Kiwanja kinauzwa, Tshs. 28 ml. Mbezi beach

MJ, sikuhizi wakazi wote wa Mbezi baada ya Lugalo wanajiita wa Mbezi Beach! wakimaanisha Dar kuna Mbezi mbili ile ya Kimara na hii ya Beach , jee umeshasikia Tegeta Beach? nako ni Mbezi Beach.<br />
<br />
Zamani kuna watu wakisoma Mbuyuni huku wakijiita walisoma O'bay!. Kuna watu wanaoishi Buguruni huku wakisoma Tambaza wanapanda mabasi ya Posta then ya Mwenge na kushukia Palm Beach na kujiita watoto wa Upanga!. Ndiyo haya sasa ya Kunduchi Salasala kuitwa Mbezi Beach ili kuhalalisha kaeneo ka high density kuizwa kwa milioni 28!.
<br />
<br />

Hahaha...mkuu Pasco heshima mbele mkuu wangu.

Umenikumbusha mbali sana kipindi niko high school Shaban Robert kuna jamaa walikuwa wanakaa kinondoni morocco lakini walikuwa wanapanda na sisi daladala za masaki, wakifika pale posta oysterbay primary school wanashuka wanatembea mpaka kinondoni morroco, kisa walikuwa ma brother men wanataka kuonekana watoto wa oysterbay...sasa haya ndiyo mambo ya kuita salasala kuwa ni mbezi beach.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom