Mwananchi Mtanzania
Member
- Jul 3, 2012
- 92
- 13
Sisi kama Watanzania inabidi tufanye kazi kwa ajili ya hatma ya taifa moja, lenye nguvu na umoja. Hivi ile hali ya zamani imekwenda wapi kwa watu wa dini zote kupendana na kushirikiana?
Mimi kama mtanzania ningependa kama Bwana Juma akitoka msikitini, kama ni usiku na njia ina vibaka, awe huru kugonga hodi kwa Yosefu amsindikize. Na kama Yosefu siku ametoka kanisani na akapata kiu, basi awe huru kuomba maji hata chakula ka bwana juma. Nina wasi wasi shutma nyingi watu wanazotoleana humu si za kweli.
Ifike kipindi tuwe na aibu. Siwezi leo nikamtukana Mkristo au Muislam, Mhaya, Mchaga, Nnyakyusa, Mhehe, Mkinga, Mbena… nk katika Jamii Forum, ati tu kwa sababu identity yangu haijulikani, wakati katika hali halisi, nina marafiki wa imani na makabila husika. Hivi unajisikiaje unavyomshutumu mtu wa imani fulani, halafu huko mabara barani unapata huduma kutoka kwake? Ni nani ambaye akienda dukani, akienda ofisini, akienda polisi, akipanda dala dala, e.t.c hua anauliza imani au kabila la mtu ambaye ana msaidia? Sasa hii tabia ya leo ya kuanza kubandikana majina: Fulani Mkabila, Fulani mdini inaanzia wapi? Ni kweli wana hizi tabia, au mengine ni matatizo yetu wenyewe?
Labda niulize tu: Kipimo cha UDINI na UKABILA ni nini? Ni idadi kubwa ya marafiki na maswahiba wa imani husika? Sidhani. Kila mtu amezaliwa, kukulia, kusoma na kuishi katika maeneo Fulani. Kwa hali hiyo basi, historia yako ya maisha ina mchango mkubwa wa aina ya marafiki zako. Kama mtu umekua katika meneo ya mchanganyiko, ni lazima utakua una mchanganyiko wa marafiki na jamaa tofauti, ukilinganisha na mtu ambaye sehemu kubwa ya maisha yake imekua ni katika aneo moja, au lenye kabila au imani Fulani ambayo hapo ndio dominant. Hivyo basi, sidhani kama kuna mtu hua anachagua azaliwe au aishi katika eneo Fulani. Hivyo basi, pahala mtu alipozaliwa, shule aliyosomea, mambo kama kama mafundisho, madrass, nature ya familia husika (mchanganyiko kiasi gani) e.t.c. hua vinachangia sana katika aina ya mchanganyiko wa marafiki.
Sasa swali la kujiuliza, ni wangapi kati yetu, wanaosema Fulani "Mdini" (iwe Mkristo or Muislamu) au ni Mkabila, wamewahi kubaguliwa kidini au kikabila na mtu husika? Hua tunatumia vigezo gani? Hisia, minong'ono, kutokuaminiana, idadi ya marafiki zake, au ni namna gani anavyopenda imani yake? Nitashangaa kama mtu akihukumiwa kwa kupenda imani yake, kwa sababu after all hiyo ni haki yake. Sidhani kama mtu ameamua kua thabiti katika Uislam au Ukristo, leo akabandikwa jina la "Mdini", kwa sababu otherwise utataka huyo Muislam au Mkristo afanye mambo kinyume na imani yake – hapo, tutatafutana lawama bure!
Imefikia wakati sisi watanzania tunapoteza hata uwezo wa kufikiri katika mambo fulani. Kwa nyakati tofauti, kwa mfano, nimesoma Mz Ruksa, na Mh Samwel Sitta, wote wakishutumiwa kua wadini, kisa tu walisema "Kiongozi bora ni Mcha Mungu"! Hivi leo msemo huu wa kiswahili wa kawaida umegeuka kua UDINI? Wote walihukumiwa "wadini" kutokana na kauli inayofanana. Kilicho wahukumu, nafikiri, ni imani zao. Ni lazima tutafakari mara mbili kabla ya kutoa kauli zetu.
Kimtazamo wangu, ukimshutumu Fulani kua ni mdini au mkabila, eti tu kwa sababu ana marafiki wengi wa imani au kabila fulani, na hilo linakukera, basi wewe ndiye mdini au mkabila. Na ni lazima uanze kua na mazoea ya kukubali hali ambayo si kila sehemu utakuta watu wenye kabila au imani yako.. wanaweza wawe wachache, au wasiwemo kabisa. Cha muhimu ni kuangalia unapata haki yako? Anayefanya kazi hiyo ana maadili na taaluma husika? Na mambo haya, si ya kuyatolea maamuzi kihisia au ki minong'ono.
Iwapo ukaangalia chama cha siasa, na ukakihukumu tu kina udini au ukabila kwa sababu ya viongozi wake, yawezekana pia una tatizo la udini au ukabila, kwani siasa za nchi hazihusiani na ibada au matambiko (kwa msemo wa Mwalimu), na hivyo basi, sioni sababu kwa nini ukereke eti ni kwa sababu gani viongozi wa chama Fulani si wa imani au kabila inayo fanana nay a kwako.
Mtu akiteua viongozi, ukaangalia tu ukaona ambao hawafanani na imani yako ni wachache, halafu ukaamua kumshutumu mfanya uteuzi ni mdini au mkabila, basi wewe ndiye una matatizo, kwa kua tunajua wazi kwamba katika teuzi za kitawala, iwe ngazi ya kijiji au hata uwaziri, kwa msemo wa Mwl Nyerere, sio nafasi za matambiko au Ibada... Hivyo basi, suala la wangapi ni kabila gani au wangapi ni dini gani, kama linakukera, basi wewe ndiye unatatizo (haijalishi unaitwa Gabriel au Hussein), na ni lazima ufanye kazi kuliondoa moyoni mwako.
Nina wasi wasi, wengi tunaotoa shutuma za UDINI au UKABILA, sisi ndio tuna matatizo, na si hao tunao watuhumu.
Mungu ibariki tanzania