Kituo cha Mafuta cha TOTAL Mlimani City na unyanyasaji/udhalilishaji kwa wananchi

Goodluck Mshana

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,271
1,119
Habari kwenu Wadau!

Kituo cha Mafuta cha Total ambacho kipo eneo la Mlimani City imekuwa na utaratibu wa hovyo wa kuwanyanyasa Watembea kwa Miguu kwa muda mrefu!

Utaratibu huo umeanza tangu kipindi cha sherehe za Christmas mpaka leo hii! Ukiwa unatembea kwa Miguu, unaendesha baiskeli au ukiwa Mazoezini hauruhusiwi kupita kwenye eneo la kituo cha mafuta!

Wapo Walinzi wa Kampuni (nitaweka Jina soon) wenye Silaha ambao wamejipanga pande zote za Sheli kuzuia watembea kwa Miguu! Utaratibu huo haukuwepo miaka yote! Iweje leo unakuja utaratibu wa ovyo kiasi hiki?

Utaratibu huo wa hovyo umepelekea watu kutengeneza njia mbadala ya kuzunguka kituo cha Mafuta kitendo ambao kimeendeleea kuharibu Mazingira kwa Wananchi kujitengenezea njia zao wenyewe!

Tunataka kujuzwa kama utaratibu huu ni mpya kwa Sheli za Mkoa wa Dar es Salaam na kwingineko Nchini au ni Ubabe wa wenyefedha? Itakumbukwa Sheli hii bado ipo kwenye hifadhi ya Barabara na hivyo kuzuia Service Road inayotokea Mlimani City kuja roundabout ya kuelekea kwa Mama Kamche to Calabash! Kitendo cha kuzuia muendelezo wa service road ndio maana watu wamekuwa wakipita chini ya Paa la Sheli hiyo!

Lakini kwenye Sheli kuna huduma za Kibenki, Supermarket na Biashara ya Vilainishi vya Magari nk.

Tunaomba Mamlaka zinazohusika, ikiwemo Ofisi ya RC Kunenge kuingilia kati unyanyasaji na uzalilishaji unaoendelea kwenye Sheli ya Total pale Mlimani City!

Goodluck Mshana
 
"Sheli" eneo nyeti, uvutaji sigara, kichunga cha sigara isiyozimwa kilichotupwa ovyo au simu za mkononi zilizowashwa zinazotumika zinaweza kutengeneza ajali ya moto au mlipuko

Hivi huwezi kuvuta sigara, kupiga simu ndani ya gari? Sheli hiyo ina miaka si chini ya 20 sasa! Hakuna matukio ya namna hiyo! Kwanza Watanzania wamestaarabika sana siku hizi! Zamani sio ajabu kukuta mtu amewasha sigara ndani ya Ngorika au Feri!

Eneo hilo limetumika kama njia kwa miaka nenda rudi! Japo ni vizuri kuchukua tahadhari kwa kuendelea kutoa Elimu kwa Umma! Sio kuzuia Watembea kwa Miguu! Otherwise wakubali eneo la Sheli likatwe kuruhusu service road inayotokea Mawasiliano ipite ili tuwaachie Sheli yao na huduma zao zote!
 
"Sheli" eneo nyeti, uvutaji sigara, kichunga cha sigara isiyozimwa kilichotupwa ovyo au simu za mkononi zilizowashwa zinazotumika zinaweza kutengeneza ajali ya moto au mlipuko

Watu wengine wa ovyo kama mleta sredi
 
Haki bila wajibu ni ukichaa. Sheli haitembelewi na chombo au mtu anayetaka kununua mafuta. Wewe unafukuza upepo (baadala ya kuweka treadmill nyumbani), unawaghasi wanaofanya biashara!

Jifunze kuheshimu ofisi za wenzako ili wakuheshimu. Aidha acha kwenda pahala huhusiki napo. Hata gari kukatiza pale bila kununua mafuta ni kosa.

Heri ya mwaka mpya
 
Ila jamani vitu vingine ni kujitaftia mengine sasa we unakatiza sheli kweli? kumbuka hayo maeneo ni hatari we unakatiza kufanya njia zako bythen mi naona ni halali wao kudhibiti movements zisizo za lazima kama izo za kukatiza katiza hovyo (nasema ivi mi mwenyewe ni mkatizaji mzuri sana wa ilo eneo).

Kudhibiti movements izo zitasaidia maana kuna watu wengine hawajui athari za kukatiza sheli hovyo na kuna wengine wanaweza pita na sigara zao, au vitu hatari kiasi cha kuhatarisha usalama wa eneo lao la kazi.

Imagine apite mtu apo alafu litokee jambo labda ni mlipuko au chochote kibaya waje waseme ulisababishwa na mpita njia kukatiza sheli we unafikiri kosa litakua la nani?

Huduma za kibenki zipo ila sio lazima ukatize sheli vile vile kuna sehemu kwa upande wa pili kuelekea Ardhi mtu anaweza pita kule na kutokea kule kule.

Ova.
 
Sheli ndio nini ?


Huna pointi hata moja , eneo la kituo Cha mafuta ni hatari au mpaka mfe Kama wale waliokufa morogoro kwa kuchota mafuta ?
Huyu ni mpuuzi mwingine kama Tundu Lissu alivyokuwa anawadanganya watanzania
 
Sheli ndio nini ?


Huna pointi hata moja , eneo la kituo Cha mafuta ni hatari au mpaka mfe Kama wale waliokufa morogoro kwa kuchota mafuta ?

Kwahiyo waliokufa Morogoro walikuwa kwenye Kituo cha Mafuta (Sheli)?

Halafu neno ‘Sheli’ ni cover term tu na ndio maana umeelewa nilichoandika na ukajibu! Kuna kitu kinaitwa ‘colloquial language’ na ‘slang’ muwe mnavijua! Msikariri!
 
Mleta mada sidhani kama unaelewa somo la kemia ata kwa kidato cha tatu. Yote ni kwa faida yako alafu bado unataka kuleta ujuaji na ofisi za watu. Watu kama wewe mleta mada mnasubiri mmfe ndo na serikali itoe tamko aje atafutwe mchawi apo basi muaribu biashara za watu. Mi nimekushangaa kweli kukomalia ofisi za watu kwa kutaka kuigeuza shortcut yako.

Mzee amka acha kung'ang'ania sheli za watu ilo ni eneo hatari. Sishangai mtu kama wewe kukatiza chini ya ile minara mikubwa (High Voltage) ya Umeme kwa kigezo ni njia yako na wakati umesha ambiwa ni hatari ila kwa akili zako utang'ang'ania kupita.

Jamani niulize watu kama hawa wakifa tutasema ni mpango wa Mungu?. Mungu huyu huyu aliye tupa Akili na Utashi.
 
Back
Top Bottom