Kitabu cha ndoa yangu, ningejua

kautipe

Member
May 6, 2011
64
6
Samahani sana waungwana. Nimewahi kununua kitabu kimoja kiitwachwo -NDOA YANGU, NINGEJUA ambacho kwa hakika mtunzi alinisaidia sana kujua kwa nini ndoa nyingi za siku hizi hazina amani. Kutokana na ukweli ulioanikwa ndani ya kitabu hicho, nimekuwa nikikitumia sana kuwasaidia watu wengi hususan vijana wanaotaka kuingia katika mambo ya ndoa, na pia kuwasaidia wale wote wanaokuja kwangu wakiwa na matatizo ya ndoa. Nikiri kwamba, wengi wamenufaika sana. Tatizo langu ni kwamba, kitabu hiki kiliazimwa na rafiki yangu ambaye ametokomea nacho mikoani. Naomba mnisaidie kwa wale ambao mmewahi kukisoma wapi kinapatikana, maana kwa hapa Mwanza nimezunguka sana sijakiona!
 
Back
Top Bottom