Kisa Cha Mlevi Na Mdada.

Keylogger

Member
Oct 13, 2016
13
14
Ni ijumaa mida ya saa 7 usiku, tangu nitoke ofisini, unajua tena mwisho wa juma nilikua na ratiba ya kuonana na rafiki yangu wa muda pale mchikichini,tukawa katika kibaa kimoja cha watu wa hali zetu ambapo bia za buku jero zinapatikana,ila pembeni kidogo kuna kibanda kina kile kinywaji cha banana, yaani kama pesa ya kununulia bingwa imeisha basi waweza sogea pale pembeni kwenye kibanda na ukapata huduma bila shaka.

Sikunywa sana nilikua najielewa, nikaanza kujisogeza kwenye kituo cha daladala pale ilala boma, yakapita magari kadhaa wa kadhaa ila sikukaa muda sana daladala linaloelekea mabibo ninakoenda likafika likitokea muhimbili.

Nami sikusita nikaingia bahati yangu kulikua na kiti kipo wazi nikakaa tukapita kituo cha kwanza msimbazi wuuuh..raundi ya bauti ya kigogo hadi kituo kipya akaingia mzee fulani nikimkadilia ana kama miaka 70 hivi konda akasema “dereva tembea”, kituo cha mbele akaingia madada fulani unajua tena mida ya saa 7 kwenda saa 8 usiku kila mtu huwa kimya akikumbuka matatizo yake kama si kusinzia, ila huwa hakuna maongezi mengi ndani ya daladala, konda akasema “sogea nyuma wengine wapande”.

Yule mzee bahati mbaya akamkanyaga yule dada, yule dada akaropoka kwa sauti "We mlevi unanikanyaga", yule mzee akasema "Samahani naomba unisamehe" yale maongezi yalinifanya niwaangalie.

Yule mzee alimuangalia vizuri usoni yule dada, dada baada ya kujua kuwa anaangaliwa na yule mzee akaropoka tena "Ushazeeka unaangalia nini nenda kalee wajukuu", mzee alimuangalia tena vizuri na akasema "Ndio nimezeeka ila ninaweza kusema we dada mbaya." dada akaropoka tena kwa sauti "Mlevi wewe mfuuuu..(sonyoo)", yule mzee kwa busara akasema " Mjukuu wangu una sura mbaya" akaendelea kusinzia.

Mmmh...unajua sifa ya pombe haijifichi, kweri yule mzee kalewa tena chakali ikanibidi nimuangalie yule dada vizuri tobaa!! kweli ana sura mbaya.

Upande wangu:
Kubari ukweri hata kama unakuumiza.

Hapa ndo nimeamka ila nikaukumbuka ule mkasa,Ni kweri yule mzee usiku ule alilewa ila asubuhi au hata ikiwa mchana pombe si itaisha? na ikiisha si atakua mtu wa kawaida labda alewe tena lakini yule dada usiku ule alikua anasura mbaya akilala akiamka asubuhi atakua na sura nzuri??

We mwenzangu una maoni gani kwenye huu mkasa??
 
Naona Leo ni wadada wadaladala tu, kuna mwingine alisema walikuwa wanampigisha CHAPUTA ndani ya gari na wewe ndio ivo tena
 
Back
Top Bottom