............nashukuru kwa ufafanuzi,moja, kwa mazoea ni kuwa chenye kukatika ni kile chenye umbo lenye kuonekana..ni kwa kwa mantiki hiyo unapata tabu kufikiri kuwa umeme nao hukatika kwa vile hauna umbo lenye kuonekana(tunaona nyaya na athari ya umeme lakini si umeme wenyewe).nadhani hapa kiswahili kilikosa neno stahiki na hivyo kikaazima kutoka lugha ya kiingereza(power cut off) na kwa makubaliano kwa vile kitu kinapokatika kunakuwa na ends mbili zisizo na muunganiko basi hewala kukosekana kwa huduma ya umeme wacha kuwe ni umeme kukatika!kwa hiyo mkuu..umeme unakatika, maji yanakatika kadhalika simu inakatwa.kuhusu waya mkuu..unakatika..ingawa kuna mkuu wangu mmoja amesema waya unavunjika, sidhani!
.............rungu,usichanganye lugha na wewe unapokuwa kazini,maana unapokuwa kazini hata maji yanaweza kuvunjika,jaribu kudhibitisha kwa kumuuliza mtu aliyepigwa rungu uone................ha........haa........haaaa,nashukuru kwa jibu.Umeme unakatika, waya unavunjika!
.....tusubiri wataalamu wa lugha......................,rungu na kirungu.............pia itafuata@Al Zagawi: Asante kwa ufafanuzi fasihi. Hii mada ukiiangalia kwa pupa inaoneka kama ni rahisi vile, lakini ukiikaribia zaidi ndio ugumu wake unavyoziidi kuongezeka. Swali langu la nyongeza ni: ipi tofauti kati ya kukatika na kuvunjika? Kijiti cha kiberiti kinakatika au kinavunjika?
Duh, hii kali!.....tusubiri wataalamu wa lugha......................,rungu na kirungu.............pia itafuata
@Al Zagawi:
Asante kwa ufafanuzi fasihi. Hii mada ukiiangalia kwa pupa inaoneka kama ni rahisi vile, lakini ukiikaribia zaidi ndio ugumu wake unavyoziidi kuongezeka. Swali langu la nyongeza ni: ipi tofauti kati ya kukatika na kuvunjika? Kijiti cha kiberiti kinakatika au kinavunjika?
Matumizi mengine ya kuvunja na kukata ni:kuvunja :1- tunaweza kusema ni kwa kutumia kitu kisicho na makali, mfano vunja mlango kwa kutumia jiwe , vunja nyumba kwa kutumia mitaimbo nk.
2- kuvunja kwa kutumia nguvu za mwili , beki wa timu A kamvunja mguu mshambuliaji wa timu B.
kukata : 1- ni kuvunja ila hili linatumika kwa kitu chenye makali, panga,kisu shoka nk . kata mti ,tawi
2- kusita kwa huduma kama maji ,umeme nk.
-Kukata kiuMatumizi mengine ya kuvunja na kukata ni:
- Kuvunja mahusiano
- Kuvunja ungo
- Kuvunja mkutano
- Kuvunja (kukata) mbavu
- Kukata shauri
- Kukata mawasiliano
- Kukata viuno
- Kukata karata
- Kukata sala
.................
Hii ni kusema kuwa hata "umeme unakatika", na hili tusilichukulie kama ni upungufu wa Kiswahili bali ni utajiri wa lugha yetu.
Mjadala huu umetulia!
Duh,amakweli kukatika kwa umeme na waya,sasa imekuwa tena kuvunja na kukata,mara ungo,haya tena viuno.Rungu nisaidie,kwani Mammamia kama alivyotujuza huu ni utajiri wa lugha yetu.kirungu na rungu tofauti ni nini?.................,Kwa haraka haraka tuu si kila kukatika kuna hasara,hata pia kuvunja.......................ukichukulia maneno ya Mammamia hapo juu utaona kuwa,kweli lugha yetu inautajiri mkubwa,unaweza kubisha lakini tafakari na chukua hatua.......................jaribu kukata,si umeme ila kiuno uone...............,vilevile waulize waliovunja ungo........je,wanajuta...............Nikupongeze sanaaaaa Mammamia,si kwa kukata kiuno au kuvunja ungo,bali kwa kutujuza upana wa lugha yetu..............kiswahili hoyeeeeeeeeeeeeMatumizi mengine ya kuvunja na kukata ni:- Kuvunja mahusiano- Kuvunja ungo- Kuvunja mkutano- Kuvunja (kukata) mbavu- Kukata shauri- Kukata mawasiliano- Kukata viuno- Kukata karata- Kukata sala.................Hii ni kusema kuwa hata "umeme unakatika", na hili tusilichukulie kama ni upungufu wa Kiswahili bali ni utajiri wa lugha yetu.
Oyeeee! Duh, aisee hata mimi sijui tofauti ya kirungu na rungu. Wacha akina X-Paster waje na tafsiri zao!..............kiswahili hoyeeeeeeeeeeee
Wana JF mnijuze,kipi kinakatika umeme au waya?
Wana JF mnijuze,kipi kinakatika umeme au waya?