Kiswahili: Kutoka kwa wakenya

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,881
Kuna mjadala ulikuwa unaendelea baina ya wakenya nami nilikuwa mfuatiliaji wa karibu. Hivi ndivyo mjadala ulivyoanzishwa na nikahisi ni somo kwa wengi!

Swahili name for resilience is ukakamavu.

Speaking of swahili,I have a challenge to all of us.
Maybe its a high time we as Kenyans cultivate more interest of this language.
It was only jana nilipokutana na mmarekani mmoja mweusi ambaye amejibatiza Otieno.Jamaa huyu ana uchu wa kijifunza Kiswahili.wazungu pia wanajikakamua kujifunza lugha 'yetu'.

Wenzangu, tuna raslimali muhimu, yaani lugha ya Kiswahili, lakini tumefumba macho jamani...

Pokeeni changa moto,mimi nikiwa mstari wa mbele kujikemea..
Ni aibu wala si ushupavu viongozi kufanya makosa ya kisarufi katika usemi wao.
Ni aibu kununua tu magazeti na majarida yaliyochapishwa kwa kiingereza.
Ni aibu kuzungumza kizungu pekee na kutupilia mbali Kiswahili sanifu.
Ni aibu kama wadau wenzangu kuwasiliana tu kwa Kiingereza.
Na ni aibu si haba kwamba ukidurusu maandishi yangu utajikwaa kwa makosa labda ya ngeli au uchaguzi wa nomino mwafaka.

Na ili tujue, ni makosa Kujibu Mzuri unaporejelea maamkio-niligundua (hivi majuzi tu)kwamba Kiswahili sanifu inatushurutisha kuitika Nzuri...kwa sababu ya uwiano wa kingeli baina ya Habari na jawabu lako..

Na haya chini ndiyo maoni ya baadhi ya waliochangia mpaka sasa:

Nakubaliana nawe.

Mbona tumetupilia mbali asili yetu - yaani lugha ya Kiswahili?

Mimi hutafsiri jarida fulani ambalo sisi huchapisha hapa Westlands. Mbona wageni kutoka nje wawe na ari sana ya kuijua lugha yetu, ilhali sisi hapa tumejitia hamnazo, kana kwamba sisi ni wageni?

Lahaula! haya basi, tuanze kwa kusoma gazeti liitwalo Taifa Leo, kisha tuingilie vitabu mbali mbali ambavyo vinaweza kupatikana katika maduka ya kuuza vitabu maalum hapa mjini.

Uwanja ni wenyu wadau wenzangu. Je, mtaipokea changamoto hii?

Sarah
ukweli mtupu,
shida iliyopo sasa hivi ni kwamba sheng imekita mizizi.
sijui tukiamua kuangamiza sheng tutaanzia wapi. Haiwezekani!
Labda tukubali sheng iwe lugha ya kiswahili ya kisasa, tusahau lugha sanifu.
English evolved from latin anyway.

Heshima zako Ndugu,

Maoni yangu ni kuwa hatuhitaji kuangamiza sheng au lugha yoyote ile, ndio maana tunakazana kuikita lugha Kiswahili. Chenye ningependekeza ni kuwa tuzidi kuikuza lugha ya Kiswahili kwa usanifu wake. Sheng inavutia kwa sababu ya kukosa nidhamu makhsusi ya kuisimamia na kuiendeleza ni kuendeleza kuashia wengine kama hatuwezi au hatutaki kutii sheria zozote za nidhamu za taaluma yoyote ile na uishi kwa ujumla basi tunaweza kupuuza hizo kanuni na kubugia raha ya utovu wa nidhamu.

Wasemaje?

Mwingine naye:

And now, Mwanzishaji, would you kindly say all that in English. I'd love to speak Kiswahili well but it is one language I have a problem with. Much like French and German. I can understand it but I am not one for heavy vocabulary like what I can see in your email.

HELP!!!

Mwingine akachangia hivi:

Come on!!! Kiswahili is too pedestrian for any serious person to use in holding a serious conversation!!!
Why do you think Jaramogi never even bothered to learn it?!

Na huyu akawa na maoni haya:

Dr ...., be a serious man. what do you mean too pedestrian? the fact that majority of us can't speak it does not mean that one cannot use it to hold a serious conversation. a big percentage of Kenyan population can only understand Kiswahili as opposed to English. then Daktari what you are saying is that your communication is limited to English speakers only, meaning you cannot reach majority of Keyans therefore you are mean with information. that is my take, do members agree with me?

Naye huyu akaona atie neno:

Kwa wanachama,

Nitarajio langu kuwa haya mazungumzo ya lugha ya Kiswhili ni muhumi sana wakati huu kuliko wakati mwingine. Kwa nini nasema hivyo? Kiswahili ni ligha ya Kitaifa na hata mataifa zaindi ya 125 zimeanza kutumia au kuhimiza watu wajifunze hii lugha.

Kwangu mimi naunga K'Ogutu mkono kuwa hii ni lugha ambayo inaeleweka na wengi hata serikali yetu imeanza kukienzi katika mambo rasmi. Kama fomu za kuchukua pasipoti sasa ziko kwa lugha mbili: Kiswahili na Kiiengereza. Na Daktari kusema kuwa hii ni ligha ya wanaotembea ni matusi kwa mwafrika na hasa Mkenya wa kawaida ambaye anakitumia kama njia yake ya mawasiliano kila siku.
Changamoto; tukienzi lugha na pia tukiuze kama lugha ya mawasiliano. Hata umoja wa mataifa inahitaji kukiorodhesha kama lugha moja ya mawasiliano. Kwa wale wanaosoma taifa leo, kulikuwa na makala jana kuhusu Afrika Mashariki yaweza kukipoteza lugha ya Kiswahili kwa mataifa ya magharibi. Kwa sababu wanakifunza na pia wamewachukua wahadhiri wa lugha ya Kiswahili na wanafunza katika vyuo vikuu.

Kama mwangaza wa jamii wacha tukiendeleze lugha hii yetu.

siku njema

Haikuishia hapo, huyu akiwa Dar es Salaam akatoa maoni hivi:

Habari wote!
"Hakuna nchi yoyote duniani isiyojivunia lugha yake, na maendeleo ya nchi yanawezekana zaidi pale ambapo luagha ya nchi hiyo inapotumika katika tafiti na uvumbuzi mbalimbali"
Tutake tusitake sisi watu wa afrika Mashariki hasa Tanzania tuna kila sababu ya kujivunia na kukienzi Kiswahili, acheni firkra potofu ya kutukuza lugha za mataifa mengine na kukashifu lugha zenu.
KISWAHILI HUTUUNGANISHA DAIMA
Mwingine akaendeleza mjadala hivi:

Kwenu wadau,

Mimi binafsi siwezi nikajidai kuwa mkwasi wa lugha ya kiswahili, lakini nakienzi lugha hichi. Na fursa kama hii inanijenga kimsamiati. kile nafahamu mimi ni kwamba lugha yoyote ile kinahitaji ubunifu wa maneno fulani au majina fulani. Hii ni sababu kwamba kuna uzinduzi wa mambo kila wakati." we are in a world of discoveries". majina au maneno fulani hayakwemo kwenye msamiati ya lugha zetu. Kwa mfano Komputa kwa Kijaluo

Mtanzania mwingine akatia neno:

Okay,
si kawaida yangu kujibu kwenye hizi forums, but dr ....., those are your views,
kwangu mimi na watanzania wenzangu wote, tunajivunia kuongea kiswahili kinachotuunganisha na makabila yote nchini na kujenga umoja wa kitaifa, kiswahili kinafundishwa mpaka chuo kikuu, hatuwezi kung'ang'ania lugha za pili, kiswahili kwetu ni heshima ni utaifa na umoja, sijui kwako...............
proud swahili speaker.

Mwingine toka Tanzania akakunwa akatoa maoni yake hivi:

Kwa kweli huu mjadala umenifanya hata mimi nitoe maoni yangu, ingawa si kawaida kufanya hivyo. Sisi watanzania tunajivunia lugha yetu ya taifa sana. Tanzania tuna makabila mengi sana na kila moja linazungumza lugha yake. Iwapo tusingekuwa na lugha ya taifa mawasiliano kati yetu yangekuwa magumu kwa namna moja au nyingine. Rafiki zangu wa West Africa wanatuonea wivu sana maana wao iwapo sio kabila moja inabidi wawasiliane kwa kiingereza au kifaransa!

Nawashauri ndugu zangu wa afrika mashariki tuendeleze lugha ya kiswahili na kujitahidi kuitumia.

Huyu naye hakuwa nyuma:

Sisi amepokea mtoto changa wenyu kuangaliana na mdomo ya Kiswahili.Anafurahi nyingi muno,kwa maongezo ya leo.

Kiswahili ndio kitukuzwe.... hapa nchini mwetu Kenya lilnalo adimu Kiswahili chetu ni lugha chipukizi mitaani kama vile sheng....Kando na hayo sisi tunalo ari ya kuitukuza lugha Kiswahili toka pwani hadi ninakotoka bara Kisumu.Tutajipa changa moto huu huu kudumisha ari yetu kama wazazi kuendeleza kiswahili sio tu kwa usemi bali kwa maandishi wa ufalsaha.

Kiswahili hoyeee......
Mwingine akahamasika akanena hivi:

Today, it is brick bats where I am concerned. Let me tell you one thing, wadau, challenge I have accepted. Karibuni, mutani sikia na kiswahili changu kiki ng'ara. Na haitakuwa sheng.

Na muwe na siku ya kuchangamuka!!! :))

Na huyu hakuwa nyuma akachangia hivi:

Kwa kweli hii kiswahili chetu yeye ni lugha mzuri sana. yeye amefurahisha mimi sana mithili ya huyu mvua ambaye ananyesha. Lakin huyu mvua wetu amenyeshea blanketi wangu!! wololo yaye!!!!

Hawakuishia hapo wakaendeleza wengine hivi:
Nanu:

Have always wanted to know the kiswahili word for "catch up with me".
May be i left you doing some tasks behind but we were to go to a
certain place together, what should i say to him or her in swahili?

Hujambo Nanu,

Utamwambia "tafadhali nipate... au nikute... au ungana nami..." itategemea muktadha wa utendi wenyewe.

Kwa mfano, kwa mchanjari wa hapo juu ni katika muktadha wa kuwa unaenda, unamusubiri na unamtarajia.

Furahia kuzungumza na kuitumia lugha ya kiswahili.

shukrani na ubarikiwe.

Huyu ni mpenzi wa ICT akadakia hivi:

Neno "facebook" limenipinga njenga! Hebu wasanii watutafsirie.
Kamau naye akachangia hivi katika kumjibu:

Naam katika ulimwengu wa teknolojia maneno mengi yatavumbuliwa na njia moja ya kuyatamka kutoka kimombo ni kuyatohoa au kuyatamka katika lugha chanzi.
Kwa uvumbuzi wa istilahai mwafaka wengi watasema tuwangoje Chimera na sheikh Nabahany watuundie istilahi na wengine kati yetu hawatakoma kusema tumuulize Swaleh Mdoe na Babuye.
Kwangu mimi “Facebook” nikitafsiri… kunradhi nikiiundia jina jipya nitapendekeza “Mtandaonyuso” kwani “Facebook” ni mtandao ambao watu hutukana na kujuana kwanamna ya picha za nyuso zao.

Nilikuwa napenda kuendelea lakini niishia hapa kwa kuwaomba wadau maoni yenu juu ya michango ya wenzetu hawa. Bahati mbaya wanatumia Mkundi wa Google hivyo mijadala mingi huwa naipata kwenye barua pepe. Kuna baadhi nimewaalika huenda tukawa nao hapa tukaona maoni yao zaidi.

Asiyeonekana!
 
Kwakweli hawa ndugu zetu wakenya wanafurahisha na kusikitisha sana wakiongea kiswahili. ukifika Nairobi utakuta hakuna mtu anajua kiingereza vizuri, hakuna anayejua kiswahili fasaha hivyo ni sheng yao tu ndo inatawala. hata hivyo wengi wanapenda kuongea kiswahili fasaha. Mimi wananionea wivu nikiongea kiswahili changu fresh.
 
Hili bandiko "liko juu" mzeya! Nimelifurahia mno.

Nimetamani ifanyike jitihada ya makusudi tuwe na mahusiano na forum nyingine hasa za nchi jirani. Kama ambavyo sote twafahamu, lugha ni kiungo na mhimili muhimu sana katika kudumisha umoja na kukuza uhusiano kwa maendeleo ya eneo husika. Ni mara chache raia wa Uganda kwa mfano akafuatilia siasa za Tanzania hata aje kwenye forum yetu. Je, tunaweza kuwavutia watu kutoka Rwanda, Kenya, Uganda.... kuja kushiriki nasi kwenye jukwaa la lugha ya Kiswahili?

Naomba kutoa pendekezo, kwamba tuwe na jukwaa maalumu la lugha, humo wajumbe washawishiwe kutumia lugha ya kiswahili pekee. Na kwenye jukwaa hilo msisitizo uwe kwenye kuzungumza lugha ya kiswahili sanifu kwa ufasaha.

Ukiishi au kuvungukwa na watu wasiojua vizuri kiingereza, nawe kiingereza chako kitakuwa kibovu. Tuamshe ari hata ifike mahala watu waanze kununua vitabu vya kiswahili na kujisomea.

Tuwavutie wengi walio wapenzi wa lugha hii. Jionee mijadala inayoendelea kwenye Kamusi Project - Karibu tuzungumze.

Tusibweteke na kujivunia kiswahili chetu tunapojilinganisha na wakenya. Pamoja na kuzungumza kiswahili vizuri, kilichonyooka, watanzania wengi hatuna kiswahili kizuri kilicho fasaha. Kwa mujibu wa waingereza, wamarekani wanazungumza kiingereza kibovu. Wale waliosomea fani ya lugha hususani kiswahili, mnaweza kulielezea hili kwa uzuri zaidi?
 
Hili bandiko "liko juu" mzeya! Nimelifurahia mno.
Mimi nakunwa sana na ongea yao, napenda tushirikiane nao kwa karibu kuhakikisha lugha hii inapanuka zaidi na zaidi.

Nimetamani ifanyike jitihada ya makusudi tuwe na mahusiano na forum nyingine hasa za nchi jirani. Kama ambavyo sote twafahamu, lugha ni kiungo na mhimili muhimu sana katika kudumisha umoja na kukuza uhusiano kwa maendeleo ya eneo husika. Ni mara chache raia wa Uganda kwa mfano akafuatilia siasa za Tanzania hata aje kwenye forum yetu. Je, tunaweza kuwavutia watu kutoka Rwanda, Kenya, Uganda.... kuja kushiriki nasi kwenye jukwaa la lugha ya Kiswahili?
Mkuu, nilishawahi kuongea na 'Bloggers' wa Kenya hadi nikaanzisha 'Kenyan Bloggers forum'! Maalum kwa ajili yao. Nikawawinda wa Uganda ili tuungane nao hapa tuweze kujadili mustakbali wa mataifa yetu. Kuna mmoja alinipikia majungu kwao, akadai sisi waTz tunawachukia wakenya. Iliniwia vigumu kuweza kuwashawishi kwani nilikuwa na majukumu mengi tu. Lakini huwa sikati tamaa, tuna wakenya wengi hapa JF. Tuna waganda wachache na Wanyarwanda wachache pia. Bado Burundi ndio sijui lakini wakongo hao nina uhakika kuwa tuko nao humu. Muhimu ni kuwakaribisha wakenya ama waganda wachache walio marafiki zetu (Ab-Titchaz, Alai, Mkenya n.k ni baadhi toka Kenya) wakiwaalika wengine tukawa na jukwaa moja la kusukuma mbele mambo haya inatuwia rahisi! Nafasi ipo kubwa tu kwa JF, tena wakihitaji jukwaa lao maalum niliwahakikishia kuwapa u-kiranja (moderation powers) wa jukwaa husika!

Naomba kutoa pendekezo, kwamba tuwe na jukwaa maalumu la lugha, humo wajumbe washawishiwe kutumia lugha ya kiswahili pekee. Na kwenye jukwaa hilo msisitizo uwe kwenye kuzungumza lugha ya kiswahili sanifu kwa ufasaha.
Shabaash, hili ndilo jukwaa lenyewe la lugha. Ndipo hapa wengi huleta maneno ambayo huwatatiza kwa lugha hii adhimu ya Kiswahili nao hutaka kupata maana zake ili wanapoongea waache kuchanganya maneno!

Ukiishi au kuvungukwa na watu wasiojua vizuri kiingereza, nawe kiingereza chako kitakuwa kibovu. Tuamshe ari hata ifike mahala watu waanze kununua vitabu vya kiswahili na kujisomea.
Mkuu mabadiliko yaanzie kwetu. Tuache kuchanganya lugha, tukiandika kiswahili basi tuhakikishe tunaandika kiswahili kweli na pale tunapoweka neno la kiingereza basi liwekwe kwenye parandesi ama yafungwe kwa alama za fungua na funga semi.

Tusibweteke na kujivunia kiswahili chetu tunapojilinganisha na wakenya. Pamoja na kuzungumza kiswahili vizuri, kilichonyooka, watanzania wengi hatuna kiswahili kizuri kilicho fasaha. Kwa mujibu wa waingereza, wamarekani wanazungumza kiingereza kibovu. Wale waliosomea fani ya lugha hususani kiswahili, mnaweza kulielezea hili kwa uzuri zaidi?.
Umenena vema, ni watanzania wachache tunaoongea kiswahili fasaha. Sarufi zimekaa vibaya, wengi ni wazuri wa kuongea lakini uandishi nao unatupiga chenga. Inapendeza tukiwa mfano kwa wengine.

Ahsante mkuu.

Asiyeonekana :)
 
Jukwaa la lugha mbona lipo, anajItahidi sana Mzee Mwanakijiji katika mashairi na hadithi tamu kwa kutumia kiswahili chepesi.
 
Nikimnukuu mwandishi wa awali aliandika hivi:

Swahili name for resilience is ukakamavu.

Speaking of swahili,I have a challenge to all of us.
Maybe its a high time we as Kenyans cultivate more interest of this language.
Huyu ana mapenzi sana na lugha hii na angependa kuona mabadiliko. Lakini uanzaji wake ulikuwa tayari una kiswa-nglish ndani yake!

It was only jana nilipokutana na mmarekani mmoja mweusi ambaye amejibatiza Otieno.Jamaa huyu ana uchu wa kijifunza Kiswahili.wazungu pia wanajikakamua kujifunza lugha 'yetu'.
Hapo juu angeandika:

Ilikuwa ni jana tu nilipokutana na mmarekani mmoja mweusi aliyejibatiza jina 'Otieno'. Jamaa huyu ana uchu wa kujifunza Kiswahili. Wazungu wanajikamua kujifunza lugha yetu.


Otieno nimeiweka kwenye upekee kwa sababu si jina lake. Halafu kuandika kuwa Wazungu pia... inaonesha (inaonyesha?) kama nasi tunajifunza!

Wenzangu, tuna raslimali muhimu, yaani lugha ya Kiswahili, lakini tumefumba macho jamani...
Binafsi naiona hii sentensi kama imekamilika.

Pokeeni changa moto,mimi nikiwa mstari wa mbele kujikemea..
Ni aibu wala si ushupavu viongozi kufanya makosa ya kisarufi katika usemi wao.
Natumaini angeandika hivi:

Pokeeni changamoto; mimi nikiwa mstari wa mbele kujikemea. Kajitahidi kweli!
Ni aibu kununua tu magazeti na majarida yaliyochapishwa kwa kiingereza.
Ni aibu kuzungumza kizungu pekee na kutupilia mbali Kiswahili sanifu.
Ni aibu kama wadau wenzangu kuwasiliana tu kwa Kiingereza.
Na ni aibu si haba kwamba ukidurusu maandishi yangu utajikwaa kwa makosa labda ya ngeli au uchaguzi wa nomino mwafaka.

Hapa kapiga bakora wengi tena naye akionesha (onyesha?) kukerwa na athali za lugha mbili katika uandishi wake.

Na ili tujue, ni makosa Kujibu Mzuri unaporejelea maamkio-niligundua (hivi majuzi tu)kwamba Kiswahili sanifu inatushurutisha kuitika Nzuri...kwa sababu ya uwiano wa kingeli baina ya Habari na jawabu lako..
Huyu anatukumbusha wengi thamani la lugha yetu. Tukilinde chetu, turinge nacho nao wajifunze kutoka kwetu.
 
Kisha kuna jamaa amejitambulisha kama mpenda IT. Maneno haya yanaweza kuwa msaada kwake na kwa wengi (ya kiswahili yako kwenye mabano):

32-bit
biti-32
about
kuhusu
accelerator
kichapuzi
accessing
ufikio
access (n)
fikio (n)
access (v)
fikia (t)
account
akaunti
actions menu
menyu-vitendo
activate
amilisha
acute
kali
adapter
adapta
add
ongeza
add-on help
msaada nyongeza
add-on
nyongeza
address
anwani
address book
kitabu cha anwani
adjust
rekebisha
administrator
mtawala
alert me
nitahadharishe
alert (n)
tahadhari
alert (v)
tahadharisha
alias
jina jingine
allocate
tenga
allocation (n)
mtengo (result)
allocation (v)
utengaji (process)
all -
ote
allow popup from this site
ruhusu udukizi kutoka tovuti hii
allow
ruhusu
alphabetic text character
kiwambo alfabeti
Alt (Alternate)
(Kbdl) Kibadala
ampersand
ampasendi
animation
uhuishaji
anonymity
ufichojina
Aperture Value
Thamani Upenyo
apparition
mzuko
appears to be
huonekana kuwa
applet
apuleti
application (s)
programu-tumizi
apply
tekeleza
arccosine
kosinitao
archive (n)
jalada (n)
archive (v)
jalidi (t)
array formula
fomula pahi
article
kikala
artificial
bandia
ASCII (American Standard Code for Information Interchange) ASCII
(Msimbo Sanifu wa Marekani wa Mabadilishano ya Habari)
assigned -
liopangiwa
asterisk
kinyota
at -
enye
attachment
funge
attribute(s)
sifa
authentication
uhalisishaji
authorization
uidhinishaji
author
mtunzi
autocomplete
kamilisha kiotomati
auto correct
rekebisha kiotomati
auto detected -
li-ogunduliwa kiotomati
auto-detect
gundua kiotomati
autoFormat (n)
Fomati Otomati (n)
autoFormat (v)
Fomati Kiotomati (t)
autoload
pakia-kiotomati
automatic detection
ugunduzi kiotomati
auto-reliable -
a kuaminika kiotomati
AutoXXX
OtoXXX
back button
kitufe rejeshi
backend
kisogoni
background color
rangi usuli
background
usuli
backslash(e)s
mkwajunyuma
backward moderated -
li-orekebishwa kinyume
bad address
anwani potofu
bandwidth
upana-bendi
bar
mwambaa
baud
baudi
BBS (Bulletin Board Service)
HUM (Huduma za Ubao wa Matangazo)
beamer
kimweko
beam
mweka
beta
beta
bevel
matemo
Bidi options
Hiyari tandawili
binary (adj)
jozi (kv)
binary (n)
jozi (n)
bit
biti
bitmap
taswidoti
blank
uwazi
blind carbon copy (bcc)
nakala fiche (bcc)
block (a command)
zuia (amri)
block device
kitunza data
blocked
iliozuiwa
block (n)
duta
body
gimba
bold (adj)
koze (kv)
bold (v)
koza (t)
bookmark link
alamisho
bookmark (v)
alamisha (t)
bookmark (v)
alamisha (t)
Boolean
Buleani
Boolean operations
matendo Buleani
border relief
nafasi-kingo
border(s)
(u)kingo
bounce
shindwa kufika
bouncing block
duta shinde
box
kisanduku
brackets
mabano
browse (for file)
vinjaria (faili)
browser
Kivinjari
browse
vinjari
bubble (n)
kiputo
buffer
bafa
bugs
hitilafu
built-in
-a ndani
bulleted list
orodha tobwe
bullet points
alama tobo
bullet
tobo
button
kitufe
buttons: exit
vitufe: toka
byte(s)
baiti
cache
kache
calculator
kikokotoo
call-in
mwito-ingia
call-out
mwito-toka
call preference
mwito teule
cancel
ghairi
caption
maelezo mafupi
capture (v)
nasa (t)
carbon copy (cc)
nakala (cc)
carriage return
kirudishi
carrying case
mfuko
CD/CD-ROM/compact disk
diski-ROM
certificate manager
Meneja Ithibati
certificate viewer
kionyesha hati
change
badili
channel (n)
mkondo (n)
character set
seti kibambo
chart
chati
chat group
kundi sogozi
chat
sogoa
check box
kisanduku tiki
check for
tafuta
check (n)
tiki (n)
checksum
namba thibitishi
check (v)
tiki (t)
children (hierarchy)
watoto (kingazi)
chime
mlio kengele
chip
chipu
choose
chagua
chooser
mchaguzi
chunks
vipande
cipher
msimbo
ciphers
misimbo
clash
siga
clear (a) -
liotanduka
clear
tandua
click
bofya
client
koteja
client-server relationship
uhusiano koteja-seva
clients
koteja
clip
pogoa
clobber
zana
clone
kloni
close (a)
-a karibu
close
funga
closer
karibu zaidi
closest
-a karibu sana
collapse
kunja
collate
pangilia
collect e-mail
sanya barua e-
colon
nukta pacha
color capabilities
uwezo kirangi
colorspace
masafa rangi
colour resolution
msongo rangi
column span
upana safu-wima
command
amuru (t)
command line invocations
miito ya mstari amri
command line (n)
mstari amri
command (n)
amri
common -
a kwawida
compatibility
utangamano
compatible
tangamana
com port (communications port)
mlango wa mawasiliano
composer
programu tunzi
compose
tunga
computer
kompyuta
computer-
literate arifu kompyuta
concatenate
funganisha
concatenations
mifunganisho
configuration file
faili sanidi
configuration
usanidi
configuration utility
programu sanidi
configure (ku)
sanidi
connection failure
unganisho shinde
connect
unganisha
controller cards
kadi dhibiti
control (n)
kidhibiti
control panel
paneli dhibiti
controls
vidhibiti
control (v)
dhibiti (t)
converge
kutana
convergence
kutano
converter
kigeuzi
convert
geuza
cookie
kuki
copy
nakili
corrupted -
li-ovurugika
corrupt
vuruga
counter
kihesabio
country code
msimbo nchi
cracker
mharabu
crash
kwama
CRC
CRC
create links
unda viungo
create
unda
credentials
hati tambulishi
credits
heko
crop
pogoa
cross-posting
usambazaji
cross-post (v)
sambaza
Ctrl (control)
Kdbt (kidhibiti)
curly brackets
mabano wimbi
curly quotes
nukuu wimbi
cursor
kasa
customized -
li-okaidishwa
customize
kaidisha
custom
kaida
cut
kata
daemon
dimoni
data area
eneodata
data bank
kanzidata
database
hifadhidata
data bit
biti data
data
data
debugging
weuaji
debug (n)
euo
debug (v)
eua
decision
uamuzi
decode
simbua
dedicated
-li-owakifishwa
default
chaguo-msingi
default
gateway lango-msingi
default search engine
injini-tafuti msingi
default value
thamani msingi
Del (delete)
Futa (futa)
delete
futa
deleting
ufutaji
deletion
mfuto
deletions
mifuto
delimiter
kitenganishi
deliver (v)
wasilisha (t)
deprecated
-li-okonga
desktop
dawati
destination
mwishilio
detect
gundua
device independent
-sochagua kifaa
device
kifaa
device manager
meneja vifaa
diagnostics
uchunguzi
dial
dayo (n)
dialogue box
kisanduku cha mawasiliano
dial out (v)
dayo nje (t)
dial tone
mlio dayo
dial-up (adj)
-a dayo
dial-up networking
mtandao simu
dial-up (v)
dayo (t)
digital camera
kamera dijiti
digital signature
saini dijiti
digit
dijiti
direction
mwelekeo
directory
saraka
disable
lemaza
disconnect
tenganisha
disk capacity
uwezo wa diski
disk
diski
disk space
nafasi ya diski
display class
daraja zinzo
displayed
zinzwe
display (n)
zinzo (n)
display (v)
zinza (t)
disposition
mpangilio
document
andiko
documentation
mwongozo
domain
kikoa
done
gotoka
double-click
bofyabofya
download
pakua
down (vi)
shuka
down (vt)
shusha
drag and drop
kokota na dondosha
drag
kokota
drawing object bar
mwambaa vichorea
driver
dreva
dual mode
modurufu
dump
dampo
dump (v)
tupa damponi (t)
dynamic IP-address
anwani-IP badilifu
edit (the action)
hariri
edit (the button)
kihariri (kitufe)
eject
fyatua
e-mail
barua e-
embedded
futike
emoticon
kikaragosi
emulator
kiigizi
enable
wezesha
encode
simba (t)
encrypted
msimbo fiche
encrypted text
matini-msimbo fiche
encryption
usimbaji fiche
enhance
boresha
enhanced
bora
enter (n)
ingizo
enter (v)
ingiza
entry
ingizo
envelope orientation
mkao wa bahasha
environment variable
kibadili kimazingira
error hitilafu
Esc (escape)
Epa (epuka)
events
matukio
executable file(s)
faili tekelezi
execute
tekeleza
exit buttons
vitufe vya kutokea
exit
toka
expand
tanua
export
hamisha
extension
tawi
external
-a nje
face type
aina ya chapa
fail
shindwa
false
si kweli
FAQ (Frequently Asked Questions)
MYM (Maswali Yaulizwayo Marakwamara)
favourite
kibwedo
field
uga
file
faili
file transfer protocol (FTP)
itifaki ya kuhawilisha faili (IKF)
filter (n)
chujio
filter (v)
chuja
find
tafuta
finish
maliza
firewall
ngome
flags
viboya
floppy disk
diski tepe
flow control
udhibiti wa mtiririko
folder
folda
font
fonti
footer
wayo
footnote
tiniwayo
format (n)
fomati (n)
format (v)
fomati (t)
forum
ukumbi
forward slash
mkwaju
frame
fremu
free (to ~ up space on disk)
toa nafasi
freeware
programu dezo
frequency
dafaa
frontend
usoni
full-screen mode
Modi skrini-nzima
FYI (For Your Information)
KTY (Kwa Taarifa Yako)
game(s)
mchezo
gateway
lango
gigabyte
gigabaiti
glossary
faharasa
grant permission
idhini ruzuku
graphic
mchoro
greater than
kubwa kuliko
guest
mgeni
hacker
mdukizi
handshake
mkono
hang up
Kata simu
hang (v)
kata
hard drive - disk
diski kuu
hardware
maunzi
hash
reli
header
kichwa
height
kimo
help
msaada
hide
ficha
highlight (v)
angaza
hint
dokezo
history
historia
home button
kitufe mwanzo
home directory
saraka kaya
home page
gombo kaya
host
mwenyeji
hypertext
matinifora
hyphenation
unganishaji
icon
ikoni
idle (n)
bwete
image
taswira
import
leta
inbox
kisanduku pokezi
inconsistency
usongombingo
inconsistent
songombingo
indent (v)
jongeza ndani

Nitaendelea... Lakini wadau naomba maneno hayo na maana zake tuyaangalie kwa mapana na kuyajadili kukikuza kiswahili chetu
 
Kuna mmoja alinipikia majungu kwao, akadai sisi waTz tunawachukia wakenya.

Sio kwamba wanadai. Ni kweli.

"Tuwe makini na shirikisho, Wakenya wana maslahi kwetu, tuwe makini nao, wanatudharau na wanataka mali zetu, wao wanadai mali zetu kuwa ni zao kama Mlima Kilimanjaro na niliwahi kuwatukana waache kuutangaza kama wao".
Mbunge wa , Anne Kilango (CCM), Same Mashariki, 10-31- 2008

"Wakenya ni wabinafsi na wanajali bidhaa za kwao huku wakiweka vikwazo vya chinichini ili Tanzania isifaidike kibiashara."
Vedastus Manyinyi(CCM), Musoma Mjini, 10-31- 2008. Daily News wamesema amesema.

Sasa kwa lugha kama hizo za Mama Mbunge utawaeleza nini wakina Ab-Titchaz ambao unasema ni Wakenya? Tuwaombe msamaha kwa majuto kwa maneno ya huyu loose canon wa Bunge.

Hayo matusi ya Mama Mbunge alitakiwa ayaseme behind closed doors, kwenye tume zao za Bunge huko. Halafu ukija kwenye open forum una condemn vikali lakini siyo kwa matusi. Sorta like the same rules of debate za forum ya JF. Lakini wabunge hawa hawana clue! Eti wanapendwa kwa sababu wanakipaka paka bungeni. Wanakipaka ndio, lakini wanatumia sense and tact wanapokipaka ? Unajitamba "niliwahi kuwatukana"!!! Ilitatua tatizo ? Sasa mbona bado unalia lia?
 
info taarifa
inner margin pambizo ndani
input box kisanduku ingizo
input ingizo
insert cells down chomeka seli chini
insert chomeka
install sakinisha (t)
integrated fungamana
interactive wasilianifu
interface kusano
Internet Wavuti
invalid batili
invite alika
IP (Internet Protocol) IP (Itifaki Wavuti)
ISP (Internet Service Provider) ISP (Mtoaji Huduma Wavuti)
italic italiki
Javascript hatiJava
jobs (e.g. print jobs) kazi (k.m. kazi za kuchapa)
join unga
junk mail barua taka
justified linganifu
keep track fuatilia
keyboard baobonye
key (on keyboard) kibonye (katika kibodi)
keyword neno msingi
kilobyte kilobaiti
kit kivunge
label lebo
LAN (local area network) LAN (mtandao kiambo)
last modified rekebisho la mwisho
last visited tembeleo la mwisho
launch zindua
layer tabaka
layout mpangilio
link kiungo
link (to) unga
list orodha
load pakia
locale -a kiambo
log file faili kumbukumbu
login (info) kuingia (maelezo)
log in ingia
log out toka
log (v) tunza kumbukumbu
lowercase herufi ndogo
mailbox sanduku la barua
mailing list orodha anwani
manager meneja
manual mwongozo
margin pambizo
mark alama
master kuu
match oanisha
maximise tanua
mean -a kati
megabyte (MB) megabaiti (MB)
member mwanachama
memory kumbukumbu
menu bar mwambaa-menyu
menu menyu
menu proxies menyu proksi
message ujumbe
microphone mikrofoni
minimise finya
mirror kioo (n)
mirror (v) akisi (t)
mismatch (v) sigana
modem (modulator-demodulator) modemu (modu-demodu)
mode modi
moderated -li-orekebishwa
modify rekebisha
monitor (n) monita
monitor (v) simamia (t)
mouse pad kata puku
mouse puku
mousewheel gurudumu puku
move (v) sogeza (t)
multimedia medianuwai
multiple recipient wapokezi anuwai
name server seva majina
navigate rambaza
network mtandao
new -pya
newsgroup kundihabari
newsletter kijarida
next ifuatayo
nickname lakabu
non-blank isoachwa tupu
none bila
notify arifu
not writeable -sioandikika
numbering uingizaji namba
objects viumbile
offline (go ~) nje ya mkondo (nenda ~)
offline nje ya mkondo
OK SAWA
online mkondoni
open fungua
open software localization project mradi wa kuswahilisha programu
huria

open source chanzo huria
operation(s) operesheni
operator opereta
optional -a hiari
option chaguo
organise pangilia
outbox kisanduku toa
outer margin pambizo nje
output zao
overwrite (v) andikiza (t)
page gombo
page orientation mkao wa gombo
paginate kurasisha
parent (hierarchy) mzazi (kingazi)
password nywila
paste bandika
path njia
pause pauzi
percentage asilimia
permission (s) ruhusa
pick twaa
picture picha
pie pai
pixels piseli
plug-in (n) programu-jalizi (n)
plug in (v) chomeka plagi (t)
pointer kidosa
point nukta (n)
point (v) dosa (t)
popup (n) kidukizo (n)
popup (v) dukizo (t)
power umeme
preferences aula
prefix kiambishi awali
press bonyeza
preview hakiki
print chapisha
printer printa
print job kazi ya kuchapisha
privacy faragha
processing uchakataji
process mchakato
program programu
progress hatua
properties sifa
protocol itifaki
Public Domain Software Programu Huria
query ulizo (n)
query (v) uliza (t)
queue (n) foleni (n)
queue (v) panga foleni (t)
quit aga
radio button kitufe redio
range masafa
read soma
reboot washa upya
receive pokea
recipient mpokezi
recover nusuru
recycle bin kisuduru
redirection uelekezaji
redo rudia
reference rejeo
Ref: Yah:
Re: Jb:
reliable -a kuaminika
reload pakia upya
remove ondoa
rename badili jina
repaginate kurasisha upya
replace badilisha
reply jibu
requirement mahitaji
reset seti upya
resource rasilimali
response jibu
restart washa upya
resume anza upya
retry jaribu upya
return rejea
retype chapa upya
round brackets mabano
rules kanuni
run endesha
save hifadhi
scale (v) skeli (t)
scanner skana
scan (v) skani (t)
schedule ratiba
screensaver kilezi
screenshot kielelezo-skrini
screen skrini
script hati
scroll bar mwambaa biringizo
scroll biringiza
search engine injini tafuti
search tafuta
sectors sekta
secure (n) salama
secure (v) salimisha
security usalama
security warning hadhari ya usalama
select all teua -ote
selection uteuzi
select teua
semi-colon nukta mkato
send tuma
separator (delimiter) kitenganishi
server seva
service huduma
session kipindi
set as seti kama
settings vipimo
set to true seti kwenye kweli
setup usanidi
share changio (n)
share (v) changia (t)
sheet laha
shortcut mkato
show onesha
shutdown zima
sidebar mwambaa pembe
signal ishara
signature saini
sign in ingia
sign off toka
sine sini
single-click bofya
site tovuti
size saizi
skip ruka
slash mkwaju
slave (adj) joli (v)
slider kitelezi
slide telezesha
small caps herufi kubwa ndogo
smiley kicheshi
software programu
sort criteria kigezo mpango
sort panga
source chanzo
spam (v) peleka barua taka (t)
spell-checker kikagua tahajia
spell checking ukaguzi tahajia
split gawa
spreadsheet lahajedwali
square brackets mabano mraba
static IP-address anwani-IP tuli
status hali
store ghili
string (n) utungo
stuck goma
style sheet laha mtindo
subject line mstari mada
submit wasilisha
subscribe jiunga
suffix kiambishi tamati
surf rambaza
suspend subirisha
syntactical error hitilafu ya kisintaksia
syntax sintaksia
system mfumo
tab key kibonye tabo
tab tabo
tag tagi
tangent tanjiti
tape tepu
target lengo
TCP (Transmission Control Protocol) IKU (Itifaki ya Kudhibiti
Urushaji)

template templeti
terminate katisha
text matini
theme mandhari
thumbnail kijipicha
tilde kiwimbi
time elapsed muda uliotumika
timeout muda umeisha
time remaining muda uliobaki
tips vidokezo
toggle gura
toolbar mwambaa zana
tool zana
topic mada
transferable hawilishika
transfer (v) hawilisha (t)
transmit rusha
trash taka
true kweli
undelete futua
underline pigia mstari
undo tengua
uninstall sakinusha
unread -siosomwa
unsubscribe jiengua
update sasisha
upgrade (v) boresha
upload pakia
uppercase herufi kubwa
URL (Uniform Resource Locator) KISARA (Kioneshi Sanifu Rasilimali)
user mtumiaji
username jina la mtumiaji
utilities vitumika
valid halali
verify thibitisha
version toleo
view angalia
view (v) angalia (t)
virtual mnemba
virus kirusi
volume ujazo
wallpaper pazia
warn (v) tahadharisha (t)
watch tazama
webmaster mtawala tovuti
web page gombo wavu
website tovuti
web wavu
widget wiji
width upana
window dirisha
wizard sogora
word processor kichakata matini
workspace ulingo
wrap fungasha
write andika
write-protected -liokingwa kuandikwa
WWW (World Wide Web) WWW (Wavu Wa Walimwengu)
 
Umeandika vyema Invisible; Onesha sio onyesha (~onya).


Natamani sana kuboresha kiswahili changu kiendelee kuwa cha kueleweka (simple swahili) kwa watu wengi lakini chenye misamiati mingi ya kawaida (sio bombatic). Si wingi wa misamiati tu, bali umahiri wa kutambua mahala muafaka pa kuyatumia. Kuboresha lugha ni ngumu sana kama husomi vitabu. JF yaweza kuwa ndiyo kitabu changu?


Pamoja na makosa yaliyojitokeza, huyu ameonyesha umahiri kunizidi,
Swahili name for resilience is ukakamavu.

Speaking of swahili,I have a challenge to all of us.
Maybe its a high time we as Kenyans cultivate more interest of this language.
It was only jana nilipokutana na mmarekani mmoja mweusi ambaye amejibatiza Otieno.Jamaa huyu ana uchu wa kijifunza Kiswahili.wazungu pia wanajikakamua kujifunza lugha 'yetu'.

Wenzangu, tuna raslimali muhimu, yaani lugha ya Kiswahili, lakini tumefumba macho jamani...

Pokeeni changa moto,mimi nikiwa mstari wa mbele kujikemea..
Ni aibu wala si ushupavu viongozi kufanya makosa ya kisarufi katika usemi wao.
Ni aibu kununua tu magazeti na majarida yaliyochapishwa kwa kiingereza.
Ni aibu kuzungumza kizungu pekee na kutupilia mbali Kiswahili sanifu.
Ni aibu kama wadau wenzangu kuwasiliana tu kwa Kiingereza.
Na ni aibu si haba kwamba ukidurusu maandishi yangu utajikwaa kwa makosa labda ya ngeli au uchaguzi wa nomino mwafaka.

Na ili tujue, ni makosa Kujibu Mzuri unaporejelea maamkio-niligundua (hivi majuzi tu)kwamba Kiswahili sanifu inatushurutisha kuitika Nzuri...kwa sababu ya uwiano wa kingeli baina ya Habari na jawabu lako..


Mara kwa mara huwa nasikia wengine wakisema "uchu wa madaraka", nami nimekuwa situmii neno hilo sehemu nyingine kama mwenzangu hapo juu kwa sababu sikumbuki kusikia likitumiwa kwa namna tofauti.


Wengi huwa tunasumbuliwa kwenye viunganishi, kuunga sentensi iwe ni kimombo au kiswahili. Mwenzetu katumia neno "baina"; nimelipenda zaidi kuliko kutumia neno "kati" badala yake.

Kabla ya kurekebisha, sentesi hapo juu ilisomeka, "Wengi huwa tunasumbuliwa na viunganishi"





.
 
Nikimnukuu mwandishi wa awali aliandika hivi:

Huyu ana mapenzi sana na lugha hii na angependa kuona mabadiliko. Lakini uanzaji wake ulikuwa tayari una kiswa-nglish ndani yake!


Hapo juu angeandika:

Ilikuwa ni jana tu nilipokutana na mmarekani mmoja mweusi aliyejibatiza jina 'Otieno'. Jamaa huyu ana uchu wa kujifunza Kiswahili. Wazungu wanajikamua kujifunza lugha yetu.


Otieno nimeiweka kwenye upekee kwa sababu si jina lake. Halafu kuandika kuwa Wazungu pia... inaonesha (inaonyesha?) kama nasi tunajifunza!

Binafsi naiona hii sentensi kama imekamilika.

Natumaini angeandika hivi:

Pokeeni changamoto; mimi nikiwa mstari wa mbele kujikemea. Kajitahidi kweli!


Hapa kapiga bakora wengi tena naye akionesha (onyesha?) kukerwa na athali za lugha mbili katika uandishi wake.

Huyu anatukumbusha wengi thamani la lugha yetu. Tukilinde chetu, turinge nacho nao wajifunze kutoka kwetu.

Mkuu umeteleza "hukutereza" kwenye utelezi(si uterezi) wa ganda la ndizi
wengi sana tunaathirika kutokana na athari za kilafudhi za lugha zetu asili.
 
Hivi neno "Spelling" kiswahili chake nini?
neno hilo nimezowea kulitumia katika uzungumzaji ula huniwia vigumu katika uandishi, naomba wajuaji wanijuze.
 
Hivi neno "Spelling" kiswahili chake nini?
neno hilo nimezowea kulitumia katika uzungumzaji ula huniwia vigumu katika uandishi, naomba wajuaji wanijuze.


Spelling = tahajia (kwa mujibu wa Kamusi Project)


Niliwauliza wenzangu hilo swali, kichwani nikiamini kabisa tafsiri ya neno "spelling" nimewahi kusikia kabla.



.
 
Jamani tukae tufahamu kwamba kenya KISWAHILI sio lugha yao ya kwanza...Mfano kama UGANDA kiswahili kilikuwa sio lugha ya kwanza lakini miaka ya hivi karibuni ndio wamepitisha na kusema kwamba kiswahili kitakuwa lugha ya Taifa......Kwa hiyo wenzetu wapo nyuma kidogo upande wa kiswahili bado hawajajua zaidi kukitamka zaidi...Tuwape time watatuzidi hata sisi wabongo
 
WanaJamii,

Sijui kama mlisoma kwenye magazeti majuzi kwamba Microsoft imezindua 'software' ya kiswahili Nairobi hivi karibuni. Please take a minute to digest taht information.

Kama kawaida Watanzania tuna maneno mengi kuhusi lugha na uzalendo, huku wenzetu wamechangamkia tenda.

Ninamfahamu mfanyakazi wa Microsoft aliyeshughulika na kutafsiri 'software ' ya microsoft. Alikuja bongo, alitafuta watu wa kufanya nao kazi, vituko tulivyo mfanyia vilimfanya akimbilie wenzetu.

Usiku huu, mtu yeyote anaejisikia 'jiongoistic' naomba atafakari funzo hili. Talk the talk? Walk the walk.

Peace from a bilingual patriot.
 
Cha kushangaza zaidi hawa wakenya ndio wafundishaji wakubwa wa kiswahili nchini Marekani, ilhali kiswahili chao ndio hicho kimekaa upande. Watanzania tuna nafasi kubwa ya kuendeleza hii lugha nje ya mipaka yetu kwa kasi ya ajabu; kinachotakiwa tu ni umakini na kujua ni kitu gani tunacho kama asset na tukitumie bila kusita.
 
Ninamfahamu mfanyakazi wa Microsoft aliyeshughulika na kutafsiri 'software ' ya microsoft. Alikuja bongo, alitafuta watu wa kufanya nao kazi...


Cha kushangaza zaidi hawa wakenya ndio wafundishaji wakubwa wa kiswahili nchini Marekani, ilhali kiswahili chao ndio hicho kimekaa upande. Watanzania tuna nafasi kubwa ya kuendeleza hii lugha nje ya mipaka yetu kwa kasi ya ajabu; kinachotakiwa tu ni umakini na kujua ni kitu gani tunacho kama asset na tukitumie bila kusita.


Mswahili wa pwani ya Tanzania ana tofauti gani na aliye pwani ya Kenya?
Mwalimu wa Kiswahili kwenye chuo cha Kenya, ana tofauti na colleague mwenzie toka Tanzania?


Nimewahi ku-download "Learn Swahili" program (Rosettastone). Nilikasirika sana nilipoanza kuisikiliza kwani sauti ilikuwa ya lafudhi ya kikenya. Wala sidhani alikuwa ni mzungumzaji wa pwani ya Kenya.

We should look forward to enter EAC; although we will lose some, we have some non-material things to gain, which are extremely valuable to us.












.
 
Wakuu,

nimejaribu kujizuia lakini nimeshindwa...hebu nitinge humu.

Kwanza kabisa Invii thank you so much for everything you have done and are doing to bring us together.Keep up the good work.

Pili kuhusu 'ukenya', (if there is such a word) na Kiswahili ni vyema kufahamu watu wa Pwani ya Kenya(ambapo mimi mmoja wao), tunaongea kiswahili tofauti kabisa na watu wa bara(hawapendi hili jina na nadhani watanipiga mawe wakislisoma).Watu wa Nairobi wanapenda sana kuongea sheng ambayo kwa kiwango kikubwa imeharibu jitihada zote za kujaribu kukuza kiswahili.

Nakumbuka nilipotia timu bongo kuja kufundisha nilikutana na waalimu kadhaa ndani ya staff room kutoka Kenya na walikua wanaongea ki-inglishi tu na kiswahili was not 'reachebo'.Mwenzio nikawa napeta tu...hata wale wajomba wa TRA walipotokea kucheki maswala ya vibali, Mama Lwakatare akawa anawaambia wakimbie waende nyumbani maana wakihojiwa basi kitanuka....this was funny!Unaona walimu mbio wanakimbia bondeni wanakwepa wajomba wa TRA...duh!

Tatu nataka kugusia ule msemo eti "wakenya wanawachukia wa-Tz".. kwa kweli whoever says such a comment ni mmbeya tu.This kinda blanket condemnations hazifai maana who is wakenya?...mimi humo simo maana toka mdogo, ilikua bomba na rahisi zaidi kuenda Tanga kuliko hata kuenda Nairobi.Kuna washkaji kibao ambao tuna-wazazi pande zote mbili za border na tulikua tukipiga biashara za batiki kila mtindo. Huyo kiongozi aliyesema kawatukana wakenya, je tumefaidi nini isipokua kukuza chuki miongoni mwa hizi jamii mbili?...Mie mwenyewe natamani nikampigie tripu nimuulize hilo swali.

Tatizo la kusema mara wakenya ni wezi au wanawachukia wabongo linatokana na jamii moja tu nayo ni wakikuyu.Iwapo umespendi m'da mwingi na hii jamii utadhani basi that is Kenya's representation.Inanikumbusha nilipoingia marekani na hawa ma-nugu(I hate the word by the way) wakawa wananiuliza mbona waafrika mnatuchukia?...hili swali lilikua too much ikabidi nitafute chanzo.

Coming to find out, ni matatizo yao na Wa-Nigeria ambayo wamereflect on all Africans.Pia kila ukipiga kona unauliwa wewe Mnigeria. Ikabidi nianze darasa la kuwaonyesha kuwa Africa is a big continent with countries in it. Si unaona Sarah Palin hayupo peke yake?

Kwa hivyo mimi nishaamua I'm beyond borders and I don't subscribe to labels and such.Lets foster this unity in ways unimaginable maana it is through this generation that a lot can be done hususan ule muungano wa EAC which to me has to start at a social level kabla hatujaanza kuhusisha serikali ama maswala ya kiuchmi.Why would we be chasing a dream like the EAC when the common man in both countries cannot get along either by design or happenstance?

Personally I played my part as a teacher na ni fahari ninapotizama na kuona wanafunzi niliowafundisha na kuwachapa viboko sasawako chuo kikuu wanasoma mambo ya nguvu.

Idumu JF, Idumu East Africa na tudumu sie kama wanajamii.

Naomba kuwasilisha.
 
Last edited:
Meanwhlie angalieni balaa ya sheng na kutafsiri bibilia...

Luke 19: 1-10

'Luka Kumi na tisa, moja hadi ashuu.'

Then Jesus entered and passed through Jericho .

--Basi Yesu akapenya Jeri na alikuwa akipitia tuu.

Now behold,there was a man called Zaccheus who was the Chief Tax collector
and was rich.

--Basi kulikuwa na msee mmoja anaitwa Zaka. Huyu Zaka alikuwa dongra wa kukwachu munde, na alikuwa sonko mbaya

And he sought to see who Jesus was, but he couldn't because of the crowd,for he was a short man.

--Zaka alijisikia kusorora huyu Yesu, lakini wapi ju ya ile kerende: alikuwa ka-pienga!

So he ran ahead and climbed up into a sycamore tree to see Him for he was going that direction.

--Zaka akajishanora akadandia miti ndio asorore vipoa juu alikuwa akichoroboka hiyo side.

And when Jesus came to the place, He looked up and saw him, and said to him

--Basi Yesu aligalavant akafika hiyo baze,akacheki mabatini akamcheki na kumshow niaje ?

"Zacchaeus,make a haste and come down, for today I must stay at your house"

--"Zaka dondoka faster faster juu leo lazima ni maintain kwa keja yako".
 
AA hah-ha-ha-ha-ha-hah... oooh, dah!


attachment.php


This is so hilarious
What is the origin of those terminologies man?




.
 

Attachments

  • 1a00e2a8.gif
    1a00e2a8.gif
    27.4 KB · Views: 1,361
Back
Top Bottom