Kitabu kipya: ''Juhudi na Changamoto'' - kalamu ya Sheikh Ponda Issa Ponda

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
KITABU KIPYA "JUHUDI NA CHANGAMOTO" KALAMU YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA

Sheikh Ponda Issa Ponda ameandika kitabu.

Mwaka ni 1998 niko ndani ya basi la Raha Leo natokea Tanga. Karibu Maghrib inaingia basi linakaribia Msikiti wa Mwembechai.

Msikiti huu ulivamiwa na askari wakakata umeme wakaingia ndani na kupiga mabomu ya machozi na baadhi ya Waislam waliokuwa ndani ya msikiti wakakamatwa na kupigwa.

Umma mzima wa Waislam ulikuwa katika huzuni.

Nikaamua nishuke hapo Mwembechai angalau nisali Maghrib hapo na kwa kitendo hiki changu iwe kama vile nimefika hapo msikitini kuwahani ndugu zangu na kutoa pole.

Msikiti wa Mwembechai ulikuwa umefikwa na makubwa. Waislam mitaani wakawa wanauliza, "Wako wapi viongozi wa Waislam?"

Nimeingia msikitini kusali. Msikiti umejaa.

Yaliyowafika Waislam hayakuwavunja nguvu. Yale yakawa kama vile ni kichocheo kwao kumwelekea Allah zaidi. Msikiti umejaa pomoni.

Niko safu za nyuma wala Imam simuoni. Kutoka safu niliyokuwa nimesimama naisikia sauti ya Sheikh Ponda anasalisha na nakijua kiraa chake.

Mashaallah utapenda kumsikiliza akisoma. Kachagua sura mnasaba na hali iliyokuwa inawakabili Waislam wa Tanzania wakati ule.

Allah anazungumza na Waislam wanaosimama bega kwa bega kuipigania dini yake kwa nafsi zao na mali zao...

Maneno ya Allah ya kuwatia moyo Waislam na jinsi Sheikh Ponda alivyokuwa anaisoma Qur'an kwa taratibu na upole nasikia baadhi ya maamuma wanalia ndani ya sala, machozi yanawatoka.

Maneno ya Allah yamefika panapotakiwa.

Naondoka Msikiti wa Mwembechai baada ya sala ya Maghrib fikra nyingi zinanipitikia.

"Wako wapi viongozi wa Waislam?"

Waislam wanauliza hadi ifikie watu kupigwa ndani ya misikiti na isiwe lolote?

Kile kitendo cha umma wa Waislam kusali nyuma ya Sheikh Ponda wakaisikiza Qur'an ndali ya sala na kumsujudia Allah nyuma yake kwangu mimi ile ilikuwa bishara tosha.

Nilihisi Sheikh Ponda In Shaa Allah iko siku atawaongoza Waislam kwa mengi.

Toka siku ile Sheikh Ponda amesimama na Waislam katika kila lililowafika na Waislam wamemkubali kama kiongozi wao.

Sheikh Ponda hakusimama kusema, ''Nichagueni.''

Katika kitabu hiki Sheikh Ponda ameeleza tatizo la udini linalokabili Tanzania, tatizo ambalo serikali inaliogopa kukubali kuwa lipo na waathirika ni Waislam.

Serikali inajua hatari ya dhulma lakini wanaamini tatizo hili litajiondoa lenyewe.

Hofu ya kutaka tatizo litambulike fikra hii linatisha serikali yenyewe kwani athari yake itafika mbali sana iwapo itakubalika kuwa lipo tatizo na linahitaji ufumbuzi.

Kupitia matukio tofauti na kupitia maisha yake mwenyewe Sheikh Ponda, msomaji atasoma na kuiona kwa ushahidi dhulma iloyojijenga dhidi ya Waislam nchini bila kificho toka uhuru wa Tanganyika upatikane mwaka wa 1961.

Katika kitabu hiki, ''Juhudi na Changamoto,'' Sheikh Ponda anamchukua msomaji kutoka tatizo moja hadi lingine kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Sheikh Ponda hakika kaifanyia nchi yetu hisani kubwa kwa kuandika kitabu hiki.

1661711083148.png
 
Udini kwenye nini?

Raisi wa sasa ni Muislamu tena ana mamlaka makubwa mno kwa katiba ya Tanzania.

Raisi muislamu ndiye mwenyekiti wa Chama , Raisi anakaimiwa na muislamu mwenzake kwenye chama.

Matajiri wakubwa wote wenye nguvu kubwa kuanzia Bakhressa, Gsm , Mo , na wengineo wote waislamu.

Wasanii wakubwa Diamond , Ally Kiba , Harmonize wote waislamu.

Au watu wote waache imani zao wawasikilize nyie peke yenu as if dini ipo moja tu hii nchi!

Kila siku kulialia bila facts zozote.
 
Kwakweli Mimi si mnunuzi wa vitabu ila Kwa Sheikh Ponda nitanunuwa kitabu chake, tujuze kinapatikana duka lipi.

Huyu ndio kiongozi pekee wa waislamu ninayemuelewa vizuri, mwanzo sikumuelewa lakini Sasa namuelewa vizuri.
 
Udini kwenye nini ?

Raisi wa sasa ni Muislamu tena ana mamlaka makubwa mno kwa katiba ya Tanzania.

Raisi muislamu ndiye mwenyekiti wa Chama , Raisi anakaimiwa na muislamu mwenzake kwenye chama .

Matajiri wakubwa wote wenye nguvu kubwa kuanzia Bakhressa, Gsm , Mo , na wengineo wote waislamu.

Wasanii wakubwa Diamond , Ally Kiba , Harmonize wote waislamu.

Huwa mnataka kitu gani zaidi ili muache kulialia mambo ya kipuuuzi na kipumbavu! (wewe na wabaguzi wenzako )

Au watu wote waache imani zao wawasikilize nyie peke yenu as if dini ipo moja tu hii nchi!

Kila siku kulialia bila facts zozote .
Randy...
Tunaweza tukafanya mjadala mzuri ikiwa tutatumia lugha nzuri zenye adabu.

Lakini lugha mfano wa "lialia," tutakaribisha wachangiaji hodari wasiokuwa na adabu.

Nasema haya kutokana na uzoefu.
 
Kwakweli Mimi si mnunuzi wa vitabu ila Kwa Sheikh Ponda nitanunuwa kitabu chake, tujuze kinapatikana duka lipi.

Huyu ndio kiongozi pekee wa waislamu ninayemuelewa vizuri, mwanzo sikumuelewa lakini Sasa namuelewa vizuri.
Matola,
Uzinduzi wa kitabu ni Jumapili September 4 Peacock Hotel.

Baada ya uzinduzi itajulikana wapi vitabu vitapatikana.

Bei ni shs: 15,000.00.
 
Randy...
Tunaweza tukafanya mjadala mzuri ikiwa tutatumia lugha nzuri zenye adabu.

Lakini lugha mfano wa "lialia," tutakaribisha wachangiaji hodari wasiokuwa na adabu.

Nasema haya kutokana na uzoefu.
Tuassume sijaandika hilo neno 'lia lia'.

Niambie udini ni upi hapo na uraisi mnao nyie !
 
Sawa mzee.

Nakutaka radhi mzee wangu.

Naomba uniambie udini upo sehemu gani.
Randy...
Nimekuwia radhi.
Ikiwa kweli uko ''serious'' kutaka kulijua somo hili ninacho kuomba ni uwe na subra ya kunisikiliza na kwa kuanzia ili uniamini kuwa nimetafiti vya kutosha nigependa kukupa CV yangu:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  5. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  6. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  8. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
  9. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  10. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
  11. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
  12. Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam
  13. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  24. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
Awards: Several Awards
Visiting Scholar: (2011)
University of Iowa, Iowa City, USA
Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED
Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
Hao aliowaweka kwenye picha, askari magereza, aliomba ruhusa yao picha zao ziwekwe hapo? nao ni waandishi wenzake? halafu, ponda ndio mdini namba moja hapa nchini na siku zote huwa anatamani kuhatarisha amani ya nchi hii kwa maslahi ya kupigania dini. kwa kifupi anatamani nchi hii iwe ya kiislam, muishi mkijua kwamba, sisi wengine hata nchi hii iwe saudi arabia, hatutabadili dini, sisi ni wakristo though tunapenda na tunakubali kuishi na dini zingine kwa amani na hatuhitaji vurugu. nchi hii ni secular, haina dini serikalini ila mioyoni mwa watu.

Lakini hata akili zenu tu zifunguke siko ingine. kweli mtu anaibuka kwamba muipiganie dini? mumpiganie allah? kwani allah hana nguvu hadi ahitaji mwanadamu ampiganie? allah au dini hiyo sio imara kuweza kujiteetea yenyewe? inahitaji nguvu au msaada wa wanadamu? kwanini asijipiganie mwenyewe? huyu mungu ana yehitaji msaada wa mwanadamu ndiye wa kumwamini na kusikiliza kweli?

Ninajua huyo sio Mungu wa Israel aliyeumba mbingu na nchi. ni mungu mwingine kabisa siye na mbingu ya kupeleka watenda mema na ni mungu wa dunia hii, ibilisi na shetani. Ndio maana siku zote mnahubiri kuua, kupigana maovi maovu kwasababu ha yo ndiyo fungu lenu.
 
KITABU KIPYA "JUHUDI NA CHANGAMOTO" KALAMU YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA

Sheikh Ponda Issa Ponda ameandika kitabu.

Mwaka ni 1998 niko ndani ya basi la Raha Leo natokea Tanga.
Karibu Maghrib inaingia basi linakaribia Msikiti wa Mwembechai.

Msikiti huu ulivamiwa na askari wakakata umeme wakaingia ndani na kupiga mabomu ya machozi na baadhi ya Waislam waliokuwa ndani ya msikiti wakakamatwa na kupigwa.

Umma mzima wa Waislam ulikuwa katika huzuni.

Nikaamua nishuke hapo Mwembechai angalau nisali Maghrib hapo na kwa kitendo hiki changu iwe kama vile nimefika hapo msikitini kuwahani ndugu zangu na kutoa pole.

Msikiti wa Mwembechai ulikuwa umefikwa na makubwa.

Waislam mitaani wakawa wanauliza, "Wako wapi viongozi wa Waislam?"
Nimeingia msikitini kusali.

Msikiti umejaa.

Yaliyowafika Waislam hayakuwavunja nguvu.

Yale yakawa kama vile ni kichocheo kwao kumwelekea Allah zaidi.
Msikiti umejaa pomoni.

Niko safu za nyuma wala Imam simuoni.

Kutoka safu niliyokuwa nimesimama naisikia sauti ya Sheikh Ponda anasalisha na nakijua kiraa chake.

Mashaallah utapenda kumsikiliza akisoma.

Kachagua sura mnasaba na hali iliyokuwa inawakabili Waislam wa Tanzania wakati ule.

Allah anazungumza na Waislam wanaosimama bega kwa bega kuipigania dini yake kwa nafsi zao na mali zao...

Maneno ya Allah ya kuwatia moyo Waislam na jinsi Sheikh Ponda alivyokuwa anaisoma Qur'an kwa taratibu na upole nasikia baadhi ya maamuma wanalia ndani ya sala, machozi yanawatoka.

Maneno ya Allah yamefika panapotakiwa.

Naondoka Msikiti wa Mwembechai baada ya sala ya Maghrib fikra nyingi zinanipitikia.

"Wako wapi viongozi wa Waislam?"

Waislam wanauliza hadi ifikie watu kupigwa ndani ya misikiti na isiwe lolote?

Kile kitendo cha umma wa Waislam kusali nyuma ya Sheikh Ponda wakaisikiza Qur'an ndali ya sala na kumsujudia Allah nyuma yake kwangu mimi ile ilikuwa bishara tosha.

Nilihisi Sheikh Ponda In Shaa Allah iko siku atawaongoza Waislam kwa mengi.

Toka siku ile Sheikh Ponda amesimama na Waislam katika kila lililowafika na Waislam wamemkubali kama kiongozi wao.

Sheikh Ponda hakusimama kusema, ''Nichagueni.''

Katika kitabu hiki Sheikh Ponda ameeleza tatizo la udini linalokabili Tanzania, tatizo ambalo serikali inaliogopa kukubali kuwa lipo na waathirika ni Waislam.

Serikali inajua hatari ya dhulma lakini wanaamini tatizo hili litajiondoa lenyewe.

Hofu ya kutaka tatizo litambulike fikra hii linatisha serikali yenyewe kwani athari yake itafika mbali sana iwapo itakubalika kuwa lipo tatizo na linahitaji ufumbuzi.

Kupitia matukio tofauti na kupitia maisha yake mwenyewe Sheikh Ponda, msomaji atasoma na kuiona kwa ushahidi dhulma iloyojijenga dhidi ya Waislam nchini bila kificho toka uhuru wa Tanganyika upatikane mwaka wa 1961.

Katika kitabu hiki, ''Juhudi na Changamoto,'' Sheikh Ponda anamchukua msomaji kutoka tatizo moja hadi lingine kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Sheikh Ponda hakika kaifanyia nchi yetu hisani kubwa kwa kuandika kitabu hiki.

View attachment 2337762
Tuliweka hapa habari hii juzi ila Watukufu wakubwa wakaifutilia mbali
 
hao aliowaweka kwenye picha, askari magereza, aliomba ruhusa yao picha zao ziwekwe hapo? nao ni waandishi wenzake? halafu, ponda ndio mdini namba moja hapa nchini na siku zote huwa anatamani kuhatarisha amani ya nchi hii kwa maslahi ya kupigania dini. kwa kifupi anatamani nchi hii iwe ya kiislam, muishi mkijua kwamba, sisi wengine hata nchi hii iwe saudi arabia, hatutabadili dini, sisi ni wakristo though tunapenda na tunakubali kuishi na dini zingine kwa amani na hatuhitaji vurugu. nchi hii ni secular, haina dini serikalini ila mioyoni mwa watu.

lakini hata akili zenu tu zifunguke siko ingine. kweli mtu anaibuka kwamba muipiganie dini? mumpiganie allah? kwani allah hana nguvu hadi ahitaji mwanadamu ampiganie? allah au dini hiyo sio imara kuweza kujiteetea yenyewe? inahitaji nguvu au msaada wa wanadamu? kwanini asijipiganie mwenyewe? huyu mungu ana yehitaji msaada wa mwanadamu ndiye wa kumwamini na kusikiliza kweli?

ninajua huyo sio Mungu wa Israel aliyeumba mbingu na nchi. ni mungu mwingine kabisa siye na mbingu ya kupeleka watenda mema na ni mungu wa dunia hii, ibilisi na shetani. ndio maana siku zote mnahubiri kuua, kupigana maovi maovu kwasababu ha yo ndiyo fungu lenu.

Tuliweka hapa habari hii juzi ila Watukufu wakubwa wakaifutilia mbali
Eryth...
Imefutwa ipi ni post ambayo mimi nimeweka?
KITABU KIPYA "JUHUDI NA CHANGAMOTO" KALAMU YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA
''Sheikh Ponda Issa Ponda ameandika kitabu.
Mwaka ni 1998 niko ndani ya basi la Raha Leo natokea Tanga.
Karibu Maghrib inaingia basi linakaribia Msikiti wa Mwembechai.
Msikiti huu ulivamiwa na askari wakakata umeme wakaingia ndani na kupiga mabomu ya machozi na baadhi ya Waislam waliokuwa ndani ya msikiti wakakamatwa na kupigwa.
Umma mzima wa Waislam ulikuwa katika huzuni.''
 
Ustadhat Samia hawezi kusaidia kuondoa hilo la udini?
JS...
Si suala la Samia.
Hili ni suala la sisi wananchi kwanza tukubali kuwa lipo tatizo na tuiambie serikali kuwa iangalie tatizo hili kuepusha maafa ambayo huenda yakatokea huko baadae.

Pa kuanzia ni hapo.
Hili suala nyeti na linaogopwa sana.
 
Randy...
Nimekuwia radhi.
Ikiwa kweli uko ''serious'' kutaka kulijua somo hili ninacho kuomba ni uwe na subra ya kunisikiliza na kwa kuanzia ili uniamini kuwa nimetafiti vya kutosha nigependa kukupa CV yangu:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  5. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  6. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  8. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam
  9. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam
  10. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam
  11. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam
  12. Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam
  13. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  24. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
Awards: Several Awards
Visiting Scholar: (2011)
University of Iowa, Iowa City, USA
Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED
Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
Sawa nimeona.

Nasubiria unionyeshe huo udini mzee wangu.
 
Randy,
1929 hawa wafuatao waliunda African Association: Cecil Matola, Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Raikes Kusi, Rawtson Watts, Ali Said Mpima, Selemani Majisu na Zibe Kidasi.

Historia ya TANU ambayo chanzo chake ni AA walipokuja kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika majina haya hayamo.

Jiulize kwa nini majina ya wazalendo hawa yamefutwa?

1661942504216.jpeg

Mzee bin Sudi

KITABU KIPYA "JUHUDI NA CHANGAMOTO" KALAMU YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA

Sheikh Ponda Issa Ponda ameandika kitabu.

Mwaka ni 1998 niko ndani ya basi la Raha Leo natokea Tanga. Karibu Maghrib inaingia basi linakaribia Msikiti wa Mwembechai.

Msikiti huu ulivamiwa na askari wakakata umeme wakaingia ndani na kupiga mabomu ya machozi na baadhi ya Waislam waliokuwa ndani ya msikiti wakakamatwa na kupigwa.

Umma mzima wa Waislam ulikuwa katika huzuni.

Nikaamua nishuke hapo Mwembechai angalau nisali Maghrib hapo na kwa kitendo hiki changu iwe kama vile nimefika hapo msikitini kuwahani ndugu zangu na kutoa pole.

Msikiti wa Mwembechai ulikuwa umefikwa na makubwa. Waislam mitaani wakawa wanauliza, "Wako wapi viongozi wa Waislam?"

Nimeingia msikitini kusali. Msikiti umejaa.

Yaliyowafika Waislam hayakuwavunja nguvu. Yale yakawa kama vile ni kichocheo kwao kumwelekea Allah zaidi. Msikiti umejaa pomoni.

Niko safu za nyuma wala Imam simuoni. Kutoka safu niliyokuwa nimesimama naisikia sauti ya Sheikh Ponda anasalisha na nakijua kiraa chake.

Mashaallah utapenda kumsikiliza akisoma. Kachagua sura mnasaba na hali iliyokuwa inawakabili Waislam wa Tanzania wakati ule.

Allah anazungumza na Waislam wanaosimama bega kwa bega kuipigania dini yake kwa nafsi zao na mali zao...

Maneno ya Allah ya kuwatia moyo Waislam na jinsi Sheikh Ponda alivyokuwa anaisoma Qur'an kwa taratibu na upole nasikia baadhi ya maamuma wanalia ndani ya sala, machozi yanawatoka.

Maneno ya Allah yamefika panapotakiwa.

Naondoka Msikiti wa Mwembechai baada ya sala ya Maghrib fikra nyingi zinanipitikia.

"Wako wapi viongozi wa Waislam?"

Waislam wanauliza hadi ifikie watu kupigwa ndani ya misikiti na isiwe lolote?

Kile kitendo cha umma wa Waislam kusali nyuma ya Sheikh Ponda wakaisikiza Qur'an ndali ya sala na kumsujudia Allah nyuma yake kwangu mimi ile ilikuwa bishara tosha.

Nilihisi Sheikh Ponda In Shaa Allah iko siku atawaongoza Waislam kwa mengi.

Toka siku ile Sheikh Ponda amesimama na Waislam katika kila lililowafika na Waislam wamemkubali kama kiongozi wao.

Sheikh Ponda hakusimama kusema, ''Nichagueni.''

Katika kitabu hiki Sheikh Ponda ameeleza tatizo la udini linalokabili Tanzania, tatizo ambalo serikali inaliogopa kukubali kuwa lipo na waathirika ni Waislam.

Serikali inajua hatari ya dhulma lakini wanaamini tatizo hili litajiondoa lenyewe.

Hofu ya kutaka tatizo litambulike fikra hii linatisha serikali yenyewe kwani athari yake itafika mbali sana iwapo itakubalika kuwa lipo tatizo na linahitaji ufumbuzi.

Kupitia matukio tofauti na kupitia maisha yake mwenyewe Sheikh Ponda, msomaji atasoma na kuiona kwa ushahidi dhulma iloyojijenga dhidi ya Waislam nchini bila kificho toka uhuru wa Tanganyika upatikane mwaka wa 1961.

Katika kitabu hiki, ''Juhudi na Changamoto,'' Sheikh Ponda anamchukua msomaji kutoka tatizo moja hadi lingine kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Sheikh Ponda hakika kaifanyia nchi yetu hisani kubwa kwa kuandika kitabu hiki.

View attachment 2337762
Going for the jugular straight out of the gate.

Ukishaelewa kwamba hakuna Mungu na habari za kuwapo Allah ni hadithi za kutungwa na watu tu, haya matatizo na mafarakano yote ya dunia yata make sense. Utaelewa kwamba dunia ambayo haina Mungu wala Allah si ajabu kuwa na matatizo na mafarakano haya.

Ila, ukiamini kuna Mungu, muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote, halafu kaumba ulimwengu wenye kuweza kuwa na matatizo na mafarakano mengi kama huu, hiyo ni contradiction kubwa sana logically.

Contradiction hii inaonesha Mungu hayupo.

Habari tunazohadithiana kuhusu kuwepo kwa Mungu, dini, Uislamu, Ukristo etc, zote ni hadithi za kutungwa na watu tu, ama kujifariji kama coping mechanism, ama kudanganyana kwa makusudi ili tutawalane, ama uvivu na ujinga wa kutaka kwenda na mapikeo bila kuhoji.

Lakini Mungu hayupo. Allah hayupo.

Dini ni siasa za kale na tamaduni za enzi zilizovikwa utakatifu wa Mungu asiyethibitishika.
 
Kiranga,
Hakuna tatizo.
Allah katufunza Waislam anasema hakuna kulazimishana katika dini.

Kisha akatuonya akasema pale Allah anapofanyiwa istizai ondokeni.

Nimekueleza haya ili usishangae utakapoona nimekukalia kimya sikujibu.

Kuanzia hapa hutonisoma katika hili.

Umetukuka Allah Muumba wa mbingu na ardhi.
 
Huna cha kujibu kwa sababu huna hoja ya kimantiki ya kujibu, kwa sababu Allah hayupo.

Ukishaleta habari za Allah hapa, hujakaa kimya.

Kama unataka kukaa kimya kuhusu Allah, usizilete habari zake hapa JF.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom