tusiinge mambo ya kigeni bali tutumie mazao yetu ya asili tutapunguza magonjwa mengi sana kwa kuwa nchi yetu imebarikiwa kila sehemu ina neema yake tuleni sana (Parachichi,Ndizi, machungwa,magimbi,zabibu, matango, tikitimaji,etc) yanapatikana pande zote za nchi
Mimi nilacha kunywa juice hizi muda mrefu sana.Ziliniongeza uzito sana mpaka zikanigharimu muda na pesa kuushusha uzito sana
Beveragemkuu mimi kwa sasa nakunywa maji tu, nina mwaka na miezi mitano tangia niache kutumia juice za makopo na soda, mkuu swali langu liko kwenye juce ya Rozela vipi hii juice ina faida zipi?
mi ni mnywaji mzuri wa juice za azam kuanzia leo napiga stop
Kitu chochote kikitengenezwa na kuwekwa ndani ya chupa ya plastiki au box kinakuwa hakiko salama ndugu.Mweeee!! Sasa mimi najiuliza hatuna kitengo cha kuangalia yote haya?? Kama zina madhara kwanini zinauzwa?? Ila si mbaya mwenye masikio na asikie...mimi nshajitoa huko..sio soda wala juice ni mwaka wa pili huu!!
Lakini naomba kujuzwa.. MziziMkavu na haya maji ya kilimanjaro sijui uhai nayo yakoje?? Ni salama kwa afya??
MziziMkavu ibarikiwe. naomba kujua faida ya juice ya ubuyu na ukwaju