Kiswahili kimezingatiwa kweli?Hii ni wizara mjue.

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
NI AFISI au OFISI?
 

Attachments

  • pemba.jpg
    pemba.jpg
    47.9 KB · Views: 330
Mahali au mahala?
Mahali au pahala?
Jambo lilolotokea au Jambo lililotokezea?
 
Hicho ndicho kiswahili fasaha kwao; vibao vya shule vimeandikwa SKULI YA....

Hiyo namba ina code number ya zamani ya zantel nafikiri ukiweka 0777 utaipata
 
Mimi nadhani kabla haujakurupuka na kuanza kutoa shutuma ungejipanga kwanza na kiswahili chako.
 
MWANDISHI YUKO RIGHT , ITS AFISI NA SIO OFISI ie ofisi ni matamshi ya kiinglish but in kiswahili aka TUKI NI AFISI , NA MASUALA NI SAHIHI PIA ! M CONSULT TUKI , MLETA STATUS BUT HIZI NAMBA ZA SIMU ZITAKUWA ZA ....... , SIO TZ !
 
P.O. Box?S.L.P.?,Fax?Tahrishi?,Tel no?Simu? Kwa kifupi hawakuwa makini katika kuandika bango hilo.
 
Kwa nyongeza tu....

Kuna kitu kinaitwa Lahaja na kwenye Lahaja kuna lugha za kitarafa(vipengele vya lugha za kieneo).......

Katika kiswahili Lahaja hutofautishwa kulingana na eneo husika,hapa tunakutana na vitu kama vile kiunguja(Kiswahili cha visiwa vya Zanzibar), Kingazija(Kiswahili cha visiwa vya Comoro), Kimvita(Kiswahili cha Mombasa) na Kiamu(Kiswahili cha Lamu n.k) .......Badhi ya maneno yametoholewa moja kwa moja na kuwa misamiati rasmi katika eneo husika mfano skuli(shule), marikiti(soko), ofisi(afisi) n.k......

Ni kama vile kiingereza kina lahaja na misamiati inayozungumzwa tofauti ndio maana kuna Kiingereza cha kimarekani(American English), Kiingereza cha uhindini( Indian English), Kiingereza cha kiaustralia(Australian English), Kiingereza cha Uingereza kwenyewe(English) na sasa kuna kiingereza cha Kinaija(Nigerian English).....Kuna misamiati(katika kiingereza) inatofautiana kati ya eneo na eneo katika hayo hapo juu.............
 
Mimi nadhani kabla haujakurupuka na kuanza kutoa shutuma ungejipanga kwanza na kiswahili chako.

Kwenye anuani naona kama kiswahili hakikutumika. Sina hakika aliyeanzisha thread alikuwa anamaanisha hilo au tofauti ya AFISI na OFISI.
Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom