Kisutu: Mahakama yampa Wema Sepetu onyo la mwisho na kumrejeshea dhamana yake

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania imemuonya msanii wa Filamu nchini humo, Wema Sepetu(30), kutokukiuka masharti ya dhamana, vinginevyo haitasita kufutia dhamana yake.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatayu, Juni 24, 2019 na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana.

Juni 17, 2019 Mahakama hiyo iliamuru mshtakiwa huyo kupelekwa rumande hadi leo Jumatatu, ili iweze kutoa uamuzi baada ya mshtakiwa huyo kujisalimisha mahakamani hapo.

Wema alijisalimisha mahakamani hapo Juni 17, 2019 baada ya Mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kutokana na kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa.

Mahakama ya Kisutu, ilitoa hati ya kumkamata Wema, Juni 11, 2019 baada ya mshtakiwa huyo kuruka dhamana.

"Mahakama inatoa onyo la mwisho kwa mshtakiwa, ikitokea mshtakiwa huyu amevuja sheria kwa kutokufika mahakamani bila taarifa, Mahakama hii haitasita kumfutia dhamana.”

“Hivyo Mahakama imekurudishia dhamana yako na utakuwa nje kwa dhamana," amesema Hakimu Kasonde wakati akisoma uamuzi wake dhidi ya mshtakiwa huyo.

Wema ambaye alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandaoni wa Istagramu kinyume cha sheria.

Hakimu Maira ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 itakapoanza kusikilizwa ushahidi.
 
Ndo hivyo
IMG-20190624-WA0019.jpeg
 
Dogo ruebn mwanasheria wake anamkaza na hilo ni ttz kubwa sasa wema anajua kupakuliewa na mwanasheria wake ndio kuchezea sheria mjinga sana
 
Dogo ruebn mwanasheria wake anamkaza na hilo ni ttz kubwa sasa wema anajua kupakuliewa na mwanasheria wake ndio kuchezea sheria mjinga sana
Mwanasheria wake si Albert Msando? Huyu jamaa anpenda sana uchi huyu nae alivujisha picha zake akiwa anatomasa makalio ya Gigy money wakiwa kwenye gari. Wote ni walewale...
 
Dogo ruebn mwanasheria wake anamkaza na hilo ni ttz kubwa sasa wema anajua kupakuliewa na mwanasheria wake ndio kuchezea sheria mjinga sana
Ha ha ha ha ha ila dogo Ben nae ana moyo
 
Wema ambaye alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandaoni wa Istagramu kinyume cha sheria.
KUNA NCHI AMBAZO RAIA WAKE 'WAMEZIBUKA' NA SERIKALI ZAO HAZINA UKALI KTK SUALA LA MAADILI. WASANII WANAOFANYA UFUSKA NA KUUSAMBAZA WANAKUWA HAWANA HATIA YYTE!

LAKINI KTK TAIFA LENYE USTAARABU KUSAMBAZA VIDEO ZA UCHAFU NI JAMBO LISILOKUBALIKA KATU.

SASA JE, HIVI NA YULE MWANAMKE ALIEVUMA BAADA YA KUSAMBAZA AKIFANYA UJINGA MKUBWA ZAIDI MAMBO YAKE YALIISHA?? KIUKWELI TUNGETAMANI KUONA HAWA WATU WANAKOMESHWA NA TAARIFA ZA KUKOMESHWA KWAO ZIWE HADHARANI ILI IWE FUNDISHO. AT LEAST KUKAMTWA KWA HUYU NA KUWEKWA GEREZANI JAPO KWA SIKU CHACHE KUTAPUNGUZA KASI YA WANAOTAKA KURUSHA UCHAFU KAMA HIVYO.
 
hii kesi inaonyesha udhaifu wa mfumo wa mahakama ya nchi hii,kesi hiyo ni kumaliza mwaka kweli wanamzungusha mtoto wa watu?,upotezaji wa mda uliotukuka,kwanza hii ishu ilikuwa ni ya kusolviwa pale central tu mambo yakaisha
 
Back
Top Bottom