Kitabu Gani uli-kisoma week hii?

Nimemaliza kusoma kitabu cha Jung Chang - Mao The Unknown Story. Kinaeleza unyama aliofanya Mao Tse Tung huko China na alivyopanda ngazi mpaka kuwa demi god aliyerudisha nyuma maendeleo ya China na kuua watu angalau milioni thelathini, muuaji aliyeua watu wengi kuliko mwingine yeyote duaniani. Katika wakati ambapo tunajadili muswada wa national security council kitabu hiki ni relevant sana kwani kinaonyesha madhara ya utamaduni wa mtu mmoja kuwa na madaraka makubwa sana.

Sasa hivi nasoma "Human Natures - Genes, Cultures and Human Prospect" cha Paul R. Ehrlich. Ndiyo kwanza nimeanza kukisoma. Dr. Jared Diamond, muandishi wa "Gun, Gems and Steel" amekisifia kwa kusema "The one book to read on human evolution" . So far nimeweza kuconfirm nilichokuwa nina suspect, kwamba ile dhana ya "miafika ndivyo tulivyo" which suggest that we are wired in a certain way i.e genetically, ni dhana potofu. Ningependa sana rafiki yangu Julius akisome hiki kitabu kinaweza kumsaidia.

check the review here http://www.fredbortz.com/review/HumanNatures.htm

A video of a discussion of the book by the author is at http://www.uctv.tv/search-details.aspx?showID=6892
 
1. "History of the Bukoba District" by Hans Cory, 1959, Lake Printing Works, Mwanza.
nimekuwa mpenzi wa kufahamu historia ya Tanzania, kwani ninadhani walimu wangu wa Historia shuleni hawakufanya kazi nzuri. Either curriculum ilikuwa mbovu au interest yangu kwenye somo ilikuwa ndogo. The latter could be as a result of the former. Kiufupi hiki kitabu ni cha muhimu kwani ni nadra sana kuweza kupata vitabu vinavyoelezea mila na desturi za watu aina fulani Tanzania. Siongelei PhD thesis kwani hizo zimekaa 'too academic' na upatikanaji wake ni mgumu, let alone, mwananchi wa kawaida kukielewa. Akina Hans Cory, John Iliffe, I Kimambo, T Rwehumbiza nk inabidi wapewe heko kwa kuweka historia ya watu wa nchi yetu katika maandishi.

2. "Outliers - the story of success" by Malcolm Gladwell, 2009, Hachette Book Group USA
Malcolm Gladwell ni mwandishi mwenye kipaji cha kuelezea matokea ya tafiti ya sayansi ya jamii kwa mwananchi wa kawaida 'layman'. Kitabu hiki na vingine vyake kama Blink, What the dog saw etc waweza kuviita ni vitabu vya 'pop-social science' kwani anaelezea 'phenomena' kadhaa zinazohusu jamii mfano katika kitabu hichi, anaongelea hasa kuhusu 'mafanikio'. Anaongelea kuhusu dhana ya vipaji, kwamba kipaji cha mtu sio kitu 'special' kwani kwa definition yake 'talent is the ability to practise, practise and more practise'. Anatoa mifano ya the Beatles, Bill Gates, Canadian Hockey teams etc. Anaelezea dhana hii kutolea mfano mstari wa Biblia ambao maarufu sasa kama "the Matthew Effect". Soma zaidi kuhusu hili hapa: [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Matthew_effect[/ame]

Pia anaelezea kuhusu jinsi gani mila za watu fulani zinaweza elezea tabia au matokeo kadhaa. Mfano wa ajali za ndege za Korean Air au Alama za juu za mitihani za wanafunzi wa kichina wanaojiunga na vyuo vya marekani n.k
tazama:
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=_yJ_mjeke58&feature=related"]YouTube- Fareed Zakaria CNN Malcolm Gladwell 2[/ame]

It is an entertaining read, and you should read it with an open mind.

Ninavipiga vyote in parallel. Moja nikiwa kwenye usafiri nikielekea/kutoka mzigoni (2) na kingine kabla ya kulala (1).
 
Kitabu cha orodha ya mafisadi wa elimu kimeandikwa na Kineirugaba Msemakweli nimemaliza kukisoma sasa hivi tu, kama hujakisoma kiafute.
 
John Gribbin's "Science: A History 1543-2001". A tour de force.
 
Nimesoma THe biggest secret,by davide icke kinaeleza jins secret society wanavyouhadaa ulimwengu,jins akina roschild wanavyozitawala nchi mbalimbali zinavyobambikiwa madeni,uwepo wa watu crossbreed ya mjusi,watu wenye upeo mkubwa ndo wanaoutawala ulimwengu,kumbe marekani pamoja na u super power wake bado ni koloni la uingereza mpaka leo
Nimesoma kitabu cha kiyosakiw why As student work for theCs student,ni kitabu kizur xn kinachokufanya usikate tamaa km huna elimu ya kutosha lakin uamin unawezakuwa tajiri na jinsi gani mitaala yetu inatufanya kuwa dormant financially na vingine vingi
 
Nimesoma THe biggest secret,by davide icke kinaeleza jins secret society wanavyouhadaa ulimwengu,jins akina roschild wanavyozitawala nchi mbalimbali zinavyobambikiwa madeni,uwepo wa watu crossbreed ya mjusi,watu wenye upeo mkubwa ndo wanaoutawala ulimwengu,kumbe marekani pamoja na u super power wake bado ni koloni la uingereza mpaka leo
Nimesoma kitabu cha kiyosakiw why As student work for theCs student,ni kitabu kizur xn kinachokufanya usikate tamaa km huna elimu ya kutosha lakin uamin unawezakuwa tajiri na jinsi gani mitaala yetu inatufanya kuwa dormant financially na vingine vingi
Japo sija wahi kuviona na kuvisoma lakini maelezo yako yame nivutia sana....
 
Back
Top Bottom