KITUKO: Nimekojolewa na mtoto kwenye basi

article

Senior Member
Sep 10, 2016
176
331
Habari za Usiku Wadau,

Nipo kwenye bus mida hii natokea Dar naelekea Dom pembeni yangu yupo mdada mwenye mtoto mwenye kama miaka mitatu hivi.

Safari inaanza huyu mama nikampa hai hakuitikia kivile mi nikapotezea.

Tumefika maeneo ya kibaigwa huyu mwanae akawa kamlaza kidizaini fulani mtoto nikaona amelala vibaya na anaumia kiuno so nikaamua kutake trouble ya kumuinua na kumlaza kwangu huku akiegemea kwa mama yake na miguu kwangu.

Safari imeenda mara dogo akawa akijipindua pindua ghafla nikaanza kuhisi ubaridi kama maji vile nimemwagiwa kumtoa yalabi nimeloa mkojo mapajani kwenye suruali yaani ghazabu fasta ikanipanda ila nikachili nikamwambia huyu Dada mwanao kanikojolea!

Huyu Dada mwenye mtoto kuona hivyo akaanza kujibalaguza samahani kaka , only that!Akamchua mtoto wake na kumpakata hata hajambadilisha nguo.

Nimeboreka hapa wwe acha tu sema sina cha kufanya na huyo dogo anaonekana mkubwa so sijui kwa nini amenikojolea!

Ugentlemen leo umenitokea puani,Du hatari hapa nanuka kojo tu.Sometimes ndio maana naonaga baadhi ya abiria wanawekaga sula ya mbuzi kwa wamama wenye watoto kumbe huwa wanakimbia issue kama hizi.

Nashauri wamama wanaosafiri na watoto ambao hawana siti wachukue taadhari za usafi ikiwemo kuwavisha Diapers watoto wao ambao bado hawajajitambua na kuwa na zana za usafi kuepuka kero kwa abiria wenzao.

Nashukuru Mungu tunaingia Dom usiku kama ingekuwa mchana kidume sijui aibu ningeficha wapi.

Usiku mwema.

ARTICLE.
 
Habari za Usiku Wadau,

Nipo kwenye bus mida hii natokea Dar naelekea Dom pembeni yangu yupo mdada mwenye mtoto mwenye kama miaka mitatu hivi.

Safari inaanza huyu mama nikampa hai hakuitikia kivile mi nikapotezea.

Tumefika maeneo ya kibaigwa huyu mwanae akawa kamlaza kidizaini fulani mtoto nikaona amelala vibaya na anaumia kiuno so nikaamua kutake trouble ya kumuinua na kumlaza kwangu huku akiengea kwa mama yake na miguu kwangu.

Safari imeenda mara dogo akawa akijipindua pindua ghafla nikaanza kuhisi ubaridi kama maji vile nimemwagiwa kumtoa yalabi nimeloa mkojo mapajani kwenye suruali yaani ghazabu fasta ikanipanda ila nikachili nikamwambia huyu Dada mwanao kanikojolea!

Huyu Dada mwenye mtoto kuona hivyo akaanza kujibalaguza samahani kaka , only that!Akamchua mtoto wake na kumpakata hata hajambadilisha nguo.

Nimeboreka hapa wwe acha tu sema sina cha kufanya na huyo dogo anaonekana mkubwa so sijuo kwa nini amenikojolea!

Ugentlemen leo umenitokea puani,Du hatari hapa nanuka kojo tu.Sometimes ndio maana naonaga baadhi ya abiria wanawekaga sula ya mbuzi kwa wamama wenye watoto kumbe huwa wanakimbia issue kama hizi.

Nashauri wamama wanaosafiri na watoto ambao hawana siti wachukue taadhari za usafi ikiwemo kuwavisha Diapers watoto wao ambao bado hawajajitambua na kuwa na zana za usafi kuepuka kero kwa abiria wenzao.

Nashukuru Mungu tunaingia Dom usiku kama ingekuwa mchana kidume sijui aibu ningeficha wapi.

Usiku mwema.

ARTICLE.
Chukua room kafanye revenge ya kumkojoLea huyo dada. .......unatakiwa ujilipe

Kwa wale mliosoma kitabu cha "the richest man in babelon
 
Mimi najiuliza kwa sauti, hivi huyo mama ana kosa gani kwenye haya yote?
1. We ndo ulimshobokea kumsalimia yeye akavunga
2. Ye alibeba mtoto wewe ndo ukakimbilia kumueka sawa na kuelekezea kengele ya mtoto upande wako.
Hivyo bas, yaeza kua hakumvisha mwanae pampers, but its your fault kuhangaika na mambo ya watu wengine.
Pole though, ukishuka shabiby, fasta rudi kama unaenda cbe hapo kwenye ofisi za allys znaangaliana na car wash. Piga maji then enjoy the city.
 
TATIZO UNAKIHEHERE ULITAKA UKAMLE MAMA WAWATU KIMASIHARA ILA VIMEKUTOKEA PUANI POLE SANA
.
.
.
"PESA ZETU TUNAKAZI NAZO"
 
Chukua room kafanye revenge ya kumkojoLea huyo dada. .......unatakiwa ujilipe

Kwa wale mliosoma kitabu cha "the richest man in babelon
Anaomekana amevulugwa fulani kama vile anachangamoto ya ndoa.Wacha nitulie tu hapa kama vile hakuna kilichotokea
 
Alimlaza mtoto kiaina kwa sababu(yawezekana)mtoto huwa akisinzia analiachia kojo.Weye uka-show some love!Ni baraka hiyo.Usifue hiyo nguo mwezi mzima.😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom