Kiwanda Cha Saruji - Wazo v/s Umiliki wa Magari Mabovu...!!!

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,076
2,445
Alfajiri ya leo tarehe 9 March 2012 nimepita Mwenge na kulikuta Lori la kubeba Saruji linalomilikiwa na Kiwanza cha Saruji cha Wazo lenye namba za usajiri T697 ATD likiwa limepinduka "miguu juu", na inaelekea dereva wake amepoteza maisha...!

Tukio hili linatokea takribani wiki moja tuu baada ya Lori jingine la kubebea saruji kuacha njia na kuparamia "pick-up" na nguzo ya umeme eneo la Tegeta-Kibaoni, nadhani pia liliua mtu mmoja...!

Ni bahati kuwa hizi ajali zinatokea maeneo ambayo kwa kawaida uwa yanakuwa na msongamano wa watu na Daladala, lakini wakati zikitokea maeneo hayo uwa hakuna msongamano wowote...! Vinginevyo maafa yanaweza kuwa makubwa mno. Kwa mfano hii ya leo imetokea eneo la Mwenge-mataa karibu kabisa eneo ambalo Daladala hushusha na kupakia abiria kutoka Tegeta, na kuelekea Ubungo,Mbezi, Buguruni, e.t.c...!

Swali ninalojiuliza, hiki kiwanda cha "Wazo" kinao mpango wowote wa kuondosha hali hii? Kwa maana kama nilivyoandika hapo juu, tunaweza kushuhudia ajali mbaya sana na ya kutisha kama hali ikiachwa hivi hivi...!


Waliopatwa na majanga ya ajali hizo mbili nawapa pole...!
 
Malori ya cement...
Malori ya kusafirisha macontainer town trip..
Malori ya mkaa...
Malori ya taka..
Landrover za Breakdown
Ni mabovu wala hayastahili kutembea.wpTrafic?wapi Sumatra!
Pale kunduchi utakuta askari wanasimamisha magari mazima wanahoji sijui reflector huki wakiiacha hiyo mindemba ikipita usukani umeshikwa na watu wawili au dereva na sterling tingo na gia
 
haya malori ambayo hufanya kazi ya kubeba cement kwa ajili ya distribution hayamilikiwi na Twiga cement (Wazo), kiwanda cha cement walichofanya ni ku outsource transporters

hata hivyo Twiga cement inabidi wawe makini na procurement ya transporters, wawe na vigezo vinavyokidhi traffic regulations
 
hii nchi kila kona ni matatizo!! Lori Linatoka Zambia na Taa Moja Nyingine Zote Zimeungua lakini Hadi Linafika Dar!! Mpinga Yupo Anapiga siasa Tu!!
 
haya magari maarufu kwa jina la(mbaula) huwa,hayaaminiki hata kidogo,kwani brek zake huwa wakati mwingi zinagoma.pale mtongani kwenye mteremko wa kwenda mbagara dreva aliwahi kuruka akaliacha gari,breki ziligoma!lilikwenda umbali mrefu bila dreva,ndio likaingia kwenye bonde,wa2 walifaidi cement sana.na ndio maana muda mwingi huwa yanatembea ucku.
 
Yani barabara ya Mwenge-Tegeta ina hatari sana hususani mida ya usiku kutokana na hayo malori. Utakuta mkweche unatoka tegeta mwanangu full speed na mahoni kama vile anashindana! Nimakuwa nikisimamishwa na traffic kuulizwa leseni,triangle na kadi za gari sijui insurance na kila kitu, haya malori nakwambia hata hivyo hayana lakini daily ndani ya barabara. Inauma sana kuona nchi inapoelekea,lakini vile vile wakulaumiwa ni sie wenyewe!
 
Back
Top Bottom