoea.

halafu yule mwenyekiti wa kamati ya ujenzi amekuwa na same position kwa zaidi ya miaka 8.

hawa waili wakiondolewa kazi itaenda.

Mimi nimeshaacha kuchangia jengo. Nakumbuka wakati tunaanzisha kanisa 14 years ago tulinunua jengo na plot kwa mkopo wa 50 milion na tukalipa within two years.

Mi nafikiri lazima mwaka huu tuanzishe kasheshe pale wakati wa hesabu za mwaka.
Caren nakubaliana na wewe kuwa kuna mambo ambayo yanaweza kuwa hayaendi mlivyotegemea lakini kwa uzoefu wangu ebu jengeni hoja ya pamoja kama washarika na kuipeleka kwenye uongozi wa usharika wenu na kuhoji mjue kwanini ujenzi hauendi kama ilivyokusudiwa, msianzishe kunji halitoleta ufumbuzi wa kudumu zaidi mimi kama mzoefu wa sharika zetu ndio mtaharibu mambo kwa kipindi kirefu zaidi

Ni mawazo yangu tu...yanaweza kukosolewa kwa namna yoyote ile na msharika wa hapo kwani kimsingi nyie ndio mnajua mambo yenu kuliko mimi au mtu mwingine nje ya pale. Asanteni
 
sasa , haya kama si majungu ninini ?
kwahiyo baraza la wazee ama mchungaji wa ushariki aje atoe majibu humu jamiiforums ? this is too low.

For your information mchungaji na mzee mmoja wa kanisa ni wadau wakubwa huku. Dont forget mchungaji wa Sinza ni graduate kwa hiyo huwa anaingia humu kupata info mbalimbali kwa ajili ya ibada.
 
Caren nakubaliana na wewe kuwa kuna mambo ambayo yanaweza kuwa hayaendi mlivyotegemea lakini kwa uzoefu wangu ebu jengeni hoja ya pamoja kama washarika na kuipeleka kwenye uongozi wa usharika wenu na kuhoji mjue kwanini ujenzi hauendi kama ilivyokusudiwa, msianzishe kunji halitoleta ufumbuzi wa kudumu zaidi mimi kama mzoefu wa sharika zetu ndio mtaharibu mambo kwa kipindi kirefu zaidi

Ni mawazo yangu tu...yanaweza kukosolewa kwa namna yoyote ile na msharika wa hapo kwani kimsingi nyie ndio mnajua mambo yenu kuliko mimi au mtu mwingine nje ya pale. Asanteni

Umesema vyema!! Bwana akuangazie.
 
Back
Top Bottom