Kiwanda cha magari tanzania

Sabode

Senior Member
Apr 11, 2008
160
21
Heshima mbele wakula.
Jamani ni hv karibuni tu nimesikia kuwa Mh waziri mkuu akitoa maelekezo ya namna ya kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana kwa kiwango ktk kiwanda chetu cha kuunda magari. NYUMBU.
Pia nilisha wahi kusikia story hiyo muda mreeefu sana ulopita. Sasa jamani swala lililo nisukuma kuandika hapa ni kuwa hata siku moja sijawahi liona hilo NYUMBU lenyewe likoje.
Na swala jingine hayo magari yanatengenezwa kwa ajili ya jeshi tu au hata raia waweza nunua?
Mali ghafi zinatoka hapa tz au nje?
Pamajo na vingine vya kuunga Scania na Opel vimeuawa na nini?
Kwa nini visirudishwe tupate ajira tuimarishe uzalishaji, hata valmet nasikia tulisha wahi kuwa na kitu ka kiwanda ya kuunganisha.
Haya mambo ni kweli jamani? yakowapi sasa? kwa nini? Why? who? when?
Kama kuna mtu ana picha ya NYUMBU naomba aniwekee hapa nilione chuma letu.
 
SABODE
Magari ya nyumbu yapo kibao. Ujenge tabia ya kwenda kwenye maonyesho ya sabasaba utayaona. Mengine mimi sina jibu ila magari ya nyumbu yapo
 
mzee hicho kiwanda cha nyumbu kwa ninavyofikiria kitakua ni magari kwaa ajili
ya jeshi. nilishawai kuliona gari oja la nyumbu, ndugu yangu halina sura hilo gari, baaaaya!, kwa jinsi lilivyo, raia sijui kama watalinunua, halina mvuto.
malighafi lazima zitakua zinatoka nje tu.
 
Na wewe, gari lishaitwa nyumbu unadhani litakuwa na sura nzuri?
 
SABODE
Magari ya nyumbu yapo kibao. Ujenge tabia ya kwenda kwenye maonyesho ya sabasaba utayaona. Mengine mimi sina jibu ila magari ya nyumbu yapo

...ah nilidhani ni kwa matumizi ya jamii kumbe wanaunga magari kwa ajili ya maonesho.
To hell with nyumbu
 
Duh!
Ka lina sura mbaya, hiyo si ishu sana suala ni kuwa yanapatikana? kama kuna mtu ana picha hebu tunaomba mtu atushushie hapa tulione na sie ambao hatuja wahi liona.

Pia kwa nini jeshi wasishirikiane na watu wa engineering kutoka vyuo vikuu may be wanaweza kuja na something better in future.
 
Mimi hawa watu wa nyumbu siwaelewi kabisa wanachofanya. Naona siasa siasa nyingi tu. Watoe data walipata kiasi gani cha hela wametengeneza magari mangapi na mipango yao ni ipi kwa siku za mbele walipa kodi tujue. Unajua kwa nchi nyingine kama Japani na Marekani vipuri vinatengenezwa na wajasiriamali. Kwa mfano mtu anaweza kuambiwa atengeneze bolt za aina fulani tu na kusupply. Sasa hawa jamaa naona wanataka kufanya kila kitu na magari hayaonekani. Tunataka magari si maonyesho ya sabasaba sijui kitu gani. Pia kwa hili naomba pia serikali iangalie mambo muhimu kama upatikanaji wa umeme na malighafi kama chuma. Iwekeze kwenye hili na haya mambo yakekuwa kilio cha wanajamii na kwa kweli tunaguswa tunaposikia mambo ya ajabu ajabu kwenye sekta za umeme na malighafi ya nchi. Viwanda vya vyuma na saruji ndio vimejenga miundo mbinu mingi tunayoiona Ulaya na kwingineko pia upatikanaji wa nishati. Nilishangaa Pinda alipotembelea Nyumbu mara kiwanda kinafanya kazi vyuma vinayeyushwa nk. Wanafanya kazi siku zote ama walitegea kwa ajili ya kiongozi?
 
Hivi niwaulize,

Tanzania kama nchi kweli kiwanda cha magari is this our priority ktk kutumia pesa za kodi?

Barabara -hatuna!

Umeme -ni mgawo!

Elimu- watoto wanakaa ktk matofali na waalimu hakuna!
Elimu ya Juu- migomo kila siku juu ya mikopo na ubora wa elimu!
Afya- Vifo watoto, wajawazito, malaria, ukimwi --juu sana!

Njaa- watu wanaishi kwa mlo mmoja!

Are our national priorities right? Something is wrong somewhere!

"Mshika yote, hukosa yote, akabaki anahangaika na Asijue na Kufanya"- Remi Ongala!
 
Technology mpaka itengemae needs to be worked on for sometime. I heard sometime back that the problem was how to fund researches done at Nyumbu. Lakini karibu kila kitu tunasema hatuna hela. Ningekuwa mimi ningelifikiria project kama Buhemba Gold mine ingeweza kutengeneza pesa za kuendesha reaserches zenye interest mustakabali na security ya nchi yetu kama hizi. Investment hii ni kubwa na inaweza kutuchukua muda mrefu kupata matunda yake.Lakini tukumbuke kuwa nchi kama Cuba, bila kukomaa na research za bi-technology, mara baada ya collapse ya ukomunist zisingeliweza kuhimili vishindo vya Marekani.Tufike mahala sasa tujiamini kama tunaweza na hii ni moja ya project zenye maslahi makubwa kwetu kama mafisadi hawataingilia kati na kutuchezesha sandakalawe
 
Ni kweli Ndahani
Hii mambo bana kwa nionavyo mimi ni kuwa uongozi bora hatuna watu creative wa kubuni na kuibua miradi, au kuboresha ile ambayo ipo na inasuasua lkn walichobakia ni kufisadi hata vile vidogog vilivyopo inatia uchungu kinyama.
 
Nchi ambayo inaendeswa kisiasa na ubabaishaji kama hii haiwezi fanikiwa lolote. Kila kiongozi ni mwanasiasa, tumeacha proffession na kukumbatia siasa na kuacha ukweli. Tuanze fuata nyao za nchi kama china ambayo ilikuwa ya kijamaa kama sisi wakafanya maamuzi magumu ya kimuundo na kifikra ndipo wakafika hapo walipo. Nchi hii hatuta weza fanikiwa kiviwanda wala kuvutia wawekezaji makini na wakubwa bila kutatua matatizo ya miundo mbinu kama upatikaji wa umeme wa uhakika, maji, mawasiliano, barabara na kuwa na taaruma muhimu kwa maendeleo ya nchi. Nchii hii ina maliasili nyingi, ebu jiulize tunazitumiaje?. kama mawazo ni kwamba wawekezaji wa kutoka nje ndio waje wazivune nasi tutafaidika basi hiyo ni ndoto.taifa liwaandae watanzania watakao weza zitumia hizo laslimali kwa maendeleo ya taifa. Mimi nilisha ishi katika nchi zenye raslimali nyingi kama TZ najua walicho fanya mpaka wakafaidika na kuendelea, hawakutegemea foreign investors tu, walijenga pia mkakati wa kuwawezesha wazawa kumiliki uchumi wao. Wanachofanya wawekezaji wa toka nje ni kuchukua chao na kuondoka na kuiacha nchi maskini. Kuonyesha kwamba nchi inaendeswa na wababaishaji nilisikia kiongozi mmoja akisema kwamba serikali ilikuwa haina mwakilishi katika migodi kadha ambayo ina hisa na wala ilikuwa haijui inavyozalisha wala mauzo yake. Hivi kweli tunahitaji watu IMF au WB watushauri hilo?. habari hizo na zingine kuhusu nchi inavyoliwa zinatia uchungu sana!!. Kuhusu kutengeneza au kutotengeneza magari, mimi nadhani tutatue matatizo ya miundombinu na hayo mengine yatawezekana. Huwezi jenga viwanda kama vya magari kwa umeme wa mgao wa Tanesco. Nchi kama China na India ambazo tunazisifu kwa maendeleo ya viwanda bado wanaupungufu wa nishati, lakini tofauti na sisi, wao wanachukua hatua madhubuti kuondoa matatizo, sisi bado tunajadili sijui mapaka lini.
 
Jamani kuna kiwanda cha magari au ni majaribio ya kuunda magari kwa kutumia vifaa vya magari mengine ya kizamani?
Hata mimi ninaweza kuamua kuunda gari langu kwa basic knowledge ya ufundi niliyonayo na kisha nikaiita jina langu MFD na hapo waandishi wataandika MF katengeneza gari!!!!!!!!! Sasa hayom magari si ni mengi?
Unajua shida ya viongozi wetu ni ile ile tu ya siku zote. Watachukua waandishi wa habari watakwenda kukagua miradi uchwara na waandishi wataandika utupu huu tunaosoma hapa. Ili mradi wapambe kazi zao zionekane nchi iko juu.
Jamani nchi imeshindwa hata kiwanda cha kutengeneza jembe alichotuachia mchina kiasi kilikufa leo watudanganye wanaweza kutengeneza gari? To hell with that lies.
Mbona huwa hatuoni wanatuwekea picha za gari hiyo wanayoita nyumbu?
Huu ni mradi mwingine wa kula pesa yetu ovyo kupitia mlango wa jeshi kama walivyofanya kwa Buhemba.
Sababu ni kwamba mambo ya jeshi are unquestionable!
 
Mimi hawa watu wa nyumbu siwaelewi kabisa wanachofanya. Naona siasa siasa nyingi tu. Watoe data walipata kiasi gani cha hela wametengeneza magari mangapi na mipango yao ni ipi kwa siku za mbele walipa kodi tujue. Unajua kwa nchi nyingine kama Japani na Marekani vipuri vinatengenezwa na wajasiriamali. Kwa mfano mtu anaweza kuambiwa atengeneze bolt za aina fulani tu na kusupply. Sasa hawa jamaa naona wanataka kufanya kila kitu na magari hayaonekani. Tunataka magari si maonyesho ya sabasaba sijui kitu gani. Pia kwa hili naomba pia serikali iangalie mambo muhimu kama upatikanaji wa umeme na malighafi kama chuma. Iwekeze kwenye hili na haya mambo yakekuwa kilio cha wanajamii na kwa kweli tunaguswa tunaposikia mambo ya ajabu ajabu kwenye sekta za umeme na malighafi ya nchi. Viwanda vya vyuma na saruji ndio vimejenga miundo mbinu mingi tunayoiona Ulaya na kwingineko pia upatikanaji wa nishati. Nilishangaa Pinda alipotembelea Nyumbu mara kiwanda kinafanya kazi vyuma vinayeyushwa nk. Wanafanya kazi siku zote ama walitegea kwa ajili ya kiongozi?

Kwakuongezea mkuu, nikweli tunaunda gari au tunaassemble parts? Vile vile kama ni kwa matumizi ya jeshi basi natumaini tutakuwa tunaexport hayo magari. Kama ni hivyo kiwanda kinachangia vipi katika pato letu la taifa. na je kuna faida kuendelea kuunda magari hayo nchini ukilinganisha na ile ya kuimport. Nauliza hivi kwa kuwa tunaweza kung'ang'ania tu kuonekana tunakiwanda cha gari wakati kinazidi kutufirisi. Kuhusu economic down turn vipi kiwanda hiki hakijatetereka maana viwanda vingi vya magari vimepata mtikisiko mkubwa.
 
Heshima mbele wakula.
Jamani ni hv karibuni tu nimesikia kuwa Mh waziri mkuu akitoa maelekezo ya namna ya kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana kwa kiwango ktk kiwanda chetu cha kuunda magari. NYUMBU.
Pia nilisha wahi kusikia story hiyo muda mreeefu sana ulopita. Sasa jamani swala lililo nisukuma kuandika hapa ni kuwa hata siku moja sijawahi liona hilo NYUMBU lenyewe likoje.
Na swala jingine hayo magari yanatengenezwa kwa ajili ya jeshi tu au hata raia waweza nunua?
Mali ghafi zinatoka hapa tz au nje?
Pamajo na vingine vya kuunga Scania na Opel vimeuawa na nini?
Kwa nini visirudishwe tupate ajira tuimarishe uzalishaji, hata valmet nasikia tulisha wahi kuwa na kitu ka kiwanda ya kuunganisha.
Haya mambo ni kweli jamani? yakowapi sasa? kwa nini? Why? who? when?
Kama kuna mtu ana picha ya NYUMBU naomba aniwekee hapa nilione chuma letu.

Gonga hapa: TATC Nyumbu, may be... may be unaweza kupata taarifa na habari zaidi.... lol!
 
Gonga hapa: TATC Nyumbu, may be... may be unaweza kupata taarifa na habari zaidi.... lol!

Duh! Asante mazee.
Anyway nilichukikuta huko hakifanani na nilvyo dhani tuko nyuuuuma. Anyway mi niona vingi ya vitu wanavyo fanya vilistahili kufanywa na VETA.
Halafu wao wangejikita katika kumboresha nyumbu wao. Halafu jingine nililodhani wafanye wangeanza kuunda viwanda vidovidogo ambavyo vingekuwa hata semi auto kwa kuanza.
Mfano:
Huko singida wakulima wanajiingiza katika kilimo cha alizeti na ukamuaji mafuta yake, wangeboresha hilo katika kuzifanya mashine za kukamua mafuta kuwa na hata semi auto production line kuazia ambapo mbegu zinaingizwa ktk kiwanda kidogo mpaka kuyatia ndani ya vibebeo iwe madumu au paketi.
Kwa kweli nilichokiona ni cha kiwango cha chini mno kulingana na muda ambao nilianza kusikia juu ya uwepo wa kiwanda hiko au sijui ni karakana tu.
Wazee au mnaonaje wenzangu hapa jamvini.
 
Hivi niwaulize,

Tanzania kama nchi kweli kiwanda cha magari is this our priority ktk kutumia pesa za kodi?

Barabara -hatuna!

Umeme -ni mgawo!

Elimu- watoto wanakaa ktk matofali na waalimu hakuna!
Elimu ya Juu- migomo kila siku juu ya mikopo na ubora wa elimu!
Afya- Vifo watoto, wajawazito, malaria, ukimwi --juu sana!

Njaa- watu wanaishi kwa mlo mmoja!

Are our national priorities right? Something is wrong somewhere!

"Mshika yote, hukosa yote, akabaki anahangaika na Asijue na Kufanya"- Remi Ongala!
Hii yote inatokana na kuwa na bora viongozi na siyo viongozi bora;ambayo inapelekea somewhere there are somethings goes wrong na hakuna hata anayejali!Ili mradi yeye(kiongozi)anapata chake basi inakuwa imetoka hiyooooo.
 
Sabode...Niliwahi kutembelea hicho wanachoita kiwanda cha kuunda magari cha Nyumbu. Kiwanda kiko sehemu inaitwa Kibaha kwa Mathias karibu 8km kutoka Barabara ya Morogoro. Nilichokuta pale si uundaji wa magari kwa mtazamo wangu kwani kwa mfano ukiangalia michoro ya sehemu mbali mbali za gari wanazodai wanaunda wao ni vitu ambavyo vilishafanyika na waundaji wengine..mathalani nikauliza muundo wa engine na differential ya hiyo nyumbu ina kitu gani zaidi tofauti na magari mengine tuliyozoea ikaonekana hakuna isipokuwa walichofanya wao ni kuumba gari yenye sura isiyoelezeka na ndio maana ni kwa matumizi ya jeshi tu. Kwani wanadai bado wako katika utafiti wa kuiboresha hiyo nyumbu eti ili ije kuuzwa kwa raia pi.

Kifupi mwonekano wa hiyo gari ya nyumbu ni kama nguruwe alivyo....Mbele ina mkato sharp na huku nyumba ni fupi sana. Muudaji hajui hata ground clearance ya gari yake sijui kama tunauunda au tuna-copy na ku-paste then tunajifariji kuwa tunauunda....
 
hayo manyumbu yana safari ndefu sana.nilishuhudi test drive ya moja laohalikufika hata mto wami likawa limekongoroka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom