Kisiasa Nini Maana ya Uteuzi wa Paul Makonda Jana?

WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (14)
1. Dr. Christina Mnzava2. Paulo Christian Makonda
3. Jesca Msambatavangu4. Julius Mtatiro
5. Katherin Saruni6. Abdallah Majura Bulembo
7. Hemedi Abdallah Panzi8. Dr. Zainab Amir Gama
9. Hassan Mohamed Wakasuvi10. Paulynus Raymond Mtendah
11. Almasi Athuman Maige12. Pamela Simon Massay
13. Kajubi Diocres Mukajangwa14. Kadari Singo
Jamani yupi katika orodha hii anatokea CHADEMA? maana hao niliowawekea RED - CUF na BLUE - CCM .
Hassani Wakasuvi ni mwenyekiti wa CCM mkoa Tabora, mwenyekiti wa vyama vya ushirika Tanzania, Mjumbe wa vyama vya ushirika Afrika na Ulimwenguni, hivi malengo yanayofanana maana yake ni nini?
 
Naomba Kuelimishwa.....hivi "malengo yanayofanana" ni nini hasa.....ni vigezo gani vilitumika kuchagua watu wenye "malengo yanayofanana"..........
 
Kijana Makonda kweli ana guts!! kawatukana viongozi wote wa dini mbili kuu Tanzania kuwa wote ni ombaomba!! eti wanaomba misaada kutoka kwa mhe Lowassa!! na mhe Malecela kamuunga mkono -----ndivyo tuleavyo watoto wetu kana kwamba hakuna miiko, kule kuchaguliwa tena kuwa mbunge kwenye bunge la katika yaonyesha kuwa taifa linaekea kubaya kuhusu malazi ya watoto.

Malazi ya watoto? Badala ya kumsifia kijana yuko vizuri na nchi inahitaji vijana wenye akili kama makonda. We unamponda. Wewe ndo walewale lowasism shenzytypes.
 
W. J. Malecela aka Le Mutuz hayupo kwenye kundi lolote?

:biggrin1::biggrin1::biggrin1:
Sifa kuu ya kwanza ni awe Mtanzania mwenye akili timamu!. kisha ndipo haya mengine yote yanafuata!.
2. Akina nani watakuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba?

Kulingana na kifungu cha 22 kifungu kidogo cha (1) aya (a), (b) na (c) cha Sheria Nambari 8 ya 2011, Wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa: Kwanza, Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili, Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.Tatu, wajumbe 166 watakaopatikana kutoka katika Taasisi zisizo za kiserikali, Jumuiya za kidini, vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa, Taasisi za elimu ya juu, shirikisho la wafanyakazi,shirikisho la wakulima,shirikisho la wafugaji, shirikisho la watu wenye mahitaji maalum, na kikundi chochote cha wananchi kinachojulikana kwa jina lolote ambacho kina malengo yanayofanana.
Pasco.
 
QUOTE=Field Marshall ES;8634302]Wiki moja iliyopita Mh. Makonda alifanya mkutano na Waandishi wa Habari na kusema maneno mazito sana kuhusiana na mbio za Urais 2015, wakatokea Viongozi wengi waliomjibu kwamba amekosea na wengine wakaamuunga mkono kuwa yupo sawa jana Rais wa Jamhuri amemteua kwenye Bunge la Katiba,

Maana yake inaweza kuwa nzito sana depending na nani anaisoma hii situation, ila kwa maneno rahisi sana bila kuchanganya habari ni kwamba Rais anku

baliana na maneno ya Makonda kwenye ule mkutano wake na waadishi, au mnasemaje?

FMES - Wazeee Wa Sauti Ya Umeme.[/QUOTE]


FUTA NENO MH TAFADHARI
 
Ukitaka kuteuliwa na serikali iliopo madarakani fanya hivi:
Itisha press conference. Mlipue Lowassa, mtukane na usimumunye maneno wala nini.
Haitapita wiki utasikia umepewa fursa serikalini
 
Jamani, ile hadithi ya mizigo iliishia wp? Kama haijaisha basi mizigo bado ni mingi na wakuiondoa ni Mm na Ww 2015 sio mbali ya nn kulalama? Waliowahi kufanya mitihani kuna muda WA pens down tatizo liko wp? Its just matter of time, Makonda is a small creacher, we need big potato to be removed.
 
W. J. Malecela aka Le Mutuz hayupo kwenye kundi lolote?

:biggrin1::biggrin1::biggrin1:


Sifa kuu ya kwanza ni awe Mtanzania mwenye akili timamu!. kisha ndipo haya mengine yote yanafuata!.
Kulingana na kifungu cha 22 kifungu kidogo cha (1) aya (a), (b) na (c) cha Sheria Nambari 8 ya 2011, Wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa: Kwanza, Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili, Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.Tatu, wajumbe 166 watakaopatikana kutoka katika Taasisi zisizo za kiserikali, Jumuiya za kidini, vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa, Taasisi za elimu ya juu, shirikisho la wafanyakazi,shirikisho la wakulima,shirikisho la wafugaji, shirikisho la watu wenye mahitaji maalum, na kikundi chochote cha wananchi kinachojulikana kwa jina lolote ambacho kina malengo yanayofanana.

Pasco.

cc: W. J. Malecela
 
CCM tunahitaji Vijana kama Makonda wenye ujasiri wa kusimama na kuhesabiwa bila kujali anything, inaitwa Speak the Truth and let the chips fall where they may!!

Nasikia Malawi wanapokea wakimbizi kudadeki!!, mtalijua jiji!!

Es
hakuna atakaekimbia nchi kamanda Lowasa amesema tutapigana na tutashinda pamoja. Lowasa Kasema wanaotaka aondoke waseme aendelee wapi?
 
Mkuu Pasco, hili ni jiwe..
LOWASSA UNA SAFARI NDEU SANA.

Mwakani 2015 Tanzania tutakuwa na uchaguzi wa Rais, na akama kawaida kutokana na udhaifu mkubwa wa vyama vyetu vya Upinzani tayari ni dhana inayokubalika wazi na kila

mwananchi wa Taifa hili kwamba ni mgombea atakayepitishwa na CCM ndiye mwenye nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo. Tayari kumekuwa na utabiri mwingi sana wa kisiasa

kutoka kwa wananchi wengi wakijaribu kuona kwa mbali nani ndani ya CCM ana nafasi kubwa ya kupewa nafasi hiyo na chama hicho kikongwe na ambacho mpaka sasa ndicho

kihistoria kimetawala kwa muda mrefu sana katika bara la Afrika kuliko vyama vyote vikongwe vya siasa. Leo Tanzania huwezi kuongelea utabiri wa Mgombea Urais wa CCM

Mwakani bila kulitaja jina la Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa sasa wa Monduli, Mheshimiwa Edward Lowassa. Aidha ni lazima umtaje kama ndiye mwenye nafasi kubwa au

hamuwezi unayemtabiri kushika nafasi, lakini kwa njia moja au nyingine ni lazima umtaje. Ni Mtanzania kama Watanzania wengine wote anayo haki ya kugombea nafasi yoyote ya

uongozi nchini kwa hiyo kwake kugombea Urais Mwakani kama inavyoeleweka sasa hivi sio kuvunja sheria au Katiba ya CCM isipokuwa ni kutimiza haki yake kisheria ya Jamhuri

ya Muungano. Mh. Lowassa ameshika nafasi nyingi sana za uongozi wa Taifa toka enzi za Awamu ya kwanza mpaka Awamu hii sasa alipoweza kufikia kuwa Waziri Mkuu, nafasi

ambayo alilazimika kuiachia aada ya tuhuma nzito za kitaifa kwamba alihusika sana na Mkataba mbovu wa umeme wa Richmond. Toka siku alipoamua mwenyewe kuachia ngazi

hiyo ya Uwaziri Mkuu, kwa maneno yake mwenyewe ya hivi karibuni huko Monduli, ni kwamba amekuwa akifanya kila analoweza kisiasa kujiweka katika mstari na ndoto zake za

siku moja kuwa Rais wa Jamhuri hii ya Tanzania na akawaomba wale wote wanaomuombea mema kumsaidia kuelekea kwenye ndoto yake hiyo iweze kutimia. Tafsiri yake ni moja

tu kwamba anajitayarisha kugombea Urais mwakani kwa tiketi ya CCM. Toka siku hiyo alipozungumza maneno hayo kumetokea mambo mengi sana ambayo kwa mimi mwanazuoni

ninayeyaangalia kwa jicho la kisayansi zaidi kuwa ni makosa makubwa sana ambayo kama kweli ana nia ya kugombea Urais mwakani, basi ana kazi kubwa sana ya kuyarekebisha

ingawa wakati nao sina uhakika kama utatosha kutokana na ukaribu sana wa uchaguzi kwani kisiasa mwakani ni karibu sana. Kambi yake imefanya makosa mengi makubwa sana

ambayo yanazidi kumpunguzia hadhi na heshima kwa wananchi kama mimi ambao siku zote tunaziangalia siasa zetu kwa jicho pana na ukweli bila kuchanganya maneno wala

kuogopa kusema ukweli wa tunachokiona. Ninachokiona ni kambi yake kukosa watu wenye uwezo mkubwa wa uelewa wa kisiasa za Taifa letu na kimatendo na kwa lugha rahisi

zaidi wengi wao sio wanasiasa wakweli bali ni wababishaji ambao wameshindwa kabisa kukaa chini na kuangalia njia nzima aliyoipitia Rais wa sasa kufikia alipo.

Rais wa sasa Jakaya Kikwete, ni mfano mkubwa sana tulionao wa nini kinatakiwa kufanywa na kisichotakiwa kufanyika ili mwananchi wa Taifa hili kama Lowassa aweze kupewa

nafasi hiyo kama vile Rais wa sasa alivyopewa wakati ulipokfikia yaani wakati wa Uchaguzi wa Mgombea wa nafasi hiyo ndani ya CCM. Rais Kikwete baada ya kukataliwa nafasi

hiyo mwaka 1995 hakupoteza muda wake mwingi kulalamika, isipokuwa alihakikisha kwamba wahusika wote ndani ya CCM wanameuelewa kwamba sio mgombea wa wasiwasi

hasa baada ya kumshambulia bila woga mbele ya umma Katibu Mkuu wa CCM wa wakati ule aliyekuwa Shemeji wa Mwalimu Baba wa Taifa kwa kuhusika sana na kumkosesha

nafasi hiyo na kitendo cha Katibu huyo kuondolewa kwenye nafasi hiyo mara baada tu ya ule uchaguzi ilikuwa ni ujumbe tosha kwa wahusika wote ndani ya CCM kwamba alikuwa

ni mgombea aliyekuwa anajua anachokifanya. Baada ya pale Rais Kikwete alijikita kwenye kujenga dhana ya kuaminiwa na Viongozi karibu wote muhimu wa CCM wa wakati huo,

akiwemo Mwenyekiti wake wa Taifa Rais Mkapa, ambaye alimuamini na kumfanya Waziri wake wa Mambo ya Nje kwa kipindi chake chote cha Miaka Kumi ya Urais, akiwa ni

Waziri wa kwanza kuweza kushika nafasi ile kwa muda mrefu kuliko Mawaziri wote wa Taifa hili waliowahi kushika nafasi hiyo. Rais Kikwete pia aliendelea kujijenga na wananchi na

Viongozi karibu wote wa Taifa hili, alijiepusha sana na migongano ya moja kwa moja na wale wote waliokuwa hawamuungi mkono na kampeni zake za kichini chini za kutafuta

kupewa nafasi ya kuwa mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi. Akajikita zaidi kwenye kuwekeza mioyoni mwa wananchi kwa kutumia kauli mali zaidi kuliko pesa, akaweza

kufanikiwa kuwaweka upande wake Viongozi wengi muhimu wa CCM wa zamani na waliokuwepo kwenye uamuzi wa mgombea Urais Mwaka 2005. Akafanikiwa kuwashika

Waasisi wa CCM kama Mzee Kawawa, Peter Kisumo na Kingunge ambao wote hao walikuwa na nafasi kubwa sana za ushawishi ndani ya chama hicho Tawala. Pia akafanikiwa

kuwashika Umoja wa Vijana wa CCM waliokuwa na sauti kubwa sana na nguvu kubwa ya kisiasa ndani ya chama hicho wakiongozwa na Kiongozi wake makini sana na mwenye

ushawishi mkubwa sana kisiasa wa wakati ule Dr. Emmanuel Nchimbi. Rais Kikwete pia akafanikiwa kuwashika wahadhiri wengi wa Vyuo Vikuu pamoja na wanafunzi wa vyuo

hivyo na akaweza kupenyeza mpaka kwenye tasnia ya Habari nchini ambako alikubalika nao sana kiasi cha waandishi wengi wa habari kukubali kwenda nje ya kanuni za medani za

uandishi wakawa wakijitokeza na kuonyesha wazi kumuunga mkono mara nyingi sana kwenye makala zao za kila siku za wakati ule.

Wakati wote huo Rais Kikwete hakuonyesha kutumia fedha sana na hata kama kuna sehemu alizitumia ilikuwa ni vigumu sana kwa jamii kuhisi kwamba anayeongea amepewa pesa ili

kumfagilia, kwa sababu usingetegemea Waasisi kama Mzee Kawawa au Kingunge kuhisiwa na Jamii kwamba wamepewa pesa ili kumuuunga mkono bali ilikubalika na jamii nzima

kwamba hawa walikuwa wanajitolea kwa kufuata maoni ya mioyo yao kutokana na waliyokwisha yafanya kwa Taifa. Washiriki karibu wote wa kambi yake ya Urais wake walioanza

kujitokeza wazi wazi baada ya wakati kutimia na hasa baada ya jina lake kupitishwa na CCM, Viongozi kama kina Waziri wa sasa wa Nje Membe, Waziri wa Afrika Mashariki MZee

Sitta, Waziri wa Katiba Chikawe walikuwa ni viongozi ambao wanakubalika sana na jamii na ni mpaka leo bado wanaheshimika sana na jamii na ushawishi mkubwa sana kisiasa

mpaka leo. Halafu pia maisha yake rahisi, kauli zake za kiungwana kwa kila mwananchi zilimsaidia sana Rais Kikwete kukubalika sana na jamii mpaka wanamuziki ambao wengi wao

walijitokeza kumuimba na kumtaja sana kwenye kazi zao za sanaa wakimuita "Mtu wa Watu". Binafsi aliendelea kujishusha chini na kujiweka sawa sana wote aliokuwa akiwahitaji

kwa karibu sana ili kutimiza lengo lake la kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Haya yote ni tofauti kabisa na yanayojitokeza sasa hivi kutokea kambi ya Mheshimiwa Lowassa, ambaye kama kweli ana nia ya kuwa mgombea Urais wa CCM basi anayo safari

ndefu sana kuliko inavyoonekana. Kosa kubwa sana la kwanza liliojitokeza kutokea kambi yake hivi karibuni ni pale washiriki wa Sherehe zake za Mwaka mpya walipoanza

kujitokeza hadharani kumuongelea na huku wakijua wazi kwamba Kanuni za CCM zipo wazi kwamba nafasi yoyote ya uongozi wa Taifa inayoshikiliwa na Kiongozi wa CCM ni

marufuku kuanza kujitokeza na kampeni dhidi yake mpaka ruhusa itakapotolewa rasmi chama hicho. Tatizo kubwa nililoliona ni nafasi za kisiasa za waliokwisha muongelea kwenye

umma tayari kwa kweli sina uhakika ni nani anayeongoza kambi hiyo lakini kama kweli ni yeye Mh. Lowassa basi anajiharibia mwenyewe kwa sababu Mwenyekiti wa CCM Singida

sio siri kwamba aligombea Ubunge akashindwa, Guninita naye aligombea Uenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar akashindwa na chama hicho Tawala kilipoteza viti viwili muhumu

sana vya Ubunge chini yake, halafu Mgeja Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye makosa yake ndiyo yameifanya CCM kupoteza viti vingi vya Ubunge Shinyanga, kwa

maana moja kwamba hawa hawakubaliki kisiasa huko Mikoani sasa iweje leo waje wamuongelee kwenye Taifa? Halafu binafsi nimeshitushwa zaidi na Mwenyekiti wa CCJ chama

ambacho kilikufa kabla hakijaanza na yeye akijitokeza kumtetea Lowassa, halafu Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Dar na yeye akijitosa kumtetea Lowassa, hivi kweli wahusika wote wa

kambi yake wanaamini kwamba hawa waliokwisha jitokeza wanaweza kuwa ndio waongeaji wakuu wa kambi hiyo na kukubalika na Taifa? Kwa maneno mengine kisiasa

wanatuambia wananchi kwamba Mh. Lowassa akishika nchi hawa ndio tuwatarajie kuwa Viongozi wetu wakuu wa Taifa?

Majuzi akatokea msemaji mwingine wa kumtetea Mh. Lowassa yaani Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, tena bila hata ya aibu akasimama na kusema Mkoa huo

hawataruhusu mgombea wao kushambuliwa na wao wakanyamaza kimya ni wapi uliwahi kusikia Rais Kikwete alipokuwa anatafuta urais akisememewa maneno kama hayo ya

kibaguzi yaliyokaa Kimkoa Mkoa? Wana maana Mh. Lowassa atakuja kuwa Rais wa Mkoa na sio Taifa tena? Wanatuambia mapema sana kwamba tutegemee Rais atakayeongoza

kwa kujali sana Mkoa wake kwanza kwa sababu ulisimama kidete kumtetea kuwa Rais? Ukiwaangalia wasemaji wake wote unabaki unajiuliza swali kama kweli wanayoyasema ni

kutoka mioyoni mwao au ni kwa sababu ya kupewa na kuahidiwa chochote na kambi hiyo maana huwezi kusema leo kwamba Kiongozi wa UVCCM Taifa Makonda na Waziri

Mkuu mstaafu Mh. Malecela walipo ongea kushambulia kambi hiyo walikuwa wametumwa au ------------, lakini huwezi kusema kwamba Mwenyekiti wa zamani wa CCJ ambaye

hatujawahi kumsikia hata mara moja akiongea kwenye umma akijitokeza ghafla na kusema maneno ambayo hayana uzito kabisa kisiasa. Kwa sababu kujiunga au kusaidia chama

chochote cha siasa Tanzania bila ya kujitangaza kwa umma sio kuvunja sheria aidha ya CCM au ya Jamhuri, ndio maana Dr. Slaa ilipobainika kwamba anazo kadi mbili za moja ya

Chadema na nyingine ya CCM, hakuna kiongozi wa CCM aliyejitokeza na kusema wataifuta kadi yake ya CCM au kumshitaki kwa sababu kama aliowataja Mwenyekiti huyo wa

chama kilichokufa kabla ya kuanza hawakuvunja Sheria. Sasa unabaki unajuliza hivi kweli Mh. Lowassa akiishia kukosa nafasi hiyo ya kuwa mgombea Urais wa CCM kweli

atawalaumu maadui zake au watetezi wake?

Mimi nilidhani angefuata njia za Rais Kikwete za kujenga madaraja na wale wote wasiomkubali tena kimya kimya, sasa ukishaanza kuwashambulia wasiokukubali mbele ya umma

kama anavyofanya anatuambia nini kuhusu uwezo wake kama Rais? Atakuwa Rais wa wale tu wanaomuunga mkono na wale wasiomuunga mkono kama Makonda na Mh. Malecela

nini itakuwa hatma yao katika Taifa ambalo yeye ni Rais? Kama kweli Mh. Lowassa ana nia ya kutimiza ndoto yake kama alivyosema mwenyewe basi ameanza vibaya sana kwa

maoni yangu kwa sababu binafsi nilidhani amejifunza sana kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge uliomuhusisha Mkwe wake kule Arumeru na kampeni ambazo alihusika nazo sana

kwenye kuziendesha kwa kushirkiana na hawa wasemaji sasa leo anapoyarudia tena makosa yale yale inastaajabisha kwamba atakuwa ni Rais au mwanasiasa wa namna gani

asiyejifunza kutokana na makosa?

Kitendo cha jana cha Rais wa sasa kumteua Paul Makonda kwenye Wabunge wapya wa Bunge la Katiba baada ya yote yaliyotokea wiki mbili zilizopita, na hotuba nzito ya Rais

Mbeya majuzi kwenye sherehe za Miaka 37 ya CCM ambayo sio siri ilikuwa inashabiana kwa njia moja au nyingine na ile ya Makonda iliyoleta kizaa zaaa na Kambi hiyo ya

Lowassa, ni dalili kuwa sana za mawingu kwamba kambi hiyo inahitaji sana marekebisho au ukaratabati. Kama kweli wana nia ya kushika dola kupitia CCM basi ni lazima wakubali

na kufuata njia na misingi ya CCM inayoongazwa na kanuni pamja na katiba ya chama hicho ambayo la msingi sana inakataza kuanza kampeni za urais mapema kabla ya

kurushusiwa na chama hicho. Lowassa akae chini na kujitafakari kama kweli hao washauri alionao sasa hivi wanaweza kumvusha kufikia kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya

CCM, ajitahidi kujenga maraja badala ya kuyabomoa kama anavyofanya sasa hivi kwa kusemewa na Viongozi ambao siosiri wengi wao hawana sifa kabisa za uongozi uliotukuka.

Walimshauri vibaya toka alipokuwa anajiuzulu u-Waziri Mkuu badala ya kusimama pale bungeni na kujitetea kama anavyofanya sasa, na sasa wanamshauri vibaya sana namna ya

kufanya kampeni zake kwenda mbele, wasemaji wake wengi wanaonekana kama waigizaji wa Cinema, sijui ni nani huko kwenye kambi yao aliyemruhusu Mwenyekiti wa zamani wa

CCJ kuongea kwa niaba yake akaikumbusha CCM machungu ya kutaka kuvunjika vipande kwa sababu CCJ sio siri ilikuwa ni tishio sana sasa kwa kuwakumbusha yale machungu

yaliyokwisha sahaulika ni kweli alikuwa anamsaidia Lowassa? Sawa inawezekana sio kweli Lowassa mwenyewe hawatumi, lakini basi awakataze wanyamaze kwanza mpaka filimbi

ikishapulizwa, lakini kwa wakati atafute washauri wengine wanaoweza kuongea mbele ya umma na kueleweka kama sio kukubalika. Ni haki ya kila Mtanzania kugombea Urais, lakini

pia ni muhimu kuheshimu kanuni za chama unachotaka kukitumia kugombea, kugombana mbele ya umma na viongozi wenzako wa Chama sidhani kama inaweza kumsaidia

mgombea na mifano ipo wazi ya Wagombea wote waliowahi kushinda nafasi hiyo ya kuiwakilisha CCM kweye Urais, hawakuwaji kugombana na yoyote ndani ya chama chao, wale

waliotaka au kuonyesha dalili za magomvi na wengine ndani ya chama hicho historia ya chama hicho CCM ipo wazi waliishia kuwekwa pembeni.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

WILLIAM MALECELA + 255 717 618 997
williammalecela.blogspot.com/willymalec@gmail.com
 
Back
Top Bottom