DOKEZO KKKT Kimara- Korogwe mnaumiza majirani zenu kwa kutiririsha maji machafu!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nilisikia siku nyingi kwamba Kanisa la KKKT Kimara Korogwe tunaloliamini kwa mambo ya kiroho, kijamii na ustawi bora ukiacha ile ahadi ya kutuandaa kwa ajili ya ulimwengu ujao kwamba unatiririsha maji machafu (kinyesi) kwa majirani zao.

Sikuamini macho yangu nilivyo shuhudia kwa macho yangu majira ya saa tano usiku watu wamelala lkn kanisa linafanya tukio hilo!!!. Mpaka ilibidi nitulie angalau siku tatu ili nikitafakari kitendo hiki kwenye jamii kikoje?

Tuliaminishwa kwamba Usifanye matendo mabaya kwa watu wa Mungu hata ukiwa peke yako usitende dhambi, sasa kusubiri watu wamelala ukaachia kinyesi kitiririke kwenye makazi ya majirani zako tuna watoto wanachezea kwenye maeneo hayo, hata watu wazima wanapitia maeneo hayo, magari yanapita, yanapack, tunaanika mahindi juani kwa ajili ya kuandaa chakula lkn kwenye hali ile tunasalimika kweli ????.

Kanisa linaendesha shughuli zake kwa masaa mengi kiasi kwamba "kila kitu kinaachwa pale" hata hivyo lina miradi ya shule, Hospitali na miradi mingine mingi fikiria mzigo unaotoka hapo kwenda kwenye majirani nikiasi gani? kuna tabu kwenye jamii inayolizunguka Kanisa!!

Viongozi wa serikali ya mtaa walishapewa taarifa maranyingi lkn hakuna kitu kilicho badilika. Tulichogundua ni kwamba viongozi wakubwa wakitaifa mara nyingi wanakuwa pale kiasi kwamba hakuna tunachoweza kulifanya hivyo inabaki kwa msemo kwamba eidha ufe au uhame hilo eneo.

Sasa swali linakuja kwamba niutamaduni wa kitanzani kutiririsha kinyesi mtaani? Kanisa linaingia kwenye kumbukumbu za kuumiza jamii ya kitanzania? Tunafanyaje kutoka kwenye hali hii ukiacha na mambo mengine yanayofanyika ambayo nayo yanaacha majirani katika hali ya sintofahamu!!

"Tunatokaje na hali hii?".

Clip zipo za ushahidi sema app naona hairuhusu ku- appload!
View attachment 2857854View attachment 2857855View attachment 2857856View attachment 2857857
Mbona attachment hazifunguki ni kwangu tu au
 
Ila taasisi kubwa kama kanisa inabidi ijenge septic tank(station chamber kubwa underground ambayo haiwezi kujaa kirahisi leo au kesho ) atleast 20 years forward
 
Kuna hatari ya majirani kupata magonjwa hatari, kama kipindupindu typhoid nk.
Sure. Ndo maana tumeamua kupiga yowe ili tupate support ya jamii ili wakemee hiyo tabia.

Inasikitisha kwamba hii taasisi inakwenda kinyume na jamii inavyotarania iwe. Social responsibility = 0
 
Sure. Ndo maana tumeamua kupiga yowe ili tupate support ya jamii ili wakemee hiyo tabia.

Inasikitisha kwamba hii taasisi inakwenda kinyume na jamii inavyotarania iwe. Social responsibility = 0
Lakini mkuu inabidi uwe na ushahidi usio na shaka.

Leta video kamili, onyesha huo uchafu unapomwaga / hilo bomba linapoishia ukiweza. Ukileta ushahidi kamili utaungwa mkono na raia wengi.

Hata hivyo ilibidi mamlaka husika iwe tayari imelifanyia uchunguzi wa kina hili jambo hadi sasa.
 
Nadhani kwa wanaofahamu mazingira ya Kimara Korogwe videos alizopandisha zinatosha kuonyesha picha ya tukio zima mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini mkuu inabidi uwe na ushahidi usio na shaka.

Leta video kamili, onyesha huo uchafu unapomwaga / hilo bomba linapoishia ukiweza. Ukileta ushahidi kamili utaungwa mkono na raia wengi.

Hata hivyo ilibidi mamlaka husika iwe tayari imelifanyia uchunguzi wa kina hili jambo hadi sasa.
Pamoja na video nilizorusha humu pia majirani wote wanashangaa sana taasisi kama kanisa kufanya kitendo hicho na sio mara ya kwanza. Viongozi wa mtaa walishapewa taarifa hizo mara nyingi wanajua, hata maeneo yanakoelekezewa huo uchafu wanajua na wanalaani sana. Wewe unayeona kutoa ushahidi unataka ushahidi gani labda ushahidi wahojiwe wanaoathirika /uchafu unakoelekezwa usikilize machungu wanayopitia, wamekata tamaa wamebaki kuomba Mungu ndo atawanusuru na hali hiyo!

Ikumbuke kuwa wanategeshea usiku watu wamelala ndo wanafanya hayo. Ilibidi tuwe na tochi zile za walizi ili picha angalau zionekane. Wakati zinachuliwa hizo picha tulimtafuta mlinzi aliyekuwa zamu kwasababu tusingeingia hilo eneo usiku huo bila kuwepo mwenyeji.
 
Back
Top Bottom