Kisingizio: Daftari la Wapiga Kura, vyombo vya dola. Sababu?

Ritz kweli bado upo kulekule.Sasa hizo chaguzi zinathibitisha vipi kuwa CCM ndiyo ya kitaifa?
 
Chadema sio chama cha kitaifa ni chama cha kikanda ndio maana umeona watanzania walivyokikataa kwenye chaguzi za udiwani, ni chama cha kikanda.

haha nini sasa kinaifanya CCM iwe ya kitaifa ktk huu uchaguzi?Wameachgua madiwani nchi nzima?Kama wao na CDM wote wanapata ushindi ktk pockets fulani fulani za nchi kwanini wawe tofauti kwa hili?
 
muhimu cdm iwe inashawishi watu makini wanaokubalika ktk jamii kugombea,kwa ujumla wananchi wameichoka ccm

Sambamba na hili,,wapo watu wanaokubalika lkn wamekuwa na woga kusimama wakigombea kwa tiketi ya Upinzani wacha elimu iwaingie,,nimeona Karatu wengi viongozi wa cdm akiwemo Masai ni wafanyabiashara na hawana uoga wa eti kunyanyaswa ktk biashara zao na ccm
 
Kuwa mstaarabu, tushindane kwa hoja, siyo vibwagizo Mkuu, Mfano M4c imezoa kata 3, ulitaka izoe ngapi, kwa nini?
ok niliuliza hivi Unaelewa mana ya VUGUVUGU la mabadiliko?

Mabadiliko huwa hayaji siku moja? Leo masikini kesho tajiri? ok Madhumuni ya M4C unayafahamu? twende kwa hoja,

Ustaarabu gani kuisifia Chadema?
 
Mzee Mwanakijiji

Mkuu,

Tathimini yako na wengine kwa haraka haraka ni rahisi kukurupuka kuwa Chadema kimeshindwa...

Hatuna sababu ya kuwa wakali wala kutafuta sababu, uzuri wanachadema tunazijua sababu,

Kwa hili ungewashauri CCM, wajitadhimini na waje na sababu kwa nini wanazidi kuporomoka...uchaguzi huu wamepoteza viti 3 vya udiwani...Chadema tumeongeza, sasa sijui nani aje na hizo sababu...

Mkuu MMK, kama Tanzania tungekuwa na Democrasia ya Kweli...Nami ningeungana nawe, kuwakosoa na kuwaponda viongozi wetu, lakini kwa jinsi uwanja wa demokrasia ulivyo, CDM wamejitahidi sana,, nikuulize kidogo tu...
1. Unafahamu kuna kesi ngapi zinazowakabili viongozi wakuu wa CDM mpaka sasa?
2. Kesi ngapi kwa mashabiki na wapenz wa Cdm mpaka sasa?
3.Kuna mashabiki wangapi wa CDM wamekufa mpaka sasa?
4.Kuna walemavu, wagonjwa, walioteswa wa CDM mpaka sasa?

MzeeMwanakijiji, Tanzania ni zaidi ya ujiavyoo..., Chadema tunawapongeza sana tena sana, endeleeni viongozi wetu tupo nyuma yenu.
Nkuunga mkono mia kwa mia Mwanakijiji leo nimesoma thread zake naona hathink big...kuna mizengwe kibao jamani tunafanyiwa wanachadema na hilo liko wazi kila mtu analiona,unaposema viongozi wetu wawajibishwe kwa lipi???sikuelewi MM..
 
Kwani huko kwenye kata hizo zingine ambazo CHADEMA wameshinda kumetumika Daftari jipya la Wapiga Kura? Huko CCM imeshindwaje kutumia ujinga wa watanzania na nguvu ya dola? Arumeru nako ni daftari jipya?
 
Ni kwanini MMK hataki kutuwekea mnyambulisho wa matokeo ya 2010 na 2012? MMK kama wewe si mnafiki tafadhari tuwekee mnyambulisho wa kila kata!!

Watu wengine jehanamu yenu itakuwa tofauti!! Hizi ngozi mnazojivisha eti muonekane wema then mtuangamize mtaishia pabaya!!
 
Ni wajibu wako kupambana na vikwazo na maonezi yote hayo. Ndiyo maana wengine tunasema kwenye wanasiasa wa Tanzania walioko upinzani Mtikila ndiyo shujaa, yeye hana longolongo bali akiona SIYO unakutana naye Mahakamani na ANAKUSHINDA!!
 
Swali la ujenzi ili.
 
Kuna paramaters nyingi tuu zimetajwa kuwa kigezo,na kuna maeneo nyingine hazikuwa na mchangi mkubwa kama kwingine.Kuna sehemu daftari kutofanyiwa arekebisho kumepunguza tuu gapa yaushindi,ila kwingine kupepungura kura muhimi kwa ushindi hasa sehemu ambayo CDM wangeshinda kwa ushindi mwembamba.Hujaoongelea vitisho kwa wana CDM iliw asitokee ktk kura,kampeni, na mengine mengi yakiwepo ununuzi wa shahada, etc.

Arumeru daftari ingebadilishwa ushindi ungeongengezeka mara dufu.Sioni kwanini unajilimit kifikra namna hii as if hujawahi sikia factor nyingine zinazotumika kulazimisha ushindi kwa CCM.Kama ni kutumia ujinga wa watanzania,hujawahi jiuliza kwa jinsi CCM walivyo desperate wapo tayari kutumia issues hatari km udini ,ukabila,na ukanda bila woga(madhara tumeyaona) ili tu washinde,ungekuwa CDM nawe ungetumia hayo ili ushinde kama CCM?Huko ni kuwa irresponsible kama MMK ktik kuandika.
 
Ni wajibu wako kupambana na vikwazo na maonezi yote hayo. Ndiyo maana wengine tunasema kwenye wanasiasa wa Tanzania walioko upinzani Mtikila ndiyo shujaa, yeye hana longolongo bali akiona SIYO unakutana naye Mahakamani na ANAKUSHINDA!!

Kama kweli ndivyo ilivyo kwamba Mtikila ndiye shujaa wa siasa za Tanzania inakuwaje hamumuungi mkono ili awasaidie kuwatoa madarakani ccm? ni miaka mingapi tumekuwa tukimsikia Mtikila lakini hatuoni mkimuunga mkono wala akileta mabadiliko ya msingi ya kisiasa nchini? Usiniambie suala la mgombea binafsi, kwani hatima yake tunaifahamu, kama una lingine la kumfanya shujaa niambie.

Chadema ndio chama pekee cha upinzani kwa sasa kinachokubalika zaidi na matokeo ya udiwani katika hizi kata 29 yameonyesha hivyo, hata cuf wenyewe wamepotezwa vibaya afadhali ya tlp angalau wameweza kuirudisha mikononi kata yao moja.

Na hizi kelele zote zinazopigwa hapa ni kwasababu Chadema ndicho chama kinachotegemewa na watanzania wengi kuwasaidia kubadilisha mustakabali wao wa maisha. Vinginevyo basi tungekuwa tunazungumza habari ya cuf ama DP hapa lakini ukweli ndio huo kwamba Chadema ndio matarajio ya wananchi.
 
Nadhani wengine wana divided mind (stagering faith) kwamba hivi kweli CCM itasalimika ama ama hivi kweli CDM itashinda? Yaani hawako katika perseverance na persistence ya ku persuade kuleta ushindi bali wanatamani kufikia ushindi kama vile unapewa zawadi expensive ambayo hukutolea jasho kuilipia.

Kwa mtu yeyote mwenye dhamira njema, mapenzi mema na mwenye kujali wenzake kulaumu makamanda walioko field ni kuwa provoke pasipo lazima na kuwakatisha tamaa..Watu wame uawa wengine wamevunjwa viungo vyao wamedhalilishwa, wameacha ku-enjoy na family zao kila siku wako barabarani then badala hata ya kupongeza huo ujasiri tunathubutu kuwalaumu? By the way kama na sisi tulishiriki ni vipi tulishindwa kuleta hiyo expectation tunayowabebesha wenzetu?

Ninakasirika na sitaki tena kusikia haya wheather tunashinda ama tunashindwa we can never give inn never give up tutaendelea na mapambano come 2015 come not; we will still continue maana dhamira yetu ni kuleta haki usawa na maendeleo na tunafanya kwa nguvu akili na uwezo wetu wote.....Shujaa wa kweli haogopi mapambano na wala hajilaumu bali anajifunza kwakadri anayopata nafasi ya kufanya hivyo....

Natamani sehemu kidogo ya uzalendo ulionao ingewezekana kumgawia huyu mtu anaitwa MM,Tanzania
yetu isingekuwa hivi ilivyo,lakini any way bado tunaendelea kumtumaini Mungu kukomboa Tz yetu kwenye
mikono ya mafisadi na vibaraka wao akina MM.
 
Ni kwanini MMK hataki kutuwekea mnyambulisho wa matokeo ya 2010 na 2012? MMK kama wewe si mnafiki tafadhari tuwekee mnyambulisho wa kila kata!!

Watu wengine jehanamu yenu itakuwa tofauti!! Hizi ngozi mnazojivisha eti muonekane wema then mtuangamize mtaishia pabaya!!

mimi tangu nipitie alichoandika humu ndani na nje ya JF sin hata chembe ya mashaka na mission ambayo huu jamaa anayo.Nasikitika ali fanikiwa sana 2010,ila this time kuna sizable number of people hawapo tayari mpatia blank cheque jsut because ni "too popular ktk media".Mwenzie Mkandara alishaumbuka na sasa ana maeneo yake kuchangia habari za akina ponda. "theory yao ya change, sijui "right thing' 'right way" watazitumia sana na mh Zitto wao na si CDM.Na by now hawawezi tena itumia kama circle ya kuwaweza wananchi ktk cyclic reasoning.
 
Kama kweli ndivyo ilivyo kwamba Mtikila ndiye shujaa wa siasa za Tanzania inakuwaje hamumuungi mkono ili awasaidie kuwatoa madarakani ccm? ni miaka mingapi tumekuwa tukimsikia Mtikila lakini hatuoni mkimuunga mkono wala akileta mabadiliko ya msingi ya kisiasa nchini? Usiniambie suala la mgombea binafsi, kwani hatima yake tunaifahamu, kama una lingine la kumfanya shujaa niambie.

Chadema ndio chama pekee cha upinzani kwa sasa kinachokubalika zaidi na matokeo ya udiwani katika hizi kata 29 yameonyesha hivyo, hata cuf wenyewe wamepotezwa vibaya afadhali ya tlp angalau wameweza kuirudisha mikononi kata yao moja.

Na hizi kelele zote zinazopigwa hapa ni kwasababu Chadema ndicho chama kinachotegemewa na watanzania wengi kuwasaidia kubadilisha mustakabali wao wa maisha. Vinginevyo basi tungekuwa tunazungumza habari ya cuf ama DP hapa lakini ukweli ndio huo kwamba Chadema ndio matarajio ya wananchi.
Unajadili mantiki yangu au maudhui ya bandiko langu??
 
JF sio mali ya Chadema ni jukwaa huru usitake kunifunga mdomo kamanda.

Huwezi kuchangia hata utumbo niuone nikuache tu nitakuwa sijakutendea haki na pia sijatekeleza wajibu wangu wa kuelemisha na kuvua watu magamba kama wewe! nipo na tafakari kilichotokea kwa chaguzi ndogo za udiwani so please hali yangu naielewa kwa sasa usini provoke nikapigwa ban bure!
 
Kama kweli ndivyo ilivyo kwamba Mtikila ndiye shujaa wa siasa za Tanzania inakuwaje hamumuungi mkono ili awasaidie kuwatoa madarakani ccm? ni miaka mingapi tumekuwa tukimsikia Mtikila lakini hatuoni mkimuunga mkono wala akileta mabadiliko ya msingi ya kisiasa nchini? Usiniambie suala la mgombea binafsi, kwani hatima yake tunaifahamu, kama una lingine la kumfanya shujaa niambie.

Chadema ndio chama pekee cha upinzani kwa sasa kinachokubalika zaidi na matokeo ya udiwani katika hizi kata 29 yameonyesha hivyo, hata cuf wenyewe wamepotezwa vibaya afadhali ya tlp angalau wameweza kuirudisha mikononi kata yao moja.

Na hizi kelele zote zinazopigwa hapa ni kwasababu Chadema ndicho chama kinachotegemewa na watanzania wengi kuwasaidia kubadilisha mustakabali wao wa maisha. Vinginevyo basi tungekuwa tunazungumza habari ya cuf ama DP hapa lakini ukweli ndio huo kwamba Chadema ndio matarajio ya wananchi.

Mkuu wangu, hoja ya msingi hapa si nani ni shujaa, bali ni dhahiri Rev. Mtikila amejipambanua kama mwanasiasa anayeweza kuidai haki hata mbele ya mahakama ndani ya mfomu huu huu ambao wengi wetu tunauona ni kandamizi.

Je ni sahihi kwa CDM kuendelea kulalamika na kuishia kutoa matamko ya kisiasa? Ni kwa nini tusiende mbali zaidi kama afanyavyo Rev. Mtikila? Je ni sahih kwa watanzania wanaonyimwa haki yao ya kuchagua viongozi wao kuendelea kulalamikia Tume ya uchaguzi badala ya kuipeleka mahakamani? Na kwa nini kitengo cha sheria ndan ya CDM kisiratibu hili?
 
Huwezi kuchangia hata utumbo niuone nikuache tu nitakuwa sijakutendea haki na pia sijatekeleza wajibu wangu wa kuelemisha na kuvua watu magamba kama wewe! nipo na tafakari kilichotokea kwa chaguzi ndogo za udiwani so please hali yangu naielewa kwa sasa usini provoke nikapigwa ban bure!

Narudia tena JF sio mali ya Chadema...usijipe majukumu ya mods.
 
Back
Top Bottom