Kiufundi bado naiona Yanga SC ni bora kuliko Azam FC na kwamba ina 85% za kushinda leo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,031
Ukiwatizama Yanga SC katika kila Idara na kuangalia Fitness yao hasa kwa Mchezaji mmoja mmoja na ukawalinganisha na wa Azam FC na current performance yao ambayo ni ya kusuasua bado nawaona Yanga SC si tu ni favourite katika Mzizima Derby ya leo bali pia ni Title Contender ambao nilishasema (japo GENTAMYCINE) mimi ni mwana Simba SC lia lia kuwa hata Msimu huu wa 2022/2023 NBC Premier League bado Yanga SC itabeba Kombe.

Ushindi mkubwa kwa Azam FC leo yenye mapungufu makubwa hasa golini (kwa Makipa wake) na safu yake ya ulinzi ni kutoka suluhu (bila kufungana) au sare (ya magoli sawa) ila wa kufungwa nawapa 85% kutokana na mtizamo wangu ambao sikulazimishi uukibali/uuamoni ila uheshimu tu.

Merry Christmas JF Members wote!
 
Kweli, maana azam bado wanajitafta kwenye ile form yao ya kushinda game nyingi, halafu ukiongeza na uchovu wa kwenda kanda ya ziwa na kurudi huku yanga yeye alikuwa anatoka avic na uwanjani kwahyo basi na mimi naona yanga yuko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuibuka na ushindi japokuwa kwenye football anything can happen
 
Huyu mwamba nilikuwa namchukulia poa nyuzi zake. Duuh jamaa ana telescopic eyes. . big up
Asante Mkuu wangu na ndiyo maana unaona hata 90% ya Wanamichezo wa hili Jukwaa la Sports ( Michezo ) wamenipigia na wanaendelea Kunipigia Kura zao nyingi GENTAMYCINE na za Kishindo katika Shindano la Member Bora wa Mwaka katika Jukwaa la Michezo
 
Ifike muda, popoma apewe heshima yake hapa JF!
Asante, Amina, Ubarikiwe Kiongozi wangu. Muda si mrefu kwa Kudra / Neema zake Mwenyezi Mungu hili Uliloliombea hapa litatokea.

Shukran pia Kiongozi wangu na ndiyo maana unaona hata 90% ya Wanamichezo wa hili Jukwaa la Sports ( Michezo ) wamenipigia na wanaendelea Kunipigia Kura zao nyingi GENTAMYCINE na za Kishindo katika Shindano la Member Bora wa Mwaka katika Jukwaa la Michezo
 
Back
Top Bottom