Kiukweli ndoa za sasa sio kwa ajili ya Mwanaume/ Mwanamke dhaifu

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
 Nimeshuhudia ndoa nne za gharama (nilizochanga Mimi) ndani ya miezi 6_9, tatu kati ya hizo zikipumulia Mashine Huku moja iliyodumu kwa Mwezi mmoja (siku ya harusi kamati ilimpa zawadi ya million 10 Bwanaharusi) ikisambaratika huku bibi harusi akitolewa mkuku au vijana wa mjini wakisema ametolewa baruti vibaya mno.

Hivi unadhani hawa wapenzi walikua hawapendani kabla ya kufunga ndoa? Kuna kitu jamaa mmoja humu alishakisema kinaitwa "red light" Taa nyekundu. kwenye uchumba Kuna tabia ambazo Mwanaume/Mwanamke anakua nazo ambazo hawezi kubadilika yaani ndio hatobadilika hata ufanyaje, mfano kama mchumba wako anapenda kuongea ongea na wanaume/ wanawake hata ukimuoa hatoacha, kama akiwa charming saana hatoacha hata ukimuoa, kama alikua ni penda penda hatoacha atatulia tu kwa muda akipata nafasi atacheat tu.

Ukitaka kukaa na Mwanamke/ Mwanaume wako kwa miaka angalau mitano Hadi kumi basi huna budi kujifanya fala na uache mengine yapite, Lakini sio kwa uasherati maana kwenye uasherati hakuna msamaha.
Nimezungumzia kua kondoo maana wanawake/ wanaume wengine ndio walivyo hutoweza kumbadilisha tabia yake hata ufanyeje utajikuta kila siku unaingia kwenye migogoro na kero, tujifunze kupuuzia na kukaa kimya.

Usipokua strong utajikuta unaoa na kufukuza maana ndivyo walivyo, unaoa Mwanamke ambae ametoka chuo unadhani huko alikua amelala na kusoma tu? Wengine wameshakutana na RPG machine gun ambazo hawawezi kuzisahau ukimuoa kama hana akili siku akikutana na EX wake atapigwa tu.

NB: MATHAYO 19:9. Nani nawaambiya ninyi, Kila mtu atakayemuacha mkewe, isipokua kwa sababu ya uasherati akaoa Mwingine azini. (Sababu pekee ya kumuacha Mwanamke ni uasherati).
 
Chuma icho kila mwanamke single mother sijui tutaoa Nini ...!

Bora ni enjoy tu# diamond ft jux
 
Zawadi wanazopokea maharusi ni lango/chanzo cha mifarakano.
TRUST ME.
Hizo zawadi zimo wanzokupa ma x wako,na zingine wanatoa ma x wake na mkeo

Mnapita mtaani na ving'ora ma x wenu wanawachora tu kudadeki,aahaaa

Kuna ndoa itabaki hapo,
 
Zawadi wanazopokea maharusi ni lango/chanzo cha mifarakano.
TRUST ME.
Hakikaa umesema kweli kitu kama hicho nishawahi kusikia kwa mtumishi wa Mungu mmoja si wote wanaokuja kwenye sherehe wanakuja na nia nzuri. Hata michango mtu anakuchangia lkn tayari ile hela kashaipeleka kwenye maagano kwa kuinuzia mabaya. Mnaingia kwenye ndoa siku mbili tu ndoa inaanza kupumilia mashine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana tuwe kama Babu zetu tuwe na wake wengi, na pia tusi ishii na hawa wake zetu nyumba moja tupote tukafanye kazi tukijiskia kurudi nyumbani turudi kuiona familia na kufanya mambo ya msingi katika ndoa.
Lakini wanawake wa siku hizi hawana hofu kama wa zamani, ukimpa kisogo tu ni kama umempa kisogo simba au chui kinachofuata kinajulikana hapo, yote kwa yote dunia ya sasa imebadilka na inaenda kasi mara 10 kuliko ya miaka ya nyuma.
 
Back
Top Bottom