Kipupwe cha Nuclear

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,238
12,751
Miaka milioni 65 iliyopita Kimondo kikubwa sana kiliipiga dunia. Wakati huo dinosaurs walikuwa wanaishi duniani.

Mgongano wa kimondo hicho na dunia ulisababisha mlipuko mkubwa uliorusha mawe na moto maelfu ya kilomita kila upande. Moshi, majivu, vumbi na mawe yalirushwa juu angani. Viumbe hai vingi vilikufa kutokana na mlipuko huo.

Baada ya mlipuko huo, yale majivu na moshi vilivyorushwa angani vilisambaa duniani kote na kuziba mwanga wa jua. Matokeo yake dunia nzima iliingia kwenye kipindi cha baridi.

Baridi ya kuganda. Ni kutokana na mlipuko huo na baridi iliyofuatia kwa miaka kadhaa ndiyo dinosaurs wakatoweka duniani.

Mwaka 1815 kulitokea mlipuko mkubwa wa Volcano kwenye mlima Tambora huko Indonesia. Mlipuko kama huo haujawahi kutokea kwa miaka 10,000 iliyopita. Mlima Tambora uliokuwa na urefu wa mita 4,300 ulisambaratishwa na hadi leo una mita 2,800.

Mlipuko huo ulisababisha wingu la majivu kuruka juu duniani. Majivu hayo yaliziba mwanga wa jua na kusababisha baridi kuingia duniani kwa miaka kadhaa iliyofuata.

Ukosefu wa mwanga wa jua ulisababisha mimea kutoota vizuri na njaa kali sana iliingia kwa miaka kadhaa iliyofuatia. Huko Ulaya watu wengi walikufa kwa njaa.

Bomu la nuclear lililopigwa mji wa Hiroshima liliua watu laki moja. Leo hii kuna mabomu yana nguvu mara 1,000 ya lile la Hiroshima. Bomu la nuclear, kama kupigwa na kimondo na mlipuko wa volcano, hurusha majivu na moshi mwingi angani.

Moshi na majivu hayo hurushwa juu sana kiasi kwamba hupita sehemu ambako mvua hutengenezwa. Matokeo yake ni kuwa hukaa huko juu kwa miaka mingi sana.

Ikitokea nchi mbili au zaidi zikapigana vita ya Nuclear basi dunia nzima itafunikwa na moshi. Moshi huo utazuia mwanga wa jua na dunia yote itaingia kwenye baridi/kipupwe cha Nyuklia(Nuclear winter).

Madhara ya kipupwe cha nyuklia ni makubwa kuliko hata ya mabomu yenyewe. Mimea duniani itashindwa kuota sababu ya kukosekana kwa mwanga wa jua na njaa kali itaingia duniani. Njaa hiyo haitachagua ulipigana vitani au haukupigana.

Tupige kelele kuwe na amani duniani.
 
madhara ya nuclear kwa sasa yanatazamiwa kuturudisha early stone age.
kutokana na ukweli kwamba yatapigwa mengi kwa wakati mmoja,ukizingatia kwamba yana nguvu kuwa zaidi kuliko hayo ya mwaka 45.
hii inaweza kufanya sehemu kubwa ya uhai wa dunia kutoweka kabisa,na sehemu chache zitakazobaki na uhai kubaki nao zikiwa katika hali mbaya bila recover kwa maelfu ya miaka kutokana na kukosa nguvu kubwa ya kujijenga upya kwa haraka.

kwahiyo mkuu kifusi,majivu na masizi itakuwa sehemu ya madhara ambayo pia yatamalizia kauhai kadogo katakakokuwa kamesalia.

zipo tetesi kwamba,huko area 5 kuna mpango wa kuchimba mahandaki kwa ajili ya kujificha endapo swala hili litajiri.
 
Back
Top Bottom