2mbaku
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 316
- 67
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imesimamisha uzalishaji pamoja na usambazaji wa dawa bandia za kupunguza makali ya ukimwi ARVs zilizokuwa zikizalishwa na kiwanda cha TPI kilichopo Arusha kutokana na kubainika kuwa ni dawa bandia ambazo tayari zilikuwa katika soko.
Hayo yamesemwa na mkurugunzi wa TFDA Hiiti Silo wakati akito ufafanuzi juu ya usitwaji wa uuzwaji wa dawa hizo mbele ya waandishi wa habari Jijini dar es salaam.
Dawa hizo ambazo kiwanda cha TPI lTd kiliuzia bohari ya dawa MSD na kugundulika kuwa ni bandia zilisitishwa kutengenezwa na kusambazwa October 4 mwaka huu kutokana na ukaguzi kufanyika mara mbili kwa lengo la kujiridhisha kutokana na wizara ya afya na ustawi wa jamii kutoa taarifa kwa uma juu ya uwepo wa dawa hizo katika mfumo wa biashara.
Silo amesema kuwa licha ya kukifungia kiwanda hicho lakini taratibu za kutoa adhabu nyingine kama kufuta leseni ndio zitafuatwa baada ya uchunguzi kukamilika kwa kuangalia kwa kiasi gani dawa hizo zilisambazwa.
Dawa hizo ambazo zinatumia jina la kibiashara TT-VIR 30 tayari zilikuwa sokoni ingawa bado madhara yake hayajathibitika kwa watumiaji lakini tayari TFDA imesema kuwa ipo katika hatua za uchunguzi.
Tayari wizara ya afya na ustawi wa jamii ilitoa taarifa kwa uma juu 7 mwaka huu juu ya uwepo wa dawa bandia za kupunguza makali ya ukimwi ingawa kumekuwepo na mkanganyiko wa taarifa ambazo zinaonekana kuwa kiwanda cha Tanzania pharmaceutical Industries TPI kinaendelea na uzalishaji wa dawa hizo
Source: Star TV