KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Waheshimiwa, naomba tafsiri ya Kiswahili ya neno 'digital' kama linavyotumika kuelezea aina za teknolojia katika Kiingereza.
Ahsante.


SteveD.
 
Wa dungu, kweli hamna anayelijua hili... basi subiri mimi nitunge tu neno jipya la Kiswahili kuwakilisha 'digital'. nitaliweka hapa si punde.. :)

SteveD.
 
Watanzania wenzangu,

Kuanzia leo, napenda kuwatangazia kuwa neno 'digital' kama litumikavyo kwenye lugha ya Kiingereza katika maswala ya teknolojia, tafsiri yake ya Kiswahili ni 'puru'.

Ifuatayo ni unyambulishaji wa neno hilo kweny matumizi katika Kiingereza na tafsiri yake kwa kiswahili.

--digital world : ulimwengu wa puru

--digitalisation : upurukushaji

--digitalised : imepurushika

--digital : puru

--digitally : kipuru


Wahakiki wa Kiswahili na BAKWATA, naomba kutoa hoja.

Shukrani.

SteveD.
 
Upurukushaji ni kumshitua mtu na kumfanya atoke mbio


Purusha = digitize
Purushika = digitized
puruisha = digitilization/digitalizing
kipurushi = digitally/digital accessory/digital mechanism


Naomba kuongezea hoja:
 
Watanzania wenzangu,

Kuanzia leo, napenda kuwatangazia kuwa neno 'digital' kama litumikavyo kwenye lugha ya Kiingereza katika maswala ya teknolojia, tafsiri yake ya Kiswahili ni 'puru'.

Ifuatayo ni unyambulishaji wa neno hilo kweny matumizi katika Kiingereza na tafsiri yake kwa kiswahili.

--digital world : ulimwengu wa puru

--digitalisation : upurukushaji

--digitalised : imepurushika

--digital : puru

--digitally : kipuru


Wahakiki wa Kiswahili na BAKWATA, naomba kutoa hoja.

Shukrani.

SteveD.
Mkuu nadhani hapo ulipitiwa, ni BAKITA (Baraza la Kiswahili la Taifa).
Nawasilisha!
 
Na neno digital kuwa ni tarakimu linatokana na ukweli kuwa technolojia ya digital inatumia number maalumu ziitwazo binary digits,yaani unapoandika maandishi yanageuzwa katika mfumo wa 0 1010101 ili yaweze kusafiri kwenda upande mwingine.Rejea herufi za html online.
 
Huwezi kuwa na tafsiri ya neno "Digital" bila ya kuwa na tasfiri ya neno "analog."

Je "analog" inatafsirijwe kwa kiswahili?
 
Huwezi kuwa na tafsiri ya neno "Digital" bila ya kuwa na tasfiri ya neno "analog."

Je "analog" inatafsirijwe kwa kiswahili?

Duuh, jambo limezua jambo.... tusaidiane ndugu zangu tuwe na tafsiri ya maneno haya...

Mkuu nadhani hapo ulipitiwa, ni BAKITA (Baraza la Kiswahili la Taifa).
Nawasilisha!

IDIMI, ahsante kwa kunisahihisha kuhusu BAKITA.

Na neno digital kuwa ni tarakimu linatokana na ukweli kuwa technolojia ya digital inatumia number maalumu ziitwazo binary digits,yaani unapoandika maandishi yanageuzwa katika mfumo wa 0 1010101 ili yaweze kusafiri kwenda upande mwingine.Rejea herufi za html online.

Augustoons, Ahsante kwa ufafanuzi wako. Labda tuendelee tu kuuliza zaidi kama unaweza kutusaidia:
Naomba tafsiri ya Kiswahili kama ipo ya maneno yafuatayo yahusianayo na computing (ukokotoshaji):

Analog,
Boolean Algebra (boolean logic),
Logic gate,
Microchip,
Integer data,
Vector,
Electronics,
Digital electronics,
Function (mathematical function),
Boolean function,
BIT,
Byte,
Variables (as in programming)
Binary numbers,
Octal numbers,
hexadecimal numbers,

Ahasnte.

SteveD.
 
Asante Mkuu
Du sasa hiki tena kibarua kigumu,lakini nitakupa baadhi lakini kwanza nikupe shule.Kanuni ya kiisimu ya ubatizaji majina inasema kwamba jina la kitu latokana aidha na matumizi ya kitu hicho, asili yake ama mvumbuzi wake ama matokeo ya kitu chenyewe ama ufananishi ama utohoaji. Mathalani ili upate tafisri nzuri ya maneno ya kisayansi ni lazima kumhusisha mwanasayansi mwenyewe na kumuuliza kwanini amekiita au wanakiita kitu hicho hivyo na wanakitumiaje.Vivyo hivyo maneno ya kisheria kwani neno hilohilo unalolijua kwa kiingereza mathalani "consideration" kisheria halimaanishi tafakari bali linamaanisha lipio.Kwa mantiki hiyo ifuatayo yaweza kuwa tafsiri ya maneno haya hapa chini hapo yaweza kuwa sio hitimishi na ndio sababu umeyaweka hapa ili wengine nao wachangie
Analog-Mfuatano hivyo analog technology ni teknologia ambayo taarifa zinatumwa kwa mfuatano fulani ambao kama chombo kimoja au herufi moja inakosewa basi mfumo mzima haufanyi kazi
Logic gate-Kizingitimantiki
Microchip-Kipandesakiti
Electronics- a kiumeme
Digital electronic-tarakimu za kiumeme/kieletroniki
Function-Kanuni
Boolean function-kanuni ya Boolean. Huyu Boole ni mvumbuzi wa hiyo kanuni
Binary number-Tarakimu au numerali ambatani za 0 na 1
Bit-yaweza kuwa kiwango au kipimo
Octal number-Namba nane
hexadecimal number-namba yenye decimali nane
variable-kibadala,kitu kinachobadilika badilika
Ahsante
 
Mrengo wa kulia kwa kiingereza extreme left-maaana yake ni msimamo wa siasa za mashariki au kulia(mathalani uliberali) wakati mrengo wa kushoto ni extreme left ambao ni msimamo wa nchi nyingi za magharibi zinazofuata ubepari lakini ukizungumzia siasa za uingereza una maana ukonzavativu au udemokrat
 
Ndugu, naomba mnipatie tafsiri au ufafanuzi wa neno 'thread' kwa kiswahili kama itumikavyo kwenye forum hii.

Je,neno jarida/daftari/ukurasa yanaweza kufaa kama tafsiri yake ya kiswahili?

Nyongeza; kwa sababu nauliza swali hii karibia na mwisho wa juma kuanza na kwenye shamlashamla za Eid, nawasihi basi kwa wale wepesiwepesi wa kuchombeza na maneno kuwa tayari nimeshafikiria neno 'kamba' na 'uzi' na nafikiri hayafai kuwakilisha neno thread kama litumikavyo kwenye forum hii. Ahsanteni.

SteveD.

Neno thread, km kitenzi (verb), linamaanisha pia tunga (to thread - kutunga). Kwa mfano, tunga uzi ktk sindano, au tunga shanga. K/hiyo, thread, km nomino (noun), linamaanisha mtungo. Kwa mfano, mtungo wa shanga.
Kwa kuwa mtungo (mmoja), km wa shanga, ni mfululizo wa vitu vingi kwa pamoja vilivyotungwa (km shanga nyingi kwa pamoja, ktk mfano wetu), basi new thread humaanisha mtungo mwingine/mpya, au mfululizo mwingine/mpya. Na km kunaongezwa kitu ktk mtungo (km kuongeza shanga kadhaa), basi kuongezwa huko tutakuita mwendelezo/muendelezo wa mtungo/mfululizo.
Hivyo ndivyo kadri nijuavyo.

Ndugu, SteveD, angalia maneno niliyoyawekea wino mwekundu hapo juu. Nadhani yangepaswa kuwa: karibu, shamrashamra, maneno.
 
Back
Top Bottom