Elections 2010 KITENDAWILI: Tegua au nipe Mji!

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Mimi: Kitendawili?
Jamii Forum: Tega.

Nitajie sekta moja, mfumo mmoja na ofisi moja ya umma inayofanya kazi yake kwa umakini. Iwe ni ile ambayo mtu yeyote, wa hali yoyote na kutoka popote, unaweza kwenda kupata huduma/haki yako bila kujuana na yoyote ukahudumiwa vizuri na kwa haraka na kuondoka katika Tanzania.

Mahakama? Polisi? Hospitali? Chuo Kikuu? Ofisi za ardhi? Tanesco? Idara ya Maji? Zima moto? Uhamiaji? Benki? Posta? Idara ya utumishi? Kitengo cha pensheni?TRA? Mortuary? Vizazi na Vifo? Air Tanzania? TTCL? Ewura? Wizara ya Elimu? Mkaguzi Mkuu wa Serikali? Mwanasheria Mkuu wa Serikali? Takukuru? Masjara za Halmashauri za Miji/Manispaa/Majiji na Wilaya? Ofisi ya Maafisa Tawala wa Wilaya na Mikoa? Ofisi za CCM? Viwango na Leseni? TBS? Dahaco? Wizara ya Afisa? Vibali vya matibabu nje? Mambo ya nje? Ofisi za balozi zetu nje? TIC? Sumatra? Interpol? Idara ya Usalama wa Taifa? Ikulu? Tume ya Haki za Binadamu?n.k

Nitajie moja na ukiipata nitadhamini confidentail undercover investigation kuhakiki chaguo lako.
 
Mmhh! Mkuu umefikiria mbali sana. Yawezekana kweli haipo miongoni mwa zote ulizozitaja.
=====

Kama haipo, sasa hawa wagombea wanaomwaga ahadi bila kuzingatia hali hii wana hakika gani kuwa ahadi zao zitatekelezwa? Mbona ufanisi wa serikali yoyote hugemea sana ofisi zake za ndani kuwa nidhamu na uadilifu katika utendaji? Believe me, hakuna mwanasiasa anayeweza kuleta mabadiliko ya kweli katika Tanzania, kama hajashughulikia paralysis ya serikali ya ofisi za serikali. Utajengaje daraja kama mhandisi wa Mkoa inabidi ahongwe na wakandarasi ili aweze kuwaelekeza namna ya kuomba tenda?
 
Kufanya kazi kwa makini hilo ni swala jipya kabisa ktk utamaduni wetu, kwani wengi wetu hatufahamu chombo makini kinapofanya kazi kwa ufanisi kinafanya vipi tofauti na tunavyoona..
 
Niliwahi kukutana na taasisi moja ambayo kwa maoni yangu ndiyo inastahili kuwa role model katika Tanzania ingawa sina hakika kama bado inastahili. Hiyo ni mamlaka ya maji ya Mkoa wa Tanga. Jamaa walikuwa wanafanyakazi yao vizuri sana. Hata hivyo niliambiwa kuwa ilikuwa chini ya mradi wa wajerumani kabla ya kuachiwa Watanzania chini ya injinia mmoja ambaye alihamishiwa EWURA kama miaka 3 uliyopita. Ndio maana nasema sina hakika kama bado wanaendelea na ufanisi wao wa zamani.
 
Kufanya kazi kwa makini hilo ni swala jipya kabisa ktk utamaduni wetu, kwani wengi wetu hatufahamu chombo makini kinapofanya kazi kwa ufanisi kinafanya vipi tofauti na tunavyoona..[/QUOTE]

Hapo kwenye maandishi makubwa ya bluu, nitafurahi kama kila atakayesoma ujumbe huu, atapaelewa maana yake, hilo tu basi!
 
Mimi: Kitendawili?
Jamii Forum: Tega.

Nitajie sekta moja, mfumo mmoja na ofisi moja ya umma inayofanya kazi yake kwa umakini. Iwe ni ile ambayo mtu yeyote, wa hali yoyote na kutoka popote, unaweza kwenda kupata huduma/haki yako bila kujuana na yoyote ukahudumiwa vizuri na kwa haraka na kuondoka katika Tanzania.

Mahakama? Polisi? Hospitali? Chuo Kikuu? Ofisi za ardhi? Tanesco? Idara ya Maji? Zima moto? Uhamiaji? Benki? Posta? Idara ya utumishi? Kitengo cha pensheni?TRA? Mortuary? Vizazi na Vifo? Air Tanzania? TTCL? Ewura? Wizara ya Elimu? Mkaguzi Mkuu wa Serikali? Mwanasheria Mkuu wa Serikali? Takukuru? Masjara za Halmashauri za Miji/Manispaa/Majiji na Wilaya? Ofisi ya Maafisa Tawala wa Wilaya na Mikoa? Ofisi za CCM? Viwango na Leseni? TBS? Dahaco? Wizara ya Afisa? Vibali vya matibabu nje? Mambo ya nje? Ofisi za balozi zetu nje? TIC? Sumatra? Interpol? Idara ya Usalama wa Taifa? Ikulu? Tume ya Haki za Binadamu?n.k

Nitajie moja na ukiipata nitadhamini confidentail undercover investigation kuhakiki chaguo lako.
Mnyongaji wa SERIKALI (ndo jibu hilo)
 
taasisi ya utoaji na upokeaji wa rushwa :confused2:
=====
Kuna mtu kaniPM kuwa ofisi anayoijua kuwa iko makini na efficient ni Registry ya Mahakama ya Rufani pale DSM. Nasikia kuna vijana wachapa kazi bila kujali kama wanamjua mtu, ila umpokea kila afikaye na kumshughulikia kwa haraka. Tupeleleze.
 
Back
Top Bottom