Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,238
- 12,751
Muandishi: N. D. Yongolo, 1953
Unaweza kukisoma ndani ya maktaba app. TuPm Kuungwa.
1 WATOTO
2 MICHEZO NA DESTURI ZA WATOTO
3 NDOA
4 DINI NA IMANI YA WANYAMWEZI
5 SHERIA NA HAKI KATIKA NCHI
6 UCHAWI 417 MATUMIZI YA DAWA
8 HOFU NA MIIKO YA VIFO
9 MAMBO YA POMBE 6510 MAMBO YA URITHI
11 JINSI WALIVYOANZA KUBADILI MAISHAYAO KAMA TULIVYOJARIBU 7
WATOTO HUTENGWA katika mafungu mbalimbali yanayoonyesha kuzaliwa kwao jinsi kulivyotokea. Basi, hapa nitajaribu kueleza habari hizi za watoto kwa kufuata mafungu kama hivi:
Baada ya mtoto kutolewa nje, akiwa wa kiume, baba yake humtengenezea upinde mdogo pamoja na mshale mmoja, kusudi apelekwe kukabidhiwa kwenye baraza la wazee wa mji (kwibanza) pamoja na upinde wake kuwa alama ya silaha za kiume. Mama wa mtoto hupika ugali kwa kitoweo cha jogoo akapeleka kule kwenye baraza la wazee wa mji; pamoja na ugali huo hupelekwa na njugu mawe au karanga za maganda zilizookwa. Baada ya kwisha kula chakula, wazee wale huchukua karanga moja moja na kila mmoja humvunjia mtoto sikioni pake. Kwa Kinyamwezi tunaita 'bupatula matwi'; kusudi lake ni kumwonya mtoto yule akue mwenye kusikia barabara. Hali kadhalika akiwa wa kike, hufuatwa kawaida ya mtoto wa kiume, isipokuwa yeye hupelekwa kwenye baraza la mabibi wa mji. Lakini si lazima kupata jogoo bali nyama ya aina yo yote hufaa tu, isipokuwa karanga lazima ziwepo. Mtoto hawezi kunyolewa nywele zake (ikiwa mimba yake ilianzia kwa dawa au tambiko) mpaka mama yake apike pombe ya kunyolewa nywele. Kila mara mama wa mtoto anyoapo nywele zake, lazima aachie fungu dogo la nywele kisogoni (‘kasunzu’) huwa alama ya uzazi.
(b) Kuzaa mapacha na mambo yawapasayo wazazi wao: Kuzaa watoto mapacha ni jambo la kuogofya sana kwa kila mzazi, maana hupata taabu kubwa mno na shughuli huwa nyingi kuliko kuzaa mtoto mmoja wa kawaida. Mzalishaji wa watoto hawa huitwa ‘Kambula' na wa pili ‘Kiyola.' Wazalishaji kazi yao kuu ni kuzindika ili mapacha wale wasije wakaleta madhara yo yote kwa wazazi wao au kwa wengine wa mlango huo. Mara nyingi mapacha hawakuachwa waishi wote; kwa sababu hudhaniwa kuwa mapacha ni wachawi na hawapatani kuishi pamoja lakini lazima mmoja wao ashindwe. Pengine kwa bahati waliweza kuishi wote wawili na hapo huwa taabu kwa wazazi wao—atakufa baba au mama yao. Kwa ajili ya hofu hiyo wazazi hushawishiwa wachague bahati njema au mbaya, yaani pacha mmoja auawe kabla ya kukua; bila hivyo mmoja wao wenyewe atakufa! Kwa ujinga wa wazazi wengi walichagua kumwua mtoto mmoja na kumwacha mmoja aishi.
Mambo yawapasayo wazazi wa mapacha: Haifuatwi taratibu kama ile ya watoto wa kawaida, bali siku ile ile watoto hutolewa nje na huitwa majina. Maana kuna majina ya peke yao. Mkubwa huitwa ‘Mutunda' na 'Doto' au pengine ‘Kulwa na Mpasa.' Tangu siku hiyo ya kuzaa wazazi husumbuliwa sana kwa kutukanwa na mtu ye yote wala hawakasiriki. Kwa sababu husemwa kuwa ati wasipofanywa hivyo balaa litawaandama daima; kufanywa vile hulifukuza balaa. Baba watoto hulazimika atafute kiasi cha Shs. 10/-, ada ya kuombea ngoma kwa mtemi au kwa chini ya mtemi; ngoma hiyo ni ya kuchezea mabibi wazee (kusendela), pia huhitajiwa mbuzi mmoja kuwapa wazee wale. Wazazi hukaa bila kunyoa mpaka watakapopata Shs. 40/- (kusonga mabasa); pesa hizo huhitajiwa na mtemi au chini ya mtemi ili kupata idhini ya kunyoa. Hapa natumia kutaja fedha ya kisasa lakini yakupasa kukumbuka kuwa zamani fedha hizo hazikuwapo; hivyo basi, walitumia simbi, kauri au mifugo na kadhalika badala ya fedha. Waipatapo fedha hiyo hupika pombe, na siku hiyo huchezwa ngoma ya ajabu kwani nyimbo zinazoimbwa hapo hazikuwa nzuri ila ni nyimbo za matusi matupu. Nyimbo hizo huimbwa ovyo bila kumjali mtu, hata kama yupo mkwe, basi atukanwe tu. Juu ya mambo hayo hakuna aliyeweza kuchukizwa, maana shabaha yao ni kufukuza balaa kama nilivyokwisha eleza hapo juu. Wazee wale huchagua tungi moja la kutumiwa na wao wote (limuntonga) wa mji ule, wa kiume na wa kike. Wakati huo huinywa pombe ile kwa nyimbo mbaya mno. Hudhaniwa kuwa hapo kuna uchawi mwingi kati ya wazee na hupimana ili kuonyeshana ufundi wao.
Wazazi wa watoto walivumilia masumbufu yote bila kunung'unika; pia kule kutoa fedha yao hawakujali maana walikuwa na hofu sana kwamba wasipofanya hivyo hawatakuwa na baraka yo yote katika maisha yao. Pengine wakati wa kuzaliwa watoto hao, wote wawili walitoka wamekufa; hapo mambo yote niliyoyataja juu huendeshwa sawasawa kama kwa watoto wazima au pengine baada ya kukua; mmoja wao akifa (kubomba ipasa), wazazi pia walidaiwa shughuli ya kulipa fedha ya kumzikia. Kazi ya kuzika mapacha ni kazi ya wanawake. Watoto wachanga huzikwa ukingoni mwa bwawa lisilokauka maji yake. Maana ya kuwazika humo ni makusudi kuyapoza makali yake. Lakini mapacha wakifa wakubwa huzikwa penye jaa, ambalo husawazishwa sawasawa bila kuonekana kaburi. Yasemwa kuwa mapacha hao wakizikwa mahali pengine wakati wa masika mvua huwa ngumu, yaani hupaa, na vile vile radi zitakuwa nyingi zaidi. Baada ya kuzika, huombolezwa kwa ngoma na nyimbo.
(c) Kuzaa mtoto azaliwaye kwa kutanguliza miguu ‘Kasindye’: Kuzaa ‘Kasindye' kulikuwa hakuna tofauti kubwa kwa yule aliyezaa mapacha; tofauti iliyokuwapo ni kuzidiana juu ya gharama ya kuwalipa wakuu wa nchi. Hutakiwa kiasi cha Shs. 40/- kwa mambo yote. Kama nilivyoeleza hapo juu kwa ajili ya mapacha, shughuli zizo hizo huhitajiwa kwa ‘Kasindye' pia. Lakini afapo, hazikwi kama mapacha. Huzikwa kama kawaida isipokuwa baada ya kuzika, huombolezwa kwa ngoma na nyimbo kama siku ya kuzaliwa wanapofanya 'kusendela.'
(d) Mtoto Kigego (‘sinkula'): Mtoto huyu huzaliwa kama kawaida ya watoto wengine lakini hutokea bahati mbaya kwake aanzapo kuota meno, ya kwanza huanzia kuota juu. Watoto wenye hali hii mara nyingi hawakuachwa kuishi; bali waliweza kuuawa mara ile kwa idhini ya wazazi wao. Kwa bahati sana, labda kabla ya kuonwa na watu wengine, kuwa mtoto fulani kaanza kuota meno ya juu, wazazi wenyewe kwa kuwahi kumkagua mtoto mapema, walijitahidi kupata dawa za kuzuia meno yasijitokeze. Yasemwa kuwa Wakifaulu basi ni bahati yake kuishi. ingawa mtoto alipata bahati ya kuishi, lakini atakapokuwa mtu mzima, mara nyingi hawi na sudi njema kama watu wengine. Kwa nadra sana wengine husema kuwa kigego hutoka na meno yake ya juu. Husemwa kuwa mtoto wa namna hiyo ni hatari kubwa kuliko aotaye meno baada ya kuzaliwa. Siku hizi mambo haya ya vigego yamefifia, bali kwa mapacha na 'kasindye' wengi bado wanaendelea nayo.
Unaweza kukisoma ndani ya maktaba app. TuPm Kuungwa.
1 WATOTO
2 MICHEZO NA DESTURI ZA WATOTO
3 NDOA
4 DINI NA IMANI YA WANYAMWEZI
5 SHERIA NA HAKI KATIKA NCHI
6 UCHAWI 417 MATUMIZI YA DAWA
8 HOFU NA MIIKO YA VIFO
9 MAMBO YA POMBE 6510 MAMBO YA URITHI
11 JINSI WALIVYOANZA KUBADILI MAISHAYAO KAMA TULIVYOJARIBU 7
WATOTO HUTENGWA katika mafungu mbalimbali yanayoonyesha kuzaliwa kwao jinsi kulivyotokea. Basi, hapa nitajaribu kueleza habari hizi za watoto kwa kufuata mafungu kama hivi:
1. WATOTO
(a) Watoto wa kawaida na jinsi ya kuwapa majina: Mtoto ye yote wa kiume au wa kike azaliwapo, mzalishaji (nsimbya) wake hutoa sheria ya kutomtoa nje kabla ya kuanguka kitovu (tluila) lakini hungoja mpaka kitovu kimeanguka; asubuhi yake ndipo hutolewa nje kusudi aitwe jina kwani tangu siku aliyozaliwa alikuwa hajaitwa jina bado. Wakati wa kumtoa nje mzalishaji humchukua mtoto mikononi mwake; hapo mtoto hupewa jina na akina mama hushangilia kwa vigelegele. Kuita majina hufuata sheria mbalimbali. Huitwa jina la babu au la bibi yake akiwa msichana; pengine mzalishaji wake humwita kwa jina lake au la wazazi wake. Lakini huenda mimba ya mtoto huyo ilikuwa ya udhia, baada ya kuzaliwa mtoto huitwa jina kulifuata jambo lililotokea kabla ya kuzaliwa kwake. Hupewa majina mojawapo la haya Maganga (mimba ya dawa) Misambwa (tambiko) Kalamata (kung'ang'ania) na kadhalika. Iwapo baba au mama akifa baada ya kuzaliwa mtoto huitwa 'Mulekwa ' au 'Kalekwa ' (yaani kaachwa au aliyeachwa). Kabla ya kumtoa mtoto nje, huwapo sheria pia humo ndani (mukinyumba), yaani takataka zote zinazofagiwa humo ndani hukusanywa pamoja na kinyesi cha mtoto na kuachwa mumo humo ndani mpaka siku ya kutoka mtoto nje ndipo takataka zote hutupwa. Hufikiri kuwa ni vibaya mno takataka zikimtangulia mtoto kutoka nje; ni hatari ya kufa.Baada ya mtoto kutolewa nje, akiwa wa kiume, baba yake humtengenezea upinde mdogo pamoja na mshale mmoja, kusudi apelekwe kukabidhiwa kwenye baraza la wazee wa mji (kwibanza) pamoja na upinde wake kuwa alama ya silaha za kiume. Mama wa mtoto hupika ugali kwa kitoweo cha jogoo akapeleka kule kwenye baraza la wazee wa mji; pamoja na ugali huo hupelekwa na njugu mawe au karanga za maganda zilizookwa. Baada ya kwisha kula chakula, wazee wale huchukua karanga moja moja na kila mmoja humvunjia mtoto sikioni pake. Kwa Kinyamwezi tunaita 'bupatula matwi'; kusudi lake ni kumwonya mtoto yule akue mwenye kusikia barabara. Hali kadhalika akiwa wa kike, hufuatwa kawaida ya mtoto wa kiume, isipokuwa yeye hupelekwa kwenye baraza la mabibi wa mji. Lakini si lazima kupata jogoo bali nyama ya aina yo yote hufaa tu, isipokuwa karanga lazima ziwepo. Mtoto hawezi kunyolewa nywele zake (ikiwa mimba yake ilianzia kwa dawa au tambiko) mpaka mama yake apike pombe ya kunyolewa nywele. Kila mara mama wa mtoto anyoapo nywele zake, lazima aachie fungu dogo la nywele kisogoni (‘kasunzu’) huwa alama ya uzazi.