kukomya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 344
- 143
Hivi Mkuu una uelewa wa namna gani? mbona hata maswali yako hayana mshiko? Unauliza lugha yenye mchango mkubwa katika maendeleo kati ya Kiswahili na Kiingereza bila ya kutaja mchango wa maendeleo gani na nchi gani, unatarajia ujibiwe vipi? Unataka useme maendeleo yaliyoko uchina, Ujerumani, Urusi, Italia, Ufaransa, na nchi kibao zisizozungumza hicho kiingereza unachokiabudu yaliletwa kwa kuzungumza Kiingereza? Ni viongozi wenye mawazo kama yako ndiyo walioididimiza lugha hii kuwa kama ilivyo, wameshindwa kuchukua hatua thabiti kuiimarisha. Inashangaza lugha inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 100 waliosambaa katika mataifa zaidi ya kumi wewe unasema si lugha ya kimataifa! Nasisitiza tena ukikiona Kiingereza ni kipana, kirefu au kinapendeza ujue nyuma ya pazia wapo watu wanaokifanya kionekane hivyo.Naomba nikuulize maswali yafuatayo:
Je, ni lugha gani kati ya kiingereza na kiswahili, inamchango mkubwa katika maendeleo ? na ni kwa nini?