Kisa cha wauwaji wa Botswana na fundisho la kuwapa watoto majina yasiyo na historia mbaya

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,372
17,919
Habari wana JF?

Leo katika pita pita yangu mitandaoni nikakutana na habari ya kunyongwa wauwaji wa dereva teksi (cab Driver/ Tax Driver) huko nchini Botswana.

Niliposoma tu ile habari kengele ya kuashiria kuna jambo baya au sio la kawaida linalo husiana na hii habari. Kengele hiyo haikuwa juu ya ukatili waliotenda hao jamaa wawili mwaka 2013 wa kumshambulia kwa kisu mara arobaini na nne (44) na kukatisha uhai wake ndugu Vicent Mopipi kule mjini Gaborone.

Kilicho amsha ubongo wangu kwa kengele ya tahadhari ni mojawapo ya majina ya wauwaji, anaitwa Moabi Mabiletsa. Nadhani hadi kufikia hapo kwa wale wenye kusoma Biblia watakumbuka jina linalo fanana na hilo, yaani Moabi au Moabu ambalo ni jina la mtu na jina la kabila la wamoabi.

Kabla sijaenda kutafuta historia ya Moabi ilibidi nirudi kuangalia habari zaidi kuhusu ya kesi ya hao wauaji. Nawaita wauaji sababu wamekutwa na hatia na wamesha nyongwa. Nilipoangalia historia ya kushindwa kwao rufaa na kesi ya awali nikakuta hawa jamaa wana historia ya uhalifu, kama hiyo haitoshi kukushitua nikakuta huyu Moabi ndiye ana historia ya kuhukumimiwa kwa makosa makubwa zaidi ya uhalifu kama ya ujambazi, na alishahukumiwa kifungo cha miaka mingi jela hapo kabla.

Nirudi kwenye historia ya wamoabi (Moabites) au ya mtu aitwae Moabi (Moab) kwenye Biblia takatifu. Huyu jamaa na nduguye Ben-ami au nimuite Amoni walikuwa watoto na wajukuu wa Luti (Lot) kwa wakati mmoja. Haujastuka kitu kwenye hiyo kauli hapo juu?

Kama unahisi nimekosea kuandika uhusiano wa hao watoto wa binti za Luti na baba yao nakuondoa wasiwasi sijakosea, hawa ni zao la dhambi ya tendo la ndoa kati ya Luti(Lot) na binti zake wawili, Hawa ni kati ya watu watatu(3) tu walio okoka toka na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu alipopiga kiberiti mji wa Sodoma na Gomora. Najua sasa wengi wameanza kupata picha ya maana ya kichwa cha habari yangu kwenye bandiko hili.

Simulizi kutoka kwenye kitabu cha Mwanzo (Genesis) zinaeleza mabinti wa Luti walimvizia baba yao alipokuwa kalewa mvinyo na kumpa uroda(penzi) ndipo kutokana na tendo hilo wakazaliwa hawa watoto na wajukuu wa Luti yaa Moab na Amoni na kuunda kabila la Moabites na Ammonites (hapa niweke sawa huyu sio Hammonize Konde Boy).

Ndio hivyo wadau, jasiri haachi asili yake, ni kama ilivyo asili ya hao mabinti wa kutoka Sodoma na Gomora waliendeleza yale waliyo yashuhudia na kuyaacha ktk ardhi ya kwao waliko zaliwa kabla ya kuhamia mji mpya baada ya adhabu ya moto. Mji huu mpya kwa sasa ni eneo la nchi ya Jordan.
Nadhani mnaona mikikimikiki ya viata na uasi wa nchini Jordan.

Unaweza kupata picha kwanini Mzee Luti kwanini alijitolea sana kwa wageni wake pale alipo watetea kwa mabazazi au wafukua mitaro(a.k.a mamende) walipotaka kuwashughulikia wageni wake. Luti aliwaomba na kuwasihi sana wale mabazazi wawachukue binti zake na kuwatendea kadiri ya tamaa yao lakini wasiwatendee ubaya huo wageni wake, na hiki ndio kisa kilicho muokoa Luti na wanawe kwenye janga lile la moto.

Kwa tukio hili unaweza kusema sababu ya hawa watoto kumtendea hivyo baba yao ni kwavile walikosa wachumba wa kuwatuliza mahitaji ya kindoa kule ugenini. Hii ni kutokana na historia ya kabila lao kama ilivyogusiwa kwenye biblia, au mabinti walikuwa na hasira na baba yao kwa kuwathamini sana wageni kuliko damu yake kiasi cha kuwatoa waliwe kibabe na mabazazi kama vile Moud wa bongo xxx rated movie alivyo mtendea yule dada aliye pata umaarufu karibuni baada ya picha lao la pilau kusambazwa mitandaoni!

Wewe ndugu msomaji utaweka maoni yako nini kiliwapelekea watoto wa Luti wampe unyumba baba yao mzazi ukiachana na maelezo ya kwenye Biblia Takatifu.

Turudi kwenye walengwa wakuu wa mada yaani wauwaji wa Botswana hasa huyo ndugu Moabi ambae ni marehemu kwa sasa. Unaweza kuona ile dhana ya kwamba ukimpa mtoto majina ya watu flani basi kuna uwezekano hao watoto wakafuata tabia za ajabu au njema za hao watangulizi wao.

Bila shaka Mshana Jr atakuja kutufafanulia usahihi wa hii dhana kama bado lakini nahisi tayari ipo humu jukwaani hivyo wafukua nyuzi walete kiunganishi (link) tujikumbushe.

Ni hayo tu wadau, nilitamani niendelee kuandika zaidi lakini najiona sina kipaji na ujuzi wa kuandika vizuri nitawachosha tu.

Namimi nasema mambo ni mengi, muda mchache , tuweke comment fupi fupi, Tusichoshane weekend hii.

Habari zaidi soma kwenye Biblia kiatbu cha Mwanzo 19:30 - 38 (Genesis 19:30 -38)
Asili ya Wamoabu na Waamoni 30Loti aliogopa kuishi mjini Soari, kwa hiyo akauhama mji huo, yeye pamoja na binti zake wawili, wakaenda kuishi pangoni, milimani. 31Wakiwa huko, binti mkubwa akamwambia dada yake, “Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanamume nchini wa kutuoa tupate watoto. 32Basi, tumlevye baba kwa divai, ili tupate kulala naye na kudumisha uzawa kwa kupata watoto kwake.” 33Usiku huo wakamlevya baba yao kwa divai, na yule binti wa kwanza akaenda akalala naye. Lakini baba yake hakujua wakati bintiye alipolala naye, wala alipoondoka.

34Kesho yake, yule binti wa kwanza akamwambia yule mdogo, “Jana usiku mimi nililala na baba; leo pia tumlevye kwa divai, kisha wewe utalala naye, na hivyo sote tutadumisha uzao kwa kupata watoto.” 35Basi, usiku huo pia wakamlevya baba yao kwa divai, kisha yule binti mdogo akaenda akalala naye. Lakini baba yake hakujua wakati bintiye alipolala naye, wala alipoondoka. 36Hivyo, binti wote wawili wa Loti wakapata mimba kutokana na baba yao. 37Yule binti wa kwanza akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Moabu. Huyo ndiye baba wa Wamoabu hadi leo. 38Yule mdogo pia akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Ben-ami. Huyo ndiye baba wa Waamoni hadi leo.
Mwanzo 19, Biblia Habari Njema (BHN) | The Bible App

ANGALIZO: Kuna weza kuwa kuna makosa kidogo ya kiuandishi au tafsiri ya majina, nitarekebisha, pia napokea maoni ya aina yote.

Pitia hapa pia BOTSWANA: Ukiua unanyongwa, hawa jamaa wamenyongwa leo asubuhi. - JamiiForums
 
Hapa kuna jambo la kujifunza kuhusu kutafuta wenza wa ndoa. Ukisoma historia ya mama wa hao binti wa Luti alikuwa na ukaidi flani, aligeuka nyuma akageuka jiwe. Watoto walifuata asili ya kukosa subira ya mama yao.

Laiti kama wangesubiria zaidi huenda ipo siku wangepata wachumba wengine wa kuwaoa na kuzaa nao watoto badla ya kuzaaa na baba yao.

Mama yao alikosa uvumilivu akakaidi maagizo ya Mungu na kugeuka nyuma kageuka jiwe(nguzo ya chumvi ), watoto walikosa uvumilivu wa kusubiria waume sahihi kisha wakaishia kuzaa na baba yao.

Ninachosema hapa kwa pande zote za jinsia tujifunze kuwa na subira tunapotafuta wenza wa kuishi nao, wazazi tujiepushe na laana flani zisije kuwaendea hadi vizazi vyetu.
 
Lot and his daughters, one of the most expensive paintings ever sold
christiesinc-20180301-0001.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani a kama majina ya matter sana. Kuna jamaa anaitwa John mzaliwa wa karibu na ziwa Nyanza lakini tabia zake za kikatili na kibabe kitu mtu anazijua
Mkuu ahsante kwa kuuliza swali hili maana umenipa nafasi ya kuthibitisha hoja ya majina na tabia.
Katika biblia ukisoma Marko 3:17 unaona Yesu aliwaita ndugu wawili Yakobo na Yohan(John) wana wa Zabedayo kwa jina la wana wa radi (son's of thunder) ngurumo.
.Jamaa walikuwa watu wenye hasira za karibu sana (short tempered) hawataki masikhala.

Kuna siku Yesu alienda kufanya mahubiri mji wa Samaria akakuta watu hawapo.
John na kaka yake wakamuomba ruhusa Yesu waombe radi ishuke toka mbinguni kuja kuwafundisha adabu wana wa Samaria.
Yesu akawakataza kisha wakaelekea zao Jerusalem.

Umejifunza nini kuhusu akina John na hasira zao na ubabe?
Walikuwa wanataka kuwatumbua wasamaria waliomkataa Yesu, waliokataa wokovu.
Wewe huoni John wa kwenu anavyo chukia watu wanaokataa kukombolewa kwenye umaskini wa dunia ya tatu?

Kingine historia ya John ni watu ambao ni survivors wa kwenye mitihani migumu sana.
John wa kwenye Biblia aliye andika nyaraka kibao na kitabu cha ufunuo ndiye mwanafunzi wa Yesu na mtume wa mwisho kufa kati ya wale 12 wa kwanza.
Huyu alishahukumiwa kifo na kufungwa huko kisiwa cha Patmos huko bahari ya Aegean nchini Uyunani au ugiriki (Greece) ile ya kale, akatumbukizwa kwenye pipa la mafuta ya moto akatoka mzima mwisho alikuja kufa kifo cha kawaida huko kwa Waefeso.
John huyu alitabiriwa kuishi muda mrefu na Yesu mwenyewe. Hili somo jingine.

Kwa hivyo jaribio la sumu au moshi kama wa mitaa ya Namungo hauwezi kumtoa kirahisi John huyo uliye msema.

Soma zaidi Mark 3:17 (Marko 3:17), na Luke 9:51 - 56 (Luka 9:51 - 56)
CC: binti kiziwi Mbwa dume Phoenix fofre
 
Mkuu ahsante kwa kuuliza swali hili maana umenipa nafasi ya kuthibitisha hoja ya majina na tabia.
Katika biblia ukisoma Marko 3:17 unaona Yesu aliwaita ndugu wawili Yakobo na Yohan(John) wana wa Zabedayo kwa jina la wana wa radi (son's of thunder) ngurumo.
.Jamaa walikuwa watu wenye hasira za karibu sana (short tempered) hawataki masikhala.

Kuna siku Yesu alienda kufanya mahubiri mji wa Samaria akakuta watu hawapo.
John na kaka yake wakamuomba ruhusa Yesu waombe radi ishuke toka mbinguni kuja kuwafundisha adabu wana wa Samaria.
Yesu akawakataza kisha wakaelekea zao Jerusalem.

Umejifunza nini kuhusu akina John na hasira zao na ubabe?
Walikuwa wanataka kuwatumbua wasamaria waliomkataa Yesu, waliokataa wokovu.
Wewe huoni John wa kwenu anavyo chukia watu wanaokataa kukombolewa kwenye umaskini wa dunia ya tatu?

Kingine historia ya John ni watu ambao ni survivors wa kwenye mitihani migumu sana.
John wa kwenye Biblia aliye andika nyaraka kibao na kitabu cha ufunuo ndiye mwanafunzi na mtume wa mwisho kufa kati ya wale 12 wa kwanza.
Huyu alishahukumiwa kifo na kufungwa huko kisiwa cha Patmos huko bahari ya Aegean nchini Greece ile ya kale, akatumbukizwa kwenye pipa la mafuta ya moto akatoka mzima mwisho alikuja kufa kifo cha kawaida huko kwa Waefeso.

Nashukuru sana kwa maelezo hayo kuhusu wakina john
 
Pengine hiyo Moabi ya Botswana haimaanishi yanayomaanishwa na Moabi ya Israel. Kuna Mushi ya Japan lakini sidhani kama inamaanisha kinachomaanishwa na Mushi ya K’Njaro.
 
Habari wana JF?

Leo katika pita pita yangu mitandaoni nikakutana na habari ya kunyongwa wauwaji wa dereva teksi (cab Driver/ Tax Driver) huko nchini Botswana.

Niliposoma tu ile habari kengele ya kuashiria kuna jambo baya au sio la kawaida linalo husiana na hii habari. Kengele hiyo haikuwa juu ya ukatili waliotenda hao jamaa wawili mwaka 2013 wa kumshambulia kwa kisu mara arobaini na nne (44) na kukatisha uhai wake ndugu Vicent Mopipi kule mjini Gaborone.

Kilicho amsha ubongo wangu kwa kengele ya tahadhari ni mojawapo ya majina ya wauwaji, anaitwa Moabi Mabiletsa. Nadhani hadi kufikia hapo kwa wale wenye kusoma Biblia watakumbuka jina linalo fanana na hilo, yaani Moabi au Moabu ambalo ni jina la mtu na jina la kabila la wamoabi.

Kabla sijaenda kutafuta historia ya Moabi ilibidi nirudi kuangalia habari zaidi kuhusu ya kesi ya hao wauaji. Nawaita wauaji sababu wamekutwa na hatia na wamesha nyongwa. Nilipoangalia historia ya kushindwa kwao rufaa na kesi ya awali nikakuta hawa jamaa wana historia ya uhalifu, kama hiyo haitoshi kukushitua nikakuta huyu Moabi ndiye ana historia ya kuhukumimiwa kwa makosa makubwa zaidi ya uhalifu kama ya ujambazi, na alishahukumiwa kifungo cha miaka mingi jela hapo kabla.

Nirudi kwenye historia ya wamoabi (Moabites) au ya mtu aitwae Moabi (Moab) kwenye Biblia takatifu. Huyu jamaa na nduguye Ben-ami au nimuite Amoni walikuwa watoto na wajukuu wa Luti (Lot) kwa wakati mmoja. Haujastuka kitu kwenye hiyo kauli hapo juu?

Kama unahisi nimekosea kuandika uhusiano wa hao watoto wa binti za Luti na baba yao nakuondoa wasiwasi sijakosea, hawa ni zao la dhambi ya tendo la ndoa kati ya Luti(Lot) na binti zake wawili, Hawa ni kati ya watu watatu(3) tu walio okoka toka na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu alipopiga kiberiti mji wa Sodoma na Gomora. Najua sasa wengi wameanza kupata picha ya maana ya kichwa cha habari yangu kwenye bandiko hili.

Simulizi kutoka kwenye kitabu cha Mwanzo (Genesis) zinaeleza mabinti wa Luti walimvizia baba yao alipokuwa kalewa mvinyo na kumpa uroda(penzi) ndipo kutokana na tendo hilo wakazaliwa hawa watoto na wajukuu wa Luti yaa Moab na Amoni na kuunda kabila la Moabites na Ammonites (hapa niweke sawa huyu sio Hammonize Konde Boy).

Ndio hivyo wadau, jasiri haachi asili yake, ni kama ilivyo asili ya hao mabinti wa kutoka Sodoma na Gomora waliendeleza yale waliyo yashuhudia na kuyaacha ktk ardhi ya kwao waliko zaliwa kabla ya kuhamia mji mpya baada ya adhabu ya moto. Mji huu mpya kwa sasa ni eneo la nchi ya Jordan.
Nadhani mnaona mikikimikiki ya viata na uasi wa nchini Jordan.

Unaweza kupata picha kwanini Mzee Luti kwanini alijitolea sana kwa wageni wake pale alipo watetea kwa mabazazi au wafukua mitaro(a.k.a mamende) walipotaka kuwashughulikia wageni wake. Luti aliwaomba na kuwasihi sana wale mabazazi wawachukue binti zake na kuwatendea kadiri ya tamaa yao lakini wasiwatendee ubaya huo wageni wake, na hiki ndio kisa kilicho muokoa Luti na wanawe kwenye janga lile la moto.

Kwa tukio hili unaweza kusema sababu ya hawa watoto kumtendea hivyo baba yao ni kwavile walikosa wachumba wa kuwatuliza mahitaji ya kindoa kule ugenini. Hii ni kutokana na historia ya kabila lao kama ilivyogusiwa kwenye biblia, au mabinti walikuwa na hasira na baba yao kwa kuwathamini sana wageni kuliko damu yake kiasi cha kuwatoa waliwe kibabe na mabazazi kama vile Moud wa bongo xxx rated movie alivyo mtendea yule dada aliye pata umaarufu karibuni baada ya picha lao la pilau kusambazwa mitandaoni!

Wewe ndugu msomaji utaweka maoni yako nini kiliwapelekea watoto wa Luti wampe unyumba baba yao mzazi ukiachana na maelezo ya kwenye Biblia Takatifu.

Turudi kwenye walengwa wakuu wa mada yaani wauwaji wa Botswana hasa huyo ndugu Moabi ambae ni marehemu kwa sasa. Unaweza kuona ile dhana ya kwamba ukimpa mtoto majina ya watu flani basi kuna uwezekano hao watoto wakafuata tabia za ajabu au njema za hao watangulizi wao.

Bila shaka Mshana Jr atakuja kutufafanulia usahihi wa hii dhana kama bado lakini nahisi tayari ipo humu jukwaani hivyo wafukua nyuzi walete kiunganishi (link) tujikumbushe.

Ni hayo tu wadau, nilitamani niendelee kuandika zaidi lakini najiona sina kipaji na ujuzi wa kuandika vizuri nitawachosha tu.

Namimi nasema mambo ni mengi, muda mchache , tuweke comment fupi fupi, Tusichoshane weekend hii.

Habari zaidi soma kwenye Biblia kiatbu cha Mwanzo 19:30 - 38 (Genesis 19:30 -38)
Asili ya Wamoabu na Waamoni 30Loti aliogopa kuishi mjini Soari, kwa hiyo akauhama mji huo, yeye pamoja na binti zake wawili, wakaenda kuishi pangoni, milimani. 31Wakiwa huko, binti mkubwa akamwambia dada yake, “Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanamume nchini wa kutuoa tupate watoto. 32Basi, tumlevye baba kwa divai, ili tupate kulala naye na kudumisha uzawa kwa kupata watoto kwake.” 33Usiku huo wakamlevya baba yao kwa divai, na yule binti wa kwanza akaenda akalala naye. Lakini baba yake hakujua wakati bintiye alipolala naye, wala alipoondoka.

34Kesho yake, yule binti wa kwanza akamwambia yule mdogo, “Jana usiku mimi nililala na baba; leo pia tumlevye kwa divai, kisha wewe utalala naye, na hivyo sote tutadumisha uzao kwa kupata watoto.” 35Basi, usiku huo pia wakamlevya baba yao kwa divai, kisha yule binti mdogo akaenda akalala naye. Lakini baba yake hakujua wakati bintiye alipolala naye, wala alipoondoka. 36Hivyo, binti wote wawili wa Loti wakapata mimba kutokana na baba yao. 37Yule binti wa kwanza akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Moabu. Huyo ndiye baba wa Wamoabu hadi leo. 38Yule mdogo pia akajifungua mtoto wa kiume, akamwita Ben-ami. Huyo ndiye baba wa Waamoni hadi leo.
Mwanzo 19, Biblia Habari Njema (BHN) | The Bible App

ANGALIZO: Kuna weza kuwa kuna makosa kidogo ya kiuandishi au tafsiri ya majina, nitarekebisha, pia napokea maoni ya aina yote.

Pitia hapa pia BOTSWANA: Ukiua unanyongwa, hawa jamaa wamenyongwa leo asubuhi. - JamiiForums
Ila inaonekana Dingi nae alikuwa na kiu na mabint zake, mashine inasimamaje sasa kama uko tungi. Lile joto na mtelezo huusikii. Wakati anapiga bao, alikuwa anajua anaota au?

Mambo ya maandiko bwana, sometimes yapo ili kufanya uwepo wa historia.
 
Ndio hivyo mkuu.
Mimi sina majibu zaidi ya hayo maandiko.
 
Mkuu ahsante kwa kuuliza swali hili maana umenipa nafasi ya kuthibitisha hoja ya majina na tabia.
Katika biblia ukisoma Marko 3:17 unaona Yesu aliwaita ndugu wawili Yakobo na Yohan(John) wana wa Zabedayo kwa jina la wana wa radi (son's of thunder) ngurumo.
.Jamaa walikuwa watu wenye hasira za karibu sana (short tempered) hawataki masikhala.

Kuna siku Yesu alienda kufanya mahubiri mji wa Samaria akakuta watu hawapo.
John na kaka yake wakamuomba ruhusa Yesu waombe radi ishuke toka mbinguni kuja kuwafundisha adabu wana wa Samaria.
Yesu akawakataza kisha wakaelekea zao Jerusalem.

Umejifunza nini kuhusu akina John na hasira zao na ubabe?
Walikuwa wanataka kuwatumbua wasamaria waliomkataa Yesu, waliokataa wokovu.
Wewe huoni John wa kwenu anavyo chukia watu wanaokataa kukombolewa kwenye umaskini wa dunia ya tatu?

Kingine historia ya John ni watu ambao ni survivors wa kwenye mitihani migumu sana.
John wa kwenye Biblia aliye andika nyaraka kibao na kitabu cha ufunuo ndiye mwanafunzi na mtume wa mwisho kufa kati ya wale 12 wa kwanza.
Huyu alishahukumiwa kifo na kufungwa huko kisiwa cha Patmos huko bahari ya Aegean nchini Greece ile ya kale, akatumbukizwa kwenye pipa la mafuta ya moto akatoka mzima mwisho alikuja kufa kifo cha kawaida huko kwa Waefeso.
John huyu alitabiriwa kuishi muda mrefu na Yesu mwenyewe. Hili somo jingine.

Kwa hivyo jaribio la sumu au moshi kama wa mitaa ya Namungo hauwezi kumtoa kirahisi John huyo uliye msema.

Soma zaidi Mark 3:17 (Marko 3:17), na Luke 9:51 - 56 (Luka 9:51 - 56)
CC: binti kiziwi Mbwa dume Phoenix fofre
Uko vzr kijana kwny kuchambua
 
Back
Top Bottom