Kisingizio: Daftari la Wapiga Kura, vyombo vya dola. Sababu?

hiyo ndio mission yake,mkuu ndio maana kashawishi uasi wa wanachama.Atakuja na posting ndeefu sana halafu hana tafiti yoyote inayoweza thibitisha kuwa hizo factors hazikuwa na effect au hata effect zake ni negligible.

Mbaya kasahau kuwa ingekuwa kinyume basi wanachama ndio wangelaumiwa kwa kutopiga kura.
Sasa atafanya tafiti vipi wakati yeye yuko Detroit? anataka watu wawajibike wakati yeye anabofya keybord akiwa Mac Donald wakati wenzake wapo kwenye Battle Field.
 
Kwani hujui Mwanakijiji ni mmoja wa waasisi wa CCJ?

Thats why" hata siku moja hakuna mtu anaweza kunishawishi kuwa MM ana dhamira ya
dhati ya kuchangia mabadiliko kwenye hili taifa zaidi ya kutaka kuharibu pale ambapo
mabadiko yanachomoza kwenye hili taifa.
 
Mkuu, nimeipenda hiyo MMJ ndio alivyo, hata wafanyeje sijawahi ona kaanzisha uzi wa kuwasifika, makamanda hawalali sie tunaona wanapambana na majitu, imagine CCM more than50 yearz wanatawala, leo tuje kuwatoa kilahisi, mpaka sasa CDM wamejitahidi na tunajivunia kuwa nao...

Ama anataka tuanzishe Chadema Halisi...?

Chadema wamefanya kazi kubwa kuwajengea watanzania hamasa ya kushiriki mchakato wa kisiasa kwa miaka mingi hii nchi ilikuwa imefanywa kama shamba la bibi, mimi sikubaliani na mtanzamo wa mwanakijiji anaongea kama mtu asiyejua ulingo wa kisiasa wa kati chama tawala na CHADEMA, CCM imenunua vyama vingine na kuiacha CHADEMA in isolation, vyama vingine vyote vimeacha kupambana na CCM vinapambana na CHADEMA! Tunawashukuru sana watanzania wanaoendelea kuiunga mkono CHADEMA! Hata kwenye maeneo ambayo hatukusimamisha wagombea 2010 LAKINI TUMEPATA KURA NYINGI SANA, mimi nachukulia huko ni kukua kwa chadema na kuporomoka kwa umaarufu wa CCM! Mwanakiji uje na sababu sijui zipi kunishawishi! Nakusubiria!
 
hiyo ndio mission yake,mkuu ndio maana kashawishi uasi wa wanachama.Atakuja na posting ndeefu sana halafu hana tafiti yoyote inayoweza thibitisha kuwa hizo factors hazikuwa na effect au hata effect zake ni negligible.

Mbaya kasahau kuwa ingekuwa kinyume basi wanachama ndio wangelaumiwa kwa kutopiga kura.

Time will tell,ukombozi uko mlangoni,hauzuiliwi na propaganda za watu kama MM.


Kwani hujui Mwanakijiji ni mmoja wa waasisi wa CCJ?

Kama ndio hivyo? kwanini Tusimuone MMJ kuwa ni9 Janga la Taifa?
YES! I mean it, kama mtu kama yeye tulitegemea ataandika makala ndefu( kiama kawaida yake) kuponda huo mfumo anabaki kuwakatisha tama wanao pambana na huo mfumo?

Madharani: kumetokea fujo kila sehemu hakuna cha Tendwa, NEC wala IGP?

Kweli Mwanakijiji unazeeka vibaya!
 
Sasa atafanya tafiti vipi wakati yeye yuko Detroit? anataka watu wawajibike wakati yeye anabofya keybord akiwa Mac Donald wakati wenzake wapo kwenye Battle Field.

Kumbe yuko Detroit, shabashi, nilifikiri naongea na mtu ambaye yupo hapa! Kumbe anafuatilia kampeni za Obama na Romney halafu anafikiri na tanzania tunaendeshe siasa hivyo! Atuambia wafuasi wangapi wa Republican au wa Democratic walipigwa ngeu kwenye kampeni zinazoendelea!
 
Daftari la wapiga kura na vyombo vya dola vitabebeshwa lawama na labda vinastahili. Lakini katika hili CHADEMA inapaswa kutoa sababu zinazoeleweka zaidi ya visingizio.

Wanachama, wapenzi, na mashabiki wa CHADEMA wanapaswa kuwa wakali kidogo (au sana) ili chama kiweze kutoa maelezo yanayoeleweka ya kwanini matokeo haya hayakuwa mazuri kama watu walivyokuwa wanaaminishwa au kutarajia. Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 CHADEMA ilitakiwa iwe inasukumwa na upepo wa ushindi lakini hali sivyo ilivyo.

Kama majibu ya kueleweka hayapo ipo haja ya haraka ya kuanza kudai watu wawajibike au wawajibishwe.

To be continued....

Kiuhalisia daftari la wapiga kura na uwepo wa shahada za wapigakura ndiyo kwa miaka mingi vitandelea kuwa changamoto kubwa ya CDM na upinzani kwa ujumla.Haviwezi kupuuzwa hata kidogo. Vimebeba haki yote ya mwananchi kupiga kura na kama vikipokwa basi hakuna haki wala ushindi halali kwenye chaguzi.

Ni rahisi sana kwa chama tawala kuproject ushindi maana takwimu zipo mikononi, kinachofanywa ni kuandaa mapema utaratibu wa kununua/kupoka shahada za kupigia kura na kucheza na orodha iliyopo kwenye daftari hii ikiwa ni pamoja na kutokulihuisha. Mchezo huu umetumika sana kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na umefanikiwa.

Hata hivyo, kitendo cha mwananchi kuuza au kukubali shahada yake ichukuliwe ili asipige kura ni tatizo linalotokana na kukosekana kwa elimu ya uraia. Yaani elimu ya uraia inayotolewa na CDM na wapinzani kwa ujumla haijatosha kiasi cha kuwafanya wananchi wafahamu umuhimu wa kupiga kura na kuleta mabadiliko katika maisha yao. Swali gumu ni Je chini ya mfumo wa ufukara uliojikita vijijini unawezaje kumshawishi mwananchi asiuze shahada yake? Akale wapi? Maana hata hiyo kesho yake hajui itakuaje.

Lakini pia ieleweke kwamba kutekeleza shughuli za kisiasa tena za upinzani katika nchi kama yetu ni kazi ngumu sana. Vifo ni vingi, mateso ni mengi, majonzi ni mengi na kwa hakika maumivu ni makubwa. Kwa viongozi wa CDM kupambana na hali kama hiyo na kuweza kufikisha vuguvugu hilo katika kiwango tunachokishuhudia kwenye matokeo haya ya udiwani na mengine mengi si kazi ndogo na ya kupuuza hata kidogo.

Tunaweza kutamani kuiona CDM kweli ikisukumwa na nguvu ya ushindi kuelekea 2015 lakini ni kwa maumivu hayo na watu kujitoa katika kukabili mateso yote hayo.Je ni akina nani wako tayari kupigwa risasi, kufunguliwa kesi zaidi ya nne mahakamani? Na tujitokeze sasa tutoke humu JF twende kwenye majukwaa. Maumivu ni makubwa kwa wachache,wengi wanasubili matunda baada ya wengi kuumia.

Uchaguzi huu mdogo wa madiwani matokeo yake ni mazuri kwa CDM, imeweza kutetea kata zake mbili na imeongeza tatu. CDM imegain na CCM imepoteza. Ni vema tukasubillil tathimini ya CDM ili tuweze kuanza kutoa lawama na hapo ndipo wanamageuzi wa kweli inabidi waanzie kujadili na kupanga mikakati ya kuutafuta ushindi mwaka 2015.
 
MMK at work..a man with mission.Kama alivyokomaa kuwa ufisadi si kitu kikubwa kwa CDM kushikia bango asa anajidhihirisha tena yupo katika mrengo gani.Startistics zinaonyesha idadi kubwa sana ya watu hawakupiga kura mwaka 2010,na wengi ni kwa vile daftari halikufanyia mabadiliko ya kuwajumusha watu,ununuzi wa shahada na mengine.Vijana wa iaka 18,na 19 ni wengi sana na kila mtu anajua kura zao zingekwenda wapi.MMK kaamua tuu kibishi kulifanya si muhimu suala la daftari.Na kaenda mbali kuchochea uasi ndani ya CDM.

Huyu ndiye mshauri wa kujitolea kwa CDM kutoka CCM.Sasa anajianda kuja na makala ndeefu sana kwa kile anachoamini kuwa kapata kit chenye mashiko ,akiamini kapata kitu toka ktk fikra ambcho ni worth kuandika maneno meengi sana.Mbaya zaidi ahjafanya hata research aone ktk parameters zote zinazotumika kuelezea matokeo ya chaguzi na Kwa kiasi gani zilichangia kubadili wingi wa kura kw aupande fulani huku zikiongeze upande mwingine.

Mkulu hana subira kama jamaa wa mbagala ili awahi haribu kabla haujaja uthibitisho utakaomzuia nia yake kutimia.Sasa anataka viongozi waseme nini wakati wengine wana majibu waliyojionea wenyewe?huyu ndie aliyeshindwa sema kama yeye ni mshauri au critics kasema hizo options hazitoshi.Sasa mwenye macho na fikra amtafutie nafasi yake.

M4C ndio imezaa kata 3 jipangeni upya msitafute mchawi.
 
Chama Kinashinda MM anaona is nothing? maovu yanazidi bastora, mikuki na mapanga yeye anaona poa tu, hakuna kilichofanyika? kweli pesa mbaya sana MM kashanunuliwa, Tumsubiri Pasco, labda atakuwa na mawazo chanya...
na huwa nafurahia analysis za Mchambuzi, siyo huyo mameno mengi yanayosukumwa kwa posho!
 
Chadema sio chama cha kitaifa ni chama cha kikanda ndio maana umeona watanzania walivyokikataa kwenye chaguzi za udiwani, ni chama cha kikanda.
 
Mzee Mwanakijiji

Hapa kidogo utakuwa umekosea. Kuanza kuleta mada ya kuaandalia uongozi wa CDM uwe na mazingira ya kuonekana kufail wakati hakuna failure hapo.

Kumbuka CDM ilikuwa na kata chache tu nadhani kufanikiwa kupata kata nyingine 3 ni maendeleo makubwa sana. Kumbuka jitihada hizi zinafanywa na watu wanaofikiria pia. Na hata kufika katika kiwango hiko cha kupata hizo kata pia ni juhudi kubwa zimetumika.

Unaposema unasubiria upate maelekezo ya nini kimetokea yanaweza yasikunufaishe wewe, zaidi ya kuwanufaisha wenyewe CDM kwenye kutambua ni wapi walipoteleza.

Hili sio anguko kwa CDM. Ni anguko kwa CCM kwa kupoteza kata. Hakuna wa kulaumiwa zaidi ya kupongezwa ingawa matarajio yamekuwa hasi kidogo. Kutafuta ukombozi sio kukaa ofisini watakufa watu wengi mpaka kufikia ukombozi kamili.
Hapana kusema kuwa kuongeza kata 3 tu kati ya 29 kwa chadema pamoja na popularity yote hii ni makosa , huo ni mwendo wa konokono kwa chama ambacho kinatarajia kushika dola hapo 2015! Ikumbukwe kuna M4C inatembea nchi nzima nilitarajia sana kuona reflection ya M4C kwenye hizi chaguzi ndogo za udiwani! Tusijipe moyo na hzi kata mbili tatu eti tumeongeza?? Viongozi wa juu waliopewa dhamana ya kuongoza chama lazima waje na majawabu haraka sana kuhusu haya:
1.Tathmini sahihi ya M4C je imeimarisha chama kwa kiasi gani na je iendelee au isimamishwe
2. Ni nini kimepelekea kupata kata chache hivo huku kukiwa na M4C na chadema kuungwa mkono na wananchi wengi kwa michango ya fedha na mawazo na kujitolea kwingi?
3.Mikakati madhubuti kwa ajili ya chaguzi ndogo za ubunge zijazo, kuna umuhimu wa kushiriki? kama ndio kwa nn? kama hapana kwa nn?
4.Mikakati madhubuti ya chaguzi za serikali za mitaa mwakani
5. Mbinu mikakati na malengo ya uchaguzi mkuu wa 2015
Tulio wengi tumevunjika moyo sana na matokeo hayo na tupo kusaidia kujua tatizo liko wapi ili lengo na azma yetu ya kushika dola na kutatua matatizo ya watanzania litimie hapo 2015!
 
M4C ndio imezaa kata 3 jipangeni upya msitafute mchawi.
Kuwa mstaarabu, tushindane kwa hoja, siyo vibwagizo Mkuu, Mfano M4c imezoa kata 3, ulitaka izoe ngapi, kwa nini?
ok niliuliza hivi Unaelewa mana ya VUGUVUGU la mabadiliko?

Mabadiliko huwa hayaji siku moja? Leo masikini kesho tajiri? ok Madhumuni ya M4C unayafahamu? twende kwa hoja,
 
Chadema sio chama cha kitaifa ni chama cha kikanda ndio maana umeona watanzania walivyokikataa kwenye chaguzi za udiwani, ni chama cha kikanda.
kaa kimya wewe gamba! kama huna mchango just keep quite!
 
Kama ndio hivyo? kwanini Tusimuone MMJ kuwa ni9 Janga la Taifa?
YES! I mean it, kama mtu kama yeye tulitegemea ataandika makala ndefu( kiama kawaida yake) kuponda huo mfumo anabaki kuwakatisha tama wanao pambana na huo mfumo?

Madharani: kumetokea fujo kila sehemu hakuna cha Tendwa, NEC wala IGP?

Kweli Mwanakijiji unazeeka vibaya!

Mwanakijijini na wenzake wameifanya kazi yao kw auamkini mkubwa sana.Na si wao tuu wapo pia wachambuzi wengine wa kisiasa ambao kazi yao ni kujenga kwanza jina huku wakipata msaada wa kukubalika na watu fulani,baada ya kujenga status ya usupa staa basi kinachofuatia ndio hii kuibuka na theories fulani huku wakienjoy status yao iliyokubalika kama great thinker.

Tutaona mengi zaidi.Kwa bahati mbaya nimesoma machapisho yake ya nyuma amabyo alikuwa kila akibanwa ana mwambia mtu akatafute,nilimbana aweze links, ingawa pia niliamua fuatilia.NIlichokuwa nikisoma nilipata mshtuko jinsi gani huyu jamaa amekuwa akipata adavantage hivyo,kuna maeneo mambo yapo wazi kabisa kuwa si agenta wa change.ila alijitahidi sana kutumia populism kuwa drag wengine ktk bandwagon.

Huyu jamaa amekuwa akimegewa vipande vidongo vya kueafanya watu wamwone kuwa naye ni mpambanaji wa ufisadi and the sort,kuwa na naye ni mshauri wa CDM na ushauri wake ilileta matokeo km alivyopredict.Ila mimi niliona vitu tofauti,alikwenda kama miangango ya CCM na CUF ilivyokwenda.Sishangai anachofanya hapa.
 
Chama Kinashinda MM anaona is nothing? maovu yanazidi bastora, mikuki na mapanga yeye anaona poa tu, hakuna kilichofanyika? kweli pesa mbaya sana MM kashanunuliwa, Tumsubiri Pasco, labda atakuwa na mawazo chanya...
na huwa nafurahia analysis za Mchambuzi, siyo huyo mameno mengi yanayosukumwa kwa posho!
Pasco hana jipya ni karani wa Lowasa.
 
Kuwa mstaarabu, tushindane kwa hoja, siyo vibwagizo Mkuu, Mfano M4c imezoa kata 3, ulitaka izoe ngapi, kwa nini?
ok niliuliza hivi Unaelewa mana ya VUGUVUGU la mabadiliko?

Mabadiliko huwa hayaji siku moja? Leo masikini kesho tajiri? ok Madhumuni ya M4C unayafahamu? twende kwa hoja,
kata tatu kati ya 29 ni achievement lakini ni sawa na mwendo wa kobe au kinyonga kuelekea kushika dola hapo 2015 lazima tukubali matokeo haya yamekuwa beyond our expectation na viongozi watupe maelezo what actually happened na pia watoe dira kwa chaguzi zijazo ila ni upuuzi kushereekea kata 5 kati ya 29 hasa kwa chadema wangekuwa ADC au PONA au UDP au TADEA walipaswa kushangilia hata kwa miezi miwili lakini for chadema noooooo!!we have to look back and plan the future of our party
 
Sasa atafanya tafiti vipi wakati yeye yuko Detroit? anataka watu wawajibike wakati yeye anabofya keybord akiwa Mac Donald wakati wenzake wapo kwenye Battle Field.

Huyu jamaa anajitahidi sana ku derail kila kitu CDM wanachosimamia ili kuwafanya invalid before 2015.Sasa katoka katika ,viongozi wa kitaifa kuingia ktk kampeni, ka downpaly ufisadi, kaingia katika daftari la wapiga kura sasa.Bado atazidi sana kuandika" irresponsibly".

Ila we hatupo hapa kushuhudia watu wakijitahidi tudanganya just beause wapo kwenye mission na wapo so naive kuthibitisha kuwa wamekuja na "great idea" na theory ya kuendesha siasa za Tanzania.
 
Kuna wakati sijui hujisahau au hukusudia ktk kuwapa ushauri na tahadhari CDM huwa anatumia "tu___,sisi,..." etc kama vile anataka jiweka ktk kundi.
 
labda ungeeleza "wajipange" ndio nini, wameongeza hizo kata 3 kutoka kwa wapigakura wale wale walioichagua ccm uchaguzi kabla ya huu. margin ya ushindi wa ccm imezidi kupungua sana (naongelea idadi ya wapiga kura waliowaunga mkono) ina maana mabalozi wa chadema wanaongezeka day come day go,
lazima, nasema tena lazima tuwapongeze wananchi kwa kutekeleza demokrasia katika mazingira magumu sana na kuonyesha kuwa ni kweli wao ndio wenye nguvu.
hushangai ccm inatumia mpaka majambazi sugu ku-terrorise voters na polisi wamebung'aa tu.

Nadhani wengine wana divided mind (stagering faith) kwamba hivi kweli CCM itasalimika ama ama hivi kweli CDM itashinda? Yaani hawako katika perseverance na persistence ya ku persuade kuleta ushindi bali wanatamani kufikia ushindi kama vile unapewa zawadi expensive ambayo hukutolea jasho kuilipia.

Kwa mtu yeyote mwenye dhamira njema, mapenzi mema na mwenye kujali wenzake kulaumu makamanda walioko field ni kuwa provoke pasipo lazima na kuwakatisha tamaa..Watu wame uawa wengine wamevunjwa viungo vyao wamedhalilishwa, wameacha ku-enjoy na family zao kila siku wako barabarani then badala hata ya kupongeza huo ujasiri tunathubutu kuwalaumu? By the way kama na sisi tulishiriki ni vipi tulishindwa kuleta hiyo expectation tunayowabebesha wenzetu?

Ninakasirika na sitaki tena kusikia haya wheather tunashinda ama tunashindwa we can never give inn never give up tutaendelea na mapambano come 2015 come not; we will still continue maana dhamira yetu ni kuleta haki usawa na maendeleo na tunafanya kwa nguvu akili na uwezo wetu wote.....Shujaa wa kweli haogopi mapambano na wala hajilaumu bali anajifunza kwakadri anayopata nafasi ya kufanya hivyo....
 
Kama ndio hivyo? kwanini Tusimuone MMJ kuwa ni9 Janga la Taifa?
YES! I mean it, kama mtu kama yeye tulitegemea ataandika makala ndefu( kiama kawaida yake) kuponda huo mfumo anabaki kuwakatisha tama wanao pambana na huo mfumo?

Madharani: kumetokea fujo kila sehemu hakuna cha Tendwa, NEC wala IGP?

Kweli Mwanakijiji unazeeka vibaya!

Kwa hayo yote MM anajifanya amefumba macho hayaoni,ningemuona ana dhamira ya dhati ya kutetea
mabadiliko kama angeanzisha topic ya kukemea vurugu na vitisho vya ccm na polisi kwenye kampeni na
hata kwenye uchaguzi.Lakini anachokimbilia haraka ni kuanzisha uzi wa kulaumu viongozi wa CDM,MM
umeshindwa kufanya kazi yako vizuri umetufanya tujue kuwa wewe ni kati ya Tiss wa Tz waliopo kwa ajili
ya maslihi yao.Umeshindwa kujificha sawa na ushauri kwenye Sign ya Invisible.
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom