Kiundwe chombo kimoja kusimamia usafiri majini

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1][/h]Written by Ashakh (Kiongozi) // 04/08/2012 // Habari // 3 Comments


Na Restuta James
3rd August 2012
Wabunge wameishauri serikali iunde chombo kimoja kitakachosajili na kusimamia usafiri wa majini kwa ufanisi mkubwa badala ya sasa ambapo kuna chombo zaidi ya kimoja.
Usafiri wa majini unasimamiwa na Mamlaka ya Kudhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na Mamlaka ya Bandari Zanzibar (ZMA).
Wabunge walitoa maoni hayo bungeni mjini hapa jana walipokuwa wakichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi, iliyowasilishwa juzi na Waziri wa wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Rukia Kassim Ahmed, alisema kukosekana na mamlaka moja ambayo inasimamia usafiri huo kunasababisha kutupiana mpira baina ya vyombo viwili vilivyopo sasa pindi ajali inapotokea.
Alisema vyombo vingi vya majini ni vibovu hivyo vinahitaji chombo kitakachofanya kazi ya kusajili meli na boti, kuzikagua na kuzisimamia ili kuhakikisha vinafanyakazi kwa mujibu ya masharti ya usajili wake.
“Japokuwa kuna Sumatra lakini usafiri wa baharini ni wa hatari, lazima tujiulize nini hatma ya maisha ya watu wetu,” alisema.
Mbunge huyo alitolea mfano ajali ya hivi karibuni ya MV Skagit iliyotokea katika eneo la Chumbe visiwani Zanzibar akieleza pia kuwa kumekuwepo na ajali kama ya MV Spice Ilenders ya mwaka jana pamoja na nyingine zilizotokea kwa boti zinazofanya safari kati ya Pemba na Tanga pamoja na zile za Unguja na Pemba.
Mbunge wa Ukonga (CCM), Eugen Mwaiposya, alisema kumekuwa na upotevu wa baadhi ya mizigo katika bandari ya Dar es Salaam na kuitaka serikali iweke mkakati mahsusi wa kuhakikisha usalama wa mizigo hiyo ili kulinda wateja wanaotumia bandari hiyo.
Kwa upande wake, mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, alihoji hatma ya kodi ya zaidi ya Sh. bilioni tatu ambazo hazikulipwa na kampuni ya Rites iliyokuwa inaendesha kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kama italipwa na kodi za Watanzania.
Alisema kampuni hiyo imeiachia TRL madeni makubwa lakini zaidi ya yote haikulipa kodi stahili serikalini jambo ambalo limewaachia Watanzania mzigo mkubwa wa kugharamia huduma kwa manufaa ya wajanja wachache.
Machali pia alisema kusuasua kwa usafiri wa reli kunatokana na hujuma zinazofanywa na wafanyabiashara wa malori ambao wanataka reli isifanyekazi kwa ufanisi kwa kuwa biashara yao itakufa.
Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Mohamed Habib Mnyaa, alihoji uhalali wa Kituo ch Ufuatiliaji na Uokoaji (MRCC), utendaji na mamlaka yake na ikiwa ni chombo cha Muungano.
“Tungependa kujua kilianza lini, mamlaka yake ikoje, ni cha Muungano? Na kama ni hivyo mbona Skagit ilipozama hiki chombo hakikuonekana badala yake ilikuja ndege moja ya jeshi na boti za Zanzibar,” alisema.
Pia Mnyaa aliitaka serikali kutaja meli nne ambazo zilikaguliwa na Sumatra mwaka jana na kusimamishwa kufanya usafirishaji baada ya kukutwa na kasoro mbalimbali na pia serikali ileleze zimefungiwa kwa muda gani.
Aidha, mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, aliishauri serikali kutengeneza mkakati au sera ya kuboresha usafiri kwenye maziwa nchini pamoja na ule wa reli hususani kwenye mikoa ambayo njia ya treni inapita.
Alisema reli ya kati inapita Singida na kuitaka Wizara ya Uchukuzi kueleza mpango wake wa kufufua reli hiyo kama utagusa njia ya Singida.
Katika hatua nyingine, mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk. Faustine Ndugulile, aliibua sakata la shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA); na kuitaka serikali ieleze hatma yake baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba liliuzwa.
“Nini kauli ya serikali kuhusu UDA, je ni mali ya nani kwa sasa na nini matokeo ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),” alisema.
CHANZO: NIPASHE
 
Upande mmoja hawaupendi muungano lakini upande wa pili hao hao wanaulizia vitu vya muungano. Tumechoka na viumbe hawa!
 
Back
Top Bottom