Kisa cha leo; kama wewe ni mzazi hakikisha unasoma

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
C& P lakini yenye fundisho. Jitahidi kusoma hadi mwisho????

KISA CHA LEO; KAMA WEWE NI MZAZI HAKIKISHA UNASOMA (Hiki ni kisa cha kweli nilichokutana nacho, majina niliyotumia na baadhi ya mambo ni ya kubuni ili kuleta ladha na kumficha aliyekumbwa na tukio hili.)

"Mama, nahisi kama Kelvin anaumwa?" Anna alimuambia Bosi wake Mama Kelvin ambaye alikuwa bize kwenye simu yake akichatI.
"Anaumwa nini?" Alijibu huku akipepesa jicho pembeni kuangalia kama atamuona huyo kelvin.
"Yuko wapi?" Aliuliza huku akirudisha macho yake kwenye simu baada ya kusikia mlio wa sms ya watsapp.
"Amekaa tu kule nnje, nimemuambia akacheze hataki, kula kwenyewe kala kwa shida".

"Hembu kamuite nimuone, asije akawa anadeka tu bure si unamjua..."
"Hapana Mama sidhani kama anadeka, unajua tangu arudi kutoka shule hajatoka humu ndani, akina John walikuja kutaka wakacheze akagoma kabisa!"

"Hee wewe! kamuite sasa nimuone kama anaumwa tumpeleke Hospitali!" Mama Kelvin alifoka Anna alikuwa akimpotezea muda tu akili yake yote ilikuwa kwenye simu.

Anna alirejea baada ya kama dakika tatu hivi akiwa amemshika kelvin mkono.
"Vipi mwanangu unaumwa?" Mama kelvin alimuuliza mwanae huku akimshika shika mahsavuni kuona kama ana homa, alimgeuza geuza bila kuona chochote.
"Hapana Mama." Kelvin alijibu kwa upole.
"Sasa mbona nasikia hutaki kula? Mhhh! Mhhh! Unahamu ya kula nini mwanangu?" Mama Kelvin aliuliza huku akilazimisha tabasamu.
"Nimeshakula!"
"Hajala, chakula chote kakiacha!" Anna alidakia.
"NImekula Dada aliniweke chakula kingi nikashindwa kukimaliza..."
"Hamna hata sijamuwekea chakula kingi..."
"Basi basi msinipigie kelele, huyu ni mvivu tu wa kula, kamuwekee chakula kiingine na sasa hivi msimamie hakikisha anakula kinaisha! Sawa mwanangu uleee na Baba yako akirudi jioni nitamuambia kesho akununulie Game, sawa." Kelvin alitingisha kichwa kukubaliana na mama yake, kwa shingo upande Anna alimchukua tena kwaajili ya kwenda kumpatia chakula.

Kelvin ambaye alikuwa na umri wa miaka saba alikuwa akisoma darasa la pili katika shule moja ya kimataifa. Kutokana na uwezo mkubwa wa wazazi wake alikuwa akikaa bweni hivyo kuja nyumbani nyakati za likizo ambapo ilikuwa ni kila baada ya miezi mitatu. Alikuwa ni mtoto wa kwanza kwa Baba na mama yake akiwa na mdogo wake wakike mwenye umri wa miaka mitatu.

Anna ambaye alianza kumlea Kelvin tangu akiwa na mwaka mmoja kama mfanyakazi wa ndani alikuwa akimfahamu vyema. Muda mwingi yeye ndiye hubaki na watoto, ingawa Mama Kelvin alikuwa ni mama tu wa nyumbani lakini hakuwa na muda sana wa kutulia nyumbani, mizunguko ya hapa na pale ilimfanya kuwa bize sana. Anna alifahamu uchangamfu wa Kelvin hivyo alipomuona karudi kapooza alihisi anaumwa na kuamua kumuambia bosi wake.

********
Hali ile ya ukimya iliendelea kwa muda kidogo lakini ikaisha, uchangamfu wa Kelvin ukarudi tena mpaka ulipowadia wakati wa kutaka kurudi shule ndipo kasheshe linguine liliibuka kwa Kelvin kukataa kwenda shule.
Kwanini hutaki kwenda ashule? Unajua nitakuchapa Kelvin Mama ayake aliongea akimlazimisha kupanda gari.

Mimi sitaki tu Mama, nataka kubaki nyumbani! Kwanini nisisomee huku kama kina Juma?
Kina huma nini? Unataka ubaki huku ili ulete michezo yako! Hakuna gari utapanda na shule utaenda.! Mama yake alifoka, akimshika kunyanyua kupanda kwenye gari. Kelvin alikuwa ambishi alijiviringisha mikononi kwa mama yake mpaka akamchoropoka na kukimbilia kwa Anna huku akilia.

Dada mimi sitaki kurudi shule! Sitaki! Sitaki!? Aliongea huku akilia, akimuomba Anna amuombee kwa Mama yake asimpeleke shule.
Kwnaini hutaki kwenda shule Kelvin kuna nini huko?? Anna aliuliza huku nayeye akitokwa na machozi.
Mimi sitaki tu kwenda! Sitaki Dada!? Aliendelea kulia.

Nyie mnanichelewesha, hamjui kuwa nina mambo mengi ya kufanya.? Mama Kelvin aliongea huku akiwafuata alimshika Kelvin mikono na kumvuruta kuelekea kwenye gari, Kelvin alijiviringishaviringisha na kumsukumamama yake kitu kilichosababisha simu yake kudondoka na kupasuka kioo.

Mshenzi kabisa wewe, ujinga gani huu unafanya!? Aliongea Mama yake huku akimzaba kofi Kelvin alianza kulia kwa nguvu lakini sasa kwa uoga aliingia kwenye gari baada ya kuona mama yake amekasirika, Anna alikuwa akiangalia tu huku akitokwa na machozi bila kulia kwa sautoi.

Miezi mitatu ilikimbia kama maji yanavyoshuka mlima, Kelvin alirejea tena kutoka shule safari hii akiwa mchngamfu kuliko kawaida yake. Alibadilika na kuwa muongeaji, wakati mwingine akiongea hata maneno ya kikubwa.
"Wewe hayo maneno umejifunzia wapi? Ndiyo mnasoma huko shule au kutukanana tu! Nitamuambia Mama yako?" Anna alimuonya mara kadhaa.

"Dada na wewe, unamaindi vitu vidogo! Kwani kusema Baby ni kitu kibaya, Baby si ni mtoto au hujui kiingereza?"
"Najua sana lakini ndiyo uniite mimi baby?"
"Sasa si nikama mtoto wangu mtu wangu wa karibu!" Kelvin alijitetea.
"Wewe endelea tu, nimesema nitamuambia mama yyako, mimi dada yako sitaki huo ujinga?"

"Au nikuite mchumba hahaha hahahaa!" Aliongea Kelvin huku akicheka.
"Kelvin nimekuambia acha ujinga nitakuzibua halafu nikamuambie na Mama! Mbona umekuwa hivyo? Ghafla unajiona umekua?"
"Kwani sijakua? Au mpaka niote matiti?"
"Wewe chizi kweli? Uote matiti kwani wewe mwanamke!" Anna alijibu huku akicheka na kutingisha kichwa kusikitika.

"Si naota tu, kwani mwanaume hawezi kuwa na matiti?" Kelvin aliuliza huku akishika T-shirt yake sehemu ya kifua na kupandisha kuonyesha ishara ya kuota matiti, huku akiitingisha kiuno chake kama mwanamke vile.
"Acha upumbavu! Wewe mtoto wa kiume!" Anna alimfokea huku akimfinya. Kelvin alianza kulia kwa nguvu, bila kusema chochote Anna aliondoka na kumuacha pale akiendelea kulia.

*********
Kama ilivyokuwa mwanzoni muda ulikimbia, likizo iliisha na Kelvin alitakiwa kurudi tena shule. Usiku Anna alikuwa akimpangia vitu vya kwenda navyo shule, wakati huo Kelvin alikuwa sebuleni na wazazi wake akiangalia Televisheni, katika fukunyua fukunyua Anna alishangaa anakutana na Condom ambazo zilikuwa zimefichwa kwenye vimfuko vidogo vya begi la shule la Kelvin.

?Mungu wangu! Huyu mtoto kapata wapi hivi vitu?? Alijikuta anaropoka kwa sauti. Alijihisi kuchanganyikiwa kwani hakujua hata kama Kelvin anajua kile ni nini, alistuka na kuanz akukagua tena na kukuta Condom nyingine zimefichwa kwenye mifuko ya kaptula ya Kelvin, nguvu zilimuishia akabaki amekaa ktu akimsubiri Kelvin kutoka sebuleni kuingia chumbani ili amuulize.

Hizi ni nini?? Anna alimuuliza baada ya Kelvin kuingia chumbani. Kwa mshituko mkubwa na kwa uoga wa hali ya juu, Kelvin alianz akurudi nyuma huku akijitetea.
Mimi sijui, hata sio zangu, sijui ni nani kaweka kwenye begi langu! Kweli sio mimi Dada!?

Sio wewe? Nani kakuambia nimezitoa kwenye begi lako??
Sio mimi! Mimi nimesema tu ?lakini sio zangu?hata sijui ni nini?....? Aliendelea kujitetea na kupongea maneno ambayo hayaeleweki.
Haya si umesema sio zako? Siumesema hujui, ngoja sas animpeklekee Baba yako ni kamuulize! Unaniambia ukweli au nampalekea Baba yako??

Alijaribu kumtishia lakini bado alikataa kusema si zake. Anna alinyanyuka akiw ana zile Condom mkononi na kuanza kutembea kuelekea mlengoni, alishika kitasa cha mlango kufungua lakini kabla hajatoka Kelvin alimkimbilia na kumshika miguu.

Usimuambie Baba, usimuambie ni zangu, usimuambia njoo nitakuambia ukweli!? Alilia huku akimvuta dada yake. Anna aliuachia mlango na kurudi kukaa kitandani.

Baada ya wote kutulia alimuambia kuanza kujielezea.
Nizangu Dada Kelvin alianza kuongea.
Zakwako unajua ni nini lakini??
Dada na wewe, si ni Condoma hizi, au unafikiri mimi mtoto! Hizi condoma kwajaili ya kufanyia mapenzi,. Ukivaa hizi hupati mimba wala ukimwi! Ghafla Kelvin alaibadilika kutoka kulia na kuongea kuhusu condom bila wasiwasi. Anna alikuwa akimuangalia tu na kumuacha atiririke.

Hizi anavaa mwanaume akifanya mapenzi. Ukivaa hizi dada hupati mimba!?
Sasa wewe unabeba za nini wakati unaenda shule? Kwanza umezipata wapi?
Kaniletea John, simama akinipa hela nilikuwa nampa aninunulie, elfu kumi kanipa zote hizi! Sasa hivi sitaki kupata mimba, nikipata mimba Baba ataniua ndiyo maana nimenunua condom.

Upate mimba kwani wewe mwanamke! Nahayo mapenzi umeanza kufanya lini mpaka uwaze habari za mimba?? Anna aliulza kwa ukali, hapo Kelvin alikaa kimya, hakutaka kuongea tena na kila alipoulizwa alimaanisha nini alikataa mpaka alipotishiwa kusemewa tena kwa baba yake ndipo alipoanza kuongea.

Alianza kutiririka michezo ambayo walikuwa wakifanyiana na baadhi watoto wenzao usiku katika mabweni yao ambapo walikuwa wakifundishana mambo ya mapenzi, usiku walikuwa wakiongozana wawili wawili kwenda chooni ambapo walikuwa wakiingiliana kinyume cha maumbile.

Peter ndiyo alitufundisha, yeye anasoma darasa la sita, hatukai bweni moja ila yeye ndiyo mpenzi wangu sasa, hataki niwe na mtu mwingine wkaati wa mapumziko ndiyo hunifanyia chooni, ila yeye yake umbile lake ni kubwa naogopa atanipa ujauzito ndiyo maana nimeamua kutumia Condom. Unafikiri Dada bila Condom sifanyi nani anataka ujauzito, si baba ataniua?? Kelvin aliongea bila wasiwasi, aliongea binti wa sekondari ambaye anaanza kujifunza mapenzi anaogopa mimba.

******
Wakati wote huo Anna alikuwa akibubujikwa na machozi akimuangalia Kelvin kwa huruma hasa namna alivyokuwa akiongea kama mtu mzima kana kwmaba kilikuwa ni kitu cha kawaida. Huku akifuta machozi alimuambia Kelvin kupanda kitandani kulala.

Usimuambie mama wala Baba Dada, wataniua wakisikia nina Bwana?? Kelvin aliongea kama mtu mzima vile.
Sitawaambia wewe lala, hii ni siri yatu.? Anna aliongea huku akimsaidia kupanda kitandani na kumfunika shuka vizuri. Alichukua begin a vitu vilivyokuwa kitandani na kuvipeleka kwenye meza kisha kuzima taa na kutoka akiwa ameshikilia zile Kondom mkononi.

Alipita sebuleni na kukuta wazazi wa Kelvin wameshaondoka, kama mwehu alitembea harakaharaka kuelekea chumbani kwao na kuanza kugonga kwa pupa, taa bado ilikuwa inawaka kuashiria kuwa bado walikuwa hawajalala, alishika kitasa cha mlango ambao ulikuwa wazi bila kuruhusiwa aliingia kwa pupa.

Mama Kelvin alikuwa wkenye kioo akivaa kofia ya kulalia kwaajili ya nywele zake huku Baba Kelvin akiwa kitandani anasomma kitabu.
Kesho Kelvin asiende shule! Sitaki aende shule!? Alifoka kana kwamba yeye ndiyo alikuwa mama Kelvin huku akizitupa zile condom kitandani kwao, hakusikia hata sauti ya Mama Kelvin iliyokuwa ikimfokea kwa kuingia mule ndani.

Huku akiacha kutengeneza nywele zake mama Kelvin alisogea nna kuziangalia zile condom, aliacha kufoka kuhusu kuingia kwake bila kugonga na kuhoji kuhusu Condom. Bila kumung'unya maneno Anna aliwaelezea kila kitu alichoelezewa na Kelvin, mama Kelvin nguvu zilimuishia na kuanza kutokwa na machozi.

Nilikuambia kipindi kile kwa Kelvin ana matatizo hukunisikia, nilipomuona tu mpole nikajua ana matatizo.? Alimalizia kuongea Anna. Mule ndani ulikuwa mshike mshike, Baba kelvini akizunguka zunguka na kibukta chake bila kujali kuwa Anna alikuwa mule ndani. Mzozo uliibuka kwa kuanza kulaumiana, Baba akimlaumu Mama kwa kumpeleka mtoto bweni wakati yupo tu na hana kazi ya kufanya na Mama akimlaumu Baba kwa kuwa bize na kazi na kuacha kuwa karibu na mtoto wa kiume ambaye alihitaji uangalizi wa Baba zaidi. Anna hakutaka kuendelea kusikiliza malumbano yao, bila kuongea chochote alitoka na kuwaacha wakiendelea kulumbana na kutupiana lawama tu.

******
Siku iliyofuata Kelvin hakupelekwa tena shule bali alipelekwa hospitalini ambapo baada ya vipimo alionekana kweli ameshaingiliwa mara nyingi kinyume cha maumbile. Wazazi wake walimtafutia mtaalamu wa saikolojia ambaye baada ya kuongea naye kwa muda aliwaambia kuwa Kelvin alishaanza kujihisi kama mwanamke, namna alivyokuwa akijizungumzia alijiona mwnaamke na kama wazai wake wangekuwa makini kidogo wangeweza kuligundua hilo mapema.

Hawakumrudisha tena kwenye ile shule lakini walienda kuripoti lile tukio ambapo baada ya uchunguzi iligundulika kuwa wanafunzi takribani 20 walikuwa wakijihusisha na ule mchezo, wakifanyiana wenyewe kwa wenyewe hasa nyakati za usiku. Wazazi wa watoto wote walohusika waliitwa na kukabidhiwa watoto wao. Zoezi lile lilifanyika kwa siri kwnai wazazi hawakutaka watoto wao kujulikana kuwa wanafanya huo mchezo na walimu hawakutaka shule yao kupata sifa mbaya na kupoteza wanafunzi.

*****MWISHO****IMEANDIKWA NA****Iddi Makengo Jr.

Idadi ya mashoga imekuwa ikiongezeka siku hadi siku. Mpaka sasa hakuna tafiti hata moja ambayo inaonyesha kuwa kuna mtu anazaliwa akiwa shoga au kujihisi kuwa shoga. Kwa kiasi kikubwa ushoga huchangiwa na mazingira na katika nchi zetu hizi kuna aina mbili za mashoga. Aina ya kwanza ni wale wa ukubwani ambao hupenda mambo rahisi rahisi na kujikuta wanageuzwa kwaajili ya pili na aina ya pili ambayo ndiyo kubwa zaidi ni ile ya wanaoharibiwa wakiwa bado watoto.

Wazazi wamekuwa mbali sana na watoto wao, jukumu la malezi limekabidhiwa walimu kwa mzazi anapoona mtoto kafikia umri wa kwenda shule humpeleke bording kwa kisingizio cha kupata elimu bora ambayo ukiangalia kwa undani ni kiingereza. Mwalimu mmoja ambaye ana stress zake za maisha hawezi kuangalia watoto 40 na kuona wanakaa katika mstari, hawezi kuwa katibu na mtoto mmoja mmoja na kujua matatizo yake.

Mtoto anaporudi likizo na kwa wale ambao hawako shule za bweni jukumu la malezi ameachiwa dada wa kazi ambaye unamlipa mshahara mdogo kiasi kwmaba hata akimuogesha mwanao na kuona tofauti hatajali. Niwkaati sasa kwa wazi kuchukua jukumu mla malezi na kuwa karibu na watoto wao ili kugundua mabadiliko yoyote yanayotokea la sivyo tutaendelea kuzlaisha mashoga kila siku kwani watoto wanajua mengi na hatuwasimamii hata katika vipindi vya Tv wanavyoangalia.
 
Saa nyingine ni bora tu kuwa na vitoto vya kike. Vipigwe mashine mpaka vikome.

Kuliko kuwa na toto la kiume bwabwa.

Eee Mungu tunusuru!!
 
Du, tunakoelekea sasa mtoto WA kiume ataangaliwa kwa ukaribu zaidi kuliko wakike
 
kuna tatizo kwenye jamii lakini hatutaki kulikubali ili tutafute jawabu.Inabidi tukae chini tujiulize ni namna gani tutalitatua hili tatizo...bado tuna uwezo wa kulizuia kwa asilimia 90 tuamkeni jamani au tutabaki bila kizazi cha wanaume.
 
Back
Top Bottom