Kisa cha swahaba wa mtume S.A.W

KASHAMBURITA

JF-Expert Member
Mar 27, 2021
200
630
KISA CHA SWAHABA WA MTUME S,A,W

Ar'wa ibn zubair ulikatwa mguu wake kwa maradhi yaliyokuwa yakimsibu.

Siku hiyo hiyo ambayo alikatwa mguu akafiwa na mtoto wake mmoja kati ya watoto saba aliokuwa nao.

Akasema Ar'wa "Ewe M/Mungu ninakushukuru kwani hakika ww ndiye uliyenipa watoto saba na leo umemchukua mmoja wapo.

Na ww ndiye uliyenipa mikono miwili pamoja na miguu miwili na leo na leo umeuchukua mguu mmoja ambao ulionipa.

Ninakuomba ewe M/Mungu unikusanyishe nami peponi hivi ulivyovichukua leo.

Zikapita siku kadhaa baada ya matukio hayo...ikatokea kipindi fulani Ar'wa akaingia msikitini akamkuta mzee mmoja mwenye umri wa utu uzima sana.

Mzee yule alikuwa akionyesha wazi juu ya uzee wake lakini mzee yule alikuwa ni kipofu haoni.

Akatokezea kijana mmoja akamwambia Ar'wa amuulize yule mzee juu ya maisha yake ya nyuma (yaliyo sababisha mpaka asione)

Ar'wah akamuuliza yule mzee juu ya maisha yake ya nyuma yaliyo sababisha mpaka asione.

Yule mzee Akasema "Ewe Ar'wah mimi nilikuwa nina mali pamoja na watoto.

Ikatokea siku moja tukiwa safarini majangwani pamoja na watoto wangu.

Tukavamiwa na majangili usiku wakawachukua watoto wangu pamoja na mali zangu.

Asubuhi kukapambazuka nikiwa nimebakiwa na mtoto mmoja tu mdogo pmj na ngamia mmoja.

Ngamia ikawa anakimbia baada ya kamba niliyomfunga kuwa imefunguka.

Mimi ikawa namkimbiza yule ngamia lkn sikufika mbali nikasikia kelele za mwanangu mdogo kwa nyuma.

Ikanibidi nigeuke kumtazama mwanangu,nilipogeuka tu nikamuona mbwa akiwa amemng'ata kichwani mwanangu.

Ikanibidi nimfukuze yule mbwa huku nikimpiga lkn ikawa tayari ameshamuua mwanangu.

Nikageuka kumfuatilia ngamia akanipiga na kwato zake usoni mpaka akanichunia na kunisababishia upofu."

Akasema Ar'wah "ulifanya nn ewe sheikh baada ya tukio hilo.?"

Yule mzee Akasema "sikufanya chochote kile zaidi ya kusema....Ewe M/Mungu ninakushukuru umechukua vyote nilivyo kuwa navyo lkn umeniachia moyo.

Moyo wa kukumbuka wewe na ulimi wa kukutaja wewe."

...........Hii ndiyo subra.....

Hawa ndiyo waliobashiriwa na M/Mungu pale aliposema M/Mungu "Kwa hakika tunawalipa wale wenye kuwa na subra malipo yasiyokuwa na hesabu."

Je sisi tuna matatizo gani kulinganisha na kama hao waliopita,mpaka tuhuzunike na kukata tamaa....Je yametufika kuwa kama ya wenzetu hao waliotangulia?????

Wenzetu walisubiri M/Mungu akawabashiria pepo,na sisi tunawaiga wao ni kwa nini sasa tushindwe...?
 
Back
Top Bottom